Saturday, December 7, 2013

MWALIKO WA KUHUDUMU!!!


Watumishi wa Mungu wengi sana hawaendi mahali kufanya HUDUMA hadi wapewe mwaliko rasmi na kutimiziwa baadhi ya masharti ikiwemo KISI fulani cha malipo au gharama. Sipingi kulipiwa gharama kwa sababu maandiko yanasema “watahubirije kama hawakupelekwa?”

Ninachotaka kuweka wazi hapa ni aina tatu za MIALIKO. Mwaliko wa kwanza, kuna wakati hujaalikwa na mtu kwenye huduma/kanisa lake ila Mungu amekualika kwenda kufanya kazi maalumu. Mwaliko wa pili, kuna wakati hujaalikwa na Mungu ila watu wanataka ukahudumu kanisani/mahali fulani. Na mwaliko wa tatu, kuna wakati utakua umealikwa na Mungu kufanya huduma na watumishi wa mahali hapo hawajakualika. Aina zote hizi za mialiko huwezi kukwepa kama wewe ni mtumishi wa Mungu, au Mwana wa Mungu kwa sababu WOTE tumeitiwa KUSUDI maalimu katika mwili wa Kristo, uwe unajua au hujui.

Umewahi kujiuliza ni mara ngapi Yesu amealikwa hekaluni kuhubiri? Kwanza wale wakuu wa DINI walikua wanatafuta namna ya kumfungia mahali hata asitembee licha ya kuhubiri hekaluni kwao. Lakini Baba yake “alimwalika” kufanya huduma na alienda MAHALI alipotakiwa na KUTIMIZA kusudi bila kusubiri “watu” kumwalika. Angalia mitume 11 wa Yesu, walikua wanawindwa na kuonekana ni VICHAA na wenye PEPO. Watu waliochanganyikiwa na wasifaa katika jamii. Wakuu waliwaona kwama mahali pa kuwafaa ni jela! Lakini ilikua ikifika “saa ya sala” utawaona wako hekaluni. Sasa usifikiri walikua wanapewa tu nafasi kule mbele kwenye viti maalumu na kuhehimiwa! No! walikua wanafanya kazi ya Mungu katika mazingira yoyote “wakati ufaao na wakati usiofaa”.

Sitaki nikupe ushuhuda binafsi lakini kwa sehemu tu nataka nikwambie mimi binafsi nimeenda mahali pengi sana bila kualikwa. Mara nyingine sikusema hata neno moja na mara nyingi hata “wenyeji” hawakujua kama nimwo katikati yao, ila huwa nahakikisha nimeacha MBEGU na FOOT PRINTS kwamba kuna “mtu wa Mungu alipita hapa”. Kuna idadi kubwa sana ya Watumishi wa Mungu wako namna hii na nimeona niweke hii SIRI hadharani ili usikae tu pale KANISANI au MAHALI popote kama boga. Wala usishawishi watu WAKUALIKE na kukupa nafasi za Mbele, Muulize Mungu kusudi lake na nini anataka ufanye kwa wakati huo. Matokeo ni mkubwa sana sana katika ulimwengu waroho ukitembea namna hii.

Ukiona mtu anafugwa kwenda mahali eti kwa sababu hela haijaingia kwenye accounti yake ya benki, jiulize swali hili, Je! Hana nauli? Na kama nauli anayo na amegoma kwenda kwa sabau hela haijaingia kwa account yake, juilize tena swali, Je! Anamtumikia nani? Kama anamtumikia Mungu, tena jiulize swali, Je! Amealikwa na Mungu au wanadamu? Na kama amealikwa na Mungu, jiulize tena swali, Je! Anatenda MAPENZI ya nani? Haya majibu ni kwa matumizi binafsi na ujipange sawasawa kuyajibu kama wewe unatarajia UZIMA wa MILELE.

Namaliazia kusema kwamba, MIALIKO maalumu ni michache sana. Mavuno yako tayari na ni MENGI. Bwana wa mavuno anasema “watenda kazi ni wachache”. Kwa bahati mbaya, hawa watendakazi wachache pia wanasubiri mialiko maalumu! Funguka Macho ya Rohoni kwa Jina la Yesu.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na Ufunuo wa KWELI ya Mungu uwe nasi sasa na hata MILELE. AMEN.

Frank Philip.

No comments:

Post a Comment