Wednesday, February 19, 2014

*USIMKOSEE MTU MAKUSUDI KWASABABU UNAJUA ATAKUSAMEHE TU UKITUBU!!!*

SHALOM!!!
Binadamu wote hatujakamilika,kila siku tunaendelea kukamilishwa,hata awe nani bado anayo madhaifu yake na kwahiyo atafanya makosa tu (Muh 7:20), Kuna wakati unaweza kufanya jambo kwa nia nzuri tu lakini wengine wasitafasiri hivyo na hivyo ukaonekana mbaya na hivyo wakapanga ubaya ama kisasi juu yako,kuna wakati unakosea na hata wewe unatambua kweli hapa nimekosea na wakati mwingine kwasababu ya hasira ama uchungu mtu anaweza kufanya ukorofi wa makusudi kwa mwingine na hivyo kumuumiza,sasa aitha umekosea bila kujua ama umekosea na ukajua ama umefanya makusudi,aliyekosewa lazima aumie sana kwa namna nyingi,na tena anaweza aiumie tu bali hata akachafuliwa jina kupoteza "credibility" kwa jamii yake.

WAJIBU WA MKOSAJI;
Ni kushuka chini bila kujali wewe ni nani wapi na una nini, na kwenda kuomba msamaha na kutafuta suluhu kwa yule uliyemkosea,ili amani na urafiki ama undugu udumu tena,maana usipofanya hivyo utaendelea kukwama maana machozi ama huzuni ya mtu mwenye haki inaweza kukwamisha mafanikio yako!


NGUVU YA ALIYEKOSEWA:
Sio jambo rahisi sana kwa mtendwa kuvumilia na kuwa stamina kama ya mwanzo,lakini ikiwa unapenda kupona basi unaweza kumfuata aliyekukosea na kuomba msamaha wewe na kumtangazia msamaha na hapo wala usiendelee kuwaza wala kulifikira tena jambo hilo,usiposamehe na ukangoja aje wewe ndio unakuwa matesoni,yamkini mwenzio akasahau kabisa,wanasema Kusamehe ni tabia ya watu wenye nguvu,mtu dhaifu hutunza kinyongo na kukosa suluhu,tena upo usemi usemao Kisasi kikubwa kuliko vyote ni KUMSAMEHE ALIYEKUKOSEA!!!


*Ukikosewa na wewe ukatafuta kulipa kisasi,utakuwa umejipalia moto zaidi maana utakuwa na hatia ya kukosea wewe na sio kukosewa tena!!

Biblia inasema:....Wana amani nyingi waishikao sheria ya Bwana na wala hawana jambo la kuwakwaza! hivyo kukwaza ni kosa na kukwazika pia ni kosa ikiwa una kweli ya Kristo ndani yako!

Tafuta kuwa na amani na watu wote kwanza kisha ndio huo utakatifu,hii ina maana hata hiyo amani sio rahisi sana lakini kama umedhamiria na unapenda amani utaitafuta kwa gharama yeyote ile, unaweza kwenda kuomba msamaha na bado wakakung'ong'a na kukuona umeishiwa na hauna lolote,lakini usijali msamaha ama amani unayoitafuta ni kwa faida yako!!

GHARAMA YA MAKOSA:
Ukimkosea mwenzio unamsababishia maumivu na mfadhaiko wa kisaikolojia na wakati mwingine anaweza kukukwama kufanya mambo yake na hata kukwama kazi zake,kwa mfano unakwenda kumuandika magazetini mwenzio vibaya ama hata kumsema kwa marafiki vibaya sana,unatarajia nini labda,maana unaweza ukadhani unafanikiwa sana kumchafua mwenzio na baadae baada ya muda unakwenda kuomba msamaha kirahisi tu,ni kweli anaweza kukusamehe na imempasa kusamehe lakini lazima ujue gharama ya msamaha ni kubwa sana sana na huwezi ilipa ila unasemehewa bure tu kama Kristo! Kwanini ni gharama? ukimkosea mwenzio na kumdhalilisha ni kama kumvua nguo mbele ya hadhara na kisha unamkimbilia kumpelekea nguo akiwa peke yake,unadhani watu watasahau kwa kuona uchi wake peupe hata kama sasa akipita umemvisha nguo?


MFANO HAI:
Kuna mtu mmoja amewahi kumsema sana mwenzake vibaya hapo zamani katika mtaa wa mji fulani,naam habari mbaya zikaenea na hata mtu huyo akashindwa kutembea kwa amani mtaani hapo,basi baadae yule jamaa alimkosea mwenzake akaona ngoja tu akaombe msamaha na kwa kuwa alijua ni rahisi tu,basi akaenda kuomba msamaha,basi alipofika kule yule mtendwa akasema nimekuelewa sana na hakika nimekusudia kukusamehe ila naomba uje kesha na jogoo ili tumchinje na tule pamoja kwa furaha,kurejesha undugu wetu....basi yule Bwana akaona aaah mbona rahisi tu,akaenda sokoni akanunua jogoo mkubwa sana na kwenda kwa yule bwana kesho kwa furaha,na alipofika yule mtendwa akasema basi sasa,tutafanya hivi....tutatembea huu mtaa wote huu ukiwa na huyo Jogoo mkononi mwako,na itakuwa tukipiga hatua,utakuwa ukimnyofoa manyonya yake na kusema "KWELI NILIKUKOSEA NDUGU YANGU NA NAOMBA RADHI" na kuyaachilia chini hayo manyonya mpaka utakapommaliza kumnyonyoa huyo jogoo naamini tutakuwa tumefika mwisho wa mtaa kisha tutarejea na kumchinja sasa(kumbuka jogoo ananyonyolewa akiwa mzima).....basi jamaa akaona mbona easy tu...basi akawa ananyoa manyoya huku jogoo akilalamika "KWI KWIII" na kuyaachia chini na walipofika mwisho wa mtaa,yule jamaa akamwambia "HIVI NDIVYO ULIVYONIFANYA KWA YALE ULIYOYASEMA,BASI NAOMBA HUYO JOGOO NIMEBEBE NA WEWE UANZE KUYAOKOTA MANYOYA YOTE ULIYOYADONDOSHA MPAKA MWISHO" hapo ndipo kazi ilikuwa ngumu,maana alijitahidi kuokota mpaka mwisho na baadae yule jamaa akasema je unaweza kuyarudishia manyonya hayo kwa jogoo na yatoshe kumfunika utupu wake? na kweli walipojaribu hayakutosha hata mgongoni, basi wakaenda nyumbani na kumchinja jogoo yule na kula pamoja,ila ndugu yule akajifunza sana kuwa usimkosee mtu kwa makusudi kwasababu ukiomba msamaha atakusamehe tu!

Hata neema ipo nyingi,je ni ruhusa kutenda dhambi??? Hapana!!

HIVYO NAKUSIHI TENA NAKUSIHI SANA,KUWA USIJE UKAJARIBU HATA SIKU MOJA KUMKOSEA AU KUMDHALILISHA MWENZIO KWA MAKUSUDI TU AU KWA KUTAKA SIFA KWA WALE WANAOKUZUNGUKA AMA KWASABABU IWAYO YOYOTE ILE,ETI KWASABABU NI MTU MUELEWA KWAHIYO UKIOMBA RADHI ATAKUSAMEHE TU,KUWA MAKINI SANA!!

N.B: Hata mimi sijakamilika na yamkini nakukosea sana bila kujua, tafadhali ninakuomba unisamehe mwenzio na wala usiniwekee fundo na usiache kuniombea ili niwe focused kwa hatma ya maisha yangu,mimi sina niliye na fundo naye moyoni na kama ukihisi labda nakuchukia,hapana ninakupenda,yamkini sijakutafuta ama hatujakaa kukutana pamoja kwasababu tu za majukumu ya hapa na pale ila kweli toka moyoni nakupenda....HII SIYO KWA MTU MAALUM,BALI YEYOTE ANAYEDHANI AMA ANAYEHISI HIVYO MOYONI MWAKE!!!
Najua wapo wengi mnaniombea na kunitakia mema basi Mungu wangu asiwashahu sawasawa na maneno yake mwenyewe...maana amezitukuza ahadi zake kuliko hata Jina lake mwenyewe,mbarikiwe!!!


Na Fredy Chavala
+255 713 883 797

MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE JANGWANI TENA!!!

HII NI SEMINA YA NENO LA MUNGU KWA AJILI YA WATU WOTE,BILA KUJALI DINI WALA MADHEHEBU YAO, NJOO ULE NENO NA UKUE KIROHO!!
HUU NI MWAKA MWINGINE TENA NA HII NI SEMINA YA KWANZA KWA DAR,PANGA KUTOKUKOSA!!
HAKUNA KIINGILIO CHOCHOTE!!!

Semina itakuwa ikirushwa moja kwa moja kupitia WAPO Fm (98.1) na UPENDO Fm (107.7)

Thursday, February 13, 2014

WASANII "KUREJEA MADHABAHUNI" NDANI GOSPEL ARTISTS BREAKFAST!!! 22/02/2014

SHALOM!
Kwa mara nyingine tena Ikiwa ni ukurasa wa kwanza wa msimu wa pili na mara ya kwanza kwa 2014, Chavala Ideas Platform (Mahali yanapozaliwa mawazo mapya na makutano ya mawazo yanayotekelezeka) kupitia Wavuti ya Kikristo Gospel Standard Base wamekuandalia tena Staftahi maalum kwa ajili ya mwili wako na nyingine kubwa zaidi kwa ajili ya roho yako wewe ulipewa kipawa na unatumika madhabahuni kwa Bwana iitwayo "GOSPEL ARTISTS BREAKFAST"
Chai hii maalum kwa ajili ya waimbaji wa aina zote za nyimbo za injili,wachezaji,wapiga vyombo,wazalishaji,wasmbazaji,watangazaji,wachekeshaji,waigizaji na kila mwenye kipawa chake anachokitumia madhabahuni itanyweka pale WORDALIVE CENTRE-Sinza Mori, Jumamosi ya tarehe 22/02/2014 Kuanzaia saa 2 asubuhi mpaka 5:59 asubuhi!
Maada au msingi wa chai hii utakuwa ni juu ya wasanii wa injili "KUREJEA MADHABAHUNI" na Mchungaji na mwanamuziki wa siku nyungi Rev.DAVID NKONE atatuhudumia!

Hii sio fursa ya kukosa na sio kwa ajili ya mtu fulani tu maalum,bali ni kwa ajili ya kila anayemaanisha kutumika madhabahuni!
Hakuna Kiingilio na ukiwahi utafanya jambo la maana zaidi!!!

Chai hii inandaliwa na MODERN EVENTS CEREMONERZ
Kwa kusirikiana na WordAlive Centre na

Imedhaminiwa na
1.Great Potentials Ltd
(......Living your Dreams by your potential!!)
2Quality Vision Picture

(Quality vision pictures inafanya Gospel Videos.na sasa kwa watu  20 wa mwanzo kuna ofa maalumu kwa mawasiliano wafike officen Kimara. 0715416961,na 657295614)

NJOO UONGEZA MAARIFA,NJOO UCHANGAMOTISHWE NA NJOO UFAHAMIANE NA MARAFIKI WENGINE,NI MATUMAINI YANGU KUWA HAUTAKUJA PEKE YAKO!!!

0713 883 797