Sunday, December 22, 2013

KAMA UNATAKA MUNGU AONEKANE NA WATU JIFUNZE HII SIRIKipimo cha UDHIHIRISHO (MANIFESTATION) wa Mungu kwenye HADHIRA (PUBLIC) ni MUDA, BIDII na HALI ya MOYO wako UKIJIHUDHURISHA mbele Zake mkiwa wenyewe wewe na Mungu pekeyenu (SIRINI).

Kama UKIJIHUDHURISHA mbele za Mungu wako kwa BIDII na kwa UELEKEVU mahali pa SIRI, basi Mungu ATAJIDHIHIRISHA mbele ya WATU hadharani.

Ukitaka Mungu aji-present kwa watu basi jifunze kuji-present kwa Mungu.

Ni aheri ukose MUDA wa kuandaa PRESENTATION kwa watu na sio MUDA wa kuji-present kwa Mungu, kwa maana unaweza ku-present kitu chochote mbele za watu ILA HUWEZI kum-present Mungu! Ndio maana kazi ya Mitume ilikua KUHUBIRI na KAZI ya Mungu likua KULITHIBITISHA hilo Neno kwa ISHARA na MAAJABU.

Kazi ya Musa ilikua kuji-present kwa Mungu na kupata maelekezo na KAZI ya Mungu ilikua KUTENDA miujiza (kuji-present) mbele za Farao!

Frank Philip.

No comments:

Post a Comment