Sunday, December 1, 2013

HILA za ADUI!!!


Ukienda mnadani na ukaona NG'OMBE aliyenona na wengine wanaonekana afya mbovu. Jua yule aliyenona zaidi yuko KARIBU na KUCHINJWA kuliko huyu mwingine ambaye havutii.

Sasa unapoanza hatua za kutaka kumpendeza Mungu (KUNONA KIROHO), utashangaa ghafla watu wanakuita HANDSOME/BEAUTIFUL na wanaanza kukufanyia mambo ambayo yanakuvuta KUTENDA dhambi. Jua ADUI anataka KUKUCHINJA! Jitambe na UPONE.

Sasa, unavyozidi kua karibu sana na MUNGU unakua KIVUTIO cha ADUI na unakua mawindo. ILA kama wewe tayari ni MALI ya adui, hana haja sana KUWINDA kilicho chake! Hao watu wanaokutaka ufanye dhmbi HAWAKUPENDI ila hawakutakii MEMA! Mtu anayetaka UFANYE DHAMBI anakuangamiza na sio KUKUPENDA.

Jifunze KUJIFUNIKA kwa DAMU ya YESU na kujificha NDANI ya Yesu ili ADUI akija asikuone wewe ila Yesu. Utakua salama.

Frank Philip.

No comments:

Post a Comment