Tuesday, June 25, 2013

HATIMAYE "CHRISTINA SHUSHO" NA "MARTHA MWAIPAJA" WAINGIA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA MSANII BORA WA AFRIKA MASHARIKI!!!!!

 UNAWEZA KUMPIGIA KURA CHRISTINA SHUSHO PAMOJA NA MARTHA MWAIPAJA ILI MMOJA WAO APATE KUSHINDA NA KUWA MWIMBAJI BORA WA INJILI WA AFRIKA MASHARIKI KWA MWAKA 2013.
HII NI MARA YA PILI BAADA YA CHRITINA SHUSHO KUINGIA KATIKA MTANANGE HUO MWAKA JANA!
INGIA MTANDAONI KWA KUFUATA LINK HII HAPA CHINI NA UPIGE KURA YAKO SASA!!!
http://www.africagospelawards.com
AU KWA URAHISI UNAWEZA UKAENDA MOJA KWA MOJA KATIKA LINK HII HAPA CHINI;
http://www.africagospelawards.com/nominations.html
UNAWEZA KUPIGA KURA MARA NYINGI UWEZAVYO NA KUWASHIRIKISHA NA WENGINE PIA, AKISHINDA MMOJA WA HAWA NI HESHIMA YA PEKEE KWA TANZANIA,MAANA HAKIKA JINA LAKE LITAFAHAMIKA HATA HUKO MBALI NA KAZI YA MUNGU ITAZIDI KUSONGA MBELE!!!

Thursday, June 20, 2013

HERE ARE FINAL TOUCHES IN TORONTO,CANADA READY FOR BISHOP ZACHARY KAKOBE TO PREACH!!!

FOR THREE DAYS....IN TORONTO,CANADA,THERE WILL BE HEAVY AND VERY STRONG ANNOINT OF JESUS CHRIST WITH MAN OF GOD, BISHOP ZACHARY KAKOBE.

EVENT SCHEDULE:

Thursday June 20 - from 7pm

Friday June 21 - from 7pm

Saturday June 22 - from 5pm

Sunday June 23 - from 5pm

BIBLICAL SIGNS AND WONDERS WITH PRAISE AND WORSHIP, WORSHIP TO BE LED BY DON MOEN, MARTHA MUNIZZI AND ON THE STAGE ALSO THERE WILL BE KRYSTAAL WHO ARE RESIDING IN CANADA!!

OFFICIAL ACCOMMODATION: TORONTO AIRPORT MARRIOTT HOTEL - RESERVATIONS FILLING UP FAST

Toronto Airport Marriott Hotel is the official accommodation for the Bishop Zachary Kakobe Toronto Miracle Healing Crusade and Restoration Retreat. The Toronto Miracle Healing Crusade which will be held at the Rexall Centre (Tennis Stadium) from June 20 - 23, 2013; will be coupled with the Restoration Retreat which will be held at the Toronto Airport Marriott Hotel, as per the following schedule:
Pastors' Breakfast Meeting With Bishop Kakobe
Subject: Church Growth and Revival Impartation Prayer
Day/Date: Friday June 21, 2013
Time: 10.00 AM

All Singles Breakfast With Bishop Kakobe
Subject: Breakthrough Prayer
Day/Date: Saturday June 22, 2013
Time: 10.00 AM

The Couples Covenant Dinner With Bishop Kakobe
Subject: Breaking the Circle of Divorce
Day/Date: Monday June 24, 2013
Time: 07:00 PM

You are strongly encouraged to arrange your accommodation at Toronto Airport Marriott Hotel and enjoy Bishop Zachary Kakobe International Ministries special discount rates. Book your Hotel rooms online 24/7, directly with Toronto Airport Marriott Hotel, 901 Dixon Road, Toronto, Ontario M9W 1J5 Canada. Reservations are filling up fast so make your reservation today.

HERE ARE SOME PICTURES BEHIND THE SCENE; 
PEOPLE AT WORK

THE STAGE
WE BELIEVE THIS CRUSADE WILL BE VERY POWERFUL!!
GOSPEL STANDARD BASE IS WISHING YOU ALL THE BEST, BISHOP ZACHARY KAKOBE WITH THE WHOLE MINISTIRIAL TEAM!!!

King Chavala-MC/Comedian
+255 713 883 797

Monday, June 17, 2013

HABARI NJEMA SANA KWA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA.....SHEREHE ZA ISHARA NA MIUJIZA!!!!

WAKAZI WA MWANZA MPOOOOOOOOO
 
Haya tena ni SHEREHE ZA
ISHARA NA MIUJIZA
Pamoja na Mtumishi wa Mungu wa Kimataifa
Mwinjilisti toka Sweden - Rev Johannes Amirtzer
Pamoja na Band yake ya SOS PRAISE TEAM Toka Sweden
 
Wakati wako ni SASAAAA!!
Walete Wagonjwa na wenye shida mbalimbali nao wataombewa na kupokea MUUJIZA wa KIMUNGU Kutoka kwa Mtumishi na Mpakwa mafuta wa Mungu Johannes Amirtzer - TOKA SWEDEN
Ni VIWANJA VYA FURAHISHA - MWANZA
JUNI 19 HADI 23, 2013
SAA 9:30 ALASIRI HADI 12:30JIONI KILA SIKU
 
HIIII SI YA KUKOSA MWALIKE NA JIRANI YAKO
 
GOSPEL STANDARD BASE BLOG INAWATAKIA BARAKA NYINGI ZA BWANA NA MAFANIKIO TELE,HALELUYA!!!!

Thursday, June 13, 2013

TANZANIA GOSPEL SINGERS' BREAKFAST....3rd Episode ON 15th June 2013!!!

SHALOM!
HABARI NJEMA KWA WAIMBAJI WOTE WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA HUSUSANI WAISHIO MKOA WA DAR ES SALAAM AU WATAKAOKUWEPO JIJINI TAREHE HIYO,MNAKARIBISWA TENA KWENYE CHAI MAALUM YA ASUBUHI ITAKAYONYWEWA JMOS YA TAR 15/06/2013 KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI MPAKA SITA NA NUSU MCHANA,

CHAI HII NI MAALUM SANA KWANI INAWAPA FURSA WAIMBAJI KUONANA,KUFAHAMIANA,KUSAIDIANA,KUSHAURIANA NA KUANZISHA MASHIRIKIANO,LAKINI JUU YA YOTE KUJIFUNZA NA KUOMBA PAMOJA....AWAMU HII YA TATU MWALIMU WA MUZIKI NA MWANAMUZIKI SAMUEL YONAH ATAKUWA AZINGUMZA KWA KINA KUHUSU MUZIKI KITAALAMU ZAIDI!


HAKUNA KIINGILIO CHOCHOTE,WEWE UKIPATA HABARI HII MWALIKE NA MWIMBAJI MWEZIO MJE WOTE!
HAIJALISHI UNAIMBA INJILI KWA MTINDO UPI...IWE HIP HOPE,RnB,BAND,SEBENE,MDUMANGE,PRAISE NA WORSHIP,KWAYA AU UNAIMBA BINAFSI BASI HII NI NAFASI YAKO!!

TUKIO HILI MUHIMU LINALETWA KWENU NA "CHAVALA IDEAS PLATFORM" KUPITIA BLOG HII YA KIKRISTO "GOSPEL STANDARD BASE" KWA UDHAMINI MKUBWA WA
King Chavala-MC
Praise Power Radio
Mitambo Solution
Christian Bloggers
Na wengine mmoja mmoja wanaoendelea kuchangia mawazo yao!!!

Kwa maelezo zaidi piga 0713 883 797

ITAMBUE NAFASI YAKO KAMA KIJANA ILI ULETE MABADILIKO KATIKA MAISHA YAKO NA JAMII KWA UJUMLA 02


SHALOM TENA WASOMAJI WANGU!!
BADO TUNAENDELEA KUJIFUNZA KAMA VIJANA....

Kama nilivyosema katika sehemu ya kwanza, ni muhimu sana kwako wewe kama kijana kujua nafasi yako katika maisha yako, ujue pia Nafasi yako katika familia yako, uelewe umuhimu ulionao kwa jamii inayokuzunguka na zaidi sana taifa lako.
Umuhimu wako haupatikani kwa kujitazama kwenye kioo na kudhani wewe ni muhimu, ni jambo linalohitaji kuwekeza katika ufahamu sahihi ama kujitambua sawa na vile Mungu alivyokusudia.

Ufike mahali uishi maisha yenye malengo na utambue thamani yako ili usinunuliwe na vitu vyenye thamani isiyolingana na wewe. Hapa inahitaji kujenga mtazamo utakaokusaidia kuwa thabiti katika maamuzi yako, ili ujenge msimamo wenye nidhamu katika maneno, mawazo na matendo yako.

 Jumla ya haya yote inahitaji kujitambua, na sasa tuendelee na maana ya kujitambua maana ni kujitambua tu ndiko kunaweza kukusaidia kujua Nafasi yako na kusimama katika zamu yako na kuleta mabadiliko uliyopangiwa na Mungu wako.

Maana ya Kujitambua
“Kujitambua ni hali ya kuwa na ufahamu au uelewa (kujua) wa kutosha juu ya maisha yako kwa ujumla pamoja na mazingira yanayokuzunguka na hivyo kukufanya uishi maisha yanayofanana au kulingana na kusudi la Mungu kwako, uishi katika ubora wa maisha yanayolingana na kiwango cha ufahamu ulionao au kiwango cha kujitambua kwako kutegemeana na nguvu ya taarifa unazopata” 
 Kijana aliyejitambua, ukimsikiliza maneno yako hutatia shaka kwamba yuko thabiti na hata ukiangalia matendo yake utaona ulinganifu wa ayasemayo na ayatenda. Kijana yoyote hawezi kujitambua mpaka amekutana na ufahamu sahihi ulio juu ya yote anayoyafahamu, aone kupungukiwa kwake kwasababu hajafahamu mambo ya msingi katika maisha yake. 

Juu ya yote ni lazima wewe kama Kijana ujue kuwa ipo sababu ya wewe kuwepo hapa duniani, lipo kusudi la wewe kuwepo hapa duniani, ipo sababu ya wewe kuwa Kijana, hii ni muhimu sana. 

Kujitambua ni kuwa na ufahamu au uelewa juu ya angalau mambo yafuatayo: 

 Historia ya asili yako au maisha yako, ni muhimu Kijana ukajua historia ya maisha yako bila kujali ilikuwa nzuri au sio nzuri, au ya kuvutia au siyo ya kuvutia ili ujue kuwa kuna mahali unatoka, kuna aina ya watu wameunganishwa na maisha yako, hii itakusaidia katika safari ya maisha yako 

 Maumbile yako, au mwili wako, ujue madhaifu ya mwili wako, uelewe na kuutambua mwili wako vizuri na kujua namna ya kuudhibiti katika mazingira tofauti tofauti 

 Kusudi la maisha yako, maono au malengo kwa pasipo kujua sababu ya wewe kuwepo duniani unapoteza maana ya kuwepo duniani 

 Makuzi na malezi yako, maana haya yanaathiri kwa kiwango kikubwa sana hali yako ya baadae, ujue melelewaje na umekua katika mazingira gani ili tabia zako na mwenendo wako zipate maana na uwe na uwezo wa kujifunza kwanini umekuwa na tabia Fulani Fulani, 

 Mazingira na jamii, taifa lako na zana nzima ya uzalendo, ujue kuwa uzalendo haufundishwi kwa kuwapa watu mali na pesa, Mungu amekupa wewe fursa ya kuzaliwa na kuishi Tanzania kwa makusudi na kama hujui basi utaishi kama mnyama na utapoteza ladha na kuwajibika 

 Hisia, utashi na ufahamu wako 

 Maneno na maamuzi yako, 

 Tabia na mwenendo UMUHIMU WA KUJITAMBUA Kujitambua ni muhimu sana kwani kunakusaidia kujua mambo juu ya maisha yako: 

 Ili kutembea au kuishi katika viwango asilia ambavyo umeumbwa navyo (The originality of you) 

 Ili kujua madhaifu uliyonayo kwa ajili ya kujua namna ya kuyashinda 

 Ili kujua thamani yako, uepuke kutumiwa vibaya, usijidharau wala kumtengenezea mtu mwingine mazingira ya kukudharau na hata usimdharau mtu mwingine 

 Ili ujua nafasi yako (majukumu) katika maisha yako na ya wale wanaokuzunguka 

 Ili kujua umuhimu ulionao kwa ajili ya kuleta matokeo yanayotarajiwa kwako 

 Itakusaidia kutumia vizuri rasilimali kama muda, watu nk 

NAAMINI LEO UMEPATA KITU CHA KUKUSAIDIA KATIKA SOMO HILI, NI MATUMAINI YANGU KUWA UTAANZA KUFANYA MABADILIKO KATIKO JAMII YAKO SASA!!
Usikose somo lojalo!
Na Mwl. Raphael Lyela kutoka Youth Kingdom Ministries,Jesus Up!
 
......LITAENDELEA!!!!!!!

TAMASHA KUBWA LA KUMSIFU MUNGU PAMOJA NA WATOTO WA MUNGU (HOCET)

 
SHALOM!!
IMETUPASA,NI VEMA NA HAKI KUMSIFU MUNGU WETU KILA SAA NA KILA WAKATI...MAANA AMETUUMBA ILI TUMWABUDU...LAKINI HIYO PEKE YAKE HAITOSHI,MTUME PAULO ANASEMA DINI ILIYO SAFI ISIYO NA TAKA MBELE ZA MUNGU BABA NI HII KUWATAZAMA YATIMA,WAJANE,WASIO NA MSAADA KATIKA DHIKI ZAO NA KUJILINDA NA DUNIA PASIPO MAWAA (YAK 1:26,27)
....BASI SASA SAFARI HII WATU WA MUNGU TUTAKUSANYIKA PAMOJA KWA AJILI YA KUMSIFU MUNGU,KUZINDUA DVD YA WATOTO WA MUNGU PAMOJA NA KUFANYA CHANGIZO LA KUWASIDIA MTAJI WA KUJIENDESHA WATOTO HAWA AMBAO WAFADHILI WAO WALIWAKIMBIA BAADA YA KUONA WANAMWAMINI MUNGU!....BASI UKIONA TANGAZO HILI NJOO UJUMUIKE NASI ILI TUTIMILIZE MAANDIKO YOTE!
WAIMBAJI WENGI SANA WATAKUWEPO KATIKA KUWASINDIKIZA WATOTO HAWA NA MALENGO MAKUBWA NI KUPATA FEDHA ZA KUTOSHA KUNUNUA CANTER,NG'OMBE WA MAZIWA PAMOJA NA MTAJI WA KUKU WA MAYAI NA NYAMA ILI SHULE HII IWEZE KUJIENDESHA PASIPO KUNGOJA MISAADA MAANA WATOTO HAWA WANAWEZA KUZALISHA NA KUJITEGEMEA HUKU WAKISOMA VIZURI NA KUSOMA NA KWA BIDII!!
IWENI MFANO WA KUIGWA!!!

UNAWEZA KUTUMA MCHANGO WAKO KWA M-PESA KWENDA 0754527955

GOSPEL STANDARD BASE BLOG TUWATAKIENI MAFANIKIO MEMA NA MNAKARIBISHWA KUTUSHIRIKISHA TENA WAKATI WOWOTE ULE MKIWA TAYARI!
President.