Wednesday, December 4, 2013

......MAANGALIZO!!!



(HATUA za HUDUMA na VIPAWA vyako)

1. Jua kutofautisha kati ya HUDUMA na BIASHARA. Msukumo wa HUDUMA hauko katika kufanya FAIDA bali kutenda kile mtu anachokifanya kwa “jamii” fulani, na hiki “kitu/shughuli” kimejikita katika Mapenzi ya Mungu. Malengo na Madhumuni ya huduma ni KUTUMIKIA sio KUTUMIKIWA. Kumbuka katika UFALME wa Mungu, hakuna aliyeacha ndugu, wazazi, au shughuli yake NYINGINE na akachagua kufanya HUDUMA katika Ufalme huu asirudishiwe mara 100! Mtihani upo katika kukaa kwa UAMINIFU na kwa SABURI ukimtizama yeye ALIYEKUTUMA na wala sio FAIDA. Ili UINULIWE unahitaji kufaulu mtihani wa UNYENYEKVU na ITAKUPASA kunyeyekea CHINI ya mkono wa Mungu ulio hodari UKISUBIRI akukweze kwa WAKATI WAKE. Huu wakati unakuja, ila ni wa kusubiri. Usidanganywe na MTU yeyote, huu ni wakati wa MAUMIVU na KUPIMWA imani yako kama kweli UKO KAZINI au unatafuta hela! UKIFAULU hapo, hakuna mahali hutakanyaga wala pesa hutapata. Hakuna ALAYE ataweza kumaliza “mavuno yako” japo kwa kweli walaji watakuwepo! Ili uweze kusimama mahali “hapa” (pa kupimwa na kusubiri kuinuliwa), katika njia ya kufikia “MAHALI pa USHINDI” wako utahitajika kufanya MAOMBI ya dhati kabisa huku ukichunga KINYWA chako maana anayekupima UVUMILIVU na IMANI yako mara nyingi sana ni YULE BWANA “unayemtumikia” ili ajue ATAKUPANDISHA cheo hadi wapi. Jinsi utakavyoshinda huu MTIHANI (interview) ndio UTAPANDA mbali zaidi.

Kumbuka mfano wa talanta (5, 2, 1), kiwango cha KUPOKEA hakikua kwa Bwana atoaye bali UWEZO wa mtumishi APOKEAYE. Ukitaka kupokea VINGI jiandae kujifua vizuri katika MAOMBI na SABURI. Huku ukila Neno kwa WINGI maana hivyo ndivyo vitendea kazi shambani mwa Bwana lakini pia ndio CHANZO cha IMANI katika Kristo. Nyenzo na vitendea kazi vya muhimu katika HUDUMA ni IMANI na MAMLAKA! Kumbuka Mamlaka inapatikana katika KUMTII Mungu katika mambo YOTE. Hivi viwili vinafanyaje kazi? IMANI ni kama FEDHA, NGUVU au UFUNGUO. Ili uweze kumiliki MAMBO fulani katika ulimwengu huu, na wa roho unahitaji hiki kitu ambacho kinaitwa IMANI. Kuna wakati utahitaji KUTEKA kambi ya adui ili ujitwalie MATEKA, bila NGUVU (imani na mamlaka) huwezi maana adui ameitwa ni “mwenye nguvu”. Kuna wakati unahitaji FUNGUO za kufunga au kufungua vitu katika ulimwengu huu na wa roho ili HUDUMA isonge mbele bila mamlaka huwezi kufurukuta.

HUDUMA inasema hivi “nimetenda ‘Mapenzi ya Mungu’ kiasi hiki na KUMRUDISHIA Mungu utukufu wake, na Mungu anasema “moja mia, au moja sitini au moja thelathini”, kulingana ni KIWANGO chako cha KUPOKEA kama MTUMISHI MWEMA na MWAMINIFU” Kwenye HUDUMA mara nyingine hakuna ulinganifu wa ULICHOPANDA na UTAKACHOVUNA kwa jinsi ya mwili. Huwezi Kupima mafanikio ya HUDUMA kwa kiwango cha PESA japo ukifanya HUDUMA LAZIMA pesa ije. Kipimo ni KIASI cha kutenda MAPENZI YA MUNGU. Ndipo huyu atapanda MBEGU ile ile katika UDONGO ule ule, huyu atavuna 100, mwingine 60 na mwingine 30!

Msukumo wa BIASHARA ni kupata PESA. Biashara inasema “nimewekeza kiwango ‘hiki’ na FAIDA lazima iwe ‘hivi’ la sivyo ni HASARA”. Sasa kumbuka kuna WATUMISHI wengi sana wanafanya KAZI ya MUNGU kama BIASHARA. Kipimo cha Mafanikio yao ni IDADI ya BIDHAA walizozalisha na kiwango cha PESA iliyoingia. FURAHA yao sio KUFANYA mapenzi ya Mungu ila ni faida wanayopata katika KAZI ya mikono yao. Mara nyingi sana WATUMISHI wa namna hii huchanganya BARAKA za MUNGU na MALI! Yaani mwenye ‘NAZO’ zaidi AMEBARIKIWA zaidi kuliko mwenye VICHACHE! Ndio maana BWANA wangu aliita kuna WACHUNGAJI wa MSHAHARA na wachungaji wa KWELI (Mchungaji mwema). Mtumishi ambaye anafanya biashara, kitu cha kwanza sio “KONDOO” (mapenzi ya Mungu) ila MSHAHARA (pesa). Sasa hiki ni KIPIMO kigumu sana na kimefichwa mbali na huwezi kuona kwa macho ya nje, ILA Mungu aonaye SIRINI hujua ni nani anafanya HUDUMA na ni yupi anafanya BIASHARA. Sasa kumbuka, haya makundi mawili yote yataleta MATUNDA kwa Ufalme wa Mungu, tofauti yao ni kitu kinaitwa THAWABU! Thawabu hulipwa MBINGUNI na MSHAHARA hulipwa DUNIANI. Hili kundi la WAFANYA BIASHARA watapata MSHAHARA (PESA) wao na Yesu akasema “wameshalipwa duniani”. Tabia yao ni kusimama MAHEKALUNI, KUPAZA SAUTI, KUSIMAMA kwenye KONA za NJIA na kuvaa KANZU NDEFU ili watu wawaone na sio MUNGU awaone”. KUJIONYESHA na MASHINDANO ya mwilini ndio JADI yao. Sawa, watashinda na kupata PESA, ila thawabu yao huko Mbinguni ni sifuri maana wamekwisha kupokea kwa WANADAMU sifa na utukufu! Wale wanaofanya HUDUMA mara ZOTE ni wanyenyekevu wa moyo, wanatanguliza Mapenzi ya Mungu na wanaogopa KUJISIFU na kugusa UTUKUFU wa Mungu. Maombi na kufunga ni sehemu ya MAZOEZI yao RASMI ya huduma, tena CONSTANTLY na sio wakati wa MATAMASHA tu. Kumbuka HUDUMA ni MAISHA sio EVENT! Hili kundi la wafanya HUDUMA mara nyingine hudhulumiwa na kulipwa kidogo (nusu pesa kama yule mama aliyeweka sarafu kwenye sanduku la hazina na Yesu akasema, “hiyo ni zaidi kuliko zile matajiri walizotoa”) lakini FAIDA yao ni KUBWA kama wametenda mapenzi ya Mungu na kurudisha UTUKUFU wake bila kuugusa hata tone. Hili kundi ni la muhimu sana kwa maana linazaa double double. MATUNDA hapa duniani na Uzima wa milele. Ila kundi la WAFANYA BIASHARA linazaa matunda hapa duniani na kukosa UZIMA wa milele! Kwa maana hata kwa MZAHA Yesu atahubiriwa na miujiza itafanyika ila wale watendao hayo watapotea milele! Chagua kukaa katika MSTARI wa Mungu usifanye kazi ya HASARA Mtumishi wa Mungu. Kila mtu na ajipime kazi yake mwenyewe na AJITAMBUE na kujipanga sawasawa asije akasema HAKUJUA! Maana usishangae Yesu anakutembelea na KIKOTO halafu usiamini, maana wale watu waliofanya biashara hekaluni wakati “ule” hawakumjua Yesu kama “mchapaji” pia! Chunga sana, Yesu ni yeye yule JANA, LEO na hata MILELE.
Matendo ya Mitume 20: 33 “Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. 34 Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. 35 Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea. 36 Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote. 37 Wakalia sana wote, wakamwangukia Paulo shingoni, wakambusu-busu, 38 wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamwona uso tena. Wakamsindikiza hata merikebuni.”

Kuna vipawa vingine vitatumika sio kama HUDUMA bali BIASHARA. Sasa, kama Mungu amekupa kufanya biashara au kazi ya kukuingizia KIPATO kwa namna yoyote USIMSAHAU Mungu katika biashara hiyo. Tafuta makusudi yake na hakikisha BISAHARA yako INAMTUKUZA Mungu na inaheshimu na KUTII makusudi ya Mungu. Kama Mtumishi wa Mungu katika BIASHARA yako, jifunze kutafuta kusudi la Mungu na kukaa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu daima. Chunga sana unavyowahudumia watu na kuweka viwango vya BEI na tozo mbalimbali. “Mungu hapendi mizani za uongo”. Pima kazi na malipo kwa ulinganifu na “usichukue zaidi ya ikupasavyo”. Na jua kwamba sio kila mara utafanya kazi/biashara kwa MASLAHI ya kibinadamu (kazi au bidhaa kuuzika kwa bei ya faida kwa namna ya kibiashara). Ukijikuta unasukumwa kufanya kitu CHOCHOTE kwa pesa tu, jua unakaribia mahali pa gumu. Ukisikia mtu anasema “hii kazi haina maslahi” na haangalii kama Mungu anataka nini ila pesa tu, ni hatari. Sio kila wakati utafanya kazi kwa malipo ya pesa, Mungu anaweza kubadili mfumo wa malipo kwa baadhi ya kazi. Usipokua makini unaweza kujikuta unajifungia milango ya muhimu wakati unakimbiza pesa na ukajikuta hufiki mbali. Pamoja na kufanya faida, REHEMA iwe ndio mhimili wa maamuzi yako ya ki-PESA au kuhudumia wateja wako.

2. Mfumo wa duniani utakulazimu kufanya mambo mabalimbali wakati wa kufanya HUDUMA na mengine ni magumu. KUMBUKA wewe ni MTUMISHI (mtumwa), kuna Bwana aliyekutuma. Ukibinafsisha HUDUMA ikawa yako itakua NZITO mabegani mwako. Kwa maana kila HUDUMA ina VITA, na Maandiko yanasema HAKUNA askari aendaye VITANI kwa GHARAMA zake! Ukifika mahali pa kujisahau ukaanza kusema “huduma yangu” huku ukisahau kua wewe ni MTUMWA na sio BWANA (boss) au MMILIKI wa hiyo HUDUMA unakaribia kufikia MAHALI pa gumu. Hata siku moja USISAHAU kwamba kuna “organization structure” ya Mungu ambayo yeye ni TOP BOSS na sisi ni vibarua tu. Sasa hapo juu yako kunaweza kua na VIONGOZI wako wa KIROHO, chunga usiwavunjie HESHIMA na ukakosa kuwasikiliza kwa KISINGIZIO cha HUDUMA na UPAKO juu yako. Imempasa KILA mmoja kuitii mamlaka iliyo kuu katika KAZI ya HUDUMA na ni vyema sana ukaitambua mamlaka “inayokuhusu” na kukaa VIZURI nayo maana inaweza ikawa SABABU ya wewe KUKUA au KUANGUKA kihuduma. Katika MFUMO huu wa Utawala, jua kuna wakati utakua na watu chini yako. ANGALIA basi kwa sababu na sisi tu wa BWANA wetu ambaye tunamtumaini KUTUBARIKI nasi tusizuie mkono wetu kuwabariki walio chini yetu na kuwatanguliza kama BWANA wetu alivyotupa mfano wa kunawisha miguu wafuasi wake. Ukitaka kua BOSS/MKUU sharti ujifunze “kuvua nguo (utukufu) na kujifunga taulo kiunoni KISHA “kuinama” (kunyenyekea) na kuwanawisha (kuwatumikia) MIGUU michafu walioko chini yako kwa USTAHIMILIVU”.

3. Katika mfumo wa kufanya kazi ya Mungu utahitaji VIBALI na michakato mingi ya KISHERIA na imekupasa kumpa KAISARI kilicho chake kwa UAMINIFU wote. Huwezi kuepuka wezi, nondo na wadudu mbalimbali (ma-promota, producer, nk.) walao maadam uko duniani. Ila jua Bwana ni fungu lako na HUTAPATA hasara kwa maana yeye anaona SIRINI na anajua shida yako na ATAKUJAZI. Kumbuka kuweka HAZINA yako Mbinguni pia maana huko hakuna kutu, nondo wala wezi. Na unahitaji ULINZI wa Mungu ili HUDUMA yako “isipukutishe majani/maua” kabla ya KUZAA, na yeye anaweza pia KUMKEMEA yeye ALAYE (Ibilisi na watu wake), ulinzi huu unaupata katika ZAKA KAMILI! Jifunze KUTOA kwa USAHIHI maana kuna faida NYINGI.
Warumi 13: “1 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 2 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 3 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. 4 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. 5 Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. 6 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. 7 Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.”

4. Huwezi kufanya HUDUMA na kutumia VIPAWA vyako bila kuwa na watu wengine katika timu. Huduma inavyozidi kukua utahitaji watu wengi zaidi. Kumbaka jambo hili siku zote, wana wa Mungu wanapojihudhurisha mbele za Mungu wao, shetani naye huja kati yao. Ni vigumu sana kutambua magugu yawapo pamoja na ngano na sio kazi yetu “kuyang’oa” maana hakuna aliyepewa huo wito na BWANA wetu ila inabidi kujichunga na kujilinda na “chachu” yao maana inaweza kuchachusha HUDUMA yako bila kujua. Yesu alikua na wanafunzi 12 na mmoja wao aliitwa “msaliti”! Kama Yesu alikuwa na timu na ndani yake kuna YUDA, jua imekupasa kuwa makini na macho ya mwili na roho kujua watu wa timu yako maana humo watakuwepo wasaliti na wengine ni hatari kuliko YUDA. Kazi ya Yuda ilikua “mweka hazina” ila alikua akiiba vitu/matoleo! Sasa chunga sana mienendo na tabia za watu wa timu yako maana jua kuna roho nyuma yao na mwisho wake huwa ni KUSALITI ili huduma ife bila kujali madhara. Kipimo kikubwa cha uaminifu wa wengi katika timu ni TAMAA ya pesa! Hii ndio ilimfanya YUDA akasaliti huduma yao na Bwana wake kwa sababu ya KIPATO cha vipade 30 tu vya fedha! Sasa jua neno hili kwamba kama YUDA ambavyo hakuila ile pesa, ndivyo wengi sana wanaomsaliti Bwana aliyewatuma huishia pasipotarajiwa kama ilivyokua kwa YUDA au zaidi. Ndani ya vikundi vingi sana wamejipenyeza akina Delilah na wamenyongelea chini HUDUMA nyingi na imebaki mazoea tu na nguvu ya ugali. Imekupasa kukaa katika Maombi ya DHATI kabisa kama timu nzima na kuwa na ratiba za KULA na kujifunza na KUSIKILIZA maagizo ya Bwana aliyewatuma kazini ili msiingie majaribuni.

5. Chanzo cha nguvu zetu ni Mungu aliyetutuma kwenye kazi yake. Huwezi kumchanganya Beliari na Mungu na ukapata matokeo mazuri. Ni jambo la kustaajabisha sana kuteremkia Misri kutafuta msaada ili usimamishe HUDUMA! Yaani unamsaidia Mungu “kutafuta msaada au mtaji kutoka kwa mungu mwingine”! Kumbuka, kukua kwa huduma ni hatua, ambazo huongozwa na Mungu. Na kukua huku kunaenda sambamba na kukua kwa IMANI yako. Kama unataka kukua kwa kasi basi kimbiza kukua kwa IMANI yako. Kwa maana “tunafanikwa katika mambo YOTE kwa kadri roho zetu zifanikiwavyo”. Kwa MAJIRA na vipindi alivyoamuru Mungu, ataleta mtaji na mahitaji ya kukuza huduma yako. Ukifika mahali “unakopa” na kujitaabisha sana ili “uwekeze” kwenye huduma kwa malengo ya KUKUA KWA HARAKA, jua unakaribia mahali sio pazuri. Kama wewe ni “mtumwa” na Bwana wako anataka ulime hatua 10 kwa siku, kwanini ushindane naye na kutaka kulima hatua 100? Je! Hizo hatua 90 za zaidi ulifanya kwa msukumo wa kumzalishia Bwana wako au “kujiongezea kipato”. Jiulize kinachokusukuma ni BIASHARA au HUDUMA? Sasa usiwe MLEGEVU katika kazi ya BWANA maana Mungu amekataa UVIVU na ULEGEVU ila tuwe na BIDII katika KUTAFUTA na KUTENDA mapenzi ya Mungu peke yake.

6. Ukiona UNAMTUMIKIA Mungu, na umefika mahali ukitaka PESA kwa ajili ya jambo fulani, na unajikuta UNACHANGISHA watu, au kuomba watu PESA “kabla” ya kumwomba “kwanza” Mungu hiyo PESA, jua unakaribia mahali pa GUMU. Epuka kua OMBAOMBA na jifunze kumtegemea Mungu kama kweli UNAMTUMIKIA Yeye. Yesu alipotaka “pesa” alituma mtu akavue samaki na kisha ampasue atoe huko sarafu! Unadhani wakati wa Yesu akina ZAKAYO hawakuwepo? Unadhani alishindwa kuwambia tu kwa URAHISI walete SADAKA/MBEGU na wakamjazia kila mahali MIJI-HELA? Angalia basi Mtumishi wa Mungu usije ukahamisha TEGEMEO lako kwa wanadamu bila kujua. Ni kweli Mungu atainua hata “mawe” yafanye kazi yake, ila chunga usije ukaanza na kutafuta misaada kwa “mawe” kama hayo ndio yamekuita katika kazi ya HUDUMA. Muombe Mungu kwa bidii, tafuta USO wake kwa bidii zote, kama atatuma MALAIKA kukuletea “mkate na gudulia la maji” au kama atatumia KUNGURU kukuletea “mkate” kama kwa Elia Mtishibi, sio juu yako kuchagua. Mtumaini yeye na kaa katika KUSUDI lake. Mojawapo ya sifa za watu wanaomtegemea Mungu katika VIPATO vyoa ni KUOGOPA sadaka na KUIHESHIMU! Yamkini hujawahi kukutana na mtumishi wa Mungu anakataa SADAKA lakini wapo wengi tu, Kumbuka habari za Elisha baada ya kumponya mtu ukoma! Ingekua leo tungeita “sadaka ya shukurani” na tungeshangilia kupokea! Sasa sisemi sadaka za shukurani ni mbaya, ila nataka uone hii KIU ghafla ya kutaka KUPOKEA kirahisi kutoka kwa WANADAMU na KUDAI kwa nguvu au kijanjajnja saa nyingine kwa kutishia watu kwa maandiko. Hatukuitwa KUKUSANYA pesa na sadaka ila kuleta ROHO za watu kwa Mungu. Pesa ikija ni sawa, ni CHAKULA CHA SAFARI tu kutuwezesha kufikilia MAKUSUDI ya Mungu na wala Pesa yenyewe sio MAKUSUDI ya MSINGI ya HUDUMA zetu labda kama tunafanya BIASHARA.

7. Majaribu lazima yaje ili kupunguza kasi ya huduma yako japo ukiyashinda UNAPANDA cheo. Kwa Ayubu shetani alisema “nikigusa kitu cha karibu naye” huyu jamaa lazima ashindwe. Ibilisi akashughulikia watoto na mali zote! Usidhani ilikua mahali pa rahisi hapo kusimama tu katika UAMINIFU na Mungu. Wakati watoto wanaangamia na mali zinaporomoka wanakuja MARAFIKI “wataabishaji” wakileta injili pori na maneno “kandamizi”. Lakini Ayubu akakaza macho kumtizama Bwana wake na akafika MAHALI pa USHINDI wake, japo ilikua ni raundi ya kwanza. Raundi ya pili Ibilisi anataka kumgusa Ayubu “karibu zaidi” ili kumchanganya na kumpotezea mwelekeo. Ibilisi anasema “mwili bwana, mwili, mtu akiguswa mwilini ataachia tu ngazi”, Mungu akatoa “go ahead”. Wakati Ayubu anapambana na MAJIPU mwili mzima, anajikuna kwa kigae maana yamkini akijikuna usaha ulikua unamwagika na kigae ndio cha kukingia, huku ananuka na kwa kawaida watu wanakaa mbali, hatamaniki, MKE wake anakuja na mpya! Akidhani anamwonea huruma, akitazama haoni tena mtu ila “maiti” na anamshauri “amkufuru Mungu” kuharakisha kufa maana anaona jamaa kilichobaki ni kifo tu na anateseka bure! Ayubu alijua bado mara hii tena atafika “MAHALI pa USHINDI” wake! Kumbuka alishinda mara dufu, na alirudishiwa kila kilichopotea maradufu!

Watumishi wengi sana wameshindwa kusimama kwasababu Ibilisi amegusa vitu vya “karibu” nao. Wengine wakati wako Busy na Mungu, huku nyuma mke/mume anakamatana na makahaba! Na ibilisi ataweka “mtu wa kuleta habari” kama ilivyokua kwa AYUBU! Ili uumie na uvunjike moyo na upunguze KASI ya huduma yako. Mara nyingine “karibu” inaweza kua watoto, wazazi, ndugu, mali au ajira alimradi ni mahali PATAKAPOKUGHARIMU na PANAUMA. Lengo ni kukukatisha tamaa mtu wa Mungu ili ukose mwelekeo na ushindwe kutimiza HUDUMA au kuzaa MATUNDA sawa na wito au KIPAWA chako. Chunga sana hili eneo maana ni gumu na limefisha HUDUMA nyingi sana za watumishi wa Mungu na wameshindwa kuzaa MATUNDA yawapasayo. Sikiliza MTUMISHI wa Mungu, KILA kitu kitapita, usiangalie kushoto wala kulia, kama ni mume au mke amekusaliti kwa kumsikiliza Ibilisi na kwa “kutokujua saa ya kujaribiwa kwake”, wewe USIKATE tamaa, SONGA mbele! Mwangalie Mungu aliyekuita na uzidi katika nguvu zake na mapenzi yake maana hapo ndipo MAHALI pa USHINDI wako.

Kwa sababu kila mtu katika Mwili wa Kristo ameitwa kwa kazi maalumu kama ilivyo viungo vya miili yetu, basi jua kama UNASHIKA njia za SHETANI sio tu kwamba UNAHARIBU huduma yako, ila pia UNAANGAMIZA huduma ya watu wa “karibu” wanaokuhusu kwa sababu kwa KUTENDA hayo MAOVU unawaumiza na kupunguza KASI ya utumishi wao. Kumbuka kuukomboa wakati maana hizi ni nyakati za uovo. Msikae tu kugombana na kubishania mambo yasiyo ya msingi na kusahau kua mna KAZI shambani mwa Bwana. Mtakapo shughulika na MAMBO ya Mungu jua HAKIKA Mungu atashughulika na mambo yenu pia na BARAKA na FURAHA vitaongezeka kwenu na kwa watu wenu wa KARIBU.

Matendo ya Mitume 20: 19 “nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na kwa machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi; 20 ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba, 21 nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo. 22 Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko;
23 isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. 24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu. 25 Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena. 26 Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina hatia kwa damu ya mtu awaye yote. 27 Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu. 28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.”

8. USHUHUDA. Kama kuna kitu kimekwamisha kazi ya Mungu ni USHUHUDA mmbaya wa watumi wa Mungu. Kumbuka, unapotenda “KITUKO” chochote hadharani au kwa SIRI ila Ibilisi amefanikiwa kukichomoza hadharani, watu wataanza kukutizama kama wewe ni mtu wa “namna ile” sawa na KITUKO ulichofanya, hata kama ilikua mara moja. Ile LEBO unayobandikwa ya hiki KITUKO ina tabia ya KUDUMU na ni NGUMU sana kuifuta kwa jinsi ya kibinadamu. Sababu ya msingi hapa ni kwamba Mungu ANASAMEHE na hakumbuki kama UKITUBU, ila wanadamu HAWASAHU hata kama umetubu. Kama ulifanya UZINZI bado watu watakutizama tu kama MZINZI kwa muda mrefu. Ibilisi naye atahakikisha habari MABAYA inaenea kwa KASI kwa sababu yeye ni “mshitaki”. Watu wengi sana wamesahau kwamba USHUHUDA ni silaha ya MUHIMU kumshinda Ibilisi, ndio maana tunasoma “nao wakamshinda kwa Damu ya Mwana-kondoo na kwa neno la ushuhuda wao..” Kama kuna kitu Ibilisi anawinda ni kupata USHUHUDA wako mmbaya na KUUSAMBAZA kila mahali. Unaposimama KUHUDUMU anawakumbusha watu na kuwaambia “msimsikilize huyu jamaa kwanza ni tapeli/mzinzi/mrushi/mwizi” nk. Mara nyingi sana watu wameshindwa kupokea Neema ya Mungu iokoayo na hata kusema kwa ujasiri “hakuna wokovu duniani” kwa sababu wanajua WALICHOONA kwa wana wa Mungu. Makosa ya ZAMANI yana NGUVU ya kuzuia MAFANIKIO yako ya sasa na ya baadae KIHUDUMA kama hujawa makini na kutafuta Neema ya kupona na MAMBO ya KALE.

Kwa upande mwingine, sio kila jambo jema laweza kuwa na USHUHUDA mzuri. Kwa lugha nyingine, sio tu kwamba USHUHUDA mmbaya ni kuanguka dhambini. Kuna mambo mengi sana katika mienendo na tabia ambayo Paulo alisema katika kitabu cha Warumi kua makini nayo. Kuna mambo IMEKUPASA kuacha kufanya kwa sababu ya UDHAIFU wa imani ya mtu mwingine sio imani yako. Mfano rahisi ni namna ya UVAAJI wa nguo. Watu wengi wameonekana kama WAHUNI tu kwa sababu ya aina ya nguo walizovaa na MUONEKANO wao katika mavazi hayo. Na wengine wamekua wabishi na kiburi hata wakiambiwa au wakionywa! Mungu atusaidie tusiwe KWAZO kwa namna yoyote. KUMBUKA kumpokea dhaifu wa imani na kumsaidia sio kumwangamiza kwa UDHAIFU wa imani yake eti kwa sababu sisi ni MIAMBA ya Imani. Hicho ni KIBURI.

NEEMA ya BWANA na IZIDI KWENU TANGU SASA na HATA MILELE. AMEN.

Frank Philip

No comments:

Post a Comment