Tuesday, October 29, 2013

ANZA NOVEMBA KWA KUMSIFU MUNGU!!!

NI MUHIMU SANA KUIWEKA HII KATIKA RATIBA ZAKO!!
ANZA MWEZI NOVEMBA KWA SIFA NA KUABUDU MBELE ZA BWANA UKIWA NA TIMU NZIMA YA NEXT LEVEL PALE CITY CHRISTIAN CENTRE-UPANGA-MKABALA NA CHUO KIKUU CHA MZUMBE!!
MUNGU AKUBARIKI!!

KILA MTU NI LAZIMA ASOME KITABU HIKI...."KUSUDI LA MAJIRA YAKO!!"

USIJARIBU HATA KIDOGO KUKOSA KUSOMA KITABU HIKI CHA AJABU NA CHENYE MENGI YANAYOKUHUSU WEWE,MAANA NI MUHIMU SANA KILA MTU KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKE!!
HAKUNA JAMBO HATARI ZAIDI DUNIANI ZAIDI YA KUISHI BILA KUJUA KUSUDI LAKO NA MBAYA ZAIDI NI WALE WAJUAO MAKUSUDI YA MAISHA YAO LAKINI HAWAJUI MAJIRA NA NYAKATI YA KUTIMILIZA YALE YAWAAPASAYO KUFANYA!!

FRED D. MSUNGU, CHURCH BOY AMEKUBALI KUTUMIWA NA BWANA NA KUAMUA KUANDIKA KITABU HIKI KIZURI SANA,NI MUHIMU UJIPATIE NAKALA YAKO NA UISOME NA KUIELEWA NA MUNGU AKUBARIKI UNAPOCHUKUA HATUA HIYO!!

KWA MAELEZO ZAIDI,WASILIANA NA MWANDISHI KWA 0653318117

Imedhaminiwa na GoStaBa
+255 713 883 797

MTU MWENYE HASIRA NA NG’OMBE WAKE!!!!
Mzee Majaliwa ni mfugaji mzuri wa ng’ombe. Anategemea ngo’mbe wake kwa kujipatia kipato, kusomesha wanawe, na kujikimu kimaisha. Bila hao ng’ombe, mzee Majaliwa hana tumaini kwa sababu amejitoa na kujikita katika ufugaji.

Mzee majaliwa ni mtu mpenda watu na anayejitoa kwa shughuli mbali mbali za kijamii. Udhaifu wake mkubwa ni HASIRA. Kila akasirishwapo na watu, yeye huenda moja kwa moja zizini na kuanza KUWAPIGA NG’OMBE WAKE KWA FIMBO HADI HASIRA IMSHUKE. Baada ya hasira kumalizika hurudi tena zizini kwa masikitiko makubwa na machozi akifikiri jinsi alivyo wapiga ngo’ombe wakati KASA SIO LAO. Akizingatia kwamba hao ng’ombe wamekua waaminifu siku zote kumpatia maziwa, mbolea, na vyanzo vingine vya mapato ikiwa ni pamoja na kua tayari KUCHINJWA BILA KULALAMIKA, ili mzee Majaliwa ajipatie fadha na faida.

Ni rahisi sana kumshangaa huyu mzee anavyopiga ng’ombe ambao hawajamkosea kitu, ila watu wengi sana wamemfanya MUNGU KAMA NG’OMBE wa Mzee majaliwa. Wanapokwazwa, kuumizwa na kuzongwa, wanampiga Mungu fimbo kwa kumtenda dhambi! Ukiwauliza eti wanasema “mume wangu ananizingua sana”, “isingekua mke wangu nisingekua hivi”, “kama maisha ni magumu na watu hawanisaidii nifanyeje?”, “nimewaomba wanisaidie wamekataa”, “kila mtu anafanya kwanini na mimi nisifanye?”, nk.

Yeremia 17:5 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. 6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. 7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni Tumaini Lake. 8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda. 9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?”

Kama unamtegemea Mungu, kwanini usimtegemee akuokoe na mashaka, mateso na maumivu yako pia? Kwanini kumtenda dhambi kwa kisingizio cha WATU kukuumiza na kutokukutenda kwa haki? Je! Utamchapa Mungu wako viboko kwa kukosewa na watu wengine hadi lini?

Frank Philip

Saturday, October 26, 2013

HATIMAYE MBUYU MKONGWE (SAMUEL SASALI) UMEANGUSHWA NA DK MILEMBE MADAHA LEO 26/10/2013!!!

CERTIFIED MR SAMUEL AND MRS MILEMBE SASALI
SASA HAWA NI MUME NA MKE RASMI NA HIVYO NDIO VYETI VYAO VYA NDOA!!
NA HIYO HATUA HAPO JUU ILIFIKA BAADA TU YA KIAPO CHA KILA MMOJA KWA MWENZAKE PAMOJA NA PETE YA AHADI YA NDOA NA KUTUNZA KIAPO HICHO
 VAA PETE HII,IWE ISHARA YA AGANO LANGU KWAKO.....
 VAA PETE HII.....
GROOM'S MEN PAMOJA NA SAMUEL SASALI

MAIDS KUMPAMBA MILEMBE
KULIKUWEPO GROOM'S MEN NA MAIDS 30 KUIPAMBA HARUSI HII YA PAPAA SEBENE!
WALIINGIA KWA FURAHA SANA NA KILA MMOJA ALIFURAHIA UCHANGAMFU WAO

MR SAMUEL AKIONGEA NA KUMSIFIA MKEWE
MRS MILEMBE MADAHA WA SAMUEL AKIONGEA
TUKAPATA KUSIKIA SAUTI ZAO,WAKASEMA NA HATIMAYE WAKAPUMZIKA KIDOGO KABLA YA KUANZA ZOEZI LA KEKI!
MR & MRS SAMUEL AND MILEMBE SASALI
HATIMAYE WALIKATA KEKI NA KULA NA

KIPEKEE WALITOA ZAWADI YA KEKI KWA WATU WAO KADHAA MUHIMU SANA, AMBAO WAMEKUWA MSAADA KWA KILA MMOJA WAO NA KWA MAHUSIANO YAO.....BAADHI YA WALIOPEWA ZAWADI YA KEKI NI PAMOJA NA WAZAZI WA PANDE ZOTE MBILI,
 MILEMBE ALIPELEKA UKWENI...
NA HUKU PIA VIVYO HIVYO!

KAMATI YA MAANDALIZI,MARAFIKI HURU,AFLEWO TEAM,DK PARVINA,PROSPER MWAKITALIMA,APOSTLE ONESMO NDEGI, LINDA TEMBA NA DK.HURUMA NKONE, MCHUNGAJI ALIYEFUNGISHA NDOA HIYO!!
KEKI KWA MCHUNGAJI NA MKE WAKE

KEKI KWA PROSPER MWAKITALIMA

KEKI KWA DK PARVINA
HATIMAYE WATU WALIKUJA KUMPONGEZA KWA KUCHEZA NA KUMRUSHA JUU SANA...
NA BAADA YA HAPO MENGI YALIENDELEA,KAMA VILE KUONA SHORT DOCUMENTARY NA HATIMAYE CHAKULA,NA HAPO WALITUMBUIZA THE VOICE,SAMWEL YONAH, AMANI KAPAMA, BOMBY JOHNSON PAMOJA NA KING CHAVALA-MC NA KIBAO MAALUM KABISA KWA MAHARUSI "SAMILEMBE"
KING CHAVALA-MC
WATU WALIKUWA WAKITOA ZAWADI MLANGONI,LAKINI KUNA BAADHI YA WATU AU MAKUNDI MAALUM YALILAZIMIKA KUPELEKA MBELE ZAWADI ZAO.
KAMATI YA MAANDALIZI ILIENDA MBELE KWA KUCHEZA KAMA HIVI
CHRISTIAN BLOGGERS NAO HAWAKUBAKI NYUMA KATIKA KUMPONGEZA MWENZAO!
"SAMILEMBE"

HATIMAYE BAADA YA YOTE WALIPIGA PICHA NA KUONDOKA KUELEKEA HUKO AMBAKO HAKUNA AJUAYE NA WAO HUJUA TU WAKISHARUDI!!

SHUKRANI NYINGI SANA KWA KAMATI YA MAANDALIZI  NA KILA ALIYEHUSIKA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE KUFANIKISHA JAMBO HILI,AHSANTE SANA MWENYEKITI NOEL TENGA KWA KUKUBALI KUTUMIKA KUBEBA JUKUMU HILI!

KWA NIABA YA TIMU NZIMA CHA YA CHAVALA MEDIA, TUNAWATAKIA KILA LAKHERI NA MAISHA MAREFU SANA YENYE FURAHA NA AMANI NA UPENDO WA KWELI WATU HAWA MUHIMU SANA KWETU,AMEN!!

IMEANDIKWA NA 
King Chavala MC
+255 713 883 797