Monday, November 19, 2012

"RAISE THE STANDARDS" ndio ulikuwa ujumbe wa MBEYA CITY CAMPUS NIGHT 2012!!!!

Katika Weekend hii Big Events za wanafunzi zenye jina La Campus Night zimechukua mkondo wake katika mikoa ya Dodoma na Mbeya.

Blogger akiripoti kutoka Mbeya ameeleza kuwa Campus Night ya Mbeya imevunja Records ya Makusanyiko ya vijana na wanafunzi katika jiji hilo, event hiyo iliyokusanya wanafunzi zaidi ya 7000 ilikuwa na theme ya Raising The Standards.
Mwimbaji wa Injili anayevuma na ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu mkoani humo Ambwene Mwansongwe ndiye aliyeteka ukumbi kila aliposimama.
Wachekeshaji wanaovuma katika tasnia ya Gospel, King Chavalla na Mc Pilipili walinogesha Campus night yaJiji la Mbeya.
 
Wanenaji Wakuu Katika Usiku huo Dr. Huruma Nkone, Dr. Kimambo, Ms Rose Mushi na Mr. Msigwa wali Raise Standards za Wanafunzi.

Dr. Huruma Nkone aliyekuwa akifundusha Spiritual Transformation usiku huo alilipuka kinjilisti na kuwaambia wanafunzi 'Usharubalo na Utoz Toz,hautainua kiwango chako cha Kiroho, isipikuwa kwa kumpokea Yesu' akinukuu andiko la kutoka kwenye kitabu cha Yohana ikisema 'Mimi ndimi njia kweli na uzima, mtu haendi kwa Baba Isipokuwa kwa njia ya Mimi"
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Dr. Kimambo alifundisha Academic and Career Challenges zinazowakabili wanafunzi.Dr. Kimambo ambaye ni Mwajiriwa wa Serikali yaUingereza nchini Tanzania alieleza 'changamoto za mfumo wa elimu na mahitaji ya soko la ajira ni tatizo linalo wakabili wanafunzi. Tatizo la Soft Skills mbali na ule ujuzi unaopatikana vyuoni ni changamoto pia.Mbali na changamoto hizo maendeleo na matumizi ya technolojia katika mfumo globalization ni changamoto inayowakabili wahitimu wa Elimu Ya Juu.
Mwanadada aliyekuwa msemaji pekee katika Campus night na mdogo wa umri kuliko wasemaji wote Dada Rose Mushi alifundisha RaisingThe Standard Of Ladies In the Campus. Rose Mushi ambaye ni Mchumi kwa taaluma na mwajiriwa wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Aliamsha hamasa kubwa ya vijana alipoanza kufundisha kutoka kwenye Kitabu Cha Mwanzo kwenye story ya Yusufu na Mke wa Potifa. Akifundisha Usiku huo Rose Mushi alisema ili kuinua Viwango vya Kiroho Vya Akina dada katika Campus inapaswa kwanza Ujue thamani yako kama Mdada, pili inakupasa kuachana na mambo yote ambayo yanakusababishia kukushikilia kwa mwanaume kama mi kufaulu, kama ni ada, kama ni laptop kama ambavyo Yusufu alimwachia vazi Mke wa Potifa.
Somo la Mahusiano lilifundishwa na Mr. Msigwa Meneja wa tawi la CRDB katika wilaya ya Mbozi. Alieleza uhusiano wowote wa mwanaume na mwanamke hauwezi kuwa mzuri kama wahusika wana uhusiano mbaya na Mungu wao.
Praise and Worship Leaders. Mr and Mrs Matthew Sasali

Event hiyo ilisimamiwa na Dr. Nyanda pamoja na Ze Blogger. Praise Team ilisimamiwa na Pastor Matthew Sasali na Rebecca Sasali
Dr. Nyanda, Rose Mushi na Papaa Ze Blogger hapo ilikuwa saa 1 Asubuhi baada ya event.

Matukio Katika Picha.
 Sehemu Ya Umati Wa watu
 Mrs. Rebecca Sasali akiongoza Praise Team
 Wanafunzi Waliotoka Mbele Kumpa Yesu Maisha Yao Zaidi ya wanafuzi 90 walimpa Yesu Maisha yao.
 Ndani Ya Uwepo
 Watu Wakienda Sawa ndani ya Ukumbi
 Full Shangwe Wanafunzi Wa Mbeya
 Chezea Nyomi
 Respected Event Manager Papaa Ze Blogger ndani ya Ukumbi
 Ukumbi Mzima Kidole namba tatuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 Watu Wakimpa Yesu Maisha Yao.
 Rose Moshi Kikazi zaidi
 Chezea Urefu
 Wakienda sawa
 Huu Mwili Khaaaa
 Pilipili Kikazi Zaidi ndani ya Mbeya
 Kikazi Zaidi hapa
 Safari Hii akaja na Style ya Sketi aiseeee ilikuwa nouma inaitwa "Usiombe Kusutwa'
 Dr. Maboko akizungumza kwenye Campus Night
 King Chavallaaaaaaaa akienda sawa ndani ya Campus Night
Jamaa kumbe akivua Kofia ni handsome sanaaaaaaaa

HABARI INAKUJIA KWA HISANI KUBWA YA PAPAA ZE BLOGGER!!!!

No comments:

Post a Comment