Thursday, May 16, 2013

JUKWAA LA KIOO......WAJUE 1st Q CHRISTIAN DANCERS,VIJANA WANAOKUJA KWA KASI NCHINI KATIKA TASNIA YA DANCE!!

Episode One......JUKWAA LA KIOO!!!

SHALOM!
KWA MARA YA KWANZA KATIKA CHUMBA HIKI KIPYA CHA "JUKWAA LA KIOO" CHINI YA UKURASA WA WA "Gospel Music" na "Talents"NA LEO KWA MARA YA KWANZA TUNAANZA NA 1ST Q DANCERS WENYE MAKAO YAO JIJINI DAR ES SALAAM,HILI NI KUNDI LENYE VIJANA MAHIRI NA NIMEBAHATIKA KUWAONA MARA KADHAA KATIKA MATUKIO KADHAA NA LEO NIMEPATA BAHATI YA KUFANYA MAHOJIANO NA MBEBA MAONO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA KUNDI HILI DADA GRACE LIFARD MLAWA,NA MAZUNGUMZO YETU YALIKUWA KAMA IFUATAVYO;

GoStaBa:Habari yako dada!

MGN:Ni nzuri sana sijui za kwako?
Mimi ni mzima sana na leo naona nikuhoji kidogo kuhusu kundi lako la 1st Q,naamini hutojali!
karinu sana wala usijali,na mimi ninafurahi kupata nafasi hii ya kuongea na Gospel Standard Base.

GoStaBa: Okey,watu wangependa kujua Kundi lenu linaitwaje?

MGN:1st Q (1st Quadrant)


GoStaBa: Nini maana ya jina hilo na kwa nini mnajiita hivyo?

MGN:1st Quadrant inatoka katika “XY plane”, ambapo AXES zote katika 1st quadrant ni chanya (Positive), ndio maana tukajiita hivyo, kama Biblia ilivyoandika katika Warumi 8:28…..Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote,Mungu hufanya kazi na wale wote wampendao katika kuwapatia mema!.......kwa hiyo nasisi tunaamini kwetu yote ni mema kwasababu tunafanya nae kazi.

GoStaBa: Kundi lenu lilianza lini na lilianzishwa na nani?

MGN:Tulianza mwezi  april mwaka 2012 kwa halisia,lakini wazo lilikuwepo tangu mwaka 2010,Kundi hili ni wazo langu(Grace) ila tulianza na watu watano nao ni Mimi,Belinda,Mgeni ,Tenes na Lisa.Lakini mpaka sasa tunao dancers 12,wakiwemo wasichana 9 na wavulana 3.


GoStaBa:Hili ni wazo jipya kwa kanisa,hususani kundi linalowahusisha wasichana wengi zaidi,Je nini  Changamoto zipi mlizopambana nazo au mnazoendelea kupambana nazo katika kukua kwenu?

MGN:Changamoto ni nyingi lakini hizi chache ndizo naweza kuzisema kwa sasa; ya kwanza ni kuwa <Sio makanisa yote yanaelewa jambo hili kwa hiyo watu hao hawawezi kuwaruhusu> ya pili<Kwa kuwa wengi wa dancers ni wanafunzi  wa secondary na vyuo hivyo muda wa kukutana kufanya mazoezi ni adimu,yaani mpaka wakati wa likizo> ya tatu <Kwasababu watu wengi bado hawajui na hawajakubali,basi kuungwa mkono bado ni kugumu na kusemwa semwa  bila  kusaidiwa> na nyingine ni <hatuko Exposed,lakini bado tunalifanyia kazi ili kuhakikisha tunafahamika> ,na nyinginezo  lakini zingine ni za kawaida na zinatatulika.

GoStaBa: Mmefanikwa kwa kiasi gani mpaka sasa?

MGN:Bado hatujafanikiwa kufikia malengo yetu lakini mpaka sasa tumeshahudhuria na kuhudumu katika matukio/matamasha zaidi 10 tangu mwaka jana mpaka sasa,yakiwemo matamasha matatu ya mwisho ya King Chavala..LAUGH AGAIN CONCERT SERIES na pia tumeshirikishwa kwenye Video ya wimbo wa “KATIKA NYUMBA YA BWANA” wa Amani Kapama.

UNAWEZA KUANGALIA VIDEO CLIP HII KAMA SAMPLE
http://www.youtube.com/watch?v=SVVuCoKZTGg

GoStaBa: Mnalelewa na nani?

MGN:Tunalelewa na Mama Mlawa na kushauriwa na Daniel,Agnes,Doreen,Patrick na wengineo

GoStaBa: Nini mategemeo au mipango yenu mbeleni?

MGN:Mategemeo yetu makubwa sio kuendesha 1st Q kama kundi bali kama ministry au organization ambayo itahusisha vipaji vingi sana walivyo navyo vijana katika kuhubiri injili na sio Dar peke yake bali Tanzania nzima.

GoStaBa: Ni jambo gani ambalo mkisaidiwa mnafikiri mtalifurahia sana kama kundi?

MGN:Tutafurahi sana kama tutapata nafasi ya kufanya kazi/kupeform mahali wa makubaliano ya muda mrefu au uhakika wa kufanya performance angalau mara moja kwa mwezi.

GoStaBa: Ni nani mnatamani kufanya nae kazi?

MGN:Yeyote Yule aliye tayari kufanya kazi nasi kwa moyo mmoja.

GoStaBa: Ni kundi gani(la ndani au nje ya nchi) ambalo mnavutiwa nalo sana na mnatamani kuwa kama wao au kuwazidi? Kwanini?

MGN:Hakuna kundi tunalotamani kuwa kwa wao au kuwazidi ila kuna makundi ambayo tunayakubali ni kama vile RIOT Dancers,DPC Dancers na mengine mengi  ya nje kama vile mastered seed group.


GoStaBa: Una neno au ushauri wowote kwa wasomaji wa Blog hii?

MGN:Naona niwape neno toka katika Biblia kitabu cha 1kor 10:31…..Basi,mlapo au mnywapo,au mtendapo neno lolote,fanyeni  yote kwa utukufu wa Mun gu….. na pia 1kor 12:5-6……tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye Yule. 6-Kisha pana tofauti ya kutenda kazi,bali  Mungu ni yeye Yule azitendaye kazi zote katika wote. Utofauti wetu (Wakristo) katika kutenda kazi usituathiri, ikiwa wote tunafanya kazi  ya Yesu Kristo  tukiongozwa na Roho mtakatifu. Amen.

GoStaBa: Ahsante sana mtumishi kwa muda wako na natumai tutaonana tena na tena!

MGN: Ahsante sana pia ninakushukuru sana na Mungu awabariki ili mzidi kungara ulimwenguni.
....................................................................................................................

BASI KWA UFUPI KAMA TULIVYOMSIKIA MBEBA MAONO NA MKURUGENZI,GRACE LIFARD MLAWA, HILO NDIO KUNDI LA DANCE LA LA 1ST Q  LENYE MAKAO YAKE JIJINI DAR ES SALAAM ,AMBALO LINAENDELEA KUKUA NA WAKO TAYARI  KUFANYA KAZI NA KANISA,MWIMBAJI,DANCERS NA MTUMISHI YEYOTE YULE ALIYE TAYARI AITHA IWE TAMASHA,IBAADA AU HATA KUFANYA VIDEO RECORDING KWA WAIMBAJI WA NDANI NA NJE YA NCHI YA TANZANIA SAWASAWA NA MISINGI NA TARATIBU ZA KUNDI HILO KWA UTUKUFU WA MUNGU.
NATAMANI TUWATIENI MOYO VIJANA HAWA WALIOAMUA KUMTUMIKIA MUNGU KUPITIA VIPAJI VYAO,BASI KWA KUJUA ZAIDI AU KUWAALIKA AU KUTAKA KUSHIRIKIANA NAO BASI WAWEZA KUWAPA KUPITIA ANAUANI ZIFUATAZO;

Simu; +255719868702, +255719406060, +255654767422
Barua pepe;lifarda1@gmail.com
Facebook; 1st Q

KARIBUNI SANA KWA MASWALI NA MAONI AMA USHAURI
+255 713 883 797
lacs.project@gmail.com

Tuesday, May 7, 2013

TANZANIA GOSPEL SINGERS' BREAKFAST-Episode 2!!

SHALOM!
KWA MARA NYINGINE TENA(YA PILI); GOSPEL STANDARD BASE Blog IMEWAANDALIA WAIMBAJI WOTE WA NYIMBO ZA INJILI,CHAI YA ASUBUHI,ITAKAYONYWEWA JUMAMOSI YA TAR 11/05/2013 KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI MPAKA SITA NA NUSU MCHANA,PALE VICTORY CHRISTIAN CENTRE-VICTORIA(KWENYE KITUO CHA MAFUTA),ZAMANI KANISA LA VCC!
HII NI CHAI MAALUM AMBAYO INAWAKUTANISHA WAIMBAJI WOTE WA NYIMBO ZA INJILI,KUANZIA WAIMBAJI WA KWAYA,BAND,VIKUNDI NA WAIMBAJI MMOJA MMOJA,NA INAHUSISHA MIZIKI YOTE YA KISWAHILI,KIINGEREZA,KILUGHA NA PIA HIP HOPE NA AINA NYINGINE ZOTE ZA MIZIKI,IKIWA WEWE UNAFANYA MUZIKI WA INJILI BASI HII INAKUHUSU SANA!
HII NI FURSA PEKEE YA KUFAHAMIANA,KUFUNDISHWA,KUCHANGAMOTISHWA,KUOMBA NA KUNYWA CHAI PAMOJA ILI KUJENGA UMOJA NA MSHIKAMANO ZAIDI KUNUA VIWANGO VYA MUZIKI WA INJILI TANZANIA!!
HAKUNA KIINGILIO CHOCHOTE ILI HAUZUILIWI KUTOA MCHANGO WAKO WOWOTE ULE!
IMEDHAMINIWA NA BLOG HII NA KUSIMAMIWA NA "CHAVALA IDEAS PLATFORM"

KWA MAELEZO ZAIDI
+255 713 883 797