Showing posts with label Madhabahuni. Show all posts
Showing posts with label Madhabahuni. Show all posts

Sunday, January 5, 2014

SIRI ya MAFANIKIO YAKO!!



SIRI ya MAFANIKIO YAKO
(UMUHIMU wa KUJIFUNZA NENO la MUNGU)

Wakati tunatarajia MEMA katika MWAKA mpya 2014 nimeona nikupe SIRI ya jinsi haya MEMA yanaweza kukujilia maishani mwako. Kumbuka sio kila AHADI ya kwenye Biblia ni yako hata ukiikiri USIKU na MCHANA. Kuna KIWANGO cha IMANI katika KUPOKEA AHADI za Mungu. Kumbuka “imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo”. Sasa nataka ujifunze kwamba unapata ZAIDI ya IMANI pale unapojifunza Neno la Mungu.

Unapojifunza Neno la Mungu KIWANGO chako cha KUMJUA Mungu kinaongezeka. Haiishii hapo, kila unapoongeza KIWANGO cha kumjua Mungu mambo mawili yanatokea (i) AMANI yako inaongezeka (ii). Mema yanakujilia. (Ayubu 22:21)

Hakuna kitu nafurahi kama kusikia feedback kwamba kuna MTU amebarikiwa na FUNDISHO la UFALME (Mambo ya Mungu). Ukisikia umebarikiwa mara nyingi sana inamaanisha umepata UFUNUO fulani (Mungu amefunuliwa kwa njia fulani zaidi katika maisha yako kupitia hilo Neno). Sasa huku mimi najua sio tu UMEBARIKIWA na kuongeza MAARIFA ya kiroho, ila na kiwango cha AMANI na KUFANIKIWA kwako katika mambo yote na MEMA yanaongezeka katika maisha ya kila siku.

Basi tusiwe wavivu kujifunza mambo ya Mungu kwa maana ANATUFUNDISHA ili tupate FAIDA. (Isaya 48:17-19). Ukiona kwenye TV (series, movies, nk.) na kusoma NOVEL na MAGAZETI unachangamka ila hata page 3 tu za mafundisho ya Neno la Mungu unaona ni MZIGO, ujue uko karibu na HASARA kama HUJAPATA tayari.

Nawatakia HERI ya MWAKA MPYA 2014.

Frank Philip

Sunday, December 22, 2013

KAMA UNATAKA MUNGU AONEKANE NA WATU JIFUNZE HII SIRI



Kipimo cha UDHIHIRISHO (MANIFESTATION) wa Mungu kwenye HADHIRA (PUBLIC) ni MUDA, BIDII na HALI ya MOYO wako UKIJIHUDHURISHA mbele Zake mkiwa wenyewe wewe na Mungu pekeyenu (SIRINI).

Kama UKIJIHUDHURISHA mbele za Mungu wako kwa BIDII na kwa UELEKEVU mahali pa SIRI, basi Mungu ATAJIDHIHIRISHA mbele ya WATU hadharani.

Ukitaka Mungu aji-present kwa watu basi jifunze kuji-present kwa Mungu.

Ni aheri ukose MUDA wa kuandaa PRESENTATION kwa watu na sio MUDA wa kuji-present kwa Mungu, kwa maana unaweza ku-present kitu chochote mbele za watu ILA HUWEZI kum-present Mungu! Ndio maana kazi ya Mitume ilikua KUHUBIRI na KAZI ya Mungu likua KULITHIBITISHA hilo Neno kwa ISHARA na MAAJABU.

Kazi ya Musa ilikua kuji-present kwa Mungu na kupata maelekezo na KAZI ya Mungu ilikua KUTENDA miujiza (kuji-present) mbele za Farao!

Frank Philip.

Sunday, December 8, 2013

NJIA YA WOKOVU!!!


Kwenye maaandiko tunajifunza kwamba watu walioanza kumfuata Yesu wakati huo wa Mitume hawakuitwa Wakristo bali waliitwa “watu wa NJIA”. Kati ya namna mbalimbali ambazo Yesu kujitambulisha, mojawapo alijiita yeye ni NJIA. Na akasema hii NJIA inatufikisha wapi. “mimi ndimi njia ya Kweli na Uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa kupita kwangu”. Hakuna njia isiyomfikisha mtu mahali fulani. Kila mtu anachagua njia kwa makusudi ya kufika mahali fulani, awe anapenda au hapendi ila kitakachomfanya afike hapo MAHALI ni njia aliyojichagulia. Yesu anashauri na kutualika akisema “ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.” (Mathayo 7:13, 14)

Nataka tujifunze hii njia ya Yesu. Hii njia ina sifa nyingi zisizovutia isipokuwa sifa moja kwamba itakufikisha kwa Baba. Kwanza watu watakaoiona hii njia ni wachache achilia mbali watakao pita juu yake. Sasa kusudi la njia ni kupita/kutembea na wala sio kukaa au kusimama. Unapoitwa kwa Yesu, ukakubali na “kukata shauri” KUMFUATA, jua umepata MWALIKO wa kutembea katika hii NJIA. Kupata mwaliko haina tofauti na kupata TIKETI ya kusafiria. Usipochukua hatua na kupanda basi huwezi kuona mambo yaliyoko njiani. Utajifariji na tiketi yako mkononi kwa sababu imeandikwa UNAKOKWENDA ila usipoanza safari hufiki huko japo pameandikwa kwenye tiketi yako.

Sifa moja ya muhimu sana ya NJIA “hii” ni wembamba wake. Tunaambiwa IMESONGA. Kuna tofauti ya wembamba na kusonga. Katika mawazo yangu napata picha ya njia ambayo iko katikati ya kuta ndefu kila upande. Kwa lugha ya kawaida ningeiita “uchochoro”. Yaani ni nyembamba lakini pia imesongwa na kuta huku na huku. Ukiwa na MAFURUSHI makubwa UNANASA hapo kwa sababu kumesonga sana. Hii hali ya kusonga/kubana huwezi kuiona kama HUJAANZA safari. Ukisikia mtu anasema WOKOVU ni “tambarare” jiulize kwamba anapita njia gani? Maana huku kumebana, yeye tambarare anaipata wapi? Bwana wetu mwenyewe alisema “ulimwenguni mnayo dhiki lakini jipeni moyo, mimi nimeushinda ulimwengu”, sasa alishinda nini kama kila mahali ni tambarare na hakuna vita?

Sasa kuna mambo mengi sana ukiyaangalia utagundua yanakupasa kufanya KAMA umeanza safari ya kumfuata YESU. Kwanza NJIA inaelekeza uelekeo (direction) ambao hujachagua wewe ila mwenye njia (Yesu). Utagundua kwamba huwezi kubeba kila kitu (kiburi, tamaa mbaya, uzinzi, uchungu, kutokusamehe, etc.) ukafanikiwa kupita kwa sababu njia imesonga. Kwa sababu hii njia ni ya kufikirika (theoretical/hypothetical) japo ni dhahiri (practical/real) wakati wa kupita inakuwa ngumu kuonekana na wachache wataiona pale watakapochukua HATUA. Usipochukua hatua na kuanza safari huwezi kuelewa maana ya KUSONGA!

Kuna mambo manne MUHIMU yatakatokuwezesha kutembea katika NJIA hii. La kwanza, kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako, kutubu na kugeuka. La pili, kujazwa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu sio NGUVU ila ni NAFSI ya Mungu japo pia Ana NGUVU. Roho Atakufundisha yote, kukukumbusha pia kukufariji uwapo njiani (hutakua yatima ujapopita nyikani). La tatu, kusoma Neno kwa BIDII tena KILA siku. Kama unavyokula chakula cha mwilini, lisha na roho yako ipate nguvu. Neno lina nguvu ya kukutakasa na kutenda mapenzi ya Mungu maishani mwako. La nne, DUMU katika maombi ili usianguke MAJARIBUNI na upate mwongozo (direction) uwapo safarini. Huwezi kutenda mapenzi ya Mungu kama wewe sio muombaji.


Kama hujasikia KUBANWA/KUZONGWA anza kujiuliza swali hili, Je! Umeanza safari? Na kama umeanza, jiulize tena Je! Hujabanwa/hujanasa kwa sababu umetua kila mizigo ya dhambi, uchungu, nk.? Kama unajua bado kuna shida ndani yako na hujatengeneza vizuri mambo na “kutaka amani na watu wote na huo utakatifu”, jiulize tena swali, Je! Uko njia nyembamba au pana? Ukipata majibu ya hayo maswali chukua hatua zipasazo.

Mambo muhimu ya kukumbuka ukiwa NJIANI (safarini). Kuna vibao vingi sana vya kukupoteza (DIVERSIONS). Kuna kona nyingi (mambo magumu na mateso) na njia-panda nyingi (mahali pa kuchagua kumtii Mungu au Ibilisi) na mara nyingi njia-panda (makutano ya barabara) hayako kwenye mteremko, ila yako kwenye mwinuko. Baada ya kuchoshwa na “safari”, unafika njia-panda, kushoto (kwa Ibilisi) ni mteremko na kulia (kwa Yesu) ni mlima zaidi! Kama UMEKAZA uso wako kwa Yesu, utapita KONA zote, na ukifika NJIA-PANDA utapinda kuelekea tena kwenye NJIA nyembamba (kwa Yesu) hata kama huko mbele ni MLIMA zaidi.

Ukizidi kuendelea na safari utagundua kuna MABANGO makubwa yameandikwa jina lako. Mengi ya haya mabango yamebeba lugha ya kukebehi, matusi, kukatisha tamaa, kukera, nk. Usiangalie MABANGO, kaza uso wako kwa Yesu kama Stefano. Sio rahisi, hata Yesu amesema sio rahisi ila njia inapitika. Wakati Stefano anapigwa mawe, hakukimbia badala yake alipiga magoti. Akatazama juu USHINDI wake ulipo! Hakutizama warusha mawe (MABANGO), hakusikiliza wanayosema wakati wanarusha mawe (ujumbe kwenye mabango), aliangalia JUU. Badala ya kuwarushia maneno ya LAANA, Stefano alikua busy kuwaombe watesi/wauaji wake msamaha. Wakati watu wanaona damu inatiririka mwilini mwake, Stefano alimwona Yesu na Jeshi la malaika watakatifu. Wakati watu wanaona mauti, Stefano anaona UZIMA wa MILELE! Akakaza USO wake kwa BWANA na kumaliza SAFARI yake salama.

Jiulize ni watumishi wangapi leo wataambiwa wana BELIZEBULI wasipigane ngumi? Jiulize ni wana wa Mungu wangapi leo wakinenewa tu jambo hata kama ni la uongo wanakwazika na kuwa wakali? Eti wanachafuliwa majina na kuvunjiwa heshima! Sawa, ila mtizame yeye aliyejiita “NJIA” ambaye tunamfuata,“Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu, aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.” (Yohana 13:2-4). Yesu alipogundua ana KILA KITU (kwa lugha ya kawaida tungesema UTAJIRI wa kila namna), na yuko kwenye njia (safarini) “Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa ALITOKA KWA MUNGU NAYE ANAKWENDA kwa Mungu” akijua hayo, alivua VAZI lake (sio kukunja shati mikono au kukunja suruali), akajifunga kitambaa kiunoni, akachukua maji (hakumtuma mtu akalete kwa maana wakati huo alikuwa ni MTUMISHI anayetumika), akainama, akawanawisha na kuwafuta kwa kitambaa (nguo iliyo mwilini mwake)! Huyu ni Bwana na NJIA tunayoifuata.

Ujumbe huu umekuja kukumbusha habari ya NJIA na yatupasayo kufanya katika NJIA hii. Mungu atupe NEEMA ya kujikagua na kupata UTHIBITISHO wa ndani kwamba tuko njiani au la! Roho anashuhudia pamoja na roho zetu kama sisi ni wana wa Mungu, naye Atatupa kutambua kwamba tuko katika njia gani kwa maana haachi kushuhudia juu ya “DHAMBI, HAKI na HUKUMU”. Msikilize Roho Mtakatifu na MAELEKEZO yote atakayokupa, UTAFIKA salama kwa BABA.

NEEMA ya BWANA wetu YESU KRISTO iwe nanyi tangu sasa na hata MILELE AMEN.

Frank Philip.

Wednesday, December 4, 2013

......MAANGALIZO!!!



(HATUA za HUDUMA na VIPAWA vyako)

1. Jua kutofautisha kati ya HUDUMA na BIASHARA. Msukumo wa HUDUMA hauko katika kufanya FAIDA bali kutenda kile mtu anachokifanya kwa “jamii” fulani, na hiki “kitu/shughuli” kimejikita katika Mapenzi ya Mungu. Malengo na Madhumuni ya huduma ni KUTUMIKIA sio KUTUMIKIWA. Kumbuka katika UFALME wa Mungu, hakuna aliyeacha ndugu, wazazi, au shughuli yake NYINGINE na akachagua kufanya HUDUMA katika Ufalme huu asirudishiwe mara 100! Mtihani upo katika kukaa kwa UAMINIFU na kwa SABURI ukimtizama yeye ALIYEKUTUMA na wala sio FAIDA. Ili UINULIWE unahitaji kufaulu mtihani wa UNYENYEKVU na ITAKUPASA kunyeyekea CHINI ya mkono wa Mungu ulio hodari UKISUBIRI akukweze kwa WAKATI WAKE. Huu wakati unakuja, ila ni wa kusubiri. Usidanganywe na MTU yeyote, huu ni wakati wa MAUMIVU na KUPIMWA imani yako kama kweli UKO KAZINI au unatafuta hela! UKIFAULU hapo, hakuna mahali hutakanyaga wala pesa hutapata. Hakuna ALAYE ataweza kumaliza “mavuno yako” japo kwa kweli walaji watakuwepo! Ili uweze kusimama mahali “hapa” (pa kupimwa na kusubiri kuinuliwa), katika njia ya kufikia “MAHALI pa USHINDI” wako utahitajika kufanya MAOMBI ya dhati kabisa huku ukichunga KINYWA chako maana anayekupima UVUMILIVU na IMANI yako mara nyingi sana ni YULE BWANA “unayemtumikia” ili ajue ATAKUPANDISHA cheo hadi wapi. Jinsi utakavyoshinda huu MTIHANI (interview) ndio UTAPANDA mbali zaidi.

Kumbuka mfano wa talanta (5, 2, 1), kiwango cha KUPOKEA hakikua kwa Bwana atoaye bali UWEZO wa mtumishi APOKEAYE. Ukitaka kupokea VINGI jiandae kujifua vizuri katika MAOMBI na SABURI. Huku ukila Neno kwa WINGI maana hivyo ndivyo vitendea kazi shambani mwa Bwana lakini pia ndio CHANZO cha IMANI katika Kristo. Nyenzo na vitendea kazi vya muhimu katika HUDUMA ni IMANI na MAMLAKA! Kumbuka Mamlaka inapatikana katika KUMTII Mungu katika mambo YOTE. Hivi viwili vinafanyaje kazi? IMANI ni kama FEDHA, NGUVU au UFUNGUO. Ili uweze kumiliki MAMBO fulani katika ulimwengu huu, na wa roho unahitaji hiki kitu ambacho kinaitwa IMANI. Kuna wakati utahitaji KUTEKA kambi ya adui ili ujitwalie MATEKA, bila NGUVU (imani na mamlaka) huwezi maana adui ameitwa ni “mwenye nguvu”. Kuna wakati unahitaji FUNGUO za kufunga au kufungua vitu katika ulimwengu huu na wa roho ili HUDUMA isonge mbele bila mamlaka huwezi kufurukuta.

HUDUMA inasema hivi “nimetenda ‘Mapenzi ya Mungu’ kiasi hiki na KUMRUDISHIA Mungu utukufu wake, na Mungu anasema “moja mia, au moja sitini au moja thelathini”, kulingana ni KIWANGO chako cha KUPOKEA kama MTUMISHI MWEMA na MWAMINIFU” Kwenye HUDUMA mara nyingine hakuna ulinganifu wa ULICHOPANDA na UTAKACHOVUNA kwa jinsi ya mwili. Huwezi Kupima mafanikio ya HUDUMA kwa kiwango cha PESA japo ukifanya HUDUMA LAZIMA pesa ije. Kipimo ni KIASI cha kutenda MAPENZI YA MUNGU. Ndipo huyu atapanda MBEGU ile ile katika UDONGO ule ule, huyu atavuna 100, mwingine 60 na mwingine 30!

Msukumo wa BIASHARA ni kupata PESA. Biashara inasema “nimewekeza kiwango ‘hiki’ na FAIDA lazima iwe ‘hivi’ la sivyo ni HASARA”. Sasa kumbuka kuna WATUMISHI wengi sana wanafanya KAZI ya MUNGU kama BIASHARA. Kipimo cha Mafanikio yao ni IDADI ya BIDHAA walizozalisha na kiwango cha PESA iliyoingia. FURAHA yao sio KUFANYA mapenzi ya Mungu ila ni faida wanayopata katika KAZI ya mikono yao. Mara nyingi sana WATUMISHI wa namna hii huchanganya BARAKA za MUNGU na MALI! Yaani mwenye ‘NAZO’ zaidi AMEBARIKIWA zaidi kuliko mwenye VICHACHE! Ndio maana BWANA wangu aliita kuna WACHUNGAJI wa MSHAHARA na wachungaji wa KWELI (Mchungaji mwema). Mtumishi ambaye anafanya biashara, kitu cha kwanza sio “KONDOO” (mapenzi ya Mungu) ila MSHAHARA (pesa). Sasa hiki ni KIPIMO kigumu sana na kimefichwa mbali na huwezi kuona kwa macho ya nje, ILA Mungu aonaye SIRINI hujua ni nani anafanya HUDUMA na ni yupi anafanya BIASHARA. Sasa kumbuka, haya makundi mawili yote yataleta MATUNDA kwa Ufalme wa Mungu, tofauti yao ni kitu kinaitwa THAWABU! Thawabu hulipwa MBINGUNI na MSHAHARA hulipwa DUNIANI. Hili kundi la WAFANYA BIASHARA watapata MSHAHARA (PESA) wao na Yesu akasema “wameshalipwa duniani”. Tabia yao ni kusimama MAHEKALUNI, KUPAZA SAUTI, KUSIMAMA kwenye KONA za NJIA na kuvaa KANZU NDEFU ili watu wawaone na sio MUNGU awaone”. KUJIONYESHA na MASHINDANO ya mwilini ndio JADI yao. Sawa, watashinda na kupata PESA, ila thawabu yao huko Mbinguni ni sifuri maana wamekwisha kupokea kwa WANADAMU sifa na utukufu! Wale wanaofanya HUDUMA mara ZOTE ni wanyenyekevu wa moyo, wanatanguliza Mapenzi ya Mungu na wanaogopa KUJISIFU na kugusa UTUKUFU wa Mungu. Maombi na kufunga ni sehemu ya MAZOEZI yao RASMI ya huduma, tena CONSTANTLY na sio wakati wa MATAMASHA tu. Kumbuka HUDUMA ni MAISHA sio EVENT! Hili kundi la wafanya HUDUMA mara nyingine hudhulumiwa na kulipwa kidogo (nusu pesa kama yule mama aliyeweka sarafu kwenye sanduku la hazina na Yesu akasema, “hiyo ni zaidi kuliko zile matajiri walizotoa”) lakini FAIDA yao ni KUBWA kama wametenda mapenzi ya Mungu na kurudisha UTUKUFU wake bila kuugusa hata tone. Hili kundi ni la muhimu sana kwa maana linazaa double double. MATUNDA hapa duniani na Uzima wa milele. Ila kundi la WAFANYA BIASHARA linazaa matunda hapa duniani na kukosa UZIMA wa milele! Kwa maana hata kwa MZAHA Yesu atahubiriwa na miujiza itafanyika ila wale watendao hayo watapotea milele! Chagua kukaa katika MSTARI wa Mungu usifanye kazi ya HASARA Mtumishi wa Mungu. Kila mtu na ajipime kazi yake mwenyewe na AJITAMBUE na kujipanga sawasawa asije akasema HAKUJUA! Maana usishangae Yesu anakutembelea na KIKOTO halafu usiamini, maana wale watu waliofanya biashara hekaluni wakati “ule” hawakumjua Yesu kama “mchapaji” pia! Chunga sana, Yesu ni yeye yule JANA, LEO na hata MILELE.
Matendo ya Mitume 20: 33 “Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. 34 Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. 35 Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea. 36 Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote. 37 Wakalia sana wote, wakamwangukia Paulo shingoni, wakambusu-busu, 38 wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamwona uso tena. Wakamsindikiza hata merikebuni.”

Kuna vipawa vingine vitatumika sio kama HUDUMA bali BIASHARA. Sasa, kama Mungu amekupa kufanya biashara au kazi ya kukuingizia KIPATO kwa namna yoyote USIMSAHAU Mungu katika biashara hiyo. Tafuta makusudi yake na hakikisha BISAHARA yako INAMTUKUZA Mungu na inaheshimu na KUTII makusudi ya Mungu. Kama Mtumishi wa Mungu katika BIASHARA yako, jifunze kutafuta kusudi la Mungu na kukaa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu daima. Chunga sana unavyowahudumia watu na kuweka viwango vya BEI na tozo mbalimbali. “Mungu hapendi mizani za uongo”. Pima kazi na malipo kwa ulinganifu na “usichukue zaidi ya ikupasavyo”. Na jua kwamba sio kila mara utafanya kazi/biashara kwa MASLAHI ya kibinadamu (kazi au bidhaa kuuzika kwa bei ya faida kwa namna ya kibiashara). Ukijikuta unasukumwa kufanya kitu CHOCHOTE kwa pesa tu, jua unakaribia mahali pa gumu. Ukisikia mtu anasema “hii kazi haina maslahi” na haangalii kama Mungu anataka nini ila pesa tu, ni hatari. Sio kila wakati utafanya kazi kwa malipo ya pesa, Mungu anaweza kubadili mfumo wa malipo kwa baadhi ya kazi. Usipokua makini unaweza kujikuta unajifungia milango ya muhimu wakati unakimbiza pesa na ukajikuta hufiki mbali. Pamoja na kufanya faida, REHEMA iwe ndio mhimili wa maamuzi yako ya ki-PESA au kuhudumia wateja wako.

2. Mfumo wa duniani utakulazimu kufanya mambo mabalimbali wakati wa kufanya HUDUMA na mengine ni magumu. KUMBUKA wewe ni MTUMISHI (mtumwa), kuna Bwana aliyekutuma. Ukibinafsisha HUDUMA ikawa yako itakua NZITO mabegani mwako. Kwa maana kila HUDUMA ina VITA, na Maandiko yanasema HAKUNA askari aendaye VITANI kwa GHARAMA zake! Ukifika mahali pa kujisahau ukaanza kusema “huduma yangu” huku ukisahau kua wewe ni MTUMWA na sio BWANA (boss) au MMILIKI wa hiyo HUDUMA unakaribia kufikia MAHALI pa gumu. Hata siku moja USISAHAU kwamba kuna “organization structure” ya Mungu ambayo yeye ni TOP BOSS na sisi ni vibarua tu. Sasa hapo juu yako kunaweza kua na VIONGOZI wako wa KIROHO, chunga usiwavunjie HESHIMA na ukakosa kuwasikiliza kwa KISINGIZIO cha HUDUMA na UPAKO juu yako. Imempasa KILA mmoja kuitii mamlaka iliyo kuu katika KAZI ya HUDUMA na ni vyema sana ukaitambua mamlaka “inayokuhusu” na kukaa VIZURI nayo maana inaweza ikawa SABABU ya wewe KUKUA au KUANGUKA kihuduma. Katika MFUMO huu wa Utawala, jua kuna wakati utakua na watu chini yako. ANGALIA basi kwa sababu na sisi tu wa BWANA wetu ambaye tunamtumaini KUTUBARIKI nasi tusizuie mkono wetu kuwabariki walio chini yetu na kuwatanguliza kama BWANA wetu alivyotupa mfano wa kunawisha miguu wafuasi wake. Ukitaka kua BOSS/MKUU sharti ujifunze “kuvua nguo (utukufu) na kujifunga taulo kiunoni KISHA “kuinama” (kunyenyekea) na kuwanawisha (kuwatumikia) MIGUU michafu walioko chini yako kwa USTAHIMILIVU”.

3. Katika mfumo wa kufanya kazi ya Mungu utahitaji VIBALI na michakato mingi ya KISHERIA na imekupasa kumpa KAISARI kilicho chake kwa UAMINIFU wote. Huwezi kuepuka wezi, nondo na wadudu mbalimbali (ma-promota, producer, nk.) walao maadam uko duniani. Ila jua Bwana ni fungu lako na HUTAPATA hasara kwa maana yeye anaona SIRINI na anajua shida yako na ATAKUJAZI. Kumbuka kuweka HAZINA yako Mbinguni pia maana huko hakuna kutu, nondo wala wezi. Na unahitaji ULINZI wa Mungu ili HUDUMA yako “isipukutishe majani/maua” kabla ya KUZAA, na yeye anaweza pia KUMKEMEA yeye ALAYE (Ibilisi na watu wake), ulinzi huu unaupata katika ZAKA KAMILI! Jifunze KUTOA kwa USAHIHI maana kuna faida NYINGI.
Warumi 13: “1 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 2 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 3 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. 4 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. 5 Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. 6 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. 7 Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.”

4. Huwezi kufanya HUDUMA na kutumia VIPAWA vyako bila kuwa na watu wengine katika timu. Huduma inavyozidi kukua utahitaji watu wengi zaidi. Kumbaka jambo hili siku zote, wana wa Mungu wanapojihudhurisha mbele za Mungu wao, shetani naye huja kati yao. Ni vigumu sana kutambua magugu yawapo pamoja na ngano na sio kazi yetu “kuyang’oa” maana hakuna aliyepewa huo wito na BWANA wetu ila inabidi kujichunga na kujilinda na “chachu” yao maana inaweza kuchachusha HUDUMA yako bila kujua. Yesu alikua na wanafunzi 12 na mmoja wao aliitwa “msaliti”! Kama Yesu alikuwa na timu na ndani yake kuna YUDA, jua imekupasa kuwa makini na macho ya mwili na roho kujua watu wa timu yako maana humo watakuwepo wasaliti na wengine ni hatari kuliko YUDA. Kazi ya Yuda ilikua “mweka hazina” ila alikua akiiba vitu/matoleo! Sasa chunga sana mienendo na tabia za watu wa timu yako maana jua kuna roho nyuma yao na mwisho wake huwa ni KUSALITI ili huduma ife bila kujali madhara. Kipimo kikubwa cha uaminifu wa wengi katika timu ni TAMAA ya pesa! Hii ndio ilimfanya YUDA akasaliti huduma yao na Bwana wake kwa sababu ya KIPATO cha vipade 30 tu vya fedha! Sasa jua neno hili kwamba kama YUDA ambavyo hakuila ile pesa, ndivyo wengi sana wanaomsaliti Bwana aliyewatuma huishia pasipotarajiwa kama ilivyokua kwa YUDA au zaidi. Ndani ya vikundi vingi sana wamejipenyeza akina Delilah na wamenyongelea chini HUDUMA nyingi na imebaki mazoea tu na nguvu ya ugali. Imekupasa kukaa katika Maombi ya DHATI kabisa kama timu nzima na kuwa na ratiba za KULA na kujifunza na KUSIKILIZA maagizo ya Bwana aliyewatuma kazini ili msiingie majaribuni.

5. Chanzo cha nguvu zetu ni Mungu aliyetutuma kwenye kazi yake. Huwezi kumchanganya Beliari na Mungu na ukapata matokeo mazuri. Ni jambo la kustaajabisha sana kuteremkia Misri kutafuta msaada ili usimamishe HUDUMA! Yaani unamsaidia Mungu “kutafuta msaada au mtaji kutoka kwa mungu mwingine”! Kumbuka, kukua kwa huduma ni hatua, ambazo huongozwa na Mungu. Na kukua huku kunaenda sambamba na kukua kwa IMANI yako. Kama unataka kukua kwa kasi basi kimbiza kukua kwa IMANI yako. Kwa maana “tunafanikwa katika mambo YOTE kwa kadri roho zetu zifanikiwavyo”. Kwa MAJIRA na vipindi alivyoamuru Mungu, ataleta mtaji na mahitaji ya kukuza huduma yako. Ukifika mahali “unakopa” na kujitaabisha sana ili “uwekeze” kwenye huduma kwa malengo ya KUKUA KWA HARAKA, jua unakaribia mahali sio pazuri. Kama wewe ni “mtumwa” na Bwana wako anataka ulime hatua 10 kwa siku, kwanini ushindane naye na kutaka kulima hatua 100? Je! Hizo hatua 90 za zaidi ulifanya kwa msukumo wa kumzalishia Bwana wako au “kujiongezea kipato”. Jiulize kinachokusukuma ni BIASHARA au HUDUMA? Sasa usiwe MLEGEVU katika kazi ya BWANA maana Mungu amekataa UVIVU na ULEGEVU ila tuwe na BIDII katika KUTAFUTA na KUTENDA mapenzi ya Mungu peke yake.

6. Ukiona UNAMTUMIKIA Mungu, na umefika mahali ukitaka PESA kwa ajili ya jambo fulani, na unajikuta UNACHANGISHA watu, au kuomba watu PESA “kabla” ya kumwomba “kwanza” Mungu hiyo PESA, jua unakaribia mahali pa GUMU. Epuka kua OMBAOMBA na jifunze kumtegemea Mungu kama kweli UNAMTUMIKIA Yeye. Yesu alipotaka “pesa” alituma mtu akavue samaki na kisha ampasue atoe huko sarafu! Unadhani wakati wa Yesu akina ZAKAYO hawakuwepo? Unadhani alishindwa kuwambia tu kwa URAHISI walete SADAKA/MBEGU na wakamjazia kila mahali MIJI-HELA? Angalia basi Mtumishi wa Mungu usije ukahamisha TEGEMEO lako kwa wanadamu bila kujua. Ni kweli Mungu atainua hata “mawe” yafanye kazi yake, ila chunga usije ukaanza na kutafuta misaada kwa “mawe” kama hayo ndio yamekuita katika kazi ya HUDUMA. Muombe Mungu kwa bidii, tafuta USO wake kwa bidii zote, kama atatuma MALAIKA kukuletea “mkate na gudulia la maji” au kama atatumia KUNGURU kukuletea “mkate” kama kwa Elia Mtishibi, sio juu yako kuchagua. Mtumaini yeye na kaa katika KUSUDI lake. Mojawapo ya sifa za watu wanaomtegemea Mungu katika VIPATO vyoa ni KUOGOPA sadaka na KUIHESHIMU! Yamkini hujawahi kukutana na mtumishi wa Mungu anakataa SADAKA lakini wapo wengi tu, Kumbuka habari za Elisha baada ya kumponya mtu ukoma! Ingekua leo tungeita “sadaka ya shukurani” na tungeshangilia kupokea! Sasa sisemi sadaka za shukurani ni mbaya, ila nataka uone hii KIU ghafla ya kutaka KUPOKEA kirahisi kutoka kwa WANADAMU na KUDAI kwa nguvu au kijanjajnja saa nyingine kwa kutishia watu kwa maandiko. Hatukuitwa KUKUSANYA pesa na sadaka ila kuleta ROHO za watu kwa Mungu. Pesa ikija ni sawa, ni CHAKULA CHA SAFARI tu kutuwezesha kufikilia MAKUSUDI ya Mungu na wala Pesa yenyewe sio MAKUSUDI ya MSINGI ya HUDUMA zetu labda kama tunafanya BIASHARA.

7. Majaribu lazima yaje ili kupunguza kasi ya huduma yako japo ukiyashinda UNAPANDA cheo. Kwa Ayubu shetani alisema “nikigusa kitu cha karibu naye” huyu jamaa lazima ashindwe. Ibilisi akashughulikia watoto na mali zote! Usidhani ilikua mahali pa rahisi hapo kusimama tu katika UAMINIFU na Mungu. Wakati watoto wanaangamia na mali zinaporomoka wanakuja MARAFIKI “wataabishaji” wakileta injili pori na maneno “kandamizi”. Lakini Ayubu akakaza macho kumtizama Bwana wake na akafika MAHALI pa USHINDI wake, japo ilikua ni raundi ya kwanza. Raundi ya pili Ibilisi anataka kumgusa Ayubu “karibu zaidi” ili kumchanganya na kumpotezea mwelekeo. Ibilisi anasema “mwili bwana, mwili, mtu akiguswa mwilini ataachia tu ngazi”, Mungu akatoa “go ahead”. Wakati Ayubu anapambana na MAJIPU mwili mzima, anajikuna kwa kigae maana yamkini akijikuna usaha ulikua unamwagika na kigae ndio cha kukingia, huku ananuka na kwa kawaida watu wanakaa mbali, hatamaniki, MKE wake anakuja na mpya! Akidhani anamwonea huruma, akitazama haoni tena mtu ila “maiti” na anamshauri “amkufuru Mungu” kuharakisha kufa maana anaona jamaa kilichobaki ni kifo tu na anateseka bure! Ayubu alijua bado mara hii tena atafika “MAHALI pa USHINDI” wake! Kumbuka alishinda mara dufu, na alirudishiwa kila kilichopotea maradufu!

Watumishi wengi sana wameshindwa kusimama kwasababu Ibilisi amegusa vitu vya “karibu” nao. Wengine wakati wako Busy na Mungu, huku nyuma mke/mume anakamatana na makahaba! Na ibilisi ataweka “mtu wa kuleta habari” kama ilivyokua kwa AYUBU! Ili uumie na uvunjike moyo na upunguze KASI ya huduma yako. Mara nyingine “karibu” inaweza kua watoto, wazazi, ndugu, mali au ajira alimradi ni mahali PATAKAPOKUGHARIMU na PANAUMA. Lengo ni kukukatisha tamaa mtu wa Mungu ili ukose mwelekeo na ushindwe kutimiza HUDUMA au kuzaa MATUNDA sawa na wito au KIPAWA chako. Chunga sana hili eneo maana ni gumu na limefisha HUDUMA nyingi sana za watumishi wa Mungu na wameshindwa kuzaa MATUNDA yawapasayo. Sikiliza MTUMISHI wa Mungu, KILA kitu kitapita, usiangalie kushoto wala kulia, kama ni mume au mke amekusaliti kwa kumsikiliza Ibilisi na kwa “kutokujua saa ya kujaribiwa kwake”, wewe USIKATE tamaa, SONGA mbele! Mwangalie Mungu aliyekuita na uzidi katika nguvu zake na mapenzi yake maana hapo ndipo MAHALI pa USHINDI wako.

Kwa sababu kila mtu katika Mwili wa Kristo ameitwa kwa kazi maalumu kama ilivyo viungo vya miili yetu, basi jua kama UNASHIKA njia za SHETANI sio tu kwamba UNAHARIBU huduma yako, ila pia UNAANGAMIZA huduma ya watu wa “karibu” wanaokuhusu kwa sababu kwa KUTENDA hayo MAOVU unawaumiza na kupunguza KASI ya utumishi wao. Kumbuka kuukomboa wakati maana hizi ni nyakati za uovo. Msikae tu kugombana na kubishania mambo yasiyo ya msingi na kusahau kua mna KAZI shambani mwa Bwana. Mtakapo shughulika na MAMBO ya Mungu jua HAKIKA Mungu atashughulika na mambo yenu pia na BARAKA na FURAHA vitaongezeka kwenu na kwa watu wenu wa KARIBU.

Matendo ya Mitume 20: 19 “nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na kwa machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi; 20 ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba, 21 nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo. 22 Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko;
23 isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. 24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu. 25 Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena. 26 Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina hatia kwa damu ya mtu awaye yote. 27 Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu. 28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.”

8. USHUHUDA. Kama kuna kitu kimekwamisha kazi ya Mungu ni USHUHUDA mmbaya wa watumi wa Mungu. Kumbuka, unapotenda “KITUKO” chochote hadharani au kwa SIRI ila Ibilisi amefanikiwa kukichomoza hadharani, watu wataanza kukutizama kama wewe ni mtu wa “namna ile” sawa na KITUKO ulichofanya, hata kama ilikua mara moja. Ile LEBO unayobandikwa ya hiki KITUKO ina tabia ya KUDUMU na ni NGUMU sana kuifuta kwa jinsi ya kibinadamu. Sababu ya msingi hapa ni kwamba Mungu ANASAMEHE na hakumbuki kama UKITUBU, ila wanadamu HAWASAHU hata kama umetubu. Kama ulifanya UZINZI bado watu watakutizama tu kama MZINZI kwa muda mrefu. Ibilisi naye atahakikisha habari MABAYA inaenea kwa KASI kwa sababu yeye ni “mshitaki”. Watu wengi sana wamesahau kwamba USHUHUDA ni silaha ya MUHIMU kumshinda Ibilisi, ndio maana tunasoma “nao wakamshinda kwa Damu ya Mwana-kondoo na kwa neno la ushuhuda wao..” Kama kuna kitu Ibilisi anawinda ni kupata USHUHUDA wako mmbaya na KUUSAMBAZA kila mahali. Unaposimama KUHUDUMU anawakumbusha watu na kuwaambia “msimsikilize huyu jamaa kwanza ni tapeli/mzinzi/mrushi/mwizi” nk. Mara nyingi sana watu wameshindwa kupokea Neema ya Mungu iokoayo na hata kusema kwa ujasiri “hakuna wokovu duniani” kwa sababu wanajua WALICHOONA kwa wana wa Mungu. Makosa ya ZAMANI yana NGUVU ya kuzuia MAFANIKIO yako ya sasa na ya baadae KIHUDUMA kama hujawa makini na kutafuta Neema ya kupona na MAMBO ya KALE.

Kwa upande mwingine, sio kila jambo jema laweza kuwa na USHUHUDA mzuri. Kwa lugha nyingine, sio tu kwamba USHUHUDA mmbaya ni kuanguka dhambini. Kuna mambo mengi sana katika mienendo na tabia ambayo Paulo alisema katika kitabu cha Warumi kua makini nayo. Kuna mambo IMEKUPASA kuacha kufanya kwa sababu ya UDHAIFU wa imani ya mtu mwingine sio imani yako. Mfano rahisi ni namna ya UVAAJI wa nguo. Watu wengi wameonekana kama WAHUNI tu kwa sababu ya aina ya nguo walizovaa na MUONEKANO wao katika mavazi hayo. Na wengine wamekua wabishi na kiburi hata wakiambiwa au wakionywa! Mungu atusaidie tusiwe KWAZO kwa namna yoyote. KUMBUKA kumpokea dhaifu wa imani na kumsaidia sio kumwangamiza kwa UDHAIFU wa imani yake eti kwa sababu sisi ni MIAMBA ya Imani. Hicho ni KIBURI.

NEEMA ya BWANA na IZIDI KWENU TANGU SASA na HATA MILELE. AMEN.

Frank Philip

Sunday, August 11, 2013

KUTOKA MADHABAHUNI......"BAADA YA KUSUBIRIA....HATIMAYE UTAMILIKI NA KUBARIKIWA!!"

SHALOM!
NAAMINI UNA JUMAPILI NJEMA HATA LEO!
SIKIA NENO LA BWANA TOKA MADHABAHUNI KWAKE KAMA VILE LINVYONENWA NA MCHUNGAJI WA VICTORY CHRISTIAN CENTRE (VCCT), MBEZI BEACH A, DAR ES SALAAM; DKT HURUMA NKONE!!


MAANDIKO; JOSHUA 1:29;11:23

Bwana Yesu asifiwe sana!
Leo ibaada yetu iko moja kwa moja kupitia Redio Wapo FM (98.1), na tutaendelea kuwa hewani moja kwa moja kupitia redio Wapo kila jumapili ya kwanza ya mwezi!

Habari hii inawahusu wana waisraeli wakiwa safarini kwenda nchi ya Ahadi chini ya Uongozi wa Joshua baada ya Muda wa Musa kuisha.
Na hapa Joshua alikuwa akipewa maagizo na mazingatio ya muhimu...Itakuwa mtakapotia miguu yenu kukanyaga nchi ile itakuwa mikononi mwenu, na muwe hodari na moyo wa ushujaa kwa maana ni haki yenu.

Wana waisraeli wakiwa na Joshua walishuhudia miujiza mingi pia ukiwapo ule wa Maji ya mto Yordni kugawanyika na wao kuvuka naam baada ya hapo Joshua na wanawaisraeli walianza kwa kuteka Yeriko na miji mingine mitatu mikubwa ya kati na kwa gia hii walikuwa wana nguvu ya kutosha kuendele kuichukua nchi nzima maana walikuwa wana mkakati bora.

NINI MUHIMU MAISHANI MWAKO SASA;
Ulipookoka umefanikiwa kuingia nchi ya ahadi; lakini bado ipo kazi ya kuendelea kuteka na kuchukua baraka zako...maana hapo kwanza kabl hujaokoka vilikuwa vinamilikiwa na shetani. Ni kweli umeweza kutikisa kuta za Yeriko na zimebomoka....naam usiishie hapo unapaswa kuendelea kuteka na kuteka mpaka hapo utakapomiliki nchi yako nzima...naamanisha ulimwengu wa wokovu wako.

 Lazima wakristo tubadilike...tuache kuamini maombi tu katika kila jambo bila kufanya jambo lingine lolote...kwa mfano hauwezi ukaomba upandishwe Cheo kazini na hali unaendelea kuchelewa kazini na kufanya uzembe mwingine haiwezekani....kama ukitimiza wajibu wako na kufanya yote yakupasayo kw haki na kwa bidiii, kwa hakika utapokea tu toka kwa Bwana...maana maandiko yanasema....KAMA MKITII MTAKULA MEMA YA NCHI!

Kumbuka hatuokoki ili tupate vitu fulani kwa Bwana kama vile fedha, majumba, waume na wake ama watoto, ila tunaokoka kwasababu tumechagu kumpenda Bwana na ukishaokoka na kuwa mwaminifu basi vyote hivyo unavyovistahili vinakujia kwa kujaa na kusukwa sukwa.

UJUMBE KWA VIJANA;
Lazima ujifunze kutulia na kusubiri,haiwezekani utoke chuo leo na utaka uendeshe Range Rover,acha kutamani kila kitu...ikiwa unavistahili basi ujue kwa hakika muda ukifika lazima utamiliki tu...vinginevyo utaumia sana ukitaka vitu visivyo saizi yako.

Natamani kama ungemtukuza Bwana katika maisha yako kwa namna ambayo watu watajiuliza wewe ni mtoto wa nani,maana ulimwengu umezoea watu wamnaopenya ni wale wenye watu wakubwa serikalini....Baraka yako ipo maana Mkono wa Mungu uko juu yako....na lazima ujue jambo moja kuwa penye Vita yako ndio penye baraka yako!

SEMA SALA HII KWA IMANI;
EEH BWAN YESU, NINAKUSHUKURU KWA NENO LAKO NA MTUMISHI WAKO, NIMESIKIA NA NIMEAMINI,NAAM NATAMANI NENO HILI LIWE HALISI MAISHANI MWANGU,NISAIDIE NIKUSIKIE KWA KINA ILI NIJUE NINI KINACHONIPASA KUFANYA KILA SIKU, MAOMBI YANGU LEO NI KUWA BWANA UNISAIDIE KILA WAKATI KUKUMBUKA KUWA VITA NI YAKO NA SIO YANGU,NIPE NEEMA YA KUWA NA SUBIRA NA KUSUBIRI BARAK YANGU, NISAIDIE KUITUMIA AKILI YANGU NA UTASHI ULIONIPA ILI NISIZEMBEE KIMKAKATI, AHSANTE YESU KWA MAANA KILA HATUA UTAKUWA NAMI,AHSANTE YESU KWA KUNISIKIA, KATIKA JINA LA YESU KRISTO,AMEN!!!

MUNGU ATUSAIDIE TUNAPOENDELEA KULITAFAKARI NENO HILI KUWA KILA MAHALI AMBAPO BWANA AMETUPA KUKANYAGA KATIKA ULIMWENGU W ROHO NA WA MWILI BASI HAPO AMETUPA KUMILIKI,NAAM UTAPATA VYOTE UNAVYOVISTAHILI KAMA UKIWA NA IMANI SAHIHI NA PIA UJUE VITA SIO YAKO BALI VITA NI YA BWANA, AMEN!

Mungu awabariki sana!!

Imeandikwa na
King Chavala MC
+255 713 883797

Saturday, August 3, 2013

KUTOKA MADHABAHUNI LEO.......NGUVU YA MATOKEO YA UKIRI WAKO!

Shalom!
Naamini uko vizuri na jumapili hii ni nzuri kwako,amen!
Ubarikiwe na uzidi kubarikiwa sawasawa na neno la Mungu lisemavyo.
Leo neno kutoka madhabahuni,linatoka madhabahu ya TAG CAPITAL CHRISTIAN CENTRE (CCC) DODOMA kama linavyonenwa na Baba Askofu Mch SAMSON MKUYU
ASKOFU MCH.SAMSON MKUYU WA TCCC, DODOMA


Neno 
  Mithali 23:7 .....Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo
  Warumi 10:9......kwa kinywa mtu hukiri na kwa moyo mtu huamini......
Waefeso 3:20....
Wagalatia 5:9....

Somo; NGUVU YA MATOKEO YA UKIRI

Maisha yetu yenye matokeo ya kuwafanya wengine kupata tafsiri ya maisha mazuri yanategemea sana na ukiri wetu.
Maandiko yanasema aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, hii inamaanisha vile ulivyoujaza moyo wako navyo,kwa maana nyingine yale unayoyawaza na kuyafikiri kila wakati ndio hayo yanaongoza na ukiri wake wake kila siku.
Ukijaza moyo wako na uchafu,udhaifu na uzembe basi kila wakati utalaumu na kunung'unika na kukiri udhaifu maishani mwako na kama ukijaza moyo wako na Neno la Mungu na habari njema basi ukiri wako utakuwa ni kushinda na kushinda kila leo.

UKIRI HUZAA IMANI
Ukisema mimi ni masikini na akili yako inasikia na kudaka hiyo na wanahusika na hilo pia wanasikia na wanakuwa na nafasi ya kulifanyia kazi ili vile ulivyokiri iwe imani na iwe kweli.
Lakini ukisema mimi ni mshindi basi na akili yako husikia na kudaka hivyo na wote wanaohusika na hali hiyo lazima imani yako iwe hivyo.

Sikia hii ....KWA KINYWA MTU HUKIRI NA KWA MOYO MTU HUAMINI
Ukiri wa kinywa chako una nguvu sana na ndio hufanya moyo wako kupata imani ya yale uliokiri.

MIMI ZAMANI NILIMWAMINI BWANA KWA MAMBO MAKUBWA NA BADO NAENDELEA KUMWAMINI,KILA MWAKA AHADI YANGU YA KUMTOLEA BWANA INAENDA IKIPANDA,KUNA WAKATI TULIKUWA TUNAENDA KAMBI YA MAOMBI MAHALI FULANI NA ILITUPASA KUBEBA VYANDARUA,LAKINI MIMI NILIMWAMBIA BWANA (nilikiri na kuamini) MBU YEYOTE ATAKANIUMA AONYE UCHUNGU NA HATA KAMA NA WADUDU WA MALERIA WASINIPATE.....NA ILIKUWA HIVYO NA BADO NAMWAMINI BWANA HATA LEO.

MAMBO YA MUHIMU;
1. Chunga sana kinywa chako na linda moyo wako
2. Jifunze kutamka yale uyaamiyo na usindi uutakao,hata kama hali yako ya sasa haiendani na yale uyatazamiayo.
Usiache kusema....NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU!
3. Unaweza kuwatania watu na ndoto zao lakini usifany utani na Bwana maana Mungu hataniwi
4. Na kila unapokiri kumbuka unatangaza vita hivyo usiruhusu shetani akuletee mawazo mengine.

.....Atukuzwe yeye awezaye kufanya zaidi ya yale tuyawazayo na kuyafikiri kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.

SISI WACHUNGAJI TUMEZOEA KUWATUBISHA WATU DHAMBI WAKATI WAO WAKIMPOKEA KRISTO,LAKINI HUWA TUNASAHAU KUTUBU JUU YA VINYWA NA MIOYO YETU NA KUWATUBISHA HAO JUU YA MAMBO MAWILI PIA.

RUDI SASA KWENYE YALE MAKABRASHA NA MADAFTARI YA NDOTO ZAKO NA UANZE KUKIRI YALE UNAYOTAMANI KUWA NAYO HAPO BAADAE KUANZIA SASA.

BWANA NA AKUBARIKI SANA NA AKUSAIDIE KUCHUNGA KINYWA CHAKO NA MOYO WAKO,KATIKA JINA LA YESU AMEN!

Imeandikwa na
King Chavala
Moja kwa moja toka Dodoma!
KANISA LA TCCC,DODOMA

Sunday, July 14, 2013

Kutoka Madhabahuni;......."CHOCHOTE KILICHOKUMEZA AU KUMEZA VITU VYAKO,KINAENDA KUTAPIKA!!!!

SHALOM!!
NENO LA MUNGU KUTOKA MADHABAHUNI LEO LINATOKA KATIKA KANISA LA VICTORY CHRISTIAN CENTRE,MBEZI BEACH A,DSM....mahali ambapo Mtumishi wa Mungu Askofu Rev. EDMUND KIVUYE from BUJUMBURA,BURUNDI amekuwa na Kongamanoi la siku mbili mahali hapo na Somo hili limekuwa ni Hitimisho la Kongamano hilo.
NAAM KARIBU UJIFUNZE NENO TOKA MADHABAHUNI!!
******************************************************************************
SOMA BIBLIA
<<Yona 2:10.......Na Mungu akamwambia yule samaki,na samaki akamtapika Yona nje ya bahari!>>

Mtumishi alianza kwa kusema....Chochote kilichokumeza lazima kitakutapika!

"AMEN" ni neno dogo sana lakini ni ufunguo mkubwa sana wa utayari wako kupokea muujiza wako....ni sawa kabisa na Ufunguo mdogo sana unaweza kufungua mlango mkubwa sana,hivyo ni muhimu kutumia ufunguo huo AMEN kila mara maishani mwako.

Unapokaa kwenye kiti lazima ujue kuwa huo ni muujiza na hivyo ukikaa kanisani lazima utegemee miujiza na wewe mwenyewe ni muujiza;Ukiristo sio maisha ya mazoea lakini ni maisha ya ufunuo na ufumbuzi kila siku.

USHUHUDA;
Mchungaji alisema mwaka 1992 mke wake aliwahi kuumwa na alipopelekwa hospitali akapimwa na kuambiwa kuambiwa ana matatizo ya nyongo na ni lazima afanyiwe upasuaji ili apone,lakini mchungaji akasema hapana mke wangu hawezi kupata kisu....basi kulikuwa na na kongamano fulani huko Uingereza naam,mchungaji akaomba ampeleke mke wake huko,na dakatari akamruhusu Mchungaji aende nae.....na huko kwenye kongamano Mchungaji/Muhubiri wa Kihindi alizaliwa Mombasa na anayeishi Amerika akasema KUna mwanamke mmoja hapa aliwahi kuumwa miaka kadhaa iliyopita na sasa anaumwa tena na kuna dhamira ya kumfanyia upasuaji....sasa amepona sasa.....Basi mchungaji huyu ambaye mke wake ni mgonjwa akaruka na kusema,AMEN!......Lakini wakati wa shuhuda mara mwanamke mmoja akapita na kusema amepona(na mchungaji akashangaa na kusema haiwezekani muujiza huu asiwe mke wangu)....basi akamtafuta sana mke wake na akamkuta amepumzika kwenye gari na basi yule mchungaji akamsimulia mke wake habari ile yote na mke wake akasema tu.....AMEN!......Na hata sasa ni mzima na hakuwahi kufanyiwa upasuaji tena,yaani muujiza wake ulipokelewa na neno,Amen tu!

Ikiwa yona aliyekuwa mkorofi lakini baada ya kuomba ndani ya tumbo la samaki,Mungu alimwamuru samaki amatapike....vipi wewe uliye mwana mwaminifu?

IKIWA UNATAKA MAMBO YAKO YALIYOMEZWA NA SAMAKI(ADUI).....BASI....OMBA!!!
Na kwa wale waliomba basi NA WASUBIRI!!

Usiruhusu watu kukukatisha tamaa kwa maneno na vijembe....eti oooh ulikuwa wapi kuomba awali hata unamsumbua Mungu sasa? au na wewe unafunga kweli? na mengineyo mengi!.....IKIWA MZAZI HAWEZI KUMFUKUZA AU KUMZIRA MTOTO AKIKOSA,HATA AKOSEE NAMNA GANI,VIPI KUHUSU MUNGU BABA WA MBINGUNI.....UKIWA TAABUNI HATA RAHANI BASI USIACHE KUKIMBILIA KWA MUNGU TU!!

Mtu hawezi kukusaidia ukiwa ndani ya tumbo la samaki ila Mungu tu aliyekuumba wewe na huyo samaki aliyekumeza.....Naam unaweza kuchangua Kumwamini Mungu Au ukaacha kumwamini kabisa na hata Biblia unaweza kuiamini au ukaacha....basi hata maishani mwetu kumejaa machaguo....Uzima na kifo ni kuchagua pia.....kufanikiwa na kushindwa ni  uchaguzi wako mwenyewe......kuzaliwa sio uchaguzi wako bali kufa masikini ni uchaguzi wako......basi watu wameamini kuwa kuwa MASIKINI NDIO UTAKATIFU!!....eti kwasababu maandiko yanasema Heri Masikini....lakini Biblia imesema Heri masikini wa roho na sio hali!

Maamuzi yako yanategemeana sana na habari ulizonazo....maana kile ulichonacho ndio kinakuongoza kufanya maamuzi!

USHUHUDA;
Kuna wakati mchungaji amewahi kushambuliwa na watu mbalimbali kwenye TV na redio na akaitwa kujibu tuhuma....lakini mchungaji akasema siji kujibu lolote maana sijisikii kujibu chochote,lakini kama inawezekana naomba dk 5 tu  nihubiri na wenye vyombo vya habari hivyo na wenyewe wakakataa kabisa....basi mchungaji akakaa kimya kabisa kwasababu hata bosi wake hakujibu kitu aliposhambuliwa (ingwa alijibu mara chache na kukaa kimya mara nyingi sana)
.....Na baada ya miaka minne sasa ni Mchunhaji pekee wa kanisa la mahali pamoja anayehubiri kwenye TV ya serikali na huo ni ushuhuda mkubwa na wengi wamejaribu kutafuta nafasi ya kuhubiri kwenye TV hiyo na wameshindwa maana mafanikio SIO PESA BALI NI MAAMUZI!!

Yakobo aliona mavazi ya Yusufu ambayo yalikuwa yamepakwa damu ya mnyama na ndugu zake na akaamua kuamini kuwa  Yusufu ameliwa na wanyama wakali.....hivyo unaweza ukaamua KUAMINI KWA YALE YANAYOONEKANA AU KUAMINI KWA YALE HALISIA(NENO LA IMANI)

KUMBUKA;
......Mara zote UONGO hupanda kupitia LIFTI lakini UKWELI hupanda kupitia NGAZI,japo ukweli huchelewa kufika juu lakini hufika na Uongo hupanda kwa spidi na kuanguka ni hivyo hivyo tu.

SASA AMUA KUAMINI KATIKA KWELI NA SIO UNACHOKIONA,MAANA UHALISIA UNAWEZA KUWA SIO SAHIHI SANA ILA KILA KWELI NI HALISI!!!

Kama samaki alikuwa na masikio ya kusikia,basi na wewe unaweza kuongea na chochote na kikakusikia....anza sasa kusema na nyumba yako au gari yako(iambie iache kula hela yako ya gereji kila siku),sema na chochote na uamini naam utapata.

ACHA KUWA MWANA DIPLOMASIA MBELE ZA MUNGU,HEBU KUWA HALISI!!
Acha maneno ya kuzungukazunguka JUST GO STRAIGHT TO THE POINT!!!

MFANO;
Hivi kama batimayo baada ya kuita YESUUUUUU MWANA WA DAUDI NIHURUMIE...na baada ya Yesu kusimama,vipi kama Batimayo angeaanza Samahani sana Yesu,samahani nimekusumbua na najua una kazi nyingi lakini........naamini Yesu asingemuelewa,lakini alisema tu NATAKA KUONA TENA!!!

STORI 1;Mungu yupo na unaweza kuamini kuwa yupo na ukamwamini au ukaacha kabisa kumwamini.....Ni kama vile watu wasemavyo oooh hakuna Mungu kabisa,maana kama angekuwepo magonjwa na matatizo yasingekuwepo.....lakini hiyo sio kweli maana uwepo wa watu walio na manywele mengi sana huko mitaani haimanishi hakuna vinyozi....NA MUNGU NDIO HIVYO ALIVYO!

STORI 2;Na kuna wakati RAIS amewahi kutembelea magereza na kuwakuta wafungwa watatu na mheshimiwa akaamua kuuliza ili apate kujua nini hasa watu hawa wako gerezani..KWANINI UKO HAPA..basi majibu yao yalikuwa hivi;
Mfungwa 1; Mimi niko hapa kwasababu mimi sio wa hapa na watu hawa wameamua kunionea...mmmh okey(Rais akajibu)
Mfungwa 2; Mimi ni masikini ndio maana niko hapa,kama  ningekuwa na fedha nisingekuwa hapa...
na Mfungwa 3; Akasema mimi hapa nilipo ni kwa neema tu....basi Raisi akashtuka na kuuliza kwanini,ina maana unafurahia kuwa hapa?....basi yule mfungwa akasema Kweli nimefanya mengi sana mabaya na ilinipasa kufa vibaya lakini nimehurumiwa na kuwekwa hapa.....Basi Raisi akapendezwa na mfungwa huyu na kuamuru aachiliwe ili asije akawachafua wale wasafi....NA HUO NDIO ULIKUWA UHURU WAKE!!!

NA SASA NATAMANI UJUE KUWA UNAWEZA KUAMINI UWEPO WA MUNGU,UNAPASWA KUAMINI NENO NA KUCHAGUA KULIAMINI MAISHANI MWAKO....KUWA HALISI NA MWAMINI BWANA BILA MASHAKA! UWE MUWAZI MBELE YA BWANA.....AMUA KUSAMEHE KILA ALIYEKUKOSEA,NAAM CHAGUA KUTII AMRI HIYO YA MUNGU YA KUSAMEHE!!!

CHOCHOTE KILICHOKUMEZA,NA KIKUTAPIKE SASA....KATIKA JINA LA YESU,AMEN!!!

(Na ibaada hiyo iliisha kwa maombi mazuri sana na Mungu pia akusaidie na wewe uwe na wakati wa kuomba mara tu baada ya kusoma neno hili....tamka neno la msamaha kwa waliokukosea naam sema na samaki huyo aliyemeza mambo yako!!!...endelea....kuomba......)

KARIBU TENA NA TENA,UJIFUNZE NENO LA MUNGU HAPA!!

Imeandikwa na
Na Mwl.Fredy E.Chavala
+255 713 883 797

Wednesday, April 3, 2013

Kutoka Madhabahuni>>>...."MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI NA UPATE MAFANIKIO"(02)

SHALOM!
Ninatumai wote tu wazima na tumesherekea vyema sikukuu ya kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo!
Jumapili hii hatukuwaletea somo toka madhabahuni,badala yake kuna somo kuhusu NGUVU YA KUFUFUKA KWAKE,ambalo utalisoma muda si murefu!

Leo nataka niendelee kidogo kuhusu KUMJUA MUNGU!!

Rejea somo la kwanza
http://gospelstandardbase.blogspot.com/2013/03/kutoka-madhabahunimjue-sana-mungu-ili.html


SASA ENDELEA!!

Nini maana ya KUMJUA MUNGU...TENA SANA?

Kumjua Mungu ni kufahamu zaidi kuhusu kwanini amekuumba,kusudi lako na anatarajia nini kwako...huwezi kujiuliza kwanini Mungu yupo ila unapaswa kujiuliza kwanini wewe upo,Mungu amekuandikia baraka nyingi sana ambazo utazipata tu ukifuata kila agizo akupalo....kumjua Mungu ni kujua neno lake,kushika amri zake,kuelewa hukumu zake,kufahamu kuhusu mamlaka yake na zaidi kujua nafasi yako katika yote hayo!!!
Ukisoma katika Kumb 28...Biblia inasema Itakuwa utapoyashika na kutunza na kufanya maagizo yangu yote baraka hizi zitaambatana nawe!!

Ukimjua Mungu utamfanya wa kwanza katika kila kitu ufanyacho na wala kamwe hutatamani ya duniani zaidi yake na ndio maana mahali pengine katika Mathayo akasema...Mtafuteni kwanza Mungu na haki yake yote na hayo mengine(ambayo mnayo) mtazidishiwa!!

SASA KWA KADRI UNAVYOMJUA MUNGU,NDIO UNAZIDI KUJUA SIRI NYINGI ZA MUNGU,NA HAPO BIBLIA INASEMA.....ILI UWE NA AMANI!

AMANI hii inayozungumziwa hapa sio utulivu kama ulimwengu huu,hapana! bali ni uhakika wa kipekee ukaao ndani ya moyo wa mwamini aupatao katika neno la Mungu pekee!!
Yesu alisema...Amani yangu nawapa, amani yangu nawaachieni,niwapavyo mimi si kama ulimwengu utoavyo! Maana yake ni kuwa amani hii nim zaidi ya amani ya ulimwengu...ni kama vile ulimwengu na sayansi ama ugunduzi unasema kutakuwa na janga ama tatizo fulani,lakini wewe ukisoma neno unagundua kuwa tatizo hilo halikutishi wala kukusumbua kwa kuwa wewe ni mtoto wa Mungu na unalindwa na Mungu na zaidi unayo mamlaka katika ulimwengu wa roho,na hivyo ukiwa na uhakika huo,utakua na amani tele hata kama ukiwa katkati ya watu wasio na amani hata kidogo!!

NA HAPO SASA MAANDIKO YANAMALIZIA KWA KUSEMA...NA NDIVYO MAFANIKIO YATAKAVYOKUJA!!

Mafanikio kibiblia sio mali wala pesa ama vitu vya kuonekana,bali ni baraka ya ukamilifu na utimilifu wa ndoto au mipango fulani aliyo nayo mtu. Afya njema,kukua kiroho,matumizi ya karama za rohoni,kujua kusudi,ulinzi na utulivu ni moja ya mafanikio makubwa sana,hayo magari na majumba huja tu maana ni matokeo ya mafanikio ya rohoni! Sasa shida moja ni kuwa watu wengi hukazia macho kwenye vitu na kusahau mmiliki wa vitu hivyo ambaye ni Mungu mwenyewe!!

KWA HIYO KUMJUA MUNGU NDIO UFUNGUO WA YOTE....KWANZA UNAPATA AMANI YA KUTOSHA NA UHAKIKA WA KILA KESHO NA JUU YA YOTE NDIO UNAYAONA MAFANIKIO MENGI MBELE YAKO!!

KUMBUKA;
Hutumtumikii Mungu au kuokoka ili tubarikiwe au tuwe matajiri,ila ukimtumikia Mungu kwa uaminifu Kufanikiwa na kubarikiwa hakuepukiki!!
BASI MUNGU ATUSAIDIE ILI TUONGEZE JUHUDI YA KUJUA ZAIDI KUHUSU MUNGU NA SIRI ZA NGUVU ZAKE,MAANA NDIPO ILIPO BARAKA YETU!
MUNGU AKUBARIKI,AMEN!


SOMO;
Na Mwl. Chavala,Fredy E.
+255 713 883 797

Sunday, March 24, 2013

Kutoka Madhabahuni>>>...."MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI NA MAFANIKIO"

MJUE SANA ILI UWE NA AMANI NDIVYO MEMA  YATAKAVYOKUJIA(01)

SHALOOOOOOM!!
NAWASALIMIA WOTE KATIKA JINA LA YESU KRISTO!
NINATUMAINI UNAENDELEA VIZURI NA MUNGU BADO NI MWEMA SANA MAISHANI MWAKO!
LEO JPILI YA TAR 24 APRIL 2013, NINAWALETEA NENO TOKA MADHABAHUNI MWA BLOG HII NA Mwalimu FREDY E.CHAVALA!
MISINGI YAKE INAJENGWA KATIKA MAANDIKO HAYA

Ayubu 22:21..."Mjue sana Mungu ili uwe na Amani ndivyo Mema yatakavyokujia."

UTANGULIZI;
#Neno hili liko wazi sana na yamkini umewahi kusoma hata maandiko haya mara nyingi sana,lakini ukijua undani wa maneno yake yamkini ukajengeka zaidi,
Neno "MJUE"- Lina misingi miwili M-JUE,M-inakuonyesha msisitizo wa Agizo, na JUA ni hali ya kujifunza ama kufahamu jambo kwa juhudi au kwa bidii, Kwa hiyo MJUE maana yake Tumia juhudi kufahamu zaidi kuhusu Mungu na maandiko hayakuishia hapo,bali yamesema "Mjue sana", maana yake mbali na msisitizo wa neno MJUE bado unasisitizwa SANA....
#Na zaidi maandiko yanasema..."ili uwe na  AMANI",maana yake Kwa kadri unavyomjua ndivyo unavyozidi kuwa na AMANI.....
#Na mwisho maandiko yanasema.."Ndivyo MEMA yatakavyokujia"... na hii inadhihirisha kuwa Ukiwa na Amani ndio unaweza kuona mafanikio/mema!

Kwa Ujumla andiko hili lina maana hii;
KWA KADRI UNAVYOJITAHIDI KUMJUA MUNGU>>>>NDIVYO UTAZIDI KUWA NA AMANI>>>>NA KWA KADRI UNAVYOZIDI KUWA NA AMANI,NDIVYO UTAZIDI KUFANIKIWA!!!

SHULE YA NENO;
Unaweza kuwa unajiuliza sasa kumjua Mungu ndio kufanyaje...Kumjua Mungu ni kufahamu Yeye ni nani kwako,kwanini amekuumba na anakutaka ufanye nini ukiwa duniani,zaidi anataka ufanye nini kwa wanadamu wenzako na Ulimwengu ufanye nini,na hapo utajifunza Vipao mbele vya Mungu,Amri na makatazo yote,ahadi,zawadi na malipo ya kila............

.......ITAENDELEA!!!


Sunday, February 17, 2013

Kutoka madhabahuni>>>HATMA (DESTINY)

SHALOM!
NAAMINI UKO SAWA NA BADO YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO!
HATA KAMA UNAPITIA MAMBO MAGUMU NATAKA NIKUTIE MOYO KUWA NEEMA YA MUNGU INAKUTOSHA NA USHINDI WAKO UKO DHAHIRI,JITAHIDI USIZIMIE MOYO,WEWE MWAMINI KRISTO TU!!
LEO TUNAPATA NENO TOKA MADHABAHU YA VICTORY CHRISTIAN CENTRE TABERNACLE(VCCT), MBEZI BEACH A KWA MCHUNGAJI DK HURUMA NKONE!
Na kabla YA Neno leo walikuwepo THE VOICE ambao wameimba wimbo wao "MAVUNO" na pia akaimba mwimbaji mwingine pamoja nao aitwae "ANGEL MAGOTI"


SOMO/MAHUBIRI YA LEO: "HATMA"
<<Mwazo 22:1-24>>
Hii ni habari ya Abrahamu na lile jaribu la Mungu kwake kuhusu kumtoa mwanae ISAKA kama sadaka ya kuteketeza, na jambo la kipekee ni kuwa Abrahamu hakumzuilia hata kidogo mwanae bali aliadhimia na kukubali kumtoa kwa Mungu,na Mungu hakusema neno mpaka alipoona uhakika wa Imani yake kwa Mungu na hapo Mungu akampatia mbadala wa sadaka na Kumwita Abrahamu "BABA WA IMANI" na yeye Abrahamu akayaita yale madhabahu "MUNGU MPAJI"(JEHOVA YIRE)

Mchungaji alianza kwa kusema:
UNAPOZUNGUMZIA HATMA,UNAZUNGUMZIA MWISHO HALISI ULIOKUSUDIWA, NA HAPA TUNAJIFUNZA MAMBO KADHAA KAMA
MUNGU ANAPOKUELEKEZA MAHALI PA KWENDA,HAKUPI HABARI KAMILI KWA WAKATI MMOJA,BALI HUWA ANAKUPA KIDOGO KIDOGO.......endelea!!!


sikia>>>MUNGU AKIKUPA HATMA(DESTINY) YA KWENDA HUWA HAKUPI MAAGIZO YOTE KWA WAKATI MMOJA LAKINI YEYE HUTOA MAAGIZO HAYO KWA HATUA,HIVYO UNATAKIWA KUTII NA KUCHUKUA HATUA YA IMANI NA KUFUATA YALE ULIYO NAYO MAANA MWISHO WA MAAGIZO YA KWANZA LAZIMA KUNA MAMBO YA PILI……Watu wengi hawako katika utumishi waliotiwa kwasababu wanataka kupata maagizo yote kabla ya kuanza safari ya utumishi wao.

ABRAHAMU ALIPOPATA MAAGIZO YA MUNGU,HAKUTAKA KUMSHIRIKISHA MTU HATA MKEWE,MAANA LAZIMA MKEWE ANGEMBISHIA TU….KIBINADAMU HATA KAMA UNGEKUWA WEWE LAZIMA UNGEGOMA TU,INAKUWAJE MUNGU ASEME ATAMFANYA ABRAHAMU BABA WA MATAIFA HALAFU AMTAKE MWANAE WA PEKEE ISAKA KAMA SADAKA?.....Hata wewe sasa Mungu akikupa maagizo unatakiwa kuyafuata na mara nyingine huhitaji kuwashirikisha watu maana mtu asiyeona hawezi kukushauri ushauri chanya!

JAMBO LINGINE LA KUSHANGAZA NI KUWA HATA ISAKA ALIKUWA MTII SANA KWA BABA YAKE IWAANDISHI WA HISTORIA WANASEMA ALIKUWA NA UWEZO WA KUMBISHIA BABA YAKE LAKINI ALITII HATA MWISHO MAANA ALIAMINI BABA YAKE ANAMPENDA NA NI MTUMISHI WA MUNGU,INGAWA ALIULIZA BABA SADAKA IKO WAPI? NA ABRAHAMU AKAMWAMBIA BWANA ATAJITWALIA MWANAKONDOO HUKO HUKO!....Sio kila mara unahitaji kubishana,wakati mwingine unahitaji kutii,maana sio kila maagizo ya Mungu hupitia njia nyepesi,na jambo la kuzingatia ni moja tu….SAUTI YA MUNGU ndio DIRA YETU,hivyo lazima uwe msikivu sana kusikia sauti ya Mungu kila hatua!!

ABRAHAMU ALIPOFIKA MLIMANI NA KUANDAA MADHABAHU,AKAMFUNGA MWANAE NA MARA ALIPOTAKA KUCHINJA SAUTI YA MUNGU IKAMWAMBIA,USIMCHINJE MWANAO ISAKA,TAZAMA PEMBENI KUNA MWANAKONDOO,HUYO MCHUKUE NA UMCHINJE,BASI ABRAHAMU AKAMFUNGUA MWANAE AMBAE NDIO MBEBA HATMA YAKE NA HATIMAYE AKAMTOA YULE MWANAKONDOO KAMA SADAKA,NA MAHALI PALE AKAMJENGEA BWANA MADHABAHU NA KUPAITA “YIRE” MUNGU MPAJI! NA ZAIDI ABRAHAMU AKAITWA BABA WA IMANI……Hata wewe unaweza ukafika mahali ambapo unaweza kuwa umeinua kisu juu kwasababu ya maagizo na mafunuo ya kale upate kuchinja na kumbe hicho unachotaka kuchinja ndio HATMA YAKO, sasa imekupasa kuwa makini na kuwa msikivu sana wa sauti ya Mungu,maana pale penye jaribu ndipo palipo na upenyo wa kutokea!

MSISITIZO MKUU NI KUWA MUNGU AMEMKUSUDIA KILA MTU HATMA YENYE MATUMAINI MEMA NA UTUKUFU MKUBWA IKIWA TU UTAAMINI NA KUTII NA KUFUATA KILA AGIZO LA MUNGU MAISHANI MWAKO BILA KUJIULIZA ULIZA!
MUNGU AKUBARIKI UNAPOENDELEA KUMTUMIKIA KWA UAMINIFU NA ROHO MTAKATIFU AKUFUNDISHE ZAIDI NA KAMA BADO HUJAMPOKEA YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO,BASI ZINGATIA KUMPOKEA SASA,KATIKA JINA LA YESU,AMEN!!

BY FREDY E. CHAVALA!!

Sunday, February 3, 2013

Kutoka Madhabahuni leo>>>NGUVU YA MUNGU KATIKATI MATATIZO ULIYO NAYO!!!

Shalom!
Natumai leo ni jumapili njema kwako na Mungu bado ana mambo anayafanya katika maisha yako!
Jumapili ya leo,Tunapata Mahubiri kutoka madhabahu ya Victory Christian Centre Tabernacle(VCCT) na Mchungaji Dk. Huruma Nkone(Mchungaji kiongozi)!
Akiwa ametoka ziara ya kitumishi nchini Sweeden leo ni jumapili yake ya kwanza na analo neno la kukujenga toka Katika maandiko matakatifu

Somo; Yohana 11:1-16,24-26
Hii ni ile habari ya Yesu na wale marafiki zake watatu waliofiwa na Ndugu yao Lazaro na ingawa Yesu alipata habari za kuumwa kwake,na hatimaye kufa kwake,bado hakuja haraka na Martha na wenzake iliwachanganya sana,kuona kwanini Yesu awaponye wengine huko na kwanini asije kumponya ndugu yao na hata saa alipokuja walimpokea kwa maneno ya kujifariji,Walimwambia umeshachelewa na hivyo amekwishakufa na tumemzika...Yesu alijibu Ugonjwa huo sio wa Kifo,na zaidi akasema Mungu atamfufua tu,bado wale ndugu hawakumuelewa Yesu na hiyo Martha alijifariji kwa kusema.....Najua atafufuka siku ile ya mwisho,lakini Yesu akasema Siyo siku ya mwisho ila leo!!

Mchungaji aliongea mambo matatu muhimu,katika somo lake la leo
1.ALISISITIZA; SIO KILA JAMBO GUMU MBELE YAKO NI LA KUKURUDISHA NYUMA AU KUUA MAFANIKIO YAKO...ila mengi huambatana na baraka ya kipekee,akasema usione mtu ana heshima au baraka fulani mara ukatamani kuwa kama yeye,bila kujua historia ya maumivu ya utukufu huo,hivyo tamani Bwana akupitishe katika mapito na mateso kwa ushindi wa utukufu huo ulio mbeleni....kama ambavyo kifo cha Lazaro kilikuwa ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu,basi na kwako yote yaliyokufa yawe ni kwa utukufu mwingi sana uliyo mbeleni!

2.PILI; USIACHE KUKIRI USHINDI HATA KATIKATI YA MATATIZO AU CHANGAMOTO ULIZONAZO AU UNAZOPITIA...kama ambavyo martha hakukata tamaa wala kulalamika na kwako iwe hivyo....wengi wakibanwa huanza kukiri kushindwa na kukiri matatizo mengine yaliyowahi kutokea huko nyuma,nataka nikutie moyo kuwa haijalishi ni magumu kiasi gani unapaswa kukiri ushindi na yale uyatazamiayo mbeleni....usiseme mimi ni bogus au wazazi wangu ni masikini au mimi sijawahi kupata hiki ama kile...bali unapaswa kukiri ushindi na kamwe usitarajie kuwashirikisha watu matatizo yako,lazima watakuvunja moyo tu maana na wao wana makubwa zaidi ya hayo yako,kwahiyo kikubwa mtazame Mungu na usiache kukiri ushindi katika JINA LA YESU,AMEN!!

3.TATU NA MWISHO; IPO NGUVU YA KUFUFUA  LOLOTE LILILOKUFA MAISHANI MWAKO!...na kimsingi ndio msingi wa somo au neno la leo, yawezekana kuna mengi yamekufa,ama ndoto zako nyingine hazina matumaini,Lakini nguvu ile ambayo ilimfufua lazaro ndiyo hiyo itakayofufua vyote vilivyokufa maishani mwako na kama unaamini sema Amen!!

NA HILO NDILO LILIKUWA NENO LA LEO,NINAOMBA MUNGU BABA NA MWANA NA ZAIDI ROHO MTAKATIFU,AMBAYE NI MWALIMU NA MSAIDIZI AKUFUNDISHE KWA KINA NA KWA UNDANI MAANA SOMO HILI LINAHITAJI UTAFAKARI WA KINA NA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU MWENYEWE,AMEN!!

Na FREDY E. CHAVALA
KUTOKA VCCT!!

Tuesday, December 25, 2012

GoStaBa Blog...TUNAWATAKIA HERI YA NOELI NA FANAKA YA MWAKA MPYA 2013!!!

SHALOM!

NATUMAI UKO VEMA NA UNAENDELEA VEMA HASA WAKATI HUU WA MWISHO WA MWAKA!!

ASHANTE KWA KUENDELEA KUTUTEMBELEA,WEWE NDIO SABABU YA SISI KUONGEZA BIDII!!

KWA NIABA YA "GOSPEL STANDARD BASE" BLOG NA WATUMISHI WOTE WANAOWEZESHA MADHABAHU HII KUWEKO, TUNAWATAKIA HERI YA NOELI NA FANAKA YA MWAKA MPYA 2013!!

JITAHIDI SANA UMFANYE AJIVUNIE KUWA NA MTOTO KAMA WEWE UKIWA UNAWAKILISHA UFALME WAKE HAPA DUNIANI!!!

KARIBU TENA NA TENA!!!!


Fredy E. Chavala
President-Chavala Ideas Platform
+255 -(713/753)- 883 797 
Dsm

Sunday, July 29, 2012

KUTOKA MADHABAHUNI...KKKT DAYOSISI YA KONDE,USHARIKA WA FOREST,MBEYA MJINI!

SERMON: MPENYO WAKO UNATEGEMEANA SANA NA MWITIKIO WAKO!
                 (YOUR BREAKTHROUGH DEPEND ON YOUR RESPONCE)

                      Na Mchungaji MATHEW J. SASALI

Leo siku nzuri aliyoifanya Bwana,nimefanikiwa kuhudhuria ibaada ya kilutheri katika usharika wa Forest,Mbeya ambako leo ilikuwa sikukuu ya Vijana katika kanisa hilo,na mimi kama mmoja wa Waalikwa niliyehudhuria ibaada pamoja na Tamasha la kumsifu na kumwabudu Mungu!
Mchungaji Mathew Sasali ambae ni Manager wa Ushindi FM radio ndio alikuwa mchungaji mwalikwa na mnenaji wa leo, ambaye leo ametulisha neno hilo la Mungu!!


....Kumb 28:1->>
Itakuwa utakapoyashika,kutunza na kuyafanya maagizo ya Mungu yote,baraka hizi zitaambatana nawe...utabarikiwa......


.....Kumb 28:15->>
Na utakaposhindwa kutenda sawasawa na hivi nikuagizavyo,laana hii itaambatana nawe....


Maisha yetu ya kila siku yanategemea sana na vile ambavyo tunaitikia mambo yale yanayokuja mbele yetu,kubarikiwa au kulaaniwa kunatokana na sisi wenyewe na sio shetani,ni dhahiri kuwa watu wengi wanapendwa sana kubarikiwa ila hawapendi kuwa na uhusiano na huyo mtoa baraka!!


Wengi hudhani baraka huja kwa kuwekewa mikono au kuombewa na ndio maana hawachi kutanga tanga huku na kule wakitafuta baraka na kuacha baraka ambazo zinawazunguka.


Sasas leo nataka tuone msingi wa baraka na mpenyo katika maisha yetu!


MPENYO KATIKA MAISHA YETU UNATEGEMEA SANA JINSI TUNAVYOITIKIA KWA


              A.NENO LA MUNGU
Ni namna gani unatii na kulifuata Neno la Mungu?
Ni mara ngapi neno limekwambia fanya hivi na wewe ukafanya vile?
Ni dhahiri kuwa imani yetu huja kwa njia ya neno na imani hiyo haiwi dhahiri mpaka matendo yaonekane wazi...Kwa mfano katika Biblia kuna mifano ya watu wengi sana ambao walitii neno la Mungu na wakapata mipenyo katika maisha yao,naomba nimseme mmoja tu na huyu ni Jemedali wa Vita NAAMANI aliyekuwa na ukoma; alipewa wito na mjakazi tu kuwa katika nchi yao(yule mjakazi) yupo mtu anayeweza kuleta majibu kwa shida yake....tunaona katika maandiko kuwa jemedali huyo aliitikia na akaenda mpaka nchi ile kumwona mtumishi wa Mungu huyo...UNAFIKIRI NI WATU WA NGAPI WENYE VYEO NA HADHI ZA JUU WANAWEZA KUTII NENO LA WATU WALIO CHINI YAO???
Na alipofika huko mtumishi yule wa Mungu hakufanya lolote lile ila alimwambia nenda kajichonvye mara 7 ndani ya mto Yordani basi....kikawaida yule jemedali alihisi kudharauliwa na akataka kugoma kufanya hivyo lakini wasaidizi wake wakamwambia..kwani ukifanya hivyo utapungua nini? na vipi kama angekwambia jambo kubwa usingelifanya?...basi Jemedali alitii neno lile na akafanya kama mtumishi alivyosema na akawa mzima hata leo...kama huamini tukifika mbinguni nikumbushe tumtafute nikuonyeshe!!!


UNAYO NAFASI KUBWA SANA YA KUPATA CHOCHOTE AMBACHO BWANA ANATAKA UPATE LAKINI,HAKIKISHA UNAITIKIA KILA NENO LA MUNGU LINAKUJA MOYONI WAKO!!!


     B. KWA WATU
Mpenyo wako pia unategemea sana jinsi unavyoitikia miito mbalimbali ya watu, Je ni mara ngapi umepata wageni na ukashindwa kuwakirimu ipasavyo? ni mara ngapi unapata wageni lakini umekuwa ukiwapuuzia?
Jinsi unavyokuza uhusiano na kutunza urafiki na kutokuchoka kutenda wema kwa watu mbalimbali wajao maishani mwako ndio unavyojitengenezea mpenyo wako wa kesho....kwa mfano tu huo wa hapo juu unaona jinsi ambavyo Naamani aliitikia wito wa wajakazi wake,lakini pia kuna wakati Ibrahimu alipokea wagen watatu na akawakirimiia sana na wale ndio wakamwambia majira kama haya mwaka ujao mkeo atakuwa na mtoto..
ANGALIA NI WATU WANGAPI UMEWAPOTEZA KWENYE MTANDAO WAKO WA WATU WA MUHIMU NA MARAFIKI!!!


      C.KWA FURSA MBALIMBALI ZINAZOTOKEA KATIKA MAISHA YAKO
Unajua kama daudi hakuitwa kumuua Goliathi lakini aliposikia matusi kwa Mungu wake,akaona hii si nafasi ya kuikosa,hivyo akajitokeza bila kujali vipingamizi vya ndugu na umri wake na akasema yeye anaweza kumuua Goliathi na akafanya hivyo na akawa mfalme!!


HIVYO NDIVYO ILIVYO HATA KWAKO,UPATAPO NAFASI HADIMU ITUMIE VEMA YAMKINI NDIO MPENYO WAKO...IWE KWENYE BIASHARA,KAZI,MAISHA,SHULE NA MENGINE KADHA WA KADHA!!!


Ahsanteni sana kwa kushiriki nasi katika neno hili na MUNGU AWABARIKINI NYOTE MNAPOOENDELEA KUYATAFAKARI MANENO HAYA NA KUYATENDEA KAZI,AMEN!!!



Tuesday, May 1, 2012

START WORSHIPING BY MEDITATING THESE DOGMATIC TRUTH ABOUT YOUR GOD!!!

I WISH IF I COULD ELABORATE MY KING,BUT HE IS INDESCRIBABLY
WELL HERE I HAVE JUST TRIED!!
HE IS MY KING!!