Showing posts with label Teachings. Show all posts
Showing posts with label Teachings. Show all posts

Monday, January 26, 2015

MAMBO MATANO NILIYOJIFUNZA KUTOKA KWA PENSELI!!

MTENGENEZAJI WA PENSELI ANAYO MAMBO 5

NIYAPENDAYO,NA HAYO NI MAFUNZO KWA PENSELI NA SISI LEO!!!

Mtengenezaji wa PENSELI aliiambia penseli haya na mimi leo ninawaambia ninyi;

1.Eeeh PENSELI popote utakapogusa utaacha ALAMA (Haijalishi ni vizuri au vibaya)
>>>NA WEWE PIA KILA UNAPOPITA MAISHANI MWAKO UNAACHA ALAMA KWA WATU.

2.Eeeh PENSELI najua unaweza kukosea mara nyingi,basi usijali,juu yako upo MFUTO ili kufuta kila alama mbaya isiyotakiwa.
>>>NA WEWE PIA NAKUAMBIA HATA UKIFANYA MAKOSA KIASI GANI,MFUTO WA DAMU YA YESU UKO JUU YAKO.....Hakuna awezaye kurudi nyuma kuanza upya,ila pale ulipo panaweza kuwa hatua ya mwanzo mpya!

3.Eeeh PENSELI,Kitu cha muhimu sana kwako ni kile ambacho KIKO NDANI YAKO(Risasi ya graphite),Hata kama uwe na umbo ama umbile lenye mapambo kiasi gani!
>>>NA WEWE PIA TAMBUA YA KUWA KUSUDI LA KUISHI NDANI YAKO NDIO MUHIMU SANA MAISHANI MWAKO KATIKA KUMPENDEZA MUNGU,YAANI LILE MUNGU ALILOKUANDIKIA na haya mengineyo ya nje ni mbwembwe tu!

4.Eeeh PENSELI Hauwezi kuandika vizuri mpaka ukubali KUCHONGWA VIZURI ili uwe sharp(sio ombi unless unataka kuwa pambo)
>>>NA WEWE LAZIMA UJUE JAMBO MOJA KUWA ILI KWENYE MAISHA YAKO UUFURAHIE MWITO WAKO,LAZIMA UKUBALI KUCHONGWA AMA KUPITIA MAGUMU ILI UJIFUNZE KUKUA NA KUKOMAA.

5.Eeeh PENSELI pamoja na yote hayo bado huwezi kuandika au kuifurahia kazi yako,ni lazima UKUBALI KUSHIKWA NA MKONO HODARI ili mwandiko au mchoro uwe bora!
>>>NA WEWE PIA LAZIMA UKUBALI KUSHIKWA NA MUNGU MWENYEWE NA KUFUATA NENO LAKE NA KILA AKITAKACHO NA HAPO NDIO UTAPONA NA KUWA NA FURAHA MAISHANI MWAKO!!!

Ubarikiwe sana kama umenielewa na ukiweza SHARE na wenzako wasome!!!

Na King Chavala MC
+255 713 883 797

Wednesday, December 10, 2014

KUHUSU KUSIFU NA KUABUDU-Sehemu ya 5(mwisho)


Shalom!
Yesu Kristo asifiwe sana!
Naamini uliyekuwa unafuatilia mfululizo huu umejifunza mengi na kubarikiwa pia,leo katika sehemu ya tano...Kuhusu kusifu na kuabudu, kama nilivyoahidi sehemu ya nne,tutaangazia mambo mawili makubwa;

I.NAMNA UNAVYOWEZA KUFANYA IBAADA YA SIFA NA KUABUDU!!
Kumfanyia Bwana ibaada,inategemeana sana na mahusiano yenu...yaani ningeweza kuwianisha na Mama na mwanae,namna ya kumlisha inategemea sana na urahisi wa mtoto huyo kula na kushiba, mwingine hula akipakatwa,mwingine hula akiwa anaoga, mwingine akiwa peke yake,muhimu ni kuwa mtoto amekula!!
Ibaada njema ni ile inayoanzia ndani ya kilindi cha moyo kabisa kwa upendo mkubwa,hivyo unaweza kufanya ibaada hiyo kwa namna nyingi,na hizi ni chache ambazo zimewahi kutumika na watumishi mbalimbali katika Biblia!
Unaweza Kumsifu na Kumwabudu Bwana:
1.Kwa kuimba,Iwe kanisani au popote pale-na hapa inaweza kuwa nyimbo za vitabuni, tenzi au zaburi au nyimbo mpya za kutoka moyoni mwako unapotafakari ukuu wa Mungu!
2.Kwa kupiga kelele-hii inaweza kuwa kelele zisizo na mpangilio au vigelege au miluzi au kelele zenye mpangilio wa nyimbo fulani!
3.Kwa kucheza -furaha ya mdundo unaoanzia ndani na sio ilimradi tu kuna muziki,na kwa habari ya kucheza unaweza kucheza hata kama hakuna muziki wowote
4.Kwa ubunifu na kazi za sanaa-mfano uchongaji,uchoraji, uigizaji na kazi nyingine za sanaa ambazo mwisho wa siku Ni Mungu ndio anasifiwa na kuabudiwa peke yake
5.Kwa kulala -unaweza ukalala namna yeyote ile kama ishara ya kujinyenyekesha mbele za Bwana
6.Kwa kupiga magoti
7.Kwa kukaa kimya mbele za Bwana
8.Kwa Kulia
9.Kwa kucheka
10.Kwa kunena kwa lugha nyingine,ziwe za duniani au lugha za kimbinguni!
11.Kwa kuomba
.....Sasa sifa na kuabudu inawiana na kuingiliana sana na maombi japo unaweza Kumsifu na Kumwabudu Bwana kwa maombi!!
Hizo ni chache katika namna nyingi,ambazo unaweza kujidhihirisha mbele za Bwana!!
Watu wengi wamechukuliwa na sifa na kuabudu ile ya kuimba na kucheza labda na kulia kanisani kwa maombi,na ni sawa tu!
Ila jambo la pili ni

II.NAMNA IMPASAVYO KUWA YEYOTE AKAAYE MBELE KUONGOZA WENGINE KATIKA IBAADA YA SIFA NA KUABUDU!
Wengi hufanya kama mazoea au utaratibu tu wa ibaada kwasababu wameshaguliwa au wamefanya mazoezi au wanajua au wana vipaji lakini ni zaidi ya hapo,imekupasa. Kuwa moyo mnyofu na Ibaada nzuri huanzia ndani yako kwanza kabla wengine hawajapotelea katika wingu,
1.Imempasa mtu huyu kuwa mtakatifu/mtauwa na anayempenda Mungu kiasi cha kupenda kumfamyia ibaada hata akiwa peke yake kabla hata kuwa mbele za watu
2.Imempasa kuwa na Neno la kutosha moyoni mwake,sio maandiko ya kukariri
3.Imempasa kuwa mwombaji, maana imempasa kusikia sauti ya Mungu wazi wazi ili awapo madhabahuni asifanye kwa mazoea
4.Imempasa kuwa na muonekano usioleta maswali kwa watu,yaani mavazi,mapambo na hata kutembea tu.
5.Imempasa kuwa na Amani na watu maana ikiwa mtu huyo ana Ugomvi au maneno maneno na watu,ibaada hiyo haiwezi kukamilika
6.Uongo,uzinzi,Umbeya, Unafiki na udhalimu wowote ule usitajwe kwake akaaye mbele za watu!...maana sifa na kuabudu kwa mwenye dhambi ni kelele mbele za Mungu!
7.Imempasa kuwa mnyenyekevu na aliye jaa hekima,na asiyejaribu kujitutumua au kujiona ni yeye na.bila yeye uwepo ule usingeshuka!
Lazima umaarufu, vyeo,elimu na hadhi viwe chini ya Utukufu wa Mungu,hivyo yeyote akaaye mbele za watu ajue kabisa kuwa yuko hapo kwa ajili ya Kumsifu na Kumuabudu Mungu tu na sio kuonekana!!
Mungu Roho mtakatifu akusaidie sote kuelewa sana zaidi ya maandishi haya,ili ibaada zetu za sifa na kuabudu, ikiwa ni za binafsi au mbele ya watu zipate kibali mbele za Mungu!
Mungu akuwezeshe na Mungu akunyenyekeshe ewe Mwabudu!!
Mpaka hapa Nimemaliza kwa habari ya Kusifu na kuabudu na ninayaacha kwako wewe kujifunza na kufundisha na kushare na wengine pia!!
*Najua utakuwa unajiuliza mbona hamna mistari ya Biblia,ndio! sitaki watu wanaokariri Nataka wanaoelewa!!!
Mungu akubariki sana wewe rafiki yangu!!
*Karibu sana katika Ulimwengu wa Kusifu na Kuabudu,kwa roho na kwa akili kwa kupenda!!

***MWISHO***
(c)King Chavvah, 2014
+255 713 883 797

KUHUSU KUSIFU NA KUABUDU-Sehemu ya 4


Shalom wana wa Mungu!

Wajoli na Wajeuri wa Bwana!
Tumekuwa na mfululizo wa kupendeza kuhusu sifa na kuabudu,na tangu tumeanza leo ni sehemu ya nne kati ya tano...na leo natamani kuzungumzia "Kwanini Sifa na kuabudu maishani mwetu" yaani muunganiko wa sifa na kuabudu na hatma za maisha yetu!
*Najua wengi tunajua Kusifu na kuabudu ni sehemu ya ibaada mbalimbali makanisani na ndio maana watu huanza kwa maombi,sijui matangazo kisha Kusifu na kuabudu, neno,sadaka na mengineyo Ila leo natamani nikujuze kuwa sifa na kuabudu ni zaidi ya hapo!!
Kusifu na kuabudu ni ibaada endelevu kila siku na kila mahali na kwa kila namna!
Ile ifanyikayo kanisani ni namna ya pamoja ya Kusifu na.kuabudu kwa upamoja na kwa utaratibu tuliojiwekea na kama watu wakibaki na picha hiyo pekee hawatafanya ibaada hiyo kwa ukamilifu!!! 

ZINGATIA UKWELI HUU!!
Kila mtu ameubwa kwa kusudi maalum hapa duniani na kila mtu amepewa uwezo fulani halisi unaomwezesha kufanya mambo yale yampasayo kwa urahisi kuliko yeyote mwingine(Yaani kwa mfano mimi sijitahidi kusheresha au kuchekesha maana ipo ndani naturally) na.uwezo huo huitwa kipaji na wazungu huongea kwa maringo zaidi "Gifts & Talents".....na kwa ujumla wake woote mambo haya ili tumwabudu Mungu!
Sasa kama tuna majukumu ya kufanya na hayo yote ni kwa ajili ya Kumwabudu Mungu na kuyafanya majukumu hayo ndio kuishi kwenyewe...tunaachaje kumwabudu Mungu??
Ile hali ya kujua kuwa hakuna jambo unaloweza kufanya kwa akili yako na uwezo wako binafsi na ule ukweli kuwa yote ufanyayo ni kwa utukufu wa Mungu....itakulazimu kuabudu tu,isipokuwa kama umeamua kuwa na Kiburi cha uzima na kujiona kama umejiumba mwenyewe!!
"Katika sifa Mungu hushuka" naamini umewahi kusikia sentensi hiyo Ila unadhani ni kwa ajili ya ile sifa ya kanisani pekee...Je hujawahi kusikia wale watu wa kale waliowahi kushinda vita kwa sifa?? Popote ambapo Yesu anasifiwa lazima uwepo wake uwe Kamilifu.... Sasa ukitaka mambo yako yaende sawia na kwa Ushindi lazima ukubali tu kujumlishia na Ibaada ya sifa na kuabudu!!

Kusifu na kuabudu ni kama vile kusema....MUNGU NI WEWE PEKE YAKO,HAYA YOTE NI YAKO,SHUKRANI TUKUZO NA SIFA ZOTE NI ZAKO,UMETUPA HIVI VYOTE KWA UTUKUFU WAKO,AHSANTE JEHOVA MAANA NI WEWE!!
Yaani kwamba sio kwa uwezo wako wala akili yako bali ni kwa Neema ya Mungu tu!!
Kusifu na kuabudu ni wakati wa shida na wakati wa raha,ukiwa na kusanyiko na hata ukiwa peke yako,ukiwa nyumbani na hata ukiwa mbali,kwa mavazi,muonekano, kelele, kula,kuongea,kufanya kazi na hata katika kujifurahisha!!
Muhimu kujua kuwa Umeumbwa ili umuabudu Mungu,utafundishwa kuwa mtumishi ama kuishi hatma yako au utafunzwa kuwa na ndoto au kuacha Alama itakayodumu ni sawa kabisa lakini msingi wa yote haya ni ili Mungu atukuzike..... Watu wamjue Mungu,waupokee Ufalme wake na wamuishi yeye....na hapo Ndio tunasema Maisha ya Ibaada,na.hiyo ibaada ndio Kusifu na Kumuabudu!!
Unaweza ukachoka Kumsifu alivyo mwema maishani mwako lakini kila uonapo watu wanakufa, wengine wanaumwa na hawa wapata shida....na hayo yawapatayo wenzio wewe huyashuhudii basi choka salama....na ukimjua Mungu sawasawa kuwa yeye hata nini kitokee duniani hakibadilishi Umungu wake...na kama ukijua ni baba yako,na AHADI zake kwako ni za milele,hutaacha kumuabudu leo kwasababu una mashida na machangamoto....Ila utamwabudu tu kwa kuwa yeye ni Mungu na tumaini lako la kesho maana ni hakika na Amina!
Mungu ni mwaminifu sana mara nyingine ni kiburi tu ndio huwa kinatufanya tumsifu na kumuabudu sana aitha tukiwa tuna vingi au tukiwa hatuna basi tunamlilia, na huo kwa hakika ni utoto!!
Basi Mungu akusaidie kuwa na maisha ya Kusifu na Kuabudu kila siku, kila wakati na kila mahali bila kujali nini wala nini na hakika uwepo wa Mungu hautapungua maishani mwako!!!
Kabla ya saa ile ya Agano nitamalizia sehemu ya tano na ya mwisho kwa habari ya mambo makubwa mawili;
i. Namna ambazo unaweza kufanya ibaada ya sifa na kuabudu
ii. Mambo yakupasayo kuzingatia uwapo mstari wa mbele katika kuwaongoza wengine katika sifa na kuabudu!!
Ahsante Bwana Yesu kwa kila asomaye na kuelewa somo hili,lisaidie Kanisa lijue kina na msingi wa Ibaada kuwa ni SIFA NA KUABUDU....maana hata Malaika, maserafi, makerubi,wazee 24,wenye uhai wa nne na Sisi watakatifu tuliyo duniani na hata saa ile ya mwisho kule mbinguni biashara ni moja tu "KUMSIFU NA KUMWABUDU MUNGU"
(Usiache kushare kwa marafiki zako)

+255 713 883 797

KUHUSU KUSIFU NA KUABUDU-Sehemu ya 3


Shalom ndugu yangu!
Naamini unaendelea vema na maisha yako na ninambariki Mungu sana kwa ajili yako na nimemwomba roho mtakatifu akusaidie kuendelea kuelewa somo hili!
Mara ya mwisho niliongelea mambo mawili makubwa kwanza ni Lazima Mtu anayetaka Kumsifu na.kumuabudu Mungu kweli lazima awe na uhusiano naye thabiti na pili katika sifa na kuabudu sio wewe au Kanisa au chochote kuinuliwa zaidi ya Mungu mwenyewe!
...Na nikaacha swali....JE NI VIUNGO VIPI HULETA UTAMU WA KUSIFU NA KUABUDU!!
Basi ninamshukuru sana Mungu kwa ajili yako na natamani niseme nawewe kwa habari ya uzuri wa sifa na kuabudu!
Sisi huwa tunadhani uzuri wa sifa ni Muziki(Melody),nyimbo tuzipendazo Sisi, mavazi yetu,mitetemeko ya waongoza sifa,machozi labda na mihemuko na hapo tunaweza kuruka na kucheza sana lakini hata kama Hayo yote huwepo au ni muhimu Ila msingi wa Utamu wa sifa na kuabudu ni haya yafuatayo;
1.Ibaada ya sifa na kuabudu yenye Utamu mbele za Mungu ni ile inayofanywa na Moyo wa kumpenda yeye,moyo Safi na wenye nia thabiti ya Kumsifu na Kumuabudu!!
2.Siyo nyimbo uzipendazo wewe ndio zinaleta utamu wa sifa mbele za Mungu,sio upendazo wewe maana sio kwa ajili yako Ila kwa ajili yake mwenyewe.... Ingawa ukizama sana utagundua kuwa kile roho mtakatifu anataka na wewe unaingiwa kupenda kile atakacho!!!
*Sasa natoa tahadhari tu.... Acha ubinafsi wa kutaka Kusifu na kuabudu kwa matakwa yako Ila msikilize sana roho ili mara zote umeona wingu lake!
3.Na tatu ni ile hamu ya kumtaka Mungu Atukuzike katika sifa na kuabudu ndio inafanya moyo wako uwe mnyenyekevu na kwa hakika Mungu ajidhihirishe na sio kuwa na hamu ya kutaka kusifiwa au kupongezwa baada ya uwepo kudhihihirika!
*Unajua Mungu akisifiwa hushuka lakini ile hamu yako ya kumuona Mungu zaidi na sio Kiasi wewe uonekane kama wewe ndio huwa unasifu na kuabudu mpaka uwepo unashuka!
4.Na mwisho;Ili ibaada ya Kusifu na kuabudu Iwe na tamu....Ni mara zote ikiwa unafanya ibaada ya sifa na kuabudu lazima uwepo umoja kati ya moyo wako au roho yako na nafsi yako na mwili wako lakini pia ikiwa mnafanya ibaada mkiwa wengi basi iwepo nia moja na mara zote muonekano wako, mkao wako na mavazi yako,yakupe nafasi ya kuwa na utulivu mbele za Mungu.... Haiwezekani ibaada ya sifa na kuabudu Iwe tamu wakati moyo na akili yako na nafsi yako havina ushirikiano....na huwezi kuwa huru kufanya chochote mbele za Mungu kama kucheza,kulia au kurukaruka hali mavazi yako yana thamani kuliko hiyo ibaada kiasi huwezi hata kupiga magoti,huwezi kucheza kwasababu ya hadhi au cheo chako au mavazi yako yanakubana au yanawakwaza wengine!!
Natamani roho mtakatifu akusaidie kuelewa haya,maana ibaada.ya sifa na.kuabudu ni ya Mungu mwenyewe na wakati wote kumbuka "ALITUUMBA ILI TUMUABUDU"
Basi wakati mwingine nitaendelea kuzungumzia kwa kina "Kwanini Sifa na kuabudu maishani mwetu? na nini uhusiano wake na makusudio ambayo Mungu alituumba nayo"


(c)King Chavvah, 2014
+255 713 883 797

KUHUSU KUSIFU NA KUABUDU-Sehemu ya 2



Shalom!
Naamini unaendelea vema hata leo,kama ulisoma sehemu ya kwanza(na kama bado nenda kwa wall yangu usome post yenye kichwa kama hiki )...nilianza kwa kujenga msingi wa Kusifu na kuabudu!
Na nikamalizia kwa swali...Nani mwabudu Mungu wa Kweli na imempasa kufanyaje???
LEO
Natamani kusisitiza mambo makubwa mawili tu katika sifa na kuabudu!!
Yaani haya yakae moyoni na kichwani mwa yeyote anayetamani kuugusa moyo wa Mungu kwa sifa na kuabudu,nayo ni haya;
1.LAZIMA KUMJUA NA KUMFAHAMU SANA HUYO MUNGU NA KUWA NA UHUSIANO NAYE.
Huwezi kufanya ibaada yeyote kwa Mungu ikawa ya maana kama unamsikia tu na humfahamu kabisa....imetupasa kumjua tena kumjua zaidi,tena kuwa na uhusiano naye wa karibu....maana kwa Kadri unavyomjua zaidi ndivyo unazidi kumpenda yeye na Kumsifu na kumuabudu kweli!....na hapo Ndio maandiko yanasema "Kusifu kwawapasa wanyofu wa mioyo"...Okey ngoja nitoe mfano huu,Kumsifu Mungu wakati hata hamna uhusiano wa karibu na sawa na kuona mjini gari aina ya Hammer ambayo iko mitaani kwenu na ukaanza kuwasimulia wenzio..."Oyaaa unaona ile hammer,yaani nyumba yetu hii unapita mtaa mmoja ndio nyumba ya mwenye gari ile aisee,yaani ile gari kali kishenzi yaani duh,Nyie Acheni tu mtaa wetu mambo Safi hahaha" sasa hapo wakikuuliza ni Tsh ngapi au umewahi kupanda au anakufahamu unabaki tu Aaah mmmm Oooh...Acha bwana hilo sio lenu, jivunie chenu...JIVUNIE MUNGU MAISHANI MWAKO,SIO KUMSIKIA TU!!
2.LAZIMA MUNGU PEKE YAKE NDIO AINUKE(AWE MAARUFU)
Yaani katika sifa na kuabudu usijitahidi kujiinua au kutaka kuonekana wewe au timu yenu au mchungaji wenu au Kanisa lenu Ila Mungu pekee Ndio wakuinuliwa!!
Kuna ukuta mwembamba sana kati ya kutafuta sifa na umaarufu au kujiona na unyenyekevu wa kutaka Mungu pekee Ndio aonekane!!
Tena sio kwa maigizo bali toka moyoni... Na ukiwa na moyo wa unyenyekevu utashangaa una Amani tele hata uende wapi au watu wawe kumi tu au vyombo visiwepo au sare zisiwepo hata usipopewa maji au nauli na popote ulipo kwa kuwa umeamua kumfanyia Mungu ibaada basi utashangaa sana udhihirisho wa nguvu za Mungu!!!
Tabia za kuonyeshana na watu ufundi wa Sauti au kucheza na kusahau kuwa malengo ni kumuabudu Bwana basi hapo ibaada yote huwa sifuri maana tumejitwalia utukufu machoni pa watu.
(Ila pia haimanishi pia kuwa sifa na kuabudu vinapaswa kufanyika ovyoovyo..ustadi unahitajika mno)
Mungu awasaidie sana wote mnaokaa mbele kuwaelekeza watu au kuwaongoza uweponi mwake ili Mjue hamfanyi kwa ajili yenu Ila.kwa ajili ya Mungu!!!
.....Je ladha ya Kusifu na kuabudu inatokana na.viungo gani???

(c)King Chavvah, 2014
+255 713 883 797

KUHUSU KUSIFU NA KUABUDU-Sehemu ya 1


Naamini uko poa na unaendelea vizuri!!
Naamini bado una akili timamu na unajielewa zaidi una hofu ya Mungu ndani yako (Kama sivyo basi hapa kwako ni pagumu)
"KUSIFU" na "KUABUDU" ni ibaada kamili mbele za Mungu,msingi wa ibaada zote na inayopaswa kufanywa kwa makini,ustadi na furaha tele kwa ajili ya Mungu na Ibaada hiyo inawapasa wanyofu wa mioyo!!
KUSIFU-Ni ibaada ya kushukuru,kushangilia, kumkubali,kumsifia,kumwadhimisha,na kumtukuza Mungu kwa matendo yake makuu aliyo,anayo na tunayoamini anaendelea kututendea.
Unaweza kumfanyia sifa kwa yale aliyoyatenda kwa wengine au hata ujumla wa matendo yake maishani mwetu!
*Mara nyingi imetafasirika kuwa sifa ni nyimbo za haraka na shangwe Ila natamani Mjue sifa zaidi ni maudhui na makusudi ya moyo wa mtaa sifa!!
KUABUDU-Ni ibaada ya unyenyekevu,heshima na adhama. Kwa Mungu kukubali,kutii na kumuadhimisha kwa sifa na tabia zake...Hapa haijalishi amefanya chochote kwako au hajajibu maombi yako kama uonavyo Ila anaabudiwa kwa JINSI ALIVYO!
Niweke msisitizo hapa yaani hata kama Huna kazi,umefeli au umeachika bado Yeye ni Mungu tu na Ni mtakatifu tu na Ni mwema tu!!!
*Pia kwa wengi imetafasirika kuwa kuabudu ni nyimbo za taratibu,za kulia na hisia kali...lakini Nataka Mjue kuwa kuabudu ni Maudhui na mwelekeo wa Moyo!!
Sasa Nani ni mwabudu halisi na Anayemsifu Mungu kweli???
Na imempasa nini mtu huyooo....??

(c)King Chavvah, 2014
+255 713 883 797

Wednesday, February 19, 2014

*USIMKOSEE MTU MAKUSUDI KWASABABU UNAJUA ATAKUSAMEHE TU UKITUBU!!!*

SHALOM!!!
Binadamu wote hatujakamilika,kila siku tunaendelea kukamilishwa,hata awe nani bado anayo madhaifu yake na kwahiyo atafanya makosa tu (Muh 7:20), Kuna wakati unaweza kufanya jambo kwa nia nzuri tu lakini wengine wasitafasiri hivyo na hivyo ukaonekana mbaya na hivyo wakapanga ubaya ama kisasi juu yako,kuna wakati unakosea na hata wewe unatambua kweli hapa nimekosea na wakati mwingine kwasababu ya hasira ama uchungu mtu anaweza kufanya ukorofi wa makusudi kwa mwingine na hivyo kumuumiza,sasa aitha umekosea bila kujua ama umekosea na ukajua ama umefanya makusudi,aliyekosewa lazima aumie sana kwa namna nyingi,na tena anaweza aiumie tu bali hata akachafuliwa jina kupoteza "credibility" kwa jamii yake.

WAJIBU WA MKOSAJI;
Ni kushuka chini bila kujali wewe ni nani wapi na una nini, na kwenda kuomba msamaha na kutafuta suluhu kwa yule uliyemkosea,ili amani na urafiki ama undugu udumu tena,maana usipofanya hivyo utaendelea kukwama maana machozi ama huzuni ya mtu mwenye haki inaweza kukwamisha mafanikio yako!


NGUVU YA ALIYEKOSEWA:
Sio jambo rahisi sana kwa mtendwa kuvumilia na kuwa stamina kama ya mwanzo,lakini ikiwa unapenda kupona basi unaweza kumfuata aliyekukosea na kuomba msamaha wewe na kumtangazia msamaha na hapo wala usiendelee kuwaza wala kulifikira tena jambo hilo,usiposamehe na ukangoja aje wewe ndio unakuwa matesoni,yamkini mwenzio akasahau kabisa,wanasema Kusamehe ni tabia ya watu wenye nguvu,mtu dhaifu hutunza kinyongo na kukosa suluhu,tena upo usemi usemao Kisasi kikubwa kuliko vyote ni KUMSAMEHE ALIYEKUKOSEA!!!


*Ukikosewa na wewe ukatafuta kulipa kisasi,utakuwa umejipalia moto zaidi maana utakuwa na hatia ya kukosea wewe na sio kukosewa tena!!

Biblia inasema:....Wana amani nyingi waishikao sheria ya Bwana na wala hawana jambo la kuwakwaza! hivyo kukwaza ni kosa na kukwazika pia ni kosa ikiwa una kweli ya Kristo ndani yako!

Tafuta kuwa na amani na watu wote kwanza kisha ndio huo utakatifu,hii ina maana hata hiyo amani sio rahisi sana lakini kama umedhamiria na unapenda amani utaitafuta kwa gharama yeyote ile, unaweza kwenda kuomba msamaha na bado wakakung'ong'a na kukuona umeishiwa na hauna lolote,lakini usijali msamaha ama amani unayoitafuta ni kwa faida yako!!

GHARAMA YA MAKOSA:
Ukimkosea mwenzio unamsababishia maumivu na mfadhaiko wa kisaikolojia na wakati mwingine anaweza kukukwama kufanya mambo yake na hata kukwama kazi zake,kwa mfano unakwenda kumuandika magazetini mwenzio vibaya ama hata kumsema kwa marafiki vibaya sana,unatarajia nini labda,maana unaweza ukadhani unafanikiwa sana kumchafua mwenzio na baadae baada ya muda unakwenda kuomba msamaha kirahisi tu,ni kweli anaweza kukusamehe na imempasa kusamehe lakini lazima ujue gharama ya msamaha ni kubwa sana sana na huwezi ilipa ila unasemehewa bure tu kama Kristo! Kwanini ni gharama? ukimkosea mwenzio na kumdhalilisha ni kama kumvua nguo mbele ya hadhara na kisha unamkimbilia kumpelekea nguo akiwa peke yake,unadhani watu watasahau kwa kuona uchi wake peupe hata kama sasa akipita umemvisha nguo?


MFANO HAI:
Kuna mtu mmoja amewahi kumsema sana mwenzake vibaya hapo zamani katika mtaa wa mji fulani,naam habari mbaya zikaenea na hata mtu huyo akashindwa kutembea kwa amani mtaani hapo,basi baadae yule jamaa alimkosea mwenzake akaona ngoja tu akaombe msamaha na kwa kuwa alijua ni rahisi tu,basi akaenda kuomba msamaha,basi alipofika kule yule mtendwa akasema nimekuelewa sana na hakika nimekusudia kukusamehe ila naomba uje kesha na jogoo ili tumchinje na tule pamoja kwa furaha,kurejesha undugu wetu....basi yule Bwana akaona aaah mbona rahisi tu,akaenda sokoni akanunua jogoo mkubwa sana na kwenda kwa yule bwana kesho kwa furaha,na alipofika yule mtendwa akasema basi sasa,tutafanya hivi....tutatembea huu mtaa wote huu ukiwa na huyo Jogoo mkononi mwako,na itakuwa tukipiga hatua,utakuwa ukimnyofoa manyonya yake na kusema "KWELI NILIKUKOSEA NDUGU YANGU NA NAOMBA RADHI" na kuyaachilia chini hayo manyonya mpaka utakapommaliza kumnyonyoa huyo jogoo naamini tutakuwa tumefika mwisho wa mtaa kisha tutarejea na kumchinja sasa(kumbuka jogoo ananyonyolewa akiwa mzima).....basi jamaa akaona mbona easy tu...basi akawa ananyoa manyoya huku jogoo akilalamika "KWI KWIII" na kuyaachia chini na walipofika mwisho wa mtaa,yule jamaa akamwambia "HIVI NDIVYO ULIVYONIFANYA KWA YALE ULIYOYASEMA,BASI NAOMBA HUYO JOGOO NIMEBEBE NA WEWE UANZE KUYAOKOTA MANYOYA YOTE ULIYOYADONDOSHA MPAKA MWISHO" hapo ndipo kazi ilikuwa ngumu,maana alijitahidi kuokota mpaka mwisho na baadae yule jamaa akasema je unaweza kuyarudishia manyonya hayo kwa jogoo na yatoshe kumfunika utupu wake? na kweli walipojaribu hayakutosha hata mgongoni, basi wakaenda nyumbani na kumchinja jogoo yule na kula pamoja,ila ndugu yule akajifunza sana kuwa usimkosee mtu kwa makusudi kwasababu ukiomba msamaha atakusamehe tu!

Hata neema ipo nyingi,je ni ruhusa kutenda dhambi??? Hapana!!

HIVYO NAKUSIHI TENA NAKUSIHI SANA,KUWA USIJE UKAJARIBU HATA SIKU MOJA KUMKOSEA AU KUMDHALILISHA MWENZIO KWA MAKUSUDI TU AU KWA KUTAKA SIFA KWA WALE WANAOKUZUNGUKA AMA KWASABABU IWAYO YOYOTE ILE,ETI KWASABABU NI MTU MUELEWA KWAHIYO UKIOMBA RADHI ATAKUSAMEHE TU,KUWA MAKINI SANA!!

N.B: Hata mimi sijakamilika na yamkini nakukosea sana bila kujua, tafadhali ninakuomba unisamehe mwenzio na wala usiniwekee fundo na usiache kuniombea ili niwe focused kwa hatma ya maisha yangu,mimi sina niliye na fundo naye moyoni na kama ukihisi labda nakuchukia,hapana ninakupenda,yamkini sijakutafuta ama hatujakaa kukutana pamoja kwasababu tu za majukumu ya hapa na pale ila kweli toka moyoni nakupenda....HII SIYO KWA MTU MAALUM,BALI YEYOTE ANAYEDHANI AMA ANAYEHISI HIVYO MOYONI MWAKE!!!
Najua wapo wengi mnaniombea na kunitakia mema basi Mungu wangu asiwashahu sawasawa na maneno yake mwenyewe...maana amezitukuza ahadi zake kuliko hata Jina lake mwenyewe,mbarikiwe!!!


Na Fredy Chavala
+255 713 883 797

Sunday, January 5, 2014

SIRI ya MAFANIKIO YAKO!!



SIRI ya MAFANIKIO YAKO
(UMUHIMU wa KUJIFUNZA NENO la MUNGU)

Wakati tunatarajia MEMA katika MWAKA mpya 2014 nimeona nikupe SIRI ya jinsi haya MEMA yanaweza kukujilia maishani mwako. Kumbuka sio kila AHADI ya kwenye Biblia ni yako hata ukiikiri USIKU na MCHANA. Kuna KIWANGO cha IMANI katika KUPOKEA AHADI za Mungu. Kumbuka “imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo”. Sasa nataka ujifunze kwamba unapata ZAIDI ya IMANI pale unapojifunza Neno la Mungu.

Unapojifunza Neno la Mungu KIWANGO chako cha KUMJUA Mungu kinaongezeka. Haiishii hapo, kila unapoongeza KIWANGO cha kumjua Mungu mambo mawili yanatokea (i) AMANI yako inaongezeka (ii). Mema yanakujilia. (Ayubu 22:21)

Hakuna kitu nafurahi kama kusikia feedback kwamba kuna MTU amebarikiwa na FUNDISHO la UFALME (Mambo ya Mungu). Ukisikia umebarikiwa mara nyingi sana inamaanisha umepata UFUNUO fulani (Mungu amefunuliwa kwa njia fulani zaidi katika maisha yako kupitia hilo Neno). Sasa huku mimi najua sio tu UMEBARIKIWA na kuongeza MAARIFA ya kiroho, ila na kiwango cha AMANI na KUFANIKIWA kwako katika mambo yote na MEMA yanaongezeka katika maisha ya kila siku.

Basi tusiwe wavivu kujifunza mambo ya Mungu kwa maana ANATUFUNDISHA ili tupate FAIDA. (Isaya 48:17-19). Ukiona kwenye TV (series, movies, nk.) na kusoma NOVEL na MAGAZETI unachangamka ila hata page 3 tu za mafundisho ya Neno la Mungu unaona ni MZIGO, ujue uko karibu na HASARA kama HUJAPATA tayari.

Nawatakia HERI ya MWAKA MPYA 2014.

Frank Philip

Saturday, January 4, 2014

UWEZO WA NENO LA MUNGU KUKUBADILISHA!!!


(Ushindi, mafanikio ya mwili na roho, amani, furaha, nk. vimefichwa kwenye Neno. Jua ni kwanini inakua ngumu huu ushindi kudhihirika kwako.)

Mara nyingi sana watu wamekua wasikilizaji wa Neno la Mungu na kuguswa kwa namna mbalimbali ila baada ya muda utagundua bado wanaendelea na tabia, mienendo, dhambi na maisha yao ya kale. Nini kimetokea? Neno walilosikia halikuwabdilisha! Kama lingewabadilisha wangeacha njia zao mbaya.

Daudi akasema “moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi”. Ina maana Neno la Mungu lina NGUVU ya kukuzuia kutenda dhambi. Utauliza ni kwa namna gani. Sikiliza, mambo yafuatayo. 1. Biblia inasema “haiwezekani kumpendeza Mungu pasipo imani” na imani huja kwa kusikia Neno la Mungu. 2. “Neno la Mungu ni taa ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu” ina maana ukiwa na Neno utaona mitego mingi sana ya Ibilisi na kuepuka isikunase. Kumbuka “mitego” ni vitu vilivyofichika kukunasa au kukuangusha. 3. “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” na “watu wanapotea kwa kutokujua Neno na Nguvu za Mungu” tunapata maarifa kutoka kwenye Neno, inamaana ukiwa na Neno uko salama na maangamizi ya adui. Haya ni baadhi tu. Swali ni kwamba kwanini watu hawabadilishwi na Neno la Mungu na wanazidi kuishi katika njia zao mbaya?

Tujifunze mambo machache ya kutusaidia katika maisha yetu na kisha tuone tanaponaje. Nitatumia mfano wa MAHUSIANO (ndoa, uchumba, kifamilia, nk.). Katika mahusiano kila mmoja huwa anakua na mahitaji kutoka kwa mwenzake. Matatizo makubwa ya kijamii yako katika mahusiano. Kufanikiwa kwa UHUSIANO unatokana na KIWANGO cha kila mmoja katika uhusiano huo kutenda WAJIBU wake na KUMPENDEZA mwenzake. Sasa sikiliza. Kama kuna SHIDA ya uhusiano jua kwamba WOTE wawili mnahitaji DAWA ambao inapatikana katika Neno la MUNGU. Utasema kwa vipi, “Mungu akitaka kuliponya taifa, au watu wa taifa fulani hulituma Neno”. Watu wakilisikia na kulitii hao watu wanapona katika SHIDA yao.


Nataka nikwambie aina 3 za mioyo. Maana Daudi alisema “moyoni mwake ameweka Neno” kwa hiyo Neno linakaa Moyoni sio kichwani. Na sehemu nyingine tunasoma “kwa moyo mtu huamini na kupokea wokovu” sio kwa kichwa mtu hukumbuka na kuamini. Sawa, sasa sikiliza. Aina za mioyo: 1. Moyo wa jiwe: Huu haupokei kitu. Ni kama jiwe la mtoni liko kwenye maji lakini ndani ni KAVU, no absorption! Paulo aliuita moyo wa aina hii kwamba ni moyo wenye “ganzi”. 2. Moyo wa nyama: Huu unapokea vizuri na ni moyo mzuri unaobadilika kama Neno likiingia humo. 3. Moyo wa KIOO: Huu ni moyo ambao UNAVUTA kila NENO kwa bidii sana ila HUAKISI kwa MTU mwingine na kuhamisha hilo Neno kama lilivyo na “kioo” kubaki kitupu. KUMBUKA ukiona umesikiliza MAFUNDISHO ya watumishi mbali mbali wa Mungu na shida yako ipo hapo iwe ya uhusiano au nyingine, jua kuna shida ya MOYO wako na sio Neno au mhubiri wala upako wao.

Umewahi kujiuliza mtu anahudhuria seminara ya NDOA, na watumishi wa Mungu wanateremsha NENO kwa UPAKO wa hali ya juu na mafunuo makubwa makubwa LAKINI shida ya ndoa imesimama kama HAKUNA kilichotokea? Shida iko wapi? Shida iko Moyoni! Kama sio JIWE basi ni KIOO! Sifa ya mtu mwenye moyo wa KIOO ni kujikusanyia MAFUNDISHO ya NGUVU ili kuthibitisha UDHAIFU wa mwenzake, mfumo au jamii inayomzunguka. Mara zote Roho Mtakatifu akileta POINT ya maana utasikia mtu anasema “unaona?” au “si nilisema?” au “hata mtumishi kasema hivyo hivyo, hii ndio shida na watu hawataki kunisikia” au “hili Neno anatakiwa fulani asikie hili”, nk. Ukijikuta una-respond kwa mtindo huu jua kuna KIOO ndani yako. Pamoja na kujikusanyia MAFUNDISHO ya kila UBORA wa juu, kama una moyo wa kioo, utakua tu ukichambua “watu” wengine kwa WINGI kwa mafundisho yako na wewe binafsi kubakia na MISHIDA yako inakukodolea macho! Kwa maana “Mkono wa Mungu haukupungua urefu wala nguvu hadi ushindwe kuokoa” sasa mbona Hauokoi? Je! Neno limepungua nguvu? La! Hasha. Yesu jina lake jingine ni Neno la Mungu, na hajawahi kushindwa KITU, ila anabisha kwenye “mlango ya moyo wako”, ukifungua utaona mwenyewe atakavyo kuhudumia na kuleta DAWA katika shida zako ZOTE. Shida sio Yesu/Neno shida ni MOYO wako! Tengeneza MOYO wako na NENO litakubadilisha bila shaka.

Mfalme Daudi yeye hakuomba UTAKASO wa moyo, aliomba moyo MPYA! Aliona hizi toba zimekua nyingi na mambo hayaendi sasa, akamwambia Mungu “niumbie moyo safi (“create” in me a clean heart!)”. Kama kuna eneo unatakiwa kushughulika nalo sana ni Moyo! Ndio maana maandiko yanasema “linda SANA moyo wako KULIKO vitu vyote ulindavyo”. Kwanini? Huko ndiko kuna SIRI ya kushinda au kushindwa kwako! Uzima unatokea humo, na mauti inatoke humo pia! Ndio maana Yesu akasema “sio kile akilacho mtu HUMNAJISI ila kile kimtokacho”. Kutokea wapi? Jibu ni MOYONI. Uzinzi, uongo, ufisadi wa kila namna, tamaa, nk, makao yao ni moyoni mwako. Shughulika na moyo nakwambia “viungo” vingine vya mwili ni mateka tu na vinatumika kama watumwa ila bwana wao anaitwa MOYO! Shughulika na bwana mkubwa “moyo” na kila kitu kitakia kimya!

Sasa watu wengi sana wako busy kujitakasa kwa Damu ya Yesu. Kweli inatakasa, lakini ukifuatilia maandiko utagundua Neno la Mungu linafanya hiyo kazi pia. “Uwatakase kwa Kweli yako, Neno lako ndio Kweli!” Ibilisi anakuweka mbali na Neno la Mungu akijua lina NGUVU ya kukutakasa na KUKUPONYA, sio tu magonjwa ila hata na matatizo na shida ZOTE za duniani (formula ya maisha yako imefichwa kwenye NENO). Ufumbuzi wa matatizo yako yote uko kwenye NENO asikudanganye mtu, unachohitaji ni UFUNUO kwenye hilo Neno, na hapo ndipo pa GUMU ila OMBA na tafuta KUSUDI la Mungu katika KILA unachokifanya itakusaidia kuwekeza nguvu na muda wako. {kwa ufafanuzi zaidi soma somo jingine humu lenye kichwa “KAZI YA MVUVI”} uone jinsi Yesu ambavyo sio mvuvi wa samaki lakini anamsaidia mvuvi mzoefu kwa kumpa NENO la maelekezo na kazi inakua rahisi na ya mafanikio makubwa.

Sasa ili Ibilisi akutese lazima akuweke mbali na Neno la Mungu, au akishindwa anashughulika na moyo wako. Kama hatupii “jiwe” basi anatupia “kioo” (lugha ya kwenye Agano jipya ina sema Ibilisi “hulinyakua Neno”), unasikia lakini ganzi tupu! ILI usije ukaamini “ukaokoka”! Hii ni vita KAMILI na ni KALI sio utani. Ndio maana sio kuombea tu ugali kabla ya kula, ombea hata Neno la Mungu kabla ya kusoma ili lizame mahali pake, upata UFUNUO na lifanye mabadiliko katika maisha yako. Usisahau uwezo wa kupokea Neno na kuleta mabadiliko ni katika moyo wako kwa hiyo ombea na moyo wako uwe kama “udongo tifutifu”, ili kila Neno likidondoka hapo lizae 1:100, 1:60, 1:30, nk. Haiwezekani usome, usikie au ukutane na Neno HALISI la Mungu uwe kama ULIVYO haiwezekani! Lazima kuna shida mahali. Mungu atusaidie kujua siri hii. AMANI na BARAKA zizidi kwenu.

Frank Philip

NGUVU ya VINYAGO ndani YAKO!!!


Nabii Elisha alikua mkulima na alikua na JOZI kadhaa za ng’ombe (MAKSAI). Alipoitwa katika kazi ya Bwana alichofanya ni KUCHINJA wale maksai na kutumia vifaa vya majembe yake kama kuni! Wakala nyama na kusherehekea mwisho wa HUDUMA ya UKULIMA. Elisha akamgeukia Eliya na kuanza kazi kwa nia moja. Kumbuka Elisha alikua na NJIA moja, hapakua na njia ya kurudi nyuma maana ALIANGAMIZA (vinyago) vya ya biashara ya kwanza!

Yesu alipomwita Petro kutoka katika biashara ya UVUVI, Petro alikuja na kuanza huduma kwa nguzu sana ila kwenye STOO yake alihifadhi zile NYAVU na MTUMBWI vya kuvulia samaki. Alipokua KARIBU na Yesu, Petro alikua na ujasiri mkubwa sana kuliko hata wenzake. ILA katika vipindi vigumu na Yesu akiwa hatua kidogo tu mbali naye wakati wa MATESO, Petro anamkana YESU! Tena mara tatu! Siku Yesu ameuwawa, Petro akapiga mahesabu na kukumbuka zile NYAVU na MTUMBWI kule stoo na KURUDI kwenye kazi yake ya kuvua samaki! Baada ya kufufuka, Yesu akaenda tena kwa “mara ya pili” kumtafuta Petro kule ziwani akiwa BUSY KUVUA SAMAKI. Kumbuka, Petro alikwisha jua kua yeye ni “mvuvi wa WATU” sasa ilikuaje akarudi kuvua samaki? Sababu ya msingi ilikua ni KUKATA TAMA na kuona “hii biashara ya kumfuata Yesu hailipi”, lakini pia bado alikua na NYAVU zake na VIFAA (VINYAGO) vya ile kazi ya zamani! Akarudi huko tena maana “vinyago” vilikuwepo na sio vya KUTAFUTA.

Katiaka maisha yetu ya zamani hakuna mtu yeyote ambaye “hakua” na VINYAGO ambavyo aliviabudu. Zile dhambi na kazi mbaya za Ibilisi. Watu wengi wameamua kumfuata Mungu ila kwenye stoo zao (MIOYONI) bado kuna VINYAGO wameweka akiba huko. Wakifika mahali PAGUMU walio wengi wanarudi “stoo” na kunyanyua kinyago maana ni rahisi kuchukua KINYAGO wakati wa majaribu kuliko KUFUNGA na KUOMBA ili MUNGU akuvushe na kukufikisha MAHALI pa USHINDI wako.



Hatari kubwa ya VINYAGO ni kwamba huwa VINASEMA. Wakati umevijaza ndani ya MOYO wako na unaenda mbele za Mungu na KUMUULIZA juu ya “jambo maishani mwako”, Mungu anasema “nitakujibu sawa na vinyago vyako”. Kwa sababu umeishi katika TAMAA na kumbukumbu (IBADA) ya vinyago vyako unapotelea humo ukizani ni Mungu amekujibu, kumbe ni “sauti ya vinyago”! Kwani hujui kwamba Mungu aliapa kwamba hatashindana na mwanadamu? Sasa jua hili, uking’ang’ania vinyago vyako jua Mungu hakunyang’anyi kwa nguvu ila utaangamia navyo usipogeuka. EZEKIEL 14: 3“Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote? 4 Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, Bwana, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake” (Umewahi kujiuliza ni kwanini maombi ya kutafuta mchumba ni MAGUMU sana, ila maombi ya HUDUMA Mungu anajibu haraka? Asikiaye na afahamu!)

Kama kuna kitu Mungu hapendi ni mtu wa nia MBILI. Joshua akawauliza wana wa Israel wachague wanamtumikia Mungu au NANI? Hakuna katikati, kama wanamfuata Mungu lazima kusema wazi na sio kujibandika LABEL mbili, moja ya Mungu na nyingine ya Ibilisi. Musa alipokua anashughulika na maasi ya Kora alisema neno hili “walio upande wa Mungu waje huku na walio upande wa Kora waende kule”. Nakwambia wale wa upande wa Kora ambao waliambudu VINYAGO vyao walijitenga kule na ardhi ikafunguka wakamezwa humo! Usisahau, mwisho wa VINYAGO ni kukuangamiza na kukumaliza bila kujua kwa sababu vinyago VINAVUTIA macho na vyafaa sana kwa CHAKULA.

Wana wa Israel walijua kabisa huko mbele kuna nchi ya ahadi inayotiririka MAZIWA na ASALI, lakini “hapa katikati” kuna KUFAULU mtihani. Lazima kupita JANGWANI miaka ya KUTOSHA, kuna mataifa kadhaa ya kupigana nayo VITA, kuna kuishi kwa kula MANA, chakula ambacho baba zao hawakukijua, na kuna masharti sio kula tu ovyo, hakuna kuokota MANA siku ya Sabato (kula kwa nidhamu). Biblia inatuambia walivaa mavazi yao na viatu vyao havikuchakaa. Inamaana hapakua na “viwalo” vya kubadili kwa wale warembo. Ghafla! watu wakakumbuka kule Misri masufuria ya nyama na kuanza kutamani VINYAGO vya zamani. Kumbuka NYOKA ZA MOTO zilikuja kuwashughuikia maana walianza manung’uniko huko jangwani. Kiu ni kali hadi Musa anamkosea Mungu maana alishindwa KUMSTAHI mbele za hao maelf ya watu ambao wako “desperate”, akakosa uvumilivu na kushindwa kufuata malekezo vizuri! Unapobanwa na mambo mengi sana ANGALIA usikose KUMSTAHI Mungu mbele za hao “watu” na kwa sababu ya VINYAGO vyako ukamvunjia Mungu heshima yake. Chunga sana maana saa ya kujaribiwa inakuja. Simama kwa uaminifu na kwa maombi na saburi. TUPA vinyago vya zamamani na uwe safi bila njia mbili mbili, Mungu atakurehemu utavuka salama la sivyo vinyago VITAKUANGAMIZA.

Kumbuka siku zote, kama ulikua na MPENZI wa zamani na sasa umeamua kumfuata Mungu, jaribu kubwa sio UZINZI tu ila ni yule jamaa/binti maana ndani yako amekua KINYAGO na kila ukifinga macho unaona kinyago “hiki hapa”. Ibilisi anajua vyema juu ya ibada ya SANAMU hivyo kila ukifunga macho, anakuletea zile VIDEO na SAUTI kwa maana VINYAGO huongea! Gafla unatamani kurudi Misri na kusahau UKOMBOZI mkuu wa MKONO wa Mungu ulionyooshwa ULIOKUOKOA. Unarudi kusujudu SANAMU na unajikuta unaingia katika mtego wa maasi ya KORA. Mambo yote yanatokea JANGWANI! Hapo ulipobanwa na UHITAJI na ADHA mbalimbali, hapo ndio KIPIMO cha UAMINIFU wako kwa Mungu wako. Jipe moyo basi maana BWANA wetu alisema “ulimwenguni mnayo dhiki laikini jipeni moyo, Mimi nimeushinda ulimwengu”, WEWE pia Utashinda. Shughulikia vinyago vyako na KUVISAHAU nawe utakua salama. AMEN.


Frank Philip

Thursday, January 2, 2014

NGUVU katika MATENDO yako!!!



NGUVU katika MATENDO yako
(Umri, mlango wa misaada kwako, uheri (less trouble) wa maisha, baraka na utajiri)

Kuna msemo uliozoeleka sana unaosema “malipo ni hapa hapa duniani”. Na kwa wenzetu wa Magharibi wanasema “what goes around comes around”. Lakini Bwana wetu alitufundisha kwamba “yale mambo tunayotaka watu watutendee inatupasa sisi pia kuwatendea hivyo”, ikiwezekana tuwatendee kwanza na bila masharti. Na “kipimo tunachowapimia wengine hicho hicho na sisi tutapimiwa”. Kumbuka sio KIPIMO hicho umetumia kumpimia mtu mmoja ila ndio KIPIMO umejichagulia watu WOTE au hata Mungu kukupimia wewe!

Ni rahisi sana kumtendea mtu WEMA baada ya yeye kukutendea wewe kwanza (kulipa wema kwa wema), ila pia ni NGUMU kumtendea wema ADUI yako au mtu USIYEMPENDA. Ndio maana Yesu alisema, “Haki yenu isipozidi ya Mafarisayo, hakika hamtauingia Ufalme wa Mungu”. Kumbuka hii HAKI haimaanishi IMANI tu ila na KUTIMIZA mambo ya KIJAMII yanayotuhusu! Yesu akazidi kufundisha akisema “kunatofauti gani kufanya jema wa watu uwapendao?” maana KILA mtu anaweza kufanya hivyo hivyo! Lakini Akatufundisha namna ya KUWEZA kwa maana ni NGUMU sana kutenda kwa namana hii. Akatufundisha KUWAPENDA adui zetu na KUWAOMBEA wanotuudhi! Huwezi kumtendea wema ADUI na mtu ANAYEKUUDHI kama HUJAJIPANGA kumowmbea! Jaribu uone, ni ngumu na hata ukiweza utaishia kunung’unika ndani yako. Mara nyingi tumesikia watu wanasema “ulinifanyia hivi na vile lakini mimi bado nakusaidi”! Hii kitu acha mara moja kwa sababu hailipi! Inaonyesha hukutoa kwa moyo mweupe ambayo ni kutoa kwa hasara! Omba kama unaona unapaswa kumsaidia mtu na ni ADUI au MTESI wako.

Mfalme Hezekia alipoambiwa na nabii kwamba “tengeneza mambo ya nyuma yako maana utakufa”, Hezekia aligeukia ukuta. Akaomba na KUMKUMBUSHA Mungu matendo yake MAZURI aliyofanya huko nyuma, Mungu akampa BONUS ya miaka 15 mbele ya kuishi. Unaweza ukashindwa kuhuasinisha UREFU wa MAISHA ya mtu na MATENDO yake moja kwa moja lakini ukiangalia kwenye maandiko utagundua kuna AMRI ya Mungu ina sema “waheshimu baba yako na mama yako ili siku zako zipate kua nyingi katika nchi, na uheri pia”. Sasa naamini huwezi kumheshimu mzazi wako MOYONI tu bila kufanya kitu. Heshima inaonyeshwa kwa matendo fulani na hayo matendo basi yana NGUVU ya kuongeza UMRI wako na kusababisha UGUMU au WEPESI (uheri) wa maisha yako hapa Duniani. Kumbuka hatuongelei majaribu wala kazi ya Ibilisi, ila ni WEWE na MATENDO yako ambayo mengi yamejikita katika TABIA yako nzuri au mbaya.

Doricas alikua mama mmoja ambaye alijitoa sana kusaidia wajane wakati ule wa Mitume. Akafa. Wale wanawake wakaona haiwezekani huyu mama afe hivi hivi tu jisi walimpenda na kufaidi vipwa vyake mbalimbali. Wakamlaza Ghorofani. Wakamwita Petro wakampa kazi ya KUFUFUA mtu “wa matendo mema” ili azidi kutenda KAZI njema! Mungu akamfufua Doricas, akampa siku zaidi za kuishi. Connection iko katika “matendo yake kwa ile jamii”.

Maandiko yanasema wazi sana kua Mungu hana upendeleo, lakini nakwambia sio kila mtu anapokea sawa na mwingine kutoka kwa Mungu huyo huyo. Sehemu ya sababu hii ni MAKUSIDI na WITO wako mbele za Mungu ila na KIASI cha utii wako katika mambo mengine ya Mungu na unavyo WATENDEA watu wengine. Yesu akasema “heri wenye rehema maana watapata rehema”. Rehema ni huruma kwa matendo. Kwa mfano, watu wawili wana shida sawa, mmoja kabla hajalia shida, watu managombania kuleta michango na misaada, huku mwingine anajitahidi kuomba na kutafuta misaada ila watu “hawaguswi” na hakuna anayemrehemu hadi anakufa na shida yake! Kumbuka, ukiwarehemu watu “wowote” nawe utapata rehema kutoka “kokote”!

Korinelio alikua “akiwapa watu VITU vingi” na alikua akisali daima. Hakua mlokole, ila alikua mtu wa MATENDO mema. Biblia inasema zile “SADAKA” zilifika Mbinguni na zikawa UKUMBUSHO mbele za Kiti cha Enzi! Kumbuka huwezi kutoa kwa kiwango hiki kama huna REHEMA ndani yako. Kwa MATENDO ya Kornelio, jinsi alivyo WAREHEMU watu, Mungu akamrehemu na kumpa zawadi ya WOKOVU yeye na NYUMBA yake! Kumbuka, wakati anatoa hivyo vitu na misaada alivyovitoa vyote viliitwa “vitu” na sio “sadaka”. LAKINI kwa Mungu unapotoa hata kama umempa mtu offer ya soda katika “kutoa kwema”, hiyo ni sadaka kamili na inaenda Mbinguni “kule ambako hakuna wezi, nondo, wala kutu iharibuyo”, na Mungu huachilia BARAKA juu yako na hutajua kwamba ni ile soda tu!

Kuna uhusiano mkubwa sana wa maisha ya kawaida ya mtu na mafanikio yake ya kiroho na hata uwezekano wa kuingia Mbinguni au kutokuingia. Dhambi iko upande mmoja, ila kuna upande wa pili ambao ni ngumu kuupima. Kwa mfano, yule kijana tajiri aliyemfuata Yesu na kumuuliza afanyeje ili aweze kuurithi ufalme wa Mungu aliambiwa “Je! Umezishika amri?” Kijana akasema NDIO, “Yesu akampenda!” ila akamwambia “uza ulivyo navyo na uwape masikini”. Kijana akageuka na kuondoka kwa maana alikua na mali nyingi. Sasa kumbuka, ninachotaka uone hapa ni 1. Kumshika Mungu ni muhimu, 2. Je! Hao jirani zako na watu waliojaa kila kona wajane, yatima, masikini, wenye shida mbali mbali umefanyaje? Yesu akasema “ni vyepesi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko TAJIRI kuingia katika Ufalme wa Mungu”! Wengi humu watajiona ni SALAMA kwa maana wanajiita wao sio MATAJIRI. Sikiliza, Utajiri una awamu zake. Utajiri unakua au kupungua kutokana na nini UNAFANYA au HUFANYI. Kila mtu kwa awamu yake aliyo sasa ni TAJIRI kwa hivyo vitu Mungu alivyokupa, na utajiri huu UNAKUA au KUPUNGUA kwa kadri unavyojipanga na Mungu ua na JAMII inayokuzunguka. Kumbuka, ukijipanga sawasawa na Mungu na Jamii kwa pamoja utabarikiwa DUNIANI na UZIMA wa milele. Ukijipanga KIJAMII zaidi utafanikiwa pia na utakua tajiri kwa maana “KILA apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu na KILA apandaye haba atavuna haba”. Mbegu ni mbegu usidanganyike ikipandwa ITAOTA tu! Hata kama aliyepanda ni Korinelio ambaye hajaokoka wala hajajazwa Roho mtakatifu, tofauti tu ni kwamba haendi mbinguni.

Lengo la somo hili ni kukufungua macho juu ya MATENDO yako ya kila siku kwa WATU wengine katika JAMII, ili uweze kuona jinsi ambavyo matendo yako yanaweza 1. Kuathiri umri wako wa kuishi 2. Uheri wa maisha yako 3. Kufungua misaada (rehema) kutoka kwa watu mbalimbali na Mungu pia, na 4. Kubarikiwa kwa Baraka za aina nyingi.

Frank Philip.

Monday, December 30, 2013

MAOMBI YENYE NGUVU.......SEHEMU ya III



 MAOMBI YENYE NGUVU
Imani ya Kupokelea Majibu ya Maombi Yako

Katika Mfululizo wa somo lenye kichwa “MAOMBI YENYE NGUVU”, nimeona nizame kidogo kwenye kipengele cha ‘iv’ cha sehemu ya II ya somo hili kinachosema “JUA kutofautisha IMANI ya KUOMBA na IMANI ya KUPOKEA”.

Mara nyingi sana watu wanachukulia SOMO la imani kwa wepesi usiostahili. Kama kuna kitu cha muhimu katika maisha ya Mkristo ni kujua FAIDA na MADHARA ya kutokuwa na IMANI. Sijui ni kwanini utasikia mara nyingi sana watumishi wa Mungu wakihusianisha imani na kushindwa kupokea majibu ya maombi lakini ni mara chache utasikia wakitia mkazo somo hili la IMANI kwa KUSUDI la KUMPENDEZA Mungu.

Kusudi la Msingi la IMANI sio kupokea majibu ya maombi yako ila KUMPENDEZA Mungu. Sababu ya msingi ni kwamba mahitaji tunayoomba kwa Mungu sio ya kila saa na kila siku, ila mambo YOTE tuyatendayo katika maisha muda wote yanahitaji IMANI ili umpendeze Mungu kwa sababu imeandikwa “haiwezekani kumpendeza pasipo imani” (Waebrania 11:6) na “kila jambo lisilofanyika katika imani ni dhambi”. Sasa jiulize kwamba unafanya mambo mangapi pasipo imani? Kutokana na mistari hii miwili najifunza kwamba LENGO la msingi la IMANI ni kumpendeza Mungu na ndipo faida zingine huja pale unapoitumia imani hiyo KUOMBA au KUPOKEA majibu ya maombi yako.

Katika sehemu hii ya III ya somo hili natamani tujifunze hiki kipengele cha IMANI ya kupokea majibu ya maombi yako. Nitatumia mfano wa NDOA ya Zakaria na Elizabeth ambao ni wazazi wa Yohana mbatizaji na Maria, mama wa Yesu.

Nitaanza na Zakaria na Elizabeti. “Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti. Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama. Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana” (Luka 1: 5-7). Hawa wawili walikuwa wakiishi maisha ya KUMTUMIKIA Mungu katika usafi na utauwa. Walitamani sana kupata mtoto na walimwomba Mungu (kwa sababu walikuwa na IMANI ya KUOMBA) kwa muda mrefu bila majibu. Haikuwasumbua kwamba hawakujibiwa, walizidi kukaa katika HUDUMA na UTUMISHI Mungu aliowaitia na waliendelea na zamu zao.

Mungu akamtuma malaika Gabriel kupeleka ujumbe kwa Zakaria akiwa madhabahuni katikati ya huduma. Malaika akasema “Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.” (Lika 1:13). Alipoambiwa habari za MAJIBU ya maombia yake, “Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi. Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema.Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake.” (Luka 1:18-20). Sasa nataka uone kwamba hawa WATUMISHI waliomba kweli ila ilipofika mahali Mungu anasema “nimesikia MAOMBI yenu na sasa najibu” bado HAWAKUSADIKI/HAWAKUAMINI kama inawezekana! Yaani hawana imani ya kupokea MAJIBU ya maombi yao! Sasa Malaika akamfanya bubu. Kwa haraka unaweza kuona kama ni ADHABU ya kutokuamini kwake (Mungu hafurahishwi na mtu wa kusita-sita/mashaka/kutokuamini kama Anaweza) ila kuna sababu ya pili ambayo ni KUHARIBU imani ile ya KUPOKEA majibu kwa UKIRI mbaya (negative confession) basi dawa ni kumnyima kuongea hadi majibu ya maombi yatokee.

Ukija kwa upande wa Maria, mama wa Yesu. Gabriel huyo huyo alikuja na habari ya kupata mtoto ila “kwa uweza wa Roho Mtakatifu”. Utagundua kwamba Maria na yeye aliuliza swali linalofanana na la Zakaria ila hakupigwa na ububu! Ujumbe huu ulimjia Maria miezi 5 baada ya Elizabeti kuwa mjamzito. Sasa wakati Maria anamuuliza Gabriel haya mambo yatakuaje, kulikuwa na SHIDA ya IMANI ya KUPOKEA huo muujiza pia. Kabla Gabriel hajaondoka ilibidi ainue imani ya Maria kwa kumpa “Neno la Mungu lililotamkwa kwa kinywa cha malaika kwa Zakaria” (“Imani huja kwa kusikia Neno la Mungu”). Baada ya Gabriel kuleta ujumbe “Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.” (Luka 1:34-38). Huu msitari wa 38 unatuonyesha imani ya Maria imeinukana na kuona INAWEZEKANA kisha Malaika akaondoka.


Tukiendelea kujifunza hapa utaona “basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda, akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti. Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu; akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu. Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana” (Luka 1: 39-45).

Hawa wanawake wawili walimshangilia Mungu kwa pamoja ila ukitizama kwa makini utagundua baada ya Elizabeti kujazwa Roho Mtakatifu, alirudia yale “maneno ya kuimarisha imani ya Maria” na mwishowe utaona kwamba anasema “aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana”. Ikimaanishwa kwamba kuna IMANI inatakiwa KUPOKEA hiyo ahadi japo kweli kabisa ni Malaika/Bwana amesema. Kumbuka siku zote, AHADI iliyoko kwenye Neno la Mungu sio yako hadi utakapokuwa na IMANI ya KUTOSHA kuimiliki/kuipata hiyo AHADI.

Tukiendelea kujifunza utaona Maria anaimba wimbo wa kumshukuru Mungu baada ya haya maneno ya Elizabeti. Maneno ya wimbo wa Maria ni marudio ya yale ambayo malaika alikwisha kusema na jinsi alikubali kusudi la Mungu kutimia kwake, huku akiona ni UPENDELEAO wa pekee kupokea BARAKA hii kubwa. Huu ni UKIRI wa kuimarisha na kulinda IMANI yake ya KUPOKEA mtoto.

Ukifuatilia zaidi utaona Maria alikaa kwa Elizabeti miezi 3. Yamkini walikuwa wakitiana moyo katika kubeba MIMBA muhimu katika maisha yao na kufikilia KUJIFUNGUA salama sawa na KUSUDI la Mungu. Sasa mara nyingi sana katika maisha yetu tumekuwa na imani nzuri tu wakati wa kuomba, ila HALI HALISI zimetufanya kuona HAIWEZEKANI KUPOKEA majibu ya maombi yetu na imekuwa kikwazo. Fikiri hii hali, binti anaambiwa atapata mimba bila kumjua mwanaume! Na upande mwingine kikongwe aliyepitiliza siku za kuzaa anaambiwa atapata mimba! Hali halisi inasema HAIWEZEKANI. Sasa kama mtu hatakuwa na IMANI, na hajui namna ya kuzimisha sauti za SAYANSI, TEKINOLOJIA na ELIMU zingine, imani ya KUPOKEA inakufa. Hata kama ni Yesu anakuja/anazaliwa, ILIBIDI Maria awe na IMANI ya KUPOKEA! Ilibidi Malaika Gabrieli ampe Maria mfano wa “jambo lisilowezekana” na jinsi ambavyo “limewezekana kwa Mungu” ili kuinua IMANI yake ya KUPOKEA.

Kitu cha kukusaidia kukuza/kupata IMANI ya kupokea majibu ya MAOMBI yako ni KUJIFUNZA matendo Makuu ya Mungu katika Biblia, na kuyatafakari usiku na mchana, na kuyataja unapotarajia MAJIBU ya maombi yako. Jifunze KUKIRI matendo makuu unayoyajua ya Mungu wetu ukiwa katika maombi kwa mfano, wakati Daudi anamkabili Goliath alisema maneno ya IMANI yake kwa Mungu, “Mimi mtumishi wako nimezoea kuchunga kondoo wa baba yangu. Kila wakati simba au dubu akija na kukamata mwanakondoo mimi humfuata na kumshambulia, nikamwokoa mwanakondoo kinywani mwake. Kama simba au dubu akinishambulia, mimi humshika ndevu zake, nikamwangusha na kumuua. Mimi mtumishi wako nimekwisha ua simba wengi na dubu wengi. Sasa, hata yule Mfilisti asiyetahiriwa, ambaye ameyatukana majeshi ya Mungu aliye hai, atakuwa kama hao. Mwenyezi-Mungu ambaye ameniokoa makuchani mwa simba na dubu, ataniokoa kutoka kwa Mfilisti huyu” (1 Samweli 17:34-37). Zungumza na HALI unayopitia na uitangazie USHINDI katika MAOMBI, itaje hiyo shida kwa jina “lake” na uiambie kwa maneno kama unazungumza na mtu, huku ukiikemea kwa Jina la Bwana wa Majeshi. Wakati huo ukitamka matendo mengine MAKUU ya Mungu ambayo yamefanyika kwa watu wengine. Kwa kufanya hivyo ghafla! Utaanza kuona Mungu ni MKUBWA kuliko hiyo shida/jambo unaloomba na IMANI yako inaongezeka wakati huo MASHAKA yakitoweka. Kumbuka Ibilisi huleta VITA katika FIKRA zetu ili kutujengea ngome, na njia mojawapo wa kumshinda ni kwa kutumia “NENO la ushuhuda na Damu ya Mwana-kondoo” (Ufunuo wa Yohana). Hii ni SIRI ya KUJAZA imani ya KUPOKELEA lakini pia kumshinda Adui azuiaye.

Mungu atusaidie kujenga IMANI zetu kwa KUJIFUNZA kwa bidii maandiko na kuomba. Hatimaye tuweze kutenda KILA jambo kwa imani kwa kusudi la kumpendeza Mungu na kuweza KUOMBA na KUPOKEA majibu ya maombi yetu kwa hiyo IMANI.

Roho Mtakatifu atufundishe NENO la Mungu na kutuwezesha kupata UFUNUO katika hilo Neno ili kujenga IMANI zetu. AMEN.

Frank Philip.

VITA KATIKA KUSAMEHE!!!


Kusamehe mtu aliyekukosea ni moja ya mambo magumu ya KIIMANI ambayo LAZIMA uweze kama unataka KUMUONA Mungu katika maisha yako.

Sababu na faida za kusamehe ni nyingi lakini nitataja chache. 1. Tunasamehe watu waliotukosea ili na sisi tusamehewe DHAMBI (madeni yetu) na Mungu. Katika sala ya Bwana kuna sehemu tunamwambia Mungu “utusamehe dhambi (deni) zetu kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea (wanaotudai). [nitarudi kueleza habari ya deni hapo baadae]. 2. Dhambi zina NGUVU ya kuficha uso wa Mungu usiuone, KUZIBA sikio lake ASIKUSIKIE na kuzuia Mkono wake USIKUOKOE. Nabii Isaya anasema hivi “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” (Isaya 59:1,2).

Kumbuka KIPIMO ya KUSAMEHEWA dhambi na madeni yako kwa Mungu UNAJIPIMIA mwenyewe kwa JINSI unavyowasamehe wengine. Na hii unamwambia/unamwomba Mungu katika sala ya Bwana kila unaposali. Kwa lugha nyingina UNAMSIHI Mungu “USINISAMEHE kama jinsi ambavyo SIWASAMEHI watu walionikosea!”. Sasa, kwanini tunasema kwamba KUSAMEHE ni VITA? Kwa sababu anayetaka USISAMEHE sio wewe ila ni IBILISI! Mtu ataniuliza nimejuaje? Angalia hapo juu Isaya anasemaje: kwanza, “ili Ibilisi afanikiwe KUKUZUIA wewe kuuona USO wa Mungu anahakikisha una DHAMBI!”, pili, “ili Mkono wa Mungu USIKUFIKILIE na kukuokoa katika SHIDA, KILIO, na MAUMIVU yako, anakufarakanisha na Mungu kwa kuweka WINGU la uovu kati yako na Mungu na KUZUIA SIKIO lake kukusikiliza”! Mungu anasema “SITAKI kusikia” maombi yako. Ibilisi anachunga sana hii SIRI ili usije ukaondoa UOVU na DHAMBI zako maana ukifanikiwa kuondoa UOVU katikati yako MKONO wa Mungu utadhihirika katika maisha yako katika mambo YOTE na utakua UMEMSHINDA Ibilisi. Sikiliza, Mungu “hulitizama Neno lake na kulitimiza”. Usije ukasema Ibilisi kamdhibiti Mungu! Haiwezekani, ila Mungu ndio kasema HUTANIONA, SITAKUSIKIA na MKONO WANGU HAUTAKUAOKOA, kama kuna UOVU katikati yako! Na Ibilisi analikamata hilo Neno na kulitumia kukutesa. [kama ulikua hujui Ibilisi ni mtendaji wa Neno kuliko watu wengi sana japo huwa analitumia kinyumenyume, na kupambana naye ni LAZIMA ujue Neno na kulitumia kama silaha yako ya VITA. Bila Neno, wewe ni mawindo rahisi ya Ibilisi]

(Yeremia 29: 11-13) “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.” Madhara ya kukaa na DHAMBI ni MENGI kuliko unavyoweza kufikiri. 1. Unajikuta unapoteza MATUMAINI (future hope). Huko mbele kwenye maisha yako unaanza kuona giza na kukata tama maana bila sababu, matumaini yanapotea ndani yako! Hii ni kazi ya Ibilisi. Kama unaona unaanza kupoteza matumaini na huko mbele ya maisha yako unaona hakuvutii usihangaike, saka WATU wa kusamehe maishani mwako! Ondoa UOVU katikati yako! Ukiwasamahe “wote” hii hali inakwisha kwa maana MATUMAINI ya mambo MAZURI ni ahadi ya MUNGU wa watu wake na Ibilisi anataka kuinyakua kutoka kwako kwa KUTOSAMEHE. Kama kuna kitu unahitaji ni MATUMAINI, hii ni nguvu ya ajabu sana inayokupa nguvu ya kusonga mbele hata kama uko katika majaribu mazito. “Abrahamu alipoiona ile ahadi…”, “Yesu alipoona huko mbele ya msalaba kuna nini….alishinda msalaba na maumivu yake yote”. Lazima uone MBELE/future na huwezi kuona kama huna MATUMAINI na Ibilisi anakuondolea MATUMAINI ili uzidi kushindwa katika VITA naye. Kitu anachotumia kukuwekea WINGU hili la kutokuona mbele ni nini? Jibu ni UOVU katikati yako! 2. Katika shida na mahitaji yetu mbali mbali huwa tunamwita Mungu. Naye anasema “mtakwenda KUNIITA na KUNIOMBA nami NITAWASIKILIZA, MTANITAFUTA na KUNIONA ila kwa BIDII”. Bidii inatakiwa kwa sababu gani? Ni VITA, Ibilisi hataki UITE na Mungu asikie, wala hataki UKIOMBA na KUMTAFUTA Mungu umuone. Sasa kwa kuwa hawezi KUMZUIA Mungu, anakuja kukudhibiti wewe kwa kuhakikisha UNASHINDWA kusamehe watu waliokukosea! Matokeo yake ni KUZUIA majibu ya maombi yako!

Mtu atauliza kwani Ibilisi anaweza kuzuia majibu ya maombi kutoka kwa Mungu? Sikiliza, Wakati Danieli anaomba, Mungu anamtuma malaika Gabriel kumpasha habari kwamba hizi siku 21 alizokua busy anaomba ajue kwamba ALIJIBU “tangu” ulipoweka NIA ya KUOMBA, (sio wakati alipoanza kuomba) ila kuna VITA hapo juu na MAJIBU ya maombi yako yamezuiliwa, hivyo nimemtuma MIKAELI ashuke kupambana ili huyu MKUU wa giza hapo anayekamata majibu ya maombi yako aachilie! Sasa, ukifuatilia sehemu nyingine utaona Danieli aliomba na alianza kwa “toba” kwanini? Ili kusafisha NJIA ya kupokea Majibu. Ndio maana tunafundishwa kwamba “kila tusimamapo kusali sameheni”! Ayubu alijua SIRI hii pia, sio kwamba alitubu kwa ajili yake tu, alitubu hata kwa ajili ya watoto wake, “isije ikawa wamemkosea Mungu mahali”, (isije ikawa…maana yake anatubu hata kama hajui dhambi iliyofanyika! Kama ipo au haipo, yeye anatubu tu na KUACHILIA). Sasa watu wengi sana wamekwama na wameteseka na kila namna ya SHIDA na MAUMIVU mengi kwa sababu WAMESHINDWA kusamehe. Sasa, hebu chukua MUDA kidogo wa kutafakari ile LIST ya mambo uliyoomba na unayotarajia Mungu kukujibu na mengine unakiri umepokea. Kisha kumbuka WATU uliogoma kuwasamehe na ulinganishe FAIDA ya kumsamehe “huyu mtu” na HASARA utakayopata kama ile LIST yako ya maombi HAIJIBWI na Mungu. Pima mwenyewe na chukua hatua. Ukiamua kusikiliza uongo wa shetani ni juu yako, Mungu analeta hili Neno AKUOKOE na KUKUHUDUMIA.

Ngoja nikwambie kitu shetani anafanya hadi unashindwa kusamehe halafu ntakwambia cha kufanya. 1. Ibilisi anajua DHAMBI zako kwa maana yeye ndio amekusababisha UFANYE au amesamabisha watu WAKUKOSEE. Kwahiyo anajua ni wapi ameweka KUFULI ya kukutesa. Ili kuimarisha ile kufuli ikamate sawasawa, unapomwaza “yule mtu” aliye kukosea ghafla unasikia HASIRA au UCHUNGU, halafu analeta VIDEO na PICHA hata na SAUTI ya “yale mambo” ili KUHUISHA ule UCHUNGU na HASIRA ndani yako. Na hii inatokea mara nyingi na UNASHINDWA kumsamehe “huyu mtu” aliyekukosea. 2. Ibilisi anakupa SABABU na VISINGIZIO vya kutokusamehe. Utasikia mtu anasema ndani ya moyo wake au kwa kinywa, “kama kweli uliamua kunisaliti wakati nipo mimi nimekukosea nini?”, “yaani pamoja na kujitahidi kufanya haya yote umeamua kunifanyia hivi?”, nk. Ukisikia SAUTI hizi ndani yako jua ni IBILISI anakuhubiria injili MFU ili ushindwe kusamehe na afanikiwe kukutenga na USO, SIKIO na MKONO wa Mungu na ukose MSAADA wa Mungu. 3. Dhambi inasema! Kila ukisimama kuomba au ukijitahidi kusimama katika BWANA unasikia “sauti ya dhambi” ikipiga kelele moyoni mwako kukuvunja UJASIRI. Kwa lugha nyingine naiita “deni ya dhambi” (guilty)! Kama umewahi kua na deni mtu anakudai na anakusumbua utaelewa nasema nini. Kila ukikumbuka lile deni ni kama “linasema” na wewe huko ndani ya moyo wako kwa sauti! Hii ni vita ya Ibilisi na HUWEZI kuzima hiyo sauti bila MSAADA wa Mungu na Damu ya Yesu. Ndio maana utasikia “kikaribieni kiti cha Rehema kwa UJASIRI kwa Damu ya Yesu”, huu ujasiri unapatikana kwa DAMU ya Yesu.

Kwa sababu MAMBO yako MAZURI na Majibu ya maombi yako kwa WATOTO, KAZI, BIASHARA, nk, yamedhibitiwa na KUTOKUSAMEHE kwako, jua IMEKUPASA kusamehe kwa FAIDA yako KWANZA na sio ya aliyekukosea. Tena, kama unataka uwepo wa Mungu ukutembelee na kukufunika kila wakati na MKONO wake kua pamoja na wewe na USIPUNGUE katika maisha yako ni LAZIMA uondoe UOVU katikati yako. Kumuona Mungu maana yake ni “kumuona akikupigania na adui zako wakishindwa huku na huku na wewe ukiwa mshindi BILA sababu”! Hii lugha ni ngumu lakini sikiliza, Mungu anasema kwa kinywa cha DAUDI kwamba “hii nchi hamkumiliki kwa sababu ya upanga wenu wala mkuki, (sio nguvu zenu, au hamkufanya chochote) ila ni nuru ya uso wangu umewaangazia” sasa kumbuka DHAMBI zako zinaficha USO wa Mungu usiuone! Kwa lugha nyingine pamoja na KUPAMBANA sana na UPANGA wako bado ni NGUMU, ila Yule aliyeondoa UOVU katikati yake nakwambia HATASHINDA kwa upanga, Mungu anatangulia mbele zake na kumpa ushindi bure! Mungu anasema “kabla ya kuomba mimi Bwana nitajibu, na mkiwa katika kunena Nitasikia”. Mungu anamwambia Danieli, “ulipotia tu nia mimi nilijibu” Sasa iweje leo watu wanafunga na kuomba na INAKWAMA? Ondoa UOVU na DHAMBI katikati yako! Sio tu kwa KUTUBU dhambi zako ILA na KUWASAMEHE walio kukosea hata kama ni NGUMU. Kumbuka kwa NJIA mbili zote kwa pamoja 1. Tubu (na geuka) na acha dhambi 2. Samehe dhambi zote watu walizokutendea. HAKIKA utamwona Mungu maishani mwako kwa namna hujawahi kutarajia.

Kwanini unapata ujasiri wa kutenda dhambi? Hii ni SIRI nyingine nataka nikupe kabla ya kumalizia kukupa DAWA ya kupona. Kufanya dhambi inahitaji ujasiri wa aina yake. Umewahi kufikiri mtu anachukua KISU anamchoma mwenzake? Bila ujasiri huwezi. Au umewahi kufikiri mtu mzima anavua NGUO zake mbele za mtu mwingine wa JINSIA tofauti na anazini? Kwa kweli inahitaji ujasiri na huu unaupata kwa Ibilisi. Sasa kabla ya kufanya “hii dhmbi” lazima akupe ujasiri. Utasikia ndani yako “kama huyu jamaa hanijali basi na mimi nafanya ngono na huyu mwingine kwa sababu angalau yeye ananijali”, “kama kila mtu anakula rushwa kwani nini na mimi nisichukue hiki kidogo tu?”, “kama amenirusha hela yangu na mimi simpi msaada”, “kama Fulani alianguka katika uzinzi na yuko kanisani mi naona hii ni ngumu kwa hiyo watu wataelewa”, “watasema mchana na usiku watalala”, “hii ni ZAWADI sio rushwa”, nk., ghafla! unapata UJASIRI kwa kufanya KITU ambacho ni KIOVU ndani yako UKISHUHUDIWA kwamba UNAMKOSEA Mungu ila Ibilisi kashakujaza UJASIRI kwa hiyo unajikaza na KUFANYA. Sasa kumbuka ukifanya dhambi “moja”, madhara huwa yanakua zaidi ya moja! 1. Unauzuia Mkono wa Mungu kukuokoa, Uso wake usikuone, na Sikio lake lisikusikie 2. Unatengwa na Mungu, 3. Unazuia majibu ya mombia yako. Haya mambo matatu yanatokea kwa pamoja! Sasa kumbuka nimetaja matatu ila ni mlolongo wa mambo mengi sana uko hapo. Kwa sababu kuzuiliwa “majibu ya maombi” yako itawaathiri na wale waliokua wanapona kwa WEWE kuwaombea! Kwa maana ni majibu ya maombi YOTE yamedhibitiwa. Unaanza kushangaa watoto wako wanateseka na uko busy kuwaombea na hakuna kinatokea! kumbe kisa HUTAKI kumsamehe baba yao, nk!

Kumbuka siku zote, Ibilisi AKIKUSUKUMA kutenda dhambi sio ili UFAIDI, NO! ni ili akutenge na Mungu na apate nafasi ya KUKUANGAMIZA! Sasa, Neema ya Mungu hututetea (hasa tunapokua wajinga). LAKINI ukilijua Neno hili na ukaufanya moyo wako MGUMU, utaangamia! Kwa maana Mungu hulituma Neno kuwaponya mataifa lakini wasipolipokea Maangamizi hufuata, ila kabla ya HUKUMU lazima Neno litangulie. Unaweza kushangaa nasema nini, lakini ukisoma maandiko utaona Nuhu alihubiri kwa miaka takriban 100 akiwaambia watu watubu, na hawataki NDIPO gharika ikaja. Sememu nyingine tunasoma “aonywaye MARA NYINGI akishupaza shingo itavunjika na dawa hapati”. Hii ina maana KABLA ya shingo kuvunjika Mungu anakuletea Neno MARA NYINGI kukuonya na ukikataa KUTII basi Ibilisi anakumaliza. Sehemu nyingine tunaambiwa kwamba Yesu atakuja kuhukumu Ulimwengu, lakini ni baada ya INJILI kuhubiriwa kwa KILA kiumbe! Ili aije sema mtu sikusikia. Hii ndio tunaita Neema! Ndani ya Neema kuna muda wa Mungu kukusubiri UTUBU, ukichezea huu muda na “kikombe kikijaa” Unaangamia! SIKIA SAUTI yake LEO na UFANYE maamuzi na KUGEUKA.

DAWA ya kupona ni KUZIUNGAMA (kutaja dhambi kwa majina yake) kwa Mungu DHAMBI zako na KUWATANGAZIA wale watu waliokukosea kwamba UMEWASAMEHE BURE! Sasa, sikiliza. Kuwatangazia watu MSAMAHA pia ni VITA, tena NGUMU sana kutokana na MAJERAHA uliyopata “ulipokosewa” na hawa watu. Ndio maana utakuta mtu ANALIA tu kila akikumbika MTESI wake, Jipe moyo, Mungu anaona MAUMIVU yako. Anza na KUMTANGAZIA huyo mtu msamahawa wake kwenye MAOMBI, kisha chukua hatua ya IMANI na kumtangazia masikioni kwamba “NIMEKUSAMEHE bure”! Na ukiona ile hali inarudi huku ndani, kimbilia magotini tena na MTANGAZIE na IBILISI kwamba hii dhambi haipo nimesamehe na Yesu kafuta kwa Damu yake. Sisitiza hili katika Maombi hadi usikie UHURU wa ndani. Ukivuka hapo ndio sasa kile kipengele ya KUSAMEHE na KUSAHAU kitaanza kuwa dhahiri kwako, la sivyo ni NGUMU kibinabadu asikudanganye mtu. Bila Mungu huwezi KUSAMEHE na KUSAHAU, tafuta msaada wa Mungu kushinda VITA ya KUSAMEHE.

Uwezo wa kusamehe mtu (tolerance) Kimungu ni ndefu hakuna awezaye kufikia. Yesu alisema 7x70 kwa siku. Tena ni mtu huyo huyo anarudia kukukosea na kuomba msamaha kwa SIKU! Unatakiwa kumsamehe, hata kama ANARUDIA makosa yale yale. Nakubaliana na wewe kwamba unaweza kukosewa mara “moja” ikawa kubwa kuliko “Elfu”! Sawa, ndio maana nasema ni VITA na unahitaji msaada ya YESU kushinda na UWEZE kusamehe maana madhara ya KUTOKUSAMEHE ni MAKUBWA kuliko unavyofikiri. Kumbuka, kama WEWE unatakiwa uwe na UWEZO wa kusamehe mara 490 kwa siku, Je! Yesu ANAWEZA kukusamehe wewe mara ngapi ukimkosea? Jifunze KUJISAMEHE na KUJIACHILIA mwenyewe maana kila dhambi ULIYOITUBU Yesu alifuta ghafla! Pale ulipoanza tu kutubu.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na Upendo wake Mungu Baba Ukae nanyi tangu sasa na hata milele.

Frank Philip.

Sunday, December 29, 2013

"UPENDO"


(Jua uhusiano kati ya UASI kwenye MAHUSIANO ya kijamii na UPENDO wako kwa Mungu)

Ukifuatilia nyakati katika maandiko utagundua kwamba tunaishi nyakati za mwisho. Tumekaribia mahali ambapo Yesu anarudi kulichukua Kanisa lake. Hakuna ajuaye ni karibu kiasi gani ila ni KARIBU. Yesu anasema yuko malangoni, anakuja.

Yesu alisema dalili ya nyakati za mwisho (Mathayo 24:3-13) na zinaonekana. Ila nataka niongelee MAASI. Huku mwisho wa nyakati tuliko tunaambiwa KUTAONGEZEKA MAASI na UPENDO wa wengi utapoa. Upendo ni kitu cha ajabu sana ambacho Mungu amewaumbia wanadamu. Mtu AKIPENDA ghafla! anakua mtu wa hatari maana huo UPENDO utamsukuma kufanya vitu bila kujali “sana” GHARAMA wala MUDA. Kwa mfano UPENDO wa mtu kwa Mungu utamsukuma huyo mtu kusimama kwa UAMINIFU mbele za Mungu hata kama anateseka na ataridhika na kila kitu kigumu na cha MAUMIVU alimradi asimtende Mungu dhambi. Sasa, UPENDO wa mtu huyu UKIPOA hutaamini vitu ataanza kufanya. Ghafla! visingizio vingi sana vinaibuka na sababu nyingi sana za MSINGI za kumkosea Mungu zinaibuka, ila ukifuatilia kinachotokea kwa huyu ndugu ni kitu kimoja tu UPENDO WAKE KWA MUNGU UMEPOA!

Sasa tunajua kabisa kwamba Mungu wetu ana NGUVU kuliko Ibilisi. Na hakuna siku ibilisi atakinga MSULI kwa Yesu akafanikiwa maana Yesu yuko juu sana katika UWEZA, sana sana ikiibuka vita atamtuma tu MIKAELI akamshughulikie huko na yeye akaendelea kumtizama BIBI ARUSI wake anayempenda sana ambaye ni KANISA. Ibilisi anachofanya hapa kwa wana wa Mungu ni KUONGEZA MAASI kati yao! USALITI katika mahusiano, biashara, familia, ndugu, huduma, nk. Huu usaliti unasababisha watu KUJERUHIWA ndani yao na UPENDO wao UNAPOA bila wao kujua! Wengi sana wamefika mahali pa gumu sana na wameweka SILAHA zao chini kwa sababu wamejeruhuwa na ADUI wakiwa KAZINI. Madhara yake yanapelekea KAZI yao kusimama shambani mwa Bwana, wamebaki KULAUMIANA na SHUHUDA MFU za watu waliowatendea mambo “mabaya” badala ya kushuhudia MATENDO makuu ya Mungu!

Watumishi wengi sana na wana wa Mungu wameacha zile SHUHUDA za “kuokoa” watu na Ibilisi ameanza kuwatumia kusambaza shuhuda KANDAMIZI za kurudisha watu nyuma! Ushuhuda ni habari NJEMA! Hili ndilo jina jingine la INJILI, habari njema kwa watu wote! Sasa, watu wengi sana wamewekeza kwenye habari MBAYA za watu na zimewavunja wengi sana moyo (hasa wachanga katika imani) na kuwajeruhi badala ya kuwajenga! Hayo MAASI ambayo yametokea, na WEWE mwana wa Mungu umejeruhiwa na umepata UCHUNGU na kwasababu hujashughulikia uchungu wako UMENAJISI wengi kanisani na madhara ya ule UASI “mmoja” umekua JANGA kubwa maana umesambaa na KUZIMISHA upendo wa WENGI kwa mara moja bila wewe kujua. Tunaonywa tuangalie “shina la UCHUNGU lisichipuke ndani yetu” maana UCHUNGU ndani ya mtu mmoja una uwezo wa kunajisi watu WENGI ambao hawakuhusika katika TUKIO lililosababisha huo uchungu. Chunga sana hili ENEO maana unaweza kujikuta umegeuka kuwa mtumishi wa Ibilisi kusambaza UCHUNGU bila kujua na ukamfanikishia Ibilisi kazi yake ya KUNAJISI watu!

Nitatoa mfano wa huduma ya Yesu. Wakati huduma ya INJILI inaendelea kwa kasi kubwa, Petro na wenzake “wako tayari kupigana kwa upanga kumtetea Yesu hadi kufa”, na ikafika mahali Petro anatoa upanga ALANI mwake kwa ajili ya kumlinda Yesu, na alijikuta anakata mtu sikio ghafla, aliona huyu jamaa anamsogelea Yesu. UPENDO kwa Bwana wake ukamsukuma “kupiga mtu”. Kabla Petro hajakaa sawa anaona YUDA, ambaye ni MTUMISHI mwenzake hapo pembeni anachukua RUSHWA, kabla hajakaa sawa anaona ANAMBUSU Yesu hadharani, kabla hajakaa sawa anaona Bwana wake AMESALITIWA LIVE na sasa ANASULUBIWA! Na aliyemsaliti ni MTUMISHI mwenzake ambaye wamefanya HUDUMA pamoja kwa takriban mika 3! Yesu alimwamini YUDA kiasi cha kumfanya MWEKA HAZINA wa HUDUMA yao. Leo machoni pa kila mmoja wao katika HUDUMA na wakiwa KAZINI anamsaliti Bwana wao! Hili jambo liliwasambaratisha wote wakatawanyika, sio kwa hofu tu ya wale waliokua wanamsulubu Yesu lakini pia ile hali ya UASI iliyojitokeza imeathiri UPENDO wao na WAKARUDI nyuma!

Kabla Petro hajakaa sawa anaulizwa “wewe si ulikua na huyu jamaa”, Petro anasema SIMJUI mtu huyu! Hataki hata kutaja jina la Yesu, safari hii anamwita “mtu huyu”! Mara tatu anamkana YESU hadharani! ila kilichotokea kabla ya hapo ni UASI mkuu na USALITI wa waziwazi! Wanafunzi walitawanyika kwa sababu “mchungaji wao amepigwa”. Petro akarudi zake KUVUA samaki ziwani, akaachana na BIASHARA ya Yesu maana UPENDO umepoa! Huyu ni Yule Petro ambaye alisema “hata wakikuacha wote mimi sitakuacha, niko tayari kufa kwa ajili yako, nk”. Sasa kimetokea nini? Upendo umepoa. Yesu alipofufuka akamtafuta tena Petro, akamuuliza “Petro UNANIPENDA?”, akarudia mara ya pili “Petro UNANIPENDA?” na mara ya tatu kurudia Petro AKALIA! Na akamwambia “Bwana unajua nakupenda…”. Ninachotaka uone hapa ni ile hali ya KUKATA TAMAA na KURUDI nyuma ya Petro baada ya VURUGU nyingi kutokea katika HUDUMA yao. Na YESU alikua ANAHUISHA ule UPENDO kati yao ambao ULIATHIRIKA. Hapo wakati Yesu anampa Petro kazi unaweza kujiuliza kwanini amuulize kwanza “unanipenda” ndio asema “LISHA KONDOO”, “CHUNGA KONDOO”, nk.? Sababu ya msingi hapa ni HUWEZI kufanya kazi ya MUNGU kama HUMPENDI! Jaribu uone halafu mbwa mwitu aje kama hujakimbia na kuacha KONDOO wanaliwa huko! Nakwambia mchungaji ANAYEPENDA kondoo zake “itamgharimu” maisha kwa kondoo hao. Sio mimi, ni maandiko yamesema.

Sasa katika maisha ya leo wengi wetu tumejeruhiwa sana na “watu” katika michakato mbalimbali ya maisha na kwa sababu UASI umeongezeka UPENDO wetu kwa Mungu na kwa “hao watu” umeathirika kwa viwango tofauti. Wengine WAMEACHA wokovu na wengine WAMERUDI nyuma. Sasa Ibilisi akifanikiwa kukurudisha nyuma, ukampa nafasi ya kurudi pale alikofukuzwa wakati unampokea Yesu, huwa anaongeza “idadi ya MAPEPO mara 7, tena wale waovu zaidi, na hali ya mtu huyu inakua mbaya kuliko ya mwanzo”! ili akifanikiwa “akuchinje” kabisa usije ukatubu!

Ukifahamu SIRI hii utagundua ni kwanini MTU akisalitiwa katika MAHUSIANO ni rahisi sana kurudi nyuma katika WOKOVU pia! Ule UASI una NGUVU ya KUPOOZA upendo wako kwa Mungu na kukumaliza kiroho USIPOANGALIA. Katika NDOA, HUDUMA, MAKANISANI, nk. kumekua na hiki kitu cha KUSALITIANA na kimeathiri kazi ya Mungu kwa kiwango kikubwa sana kwa sababu kimegusa eneo nyeti la UPENDO. Ni jambo la kusikitisha sana “mmoja” katika HUDUMA au NDOA anakua AGENT wa shetani “kwa muda” (bila kujua) kama ilivyokua kwa YUDA. Na kwa kipindi kifupi anatumika kufanya KITU ambacho kitasambaratisha HUDUMA au NDOA moja kwa moja. Ibilisi akimwachia huyu mtu (kwa maana ilikua kwa kitambo tu) akizinduka, anajuta! Ndio maana YUDA alikimbilia KITANZI na wala ile RUSHWA hakuila! Alisikia vibaya sana baada ya KUFANYA ule UASI na USALITI na akachukua ile HELA na kuirudisha kwa wenyewe! Too LATE! Yesu yuko msalabani saa hizo na huku huduma ishasambaratika WATUMISHI wenzake akina Petro nao “washaharibu” na akina Yohana na wenzake washatokomea kusikojulikana. Yesu alipofufuka alifanya kazi ya KUWAKUSANYA hawa wanafunzi wake kwa UPYA baada ya kusambaratika vibaya.

Angalia mambo ya kwanza uyape umuhimu wa kwanza. Watu wengi sana wako busy na HUDUMA na kusahau kwamba UPENDO ni msingi wa YOTE. Mungu havutiwi sana na hayo mambo kama HUMPENDI, na utakosa Ufalme wa Mungu usipojipanga pamoja na huduma yako kubwa nchi nzima au hata dunia nzima. Kumbuka (1 Wakorintho 13:1,2) “Tena nijapokuwa na UNABII, na kujua SIRI zote na MAARIFA yote, nijapokuwa na IMANI TIMILIFU kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina UPENDO, si kitu mimi. 2 Tena NIKITOA MALI ZANGU ZOTE kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.” Shughulikia eneo lako la UPENDO wa KWANZA na Yesu. Fanya “toba” ya dhati ukikiri (kutaja kwa jina) pale “ulipoa anguka” maana unatakiwa UPAKUMBUKE na kumwambia Yesu, na kisha omba “maombi” yako ya dhati ili KUHUISHA ule UPENDO wa kwanza, na utaona mabadiliko na BARAKA zikimiminika kwako kwa namna ya tofauti.

Lengo la somo hili ni kukutahadharisha kuwa tuko nyakati za hatari. UASI ni mwingi na usipoangalia unaweza KUPOOZA UPENDO wako wa KWANZA! Na Yesu anasema na wewe akijua “umeuacha ule UPENDO wako wa kwanza”, ule ambao ulikuweka chini ukasoma Neno na kuomba na KUSHUHUDIA au kumtumikia Mungu katika ngazi mbali mbali. Naye anasema “kumbuka ni wapi ulipoanguka ukatubu”. Fanya HARAKA kwa sababu hizo njia za YUDA kweli zitakupa HELA, ila ni vipande 30 tu! Kumbuka thamani ya DAMU ya Yesu iliyokununua, FANYA uamuzi LEO kama UNAZIDI kumsaliti MWANA wa MUNGU au unamrudia. Mungu atusaidie kufanya maamuzi sahihi. NEEMA ya BWANA na iwe JUU yako tangu SASA na hata milele. AMEN.

Frank Philip.