Saturday, January 26, 2013

HII NI TAARIFA YA MWIMBAJI WA KITANZANIA WA NYIMBO ZA INJILI "RACHEL SCHARP" ANAYEISHI NCHINI SWEEDEN KWA WATANZANIA WOTE KUPITIA VYOMBO VYA HABARI WEEKEND HII!!


Press release

KARUBUNI sana wanahabari katika hafla yetu hii fupi yenye lengo la kumpa Mungu wetu utukufu.
Mimi ninaitwa Rachel Scharp, ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili, ninaishi Malmo, Sweden. Lakini kwa
sasa nipo nyumbani kwa ajili ya utambulisho wa Albamu yangu ya Muziki wa injili.
Uimbaji kwangu ni maisha kwa kuwa nilianza kuupenda muziki na kuimba kuimba nikiwa mdogo sana,
nilikuwa nikitunga nyimbo na kuwafundisha wadogo zangu. Tuliimba nyimbo hizo jioni, haswa kipindi
kile cha ugawaji ikiwa zamu ya Kaya yetu, ile foleni ya kununua mchele ilivyokuwa ndefu chakula
kilikuwa kinachelewa, ili wadogo zangu wasilale bila kula na furaha ya kusubiria ubwabwa na maharage
basi tunaimba kusubiria msosi, Wakati huo hakukiuwa na Tv. kama ilivyo sasa.

Niliimba Kwaya ya shule pale “Jangwani Secondary” pia niliongoza sifa na kuabudu Kwenye fellowship
katika kanisa la Msewe Lutheran . Nilikuwa nikiandika nyimbo nyingi nikitegemea kupata fursa ya
kurekodi au kuimba na Kwaya nyimbo zangu, lakini sikupata fursa hiyo.

Kwa sasa ninaimba Kwaya kanisa la Elim Pentecostal huko Malmo kusini mwa Sweden, ninaongoza sifa
na kuabudu. Ninaimba pia kwenye kundi linaloitwa Shalom International ambalo ni muunganiko wa
waimbaji kutoka makanisa mbalimbali ya kiroho yaliyopo mjini Malmo. Nilipata fursa ya kurekodi album
yangu ya kwanza mwaka 2008 ikazinduliwa huko Sweden, Mai mwaka, 2009 nikisindikizwa na dada
Upendo Kilahiro. Album hiyo niliita 'Naringa na Yesu' yenye nyimbo 9, iko Kwenye mfumo wa sauti tu.

Leo ninatambulisha album yangu ya pili yenye jina la 'Ni Mungu wa ajabu'. Album hii Ina nyimbo kumi
zilizo Kwenye mfumo wa sauti (audio), na 8 Kwenye mfumo wa picha na sauti (DVD).
Nimerekodi album hii Oktoba mwaka 2011 nchini Sweden, kwa upande wa mpangilio wa vyombo na
muziki nikisaidiwa na Paalab Nyarko, kutoka Ghana na producer Zolile Matikinga(Zorro) - kutoka South
Afrika.

Mwanzoni mwa mwaka 2012 niliongeza baadhi ya vionjo vya muziki kwenye studio za New Life band
Arusha, vionjo nilivyoingiza ni gitaa la solo lililopigwa na Godlucky Matingisa wa New life band Arusha,
Base Gitaa limepigwa na Wilsson Godfrey Mtangoo. Ngoma zilipigwa na Fujo Makaranga . Na sauti pia
niliingiza hapo Arusha nikisaidiwa na Jackson Benty, chini usimamizi na uangalizi wa producer Wilsson
Mtangoo. Mwalimu wa sauti mchungaji David Nkone.

Video imerekodiwa na UMU production Arusha chini ya uongozi wa Jojo Jose Mwakajila. Video hii
imerekodiwa Sweden (Malmo), Ujerumani (Berlin), Tanzania (Dar es Salaam, Bagamoyo, Arusha ,Moshi,
Serengeti).

Midundo ya nyimbo hizi ni ya kiasili (kitamaduni), Napenda nyimbo zenye vionjo vya Kiafrika na
kitanzania zaidi. Nimeimba kwa kiswahili na kiingereza pia. Na nyimbo nyingi ni za kiswahili, hii
haimaanishi kwamba soko liko nchi wanazoongea kiswahili tu. cha kushangaza ni kwamba pia nch za
Scandinavia wanapenda sana kiswahili na kukithamini, na nafikiri kuliko hata sisi wenye lugha.

Wanasema kwamba ni lugha yenye sauti tamu nami sina budi kujivunia na kuiendeleza na huku
nikimsifu Mungu na kupeleka ujumbe kwa Watu wake.

Nyimbo hizi zimebeba jumbe mbalimbali, kuna za kumsifu Mungu na matendo yake makuu, kuna za
maonyo na kuna za kutia moyo kwa safari hii ngumu ya kwenda mbinguni.
Ningependa sana watu wapate ujumbe huu na wakutane na Mungu katika maeneo hayo tofauti kama
nilivyoeleza mwanzoni kuwa kuna kumsifu na kumwabudu Mungu, kuonywa na kutiwa moyo pia.
Inategemea mtu yuko kwenye hali gani na ana mahitaji gani.

WITO WANGU KWA JAMII

kwanza ni kupenda na kuthamini kile tulicho nacho Mungu alicho tupatia.
Kwanza kwa sisi wakristo tumepewa Neema hii ya wokovu tunatakiwa tuipende, tuithamini, tuitunze na
tuiendeleze, tusiichezee na tuwafanye wengine pia waijue na waipate.
Kama tusipoipenda, tusipoithamini, kujivunia na kuilinda, wengine hawatajua thamani yake.

Nikaja kwenye jamii yetu kwa sasa tunapenda sana kuiga kutoka nje tunaacha ya kwetu, sikatai kuiga
yale yaletayo maendeleo, na tunahitaji kujifunza kutoka kwa walioendelea, lakini si kwamba tuvipuuzie
vya kwetu. Kuna vyetu vinavyohitaji mwendelezo.na tena vikawa vizuri sana na wa nje wakaiga kutoka
kwetu. Kwa Mfano; muziki wetu , lugha yetu na vingine vingi.

Kwa upande wa muziki, watanzania siku hizi wanapenda sana muziki kutoka Afrika kusini, ni mzuri sana
hata mimi napendezwa nao. Naona sasa waimbaji wengi wanapenda kupiga mtindo huo. Ule ni muziki
wa asili wa ngoma zao za kienyeji ukawekwa/ukaongozewa vionjo vya kisasa.

Sasa na sisi tutakapopiga muziki huo hautakuwa mzuri kama wanavyopiga Joyous Celebration kwa kuwa
ndio asili yao. Swali ni kwamba, kwa nini na sisi watanzania tusitengeneze lizombe letu au Mdumange au
Sindimba na hata Mdundiko tukaweka vionjo vya kisasa ukawa mzuri tu na wao waige kutoka kwetu?
Nilazima tujitahidi jamani tuwe na utambulisho wetu (identity). Kwamba ukisikika muziki uutambue
mmmh Huu ni muziki wa Tanzania, tunahitaji ubunifu tu kuondoa uvivu wa kufikiri. Kama tukitulia na
kubuni na kutumia vipawa tulivyopewa na Mungu tutafika mbali sana na sio kupita njia ya mkato ya
kuiga tu.
Namalizia kwa kuwaambia watanzania, tusiende kwa mazoea eti watu wamezoea hivi. Huu ni wakati wa
mabadiliko, tubadilike turudi kwetu. Tutafika mbali. watanzania tunaweza, na kuleta mabadiliko ni mimi
na wewe.

Asanteni sana kwa kuja kushiriki pamoja nami tukio hili la Baraka. Mungu awabariki sana.

Rachel Scharp

Saturday, January 12, 2013

Tuesday, January 8, 2013

MAISHA YA UREMBO NA WOKOVU(2)

SHALOM WATUMISHI WA MUNGU!!!
MWAKA JANA MWISHONI TULIANZA KWA KUANGALIA MAISHA YA UREMBO NA WOKOVU NA SASA NI MUENDELEZO WA PALE SOMO LILIPOSHIA...

"UREMBO WAKO UNAVYOWEZA KUTUMIKA KATIKA MATANGAZO MBALIMBALI"

IKIWA wewe ni mrembo,Urembo wako unaweza Kutumika katika matangazo mbalimbali ya bidhaa: katika kipengele hiki, unaweza kutumika katika kutangaza biashara mbalimbali ilimradi tu sio kwa style iliyo nje ya maadili ya wokovu au sio katika bidhaa ambazo hazimpendezi Mungu kama kilevi nk.

Pia katika matangazo haya, hata kama ni tangazo la bidhaa kama mafuta, sabuni, au makampuni ya simu nk. Utaangalia ni sehemu gani tangazo hilo linafanyikia na ni aina gani ya mavazi unayotakiwa kuvaa, kama ni mavazi ya heshima sio mbaya kama ukifanya kwani itakuingizia kipato.

Katika suala hili la urembo, mtu wa Mungu kupendeza na kuonekana nadhifu sio dhambi jamani, kwasababu utamkuta mtu zile nguo mbaya mbaya ndo anaenda nazo kanisani, ila ukimkuta amealikwa sehemu unaweza kumsahau, anavaa vizuri sana na anapendeza. Hebu tubadilike, tuwe smart wakati wote, na hata kama una nguo zako mbili tu, jaribu kuziweka katika hali ya usafi. Na hakikisha umepaka deodorant yako vizuri (hii ni muhimu sana wapendwa, maana tunapokua makanisani tunacheza kwa furaha tukimtukuza Mungu wetu, huwa hatujali hata tukitoka jasho kiasi gani, ila unapokuwa umepaka deodorant utaepukana na kukwaza wengine, badala ya kuzama katika kumsifu Mungu, harufu ya jasho lako inawaharibia step) na pia unajipaka perfume kama unayo ila sio lazima, osha na utengeneza nywele zako vizuri, pasi nguo zako nk. Hakikisha kupitia wewe, kuanzia tabia yako, mpaka muonekano wako wa nje vinamtukuza Mungu, sio watu ambao hawajaokoka wakikuona waseme kama wokovu wenyewe mtu anakua rough hivi siokoki, hii ni mbaya kabisa wapendwa katika Kristo.

Mungu atusaidie ili tuweze kumtukuza kuanzia kwenye matendo, kuongea kwetu na muonekano wetu wa nje.
Yesu akubariki.

Na Upendo Benson

.......ITAENDELEA!!!!

Sunday, January 6, 2013

A DEEP SUMMARY ON.... PRAISE AND WORSHIP....(12)

Being my first sermon of the year and the last in a series of A  Deep Summary session on Praise and Worship, I am grateful to God for taking us through this journey as we have been exploring some truths and facts about praise and worship.

Today we are going to see the role of music in praise and worship. Personally, I love music, the whole issue of singing and playing musical instruments!
I remember when I was a child, I was shy if not afraid of singing in front of people. I was in a Sunday School Choir but in really sense it was just because I could not quit, being a child I had to listen to my elders and be in the choir.
As I was growing, I met different people who did so much with music and I was inspired and since then, I knew that God has put some music in me.

There are different kinds of songs and music that people sing. Let us see how does music relate to praise and worship. First of all, the bible encourages us to praise God with musical instruments. If you read from the book of Psalms 150, there are different instruments mentioned which can be used to praise God. You can play instruments with a heart of worship, with a heart of praise.

We also read from Psalms 27:6 "Then my head will be exalted
above the enemies who surround me;
at his tabernacle will I sacrifice with shouts of joy;
I will sing and make music to the Lord.NIV
The Psalmist plans to sing and make music to the Lord as a way of giving Him praise!


One thing to remember is that, the relationship the musician has with God is more important than the music itself. Being an important sector, even David put special people (1 Chronicles 6:31-32 "These are the men David put in charge of the music in the house of the Lord after the ark came to rest there. 32 They ministered with music before the tabernacle, the Tent of Meeting, until Solomon built the temple of the Lord in Jerusalem. They performed their duties according to the regulations laid down for them. "
NIV)

We have seen the meaning and so much explanation on praise and worship in the previous lessons, all that can be put in music.
A few things to keep in mind


  • Spiritual music comes from spiritual people.
  • It is a good thing to seek standards in music but remember your heart sings louder than your mouth so be careful of what it fills your heart.
  • We can use music as a vessel to carry the praise and the worship from our hearts.
  • The tempo of the music does not specify whether we are praising or worshiping.
I give all the glory and honor to God Almighty! God bless you so much with all the blessings both physically and spiritually...!!!


                                       THE END!

Wednesday, January 2, 2013

HERI YA MWAKA MPYA 2013 NA KARIBU TENA GoStaBa Blog KWA AWAMU NYINGINE TENA!!!

Shalom!!

Nawasalimia watu wote katika Jina la Yesu lipitalo majina yote!!! Naamini kila mmoja ni mzima wa afya, zaidi wewe unayesoma hapa sasa!!

HONGERA SANA KUCHAGULIWA KUONA MWAKA 2013, NINATAMBUA SIO KWA UJANJA,AKILI AU UWEZO WETU BALI NI KWA NEEMA YA MUNGU!!

Mambo muhimu ya kuzingatia ni haya;

1.UMERUHUSIWA KUONA MWAKA MPYA 2013, SI KWASABABU UNA STAHILI SANA KULIKO WALIOTANGULIA, HIVYO NI NAFASI YAKO YA KIPEKEE KUJENGA UKUTA MAHALI PALIPOBOMOKA ILI SASA UWEPO UKAMILIFU NDANI YAKO.

2. UMEBAHATIKA KUINGIA MWAKA 2013 KWASABABU HUJAMALIZA KAZI ZAKO, HIVYO USIJARIBU KUISHI KIHASARA HASARA,HAKIKISHA UNAISHI MAKUSUDI YA MUNGU KILA SIKU!

3. MUNGU AMEKUACHA UISHI TENA MWAKA HUU 2013 KWASABABU ANA AGENDA NA WEWE, NI MUHIMU SANA KUOMBA ILI UJUE BWANA ANA AJENDA GANI NA WEWE,HILI NI MUHIMU KUMSIKIA MUNGU VIZURI MAANA KILA MTU ANA AJENDA TOFAUTI NA MWINGINE!!

Yamkini umepokea nabii nyingi sana kwa habari ya mwaka huu mpya,lakini  nataka nikwambie hakuna hata mmoja utakaotimia maishani mwako kama ukiwa nje ya network ya Mungu,inakupasa kubaki nyumbani kwa Bwana,kuomba sana, Kula neno la Mungu na kumwamini Mungu bila shaka yeyote ndani yako!!

INAWEZEKANA MWAKA HUU UKAWA MZURI SANA KWA WENGINE ILA UKAWA MGUMU SANA KWAKO,YOTE YANATEGEMEANA NA IMANI YAKO NA KUJIPANGA KWAKO MBELE ZA MUNGU!!!

Kipekee ninamshukuru Mungu kuingia mwaka mpya na ninaamini nina mengi sana ya kufanya katika Ulimwengu huu,ahsante kwa technolojia kunifanyia madhabahu ya kanisa hili huru la mtandaoni,naamini umeendelea kujifunza mengi na ni matarajio yangu kuwa utajifunza mengi zaidi!!

KWA NIABA YA TIMU NZIMA YA BLOG HII,NINAOMBA NIWATAKIENI KILA LAKHERI NA MAFANIKIO MENGI KATIKA MWAKA HUU WA 2013 NA KARIBU TUENDELEE KUJIFUNZA NA KUKUA KIROHO KWA KUSUDI TU LA KUUJENGA UFALME WA MUNGU HAPA DUNIANI,AMEN!!

Na 
Fredy E.Chavala
President-Chavala Ideas Platform
Box 34048
Dar es salaam
+255-(713/753)-883 797
lacs.project@gmail.com