Showing posts with label Youth Platform. Show all posts
Showing posts with label Youth Platform. Show all posts

Thursday, July 23, 2015

“KIJANA NA MALENGO”


Shalom ndugu msomaji,yaani Amani iwe kwako!
Habari yako kijana? Naamini unasoma hapa ukiwa na utulivu kabisa moyoni na akili timamu kichwani!

Najisikia vizuri kusema nawe kwa habari ya “KIJANA NA MALENGO”
Kwanza natamani tuanze kwanza kwa tafakari na maana ya maneno haya mawili:
KIJANA: Ziko tafasiri nyingi kuhusu kijana ila mimi niseme tu, Kijana/Ujana ni hatua ya kati ya ukuuaji wa binadamu toka “Utoto” kwenda “Utu Uzima/Uzee”; na ndio katika hatua hii mtu anakuwa na nguvu nyingi,ari kubwa ya kufanya mambo, uwezo wa kufanya chochote na udadisi wa kutaka kujaribu kila kitu.  Kijana kwasababu anazo nguvu anategemewa nay eye mwenyewe,familia na jamii yake, nchi yake, dunia yake na hata Kanisa na Mungu wake.

MALENGO: Ni mipango, mikakati na matazamio yenye nia, yanayojenga tumaini la mwongozo wa kesho ya mtu. Malengo ni shabaha ya mbali ya kuifikia, ambayo humpa mtu ujasiri na juhudi ya kufika pale. Malengo ni ramani na barabara ya kupita kufikia hatma yako. Unaweza kutafasiri Mipango peke yake, lakini hakuna mipango wala mikakati bila Malengo na hakuna ndoto ya maana bila Malengo.

Kabla ya kuianza safari malengo huwa ni mipango tu,ila mara unapofikia mwisho wa safari hiyo, malengo huwa ni faida ya matokeo ya safari hiyo!

SASA KWANINI KIJANA NA MALENGO?

Ujana ndio hatua amabayo mtu ana nguvu ya kupanga na kutenda,na ni hatua ambayo mtu amepevuka kimajukumu na anategewa na kila amtazamaye, hususani yeye mwenyewe binafsi, hivyo ni muhimu kuwa na ndoto ama maono makubwa, si juu yake binafsi,maana huo ni ubinafsi, bali kwa ajili ya watu wengine wanaomhusu kama jamii yake, Taifa lake na kanisa kwa ujumla!
Sasa hayo maono na ndoto kubwa haziwezi kufikiwa ama kutimia kwa mara moja, ni hatua kwa hatua, na hapo ndio tunapata umuhimu sasa wa kujiwekea malengo ambayo hufikiwa kupitia mipango.

Ni Zaidi ya muhimu,kwa kijana kuweka malengo kwasababu zifuatazo;

1.       “Asiyejua aendako huwa hapotei, na kila njia aishikayo ni sahihi kwake”

Msemo huu unamaanisha kuwa bila kujua unakotaka kwenda kila njia iliyo mbele yako itakufikisha, uhalisia ni kuwa ukifuata njia yoyote utafika mahali njia inakofika na sio wewe unakopaswa kufika, huapaswi kupoteza muda, nguvu na rasilimali kubahatisha kufanya mambo, maana maisha sio bahati nasibu na wala sio mazoezi, ila ndio yanaendelea hivyo, kila sekunde ipitayo ndio imeshapita na kila hatua urukayo ndio umehsaruka, sasa ili uwe makini, uwe na hakika na safari yako kuelekea kesho yako, ni muhimu sana kujiwekea malengo, ambayo yanakuwa kama ramani yako kuifikia hatma ya matarajio yako maishani.

2.       “Huwezi kupima kipimo chochote bila kipimio, na huwezi kufananisha kitu chochote bila kifananishio”

Sijui kama ni lugha sahihi, lakini kimsingi kila kipimo kinachofahamika hapa duniani kina kifaa Fulani ambacho huitwa “kipimio” kwa mfano uzito utapimwa kwa mzani; hali kadhalika urefu,kina, ukubwa, ujazo na vinginevyo navyo vina vipimo vyake. Pia huwezi kufananisha kitu,bila kuwa na kingine cha kufananishia, yaani huwezi kusema huyu Anafanana au huyu ni mfupi ama huyu ni mnene bila kwanza kuwa na mwingine aitha halisi au kichwani mwako unayemfanisha ama kumlinganisha naye. Naam na Malengo ni kama Kipimio cha shabaha yako na kifananishio akilini mwako ambavyo vitakusaidia uwe na juhudi na nia thabiti ili ufike mahali ambapo unaweza sasa kupima uhalisia na kipimio kiitwacho malengo na kufanisha na kifananishio hicho. Ukiweka malengo ni kama unayo picha halisi kichwani ambayo bado kuifikia, na mara utakapoendelea na kufika hatua Fulani, ni rahisi kuangalia uhalisia wa jambo kama umefika ama unakaribia ile picha ya malengo iliyo kichwani mwako.

3.       Malengo kama picha ya shabaha, yatukusaidia kuamua na kupanga vema juu ya mahitaji yahitajikayo kufika pale. Yaani ukiwa na ile picha ambayo unatamani kuifikia, ni rahisi sasa kujua unahitaji nini na unamwitaji nani kwa hatua gani na kwa muda gani ili kuitimiliza hiyo nadharia ambayo sasa ni picha na iwe halisi.

4.       Malengo ni kichochezi chanya cha juhudi ya mtu kutumia sawasawa uwezo wake wa juu ili kupata matokeo bora ya kile anachokitarajia. Bila malengo mtu anaweza kubweteka na kutumia kiasi kidogo sana cha uwezo wake wa kufikiri na kutenda, na akajikuta anapoteza muda wake na nguvu zake kwa mambo yasiyoeleweka na yasiyo na tija.

Pamoja na yote hayo, malengo sio bima ya kufikia hatma ya jambo lako, unaweza ukashindwa na kuanguka mara kadhaa katika jambo hilo, naam hata ukaamua kubadilisha namna ya kufanya jambo hilo, lakini bado Malengo yanabaki kuwa dira, ama shabaha ambayo kwa njia yeyote ile lazima uifikie na labda na kuipitiliza kabisa.

Ili upange malengo vema yanaweza kufikiwa ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo;

i.Ni lazima Uwe na taarifa sahihi na za kutosha kuhusu jambo hilo unalolipangia malengo, na hata kama sio zote basi zile za msingi zinazokupa ujasiri wa kuamini kuwa inawezekana;

ii. Kama ni jambo la kitaalamu, basi uwe na hakika na ujuzi ulio nao, ama uwe na hakika na wataalamu ulio nao na ujiridhishe na ujuzi ama taarifa walizo nazo kuwa zimethibitishwa.

iii. Lazima uzingatie matumizi mazuri ya muda, upange mipango inayoweza kutekelezeka katika muda unaoamini unafaa, usijibane sana ukalipua na usijipe mwingi kupitiliza ukabweteka.

iv. Lazima uwe na hakika na mahitaji pamoja rasilimali zinazohitajika ili kufikia malengo yako, na hapa namaanisha zote, yaani rasilimali watu, rasilimali vitu na fedha.

v. Lazima mazingira yawe yanaruhusu bila shida jambo hilo, yaani mazingira asili pamoja mazingira ya utawala wa nchi. Lazima uwe na hakika kuwa unalotaka kufanya haligombani na mazingira wa sharia na taratibu za nchi.

Lakini pia malengo humfanya mtu azidi kujifunza na kutafuta taarifa Zaidi kuhusu jambo ambalo ameanza kulifanya, pia malengo yanamsaidia mtu kupata watu sahihi wa kushirikiana nao, mahali sahihi pa kufanya jambo kwa wakati sahihi.

Najua unayo maono na ndoto nyingi sana kijana, na unatamani kama zingetimia hata kesho, najua unatamani kuishi maisha Fulani hivi yasiyo na bugudha na unatamani kuwa akina Fulani wenye hela zao, ni sawa inawezekana kabisa kuwa vyovyote utakavyo, na Mungu ameweka uwezo ndani yako kutimiza chochote ukusudiacho kufanya, sasa ili ufike huko utakapo, kwanza imekupasa kujitambua vema na kujikubali, kuwa wewe mwenyewe halisi na wala usitamani kuwa kama yeyote yule umtamaniye, maana hata ufanye juhudi gani hautaweza; Usishindane na yeyote wala usigombane na mtu, wewe tazama mbele yako, ona ile picha kicwani mwako unayotaka kuwa, kisha panga mikakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu ambayo itakuwezesha kuyafikia malengo yako. Usitamani kufika haraka, uwe na subira na usiruke hatua wala kutaka njia za mkato, tembea hatua kwa hatua, ongeza juhudi, imarisha Imani yako na nia na kaa mahali sahihi na watu sahihi kila siku, na mimi ninayo hakika kuwa lazima utayafikia tu malengo yako siku moja.

Kijana malengo yatakusaidia kuwa na adabu na muono wa mbali katika yale uyafanyayo sasa, unataka kuwa mwandishi mzuri, jiwekee malengo ya kusoma vitabu kadhaa kila mwezi; Unataka kuwa kiongozi, jiwekee malengo ya kufanya jambo moja la kijamii kila baada ya wakati Fulani; Ama niseme unacheza mpira sawa, basi jiwekee malengo ya kucheza mpira Afrika ama duniani na anza juhudi ya zoezi sasa, Una malengo ya kuajiriwa mahali Fulani, basi anza kujifunza kidogo kidogo kuhusu watu hao, naam ukipata nafasi ya kufanya mazoezi hapo, fanya Zaidi yaw engine, kwa uaminifu na juhudi kubwa nao hawatakusahau hata iweje. Unatamani kujiajiri ama kuja kuwa mfanya biashara mkubwa duniani, ni vema, basi jiwekee malengo ya kuweka akiba na kuanza kuzungusha hela kidogo kidogo na uone kama hautayafikia malengo yako.

Najua unaweza kuwa unatamani kuwa maarufu, sijui ni kwanini na yamkini hata wewe mwenyewe hujui hasa kwanini unatamani, ila nataka nikwambie kitu kimoja tu, kama ukiwa halisi, ukiwa makini na nia thabiti katika yale uyafanyayo kwa juhudi na uthabiti mkubwa, basi uwe na hakika, kazi yako itakutangaza tu, na kwakuwa hakuna pilau nzuri ipikwayo isinukie, basi nawe kupitia hayo uyatendayo utakuwa maarufu tu, hata kama hutaki!

Mungu akubariki na kukuwezesha katika yote ufanyayo, naam na Roho wake wa Ufahamu akufundishe na kukufunulia yale yote unayohitaji kuyajua ili kutimiliza kusudi la kuishi kwako hapa duniani kwa faida yako na wote wanaokutegemea….Nenda sasa kijana ukajiwekee MALENGO, Na saa ile ikifika YAKATIMIE! Amen!



Na
 Fredy Erasto Chavala (King Chavala-MC)
(Mwalimu na Mshauri wa Vijana/ Mzungumzaji wa hadhira/Mshereheshaji/Mchekeshaji/Mwandishi na Mtaalamu wa Biashara na Utawala kitaaluma)
+255 713 883 797

Barua pepe: lacs.project@gmail.com

Saturday, October 26, 2013

HATIMAYE MBUYU MKONGWE (SAMUEL SASALI) UMEANGUSHWA NA DK MILEMBE MADAHA LEO 26/10/2013!!!

CERTIFIED MR SAMUEL AND MRS MILEMBE SASALI
SASA HAWA NI MUME NA MKE RASMI NA HIVYO NDIO VYETI VYAO VYA NDOA!!
NA HIYO HATUA HAPO JUU ILIFIKA BAADA TU YA KIAPO CHA KILA MMOJA KWA MWENZAKE PAMOJA NA PETE YA AHADI YA NDOA NA KUTUNZA KIAPO HICHO
 VAA PETE HII,IWE ISHARA YA AGANO LANGU KWAKO.....
 VAA PETE HII.....
GROOM'S MEN PAMOJA NA SAMUEL SASALI

MAIDS KUMPAMBA MILEMBE
KULIKUWEPO GROOM'S MEN NA MAIDS 30 KUIPAMBA HARUSI HII YA PAPAA SEBENE!
WALIINGIA KWA FURAHA SANA NA KILA MMOJA ALIFURAHIA UCHANGAMFU WAO

MR SAMUEL AKIONGEA NA KUMSIFIA MKEWE
MRS MILEMBE MADAHA WA SAMUEL AKIONGEA
TUKAPATA KUSIKIA SAUTI ZAO,WAKASEMA NA HATIMAYE WAKAPUMZIKA KIDOGO KABLA YA KUANZA ZOEZI LA KEKI!
MR & MRS SAMUEL AND MILEMBE SASALI
HATIMAYE WALIKATA KEKI NA KULA NA

KIPEKEE WALITOA ZAWADI YA KEKI KWA WATU WAO KADHAA MUHIMU SANA, AMBAO WAMEKUWA MSAADA KWA KILA MMOJA WAO NA KWA MAHUSIANO YAO.....BAADHI YA WALIOPEWA ZAWADI YA KEKI NI PAMOJA NA WAZAZI WA PANDE ZOTE MBILI,
 MILEMBE ALIPELEKA UKWENI...
NA HUKU PIA VIVYO HIVYO!

KAMATI YA MAANDALIZI,MARAFIKI HURU,AFLEWO TEAM,DK PARVINA,PROSPER MWAKITALIMA,APOSTLE ONESMO NDEGI, LINDA TEMBA NA DK.HURUMA NKONE, MCHUNGAJI ALIYEFUNGISHA NDOA HIYO!!
KEKI KWA MCHUNGAJI NA MKE WAKE

KEKI KWA PROSPER MWAKITALIMA

KEKI KWA DK PARVINA
HATIMAYE WATU WALIKUJA KUMPONGEZA KWA KUCHEZA NA KUMRUSHA JUU SANA...
NA BAADA YA HAPO MENGI YALIENDELEA,KAMA VILE KUONA SHORT DOCUMENTARY NA HATIMAYE CHAKULA,NA HAPO WALITUMBUIZA THE VOICE,SAMWEL YONAH, AMANI KAPAMA, BOMBY JOHNSON PAMOJA NA KING CHAVALA-MC NA KIBAO MAALUM KABISA KWA MAHARUSI "SAMILEMBE"
KING CHAVALA-MC
WATU WALIKUWA WAKITOA ZAWADI MLANGONI,LAKINI KUNA BAADHI YA WATU AU MAKUNDI MAALUM YALILAZIMIKA KUPELEKA MBELE ZAWADI ZAO.
KAMATI YA MAANDALIZI ILIENDA MBELE KWA KUCHEZA KAMA HIVI
CHRISTIAN BLOGGERS NAO HAWAKUBAKI NYUMA KATIKA KUMPONGEZA MWENZAO!
"SAMILEMBE"

HATIMAYE BAADA YA YOTE WALIPIGA PICHA NA KUONDOKA KUELEKEA HUKO AMBAKO HAKUNA AJUAYE NA WAO HUJUA TU WAKISHARUDI!!

SHUKRANI NYINGI SANA KWA KAMATI YA MAANDALIZI  NA KILA ALIYEHUSIKA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE KUFANIKISHA JAMBO HILI,AHSANTE SANA MWENYEKITI NOEL TENGA KWA KUKUBALI KUTUMIKA KUBEBA JUKUMU HILI!

KWA NIABA YA TIMU NZIMA CHA YA CHAVALA MEDIA, TUNAWATAKIA KILA LAKHERI NA MAISHA MAREFU SANA YENYE FURAHA NA AMANI NA UPENDO WA KWELI WATU HAWA MUHIMU SANA KWETU,AMEN!!

IMEANDIKWA NA 
King Chavala MC
+255 713 883 797

Thursday, August 8, 2013

JUMAPILI HII TUNAKUTANA KWA IBAADA MOJA TU...KUSIFU NA KUABUDU TU!!

VIJANA,WABABA NA WAMAMA KUTOKA PANDE ZOTE ZA JIJI LA DAR ES SALAAM NJOONI PAMOJA TUMSIFU NA KUMWABUDU BWANA JUMAPILI HII PAKE TAG MAGOMENI, HII NI BURE NA SI YA KUKOSA KWA MTU YEYOTE!!!
UKIPATA TAARIFA HIZI MTAARIFU NA MWENZAKO!!!

Wednesday, July 24, 2013

YOUTH PRAYER CAMP (3KAVU) KUFANYIKA BOKO TAFES CENTRE!!!

SHALOM!
NINAWASALIMIA KATIKA JINA LA YESU LIPITALO MAJINA YOTE!
NAAMINI MKO VIZURI NA MNAENDELEA VEMA NA MAISHA YENU YA KILA SIKU; KWA KADRI UNAVYOAHANGAIKA KUOGA,KUVAA,KULA NA KUSOMA KILA SIKU,IMEKUPASA KUTIA JUHUDI ZAIDI KATIKA KUIMARISHA KIROHO CHAKO KILICHO MSINGI WA KILA KINACHOONEKANA. NA NDIO MAANA KUNA MAHALI TUNAONA YOHANA AKIMWAMBIA GAYO.....MPENZI NAOMBA UFANIKIWA KAMA ROHO YAKO IFANIKIWAVYO.....HII INA MAANA MAFANIKIO YOTE YA NJE NI SAMBAMBA NA MAFANIKIO YA ROHO YAKO.

KWA KUTAMBUA UMUHIMU HUO WA KUONGEZA UKARIBU WAKO NA MUNGU KWA KUUTIISHA NA KUUTAABISHA MWILI HUU WENYE MAROROSO YASIYOKWISHA, HUDUMA YA VIJANA, THE BRIDGE ILIYO CHINI YA KANISA LA VICTORY CHRISTIAN CENTRE TABERNACLE (VCCT) IMEANDAA KAMBI MAALUM YA MAOMBI YA KUFUNGA KWA SIKU TATU KWA AJILI YA VIJANA WOTE WANAWIWA KUMTAFUTA MUNGU KWA BIDII.

KAMBI HIYO ITAANZA SIKU YA IJUMAA SAMBAMBA NA MAOMBI YA KUFUNGA KUANZIA IJUMAA(WENGINE WANAANZA ALHAMISI) MPAKA JUMAPILI AMBAPO TUTAFUNGUA PAMOJA BAADA YA IBAADA YA KWANZA KANISANI PALE VCCT, MBEZI BEACH A.

MAOMBI HAYA NI YA KUFUNGA KWA SIKU TATU KAVU MFULULIZO NA HAKUNA GHARAMA ZA KIINGILIO ZAIDI YA KULIPIA MALAZI AMBAYO NI TSH 5000/= KWA SIKU MOJA(HIVYO KILA MSHIRIKI ATADAIWA 10,000/= KWA CAMP HIYO).MAOMBI HAYA YATAFANYIKA KATIKA KITUO KINACHOITWA "BOKO TAFES CENTRE|

KWA WALE WANAOENDA TUTAKUTANA IJUMAA JIONI PALE VCC-VICTORIA TAYARI KWA AJILI YA SAFARI YA PAMOJA MAJIRA YA SAA MOJA NA NUSU JIONI.

MSISITIZO WA MAOMBI HAYA NI "KUFINYANGWA NA BWANA KWA UPYA" ILI UWEZE KUTEKA BARAKA ZAKO KWA NGUVU!!

MUHIMU KUBEBA BIBLIA,NOTEPAD,KALAMU,CHANDARUA,SHUKA,SABUNI,MSWAKI, SURUALI NA KANGA( KWA WASICHANA)MAFUTA NA NGUO ZA KUVAA JUMAPILI KANISANI (MAANA SAFARI ITAKUWA NI MOJAKWAMOJA TOKA CAMP MPAKA KANISANI)

KUTOKA UPANDE WOWOTW WA JIJI,BILA KUJALI KANISA WALA DHEHEBU LAKO, MRADI UNAMWAMINI MUNGU KUPITIA YESU KRISTO,BASI USISITE UNAKARIBISHWA SANA,KWA MAELEZO ZAIDI/KUJIANDIKISHA AU KUCHANGIA WANAENDA BASI WASILIANA NA WAANDAAJI KUPITIA;

0754 710 410/0713 883 797/0713 209056
IMETOLEWA NA THE BRIDGE YOUTH MINISTRIES,VCCT!

@IMEDHAMINIWA NA GOSPEL STANDARD BASE Blog.

Wednesday, July 17, 2013

HUYU NI"RAPHAEL JOACHIM LYELA" MTUMISHI AMBAYE ALIYEKAA MIEZI 11 TUMBONI NA KUISHI MTAANI KAMA CHOKORAA!!!

SHALOM WANDUGU!!
NINAWASALIMIA WOTE KATIKA JINA LA BWANA YESU KRISTO!
NINAAMINI KILA MMOJA YUKO POA NA ANAMTUKUZA KRISTO,HUSUSANI WEWE UNAYESOMA HAPA SASA HIVI!
LEO KIPEKEE NINAWALETEA HISTORIA YENYE USHUHUDA MZITO WA MAISHA YA MTUMISHI WA MUNGU AMBAYE BADO NI KIJANA INGAWA ni BABA na ANA WATOTO WENGI SANA TANZANIA NZIMA, HUYU NDIO MBEBA MAONO NA MUANZISHAJI WA HUDUMA IITWAYO "YKM-YOUTH KINGDOM MINISTRIES...Jesus Up!" 

Yamkini na wewe umewahi kupokea message nyingi sana toka katika huduma hii na yamkini umesaidika sana sana....Mtumishi huyu amekuwa anajighulisha sana na maisha na maendeleo ya vijana....yamkini umewahi kumuona chuoni au shuleni aukanisani kwako akihudumu ama umewahi kumsikia redioni akiongea au umewahi kusoma kitabu chake au umewahi kununua CD zake za mafundisho,basi binafsi nilipata fursa ya KUMHOJI KAKA HUYU MWENYE HISTORIA YA KIPEE YENYE KUOGOPESHA LAKINI INAYOTIA MOYO SANA MAANA SASA ANAMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII!

(Basi yafuatayo ndio mazungumzo yetu yalivyokuwa na maelezo yote yameandikwa kama mwenyewe alivyojieleza)

UTAMBULISHO RASMI;
Jina Kamili: Raphael Joachim Lyela

Familia;Nimemuoa Angela Godfrey Raphael
Asili;Mfipa Original toka Rukwa-Sumbawanga
Huyu ni Mtoto wa  3 kati ya 6 wa familia ya Mzee J.Lyela.



TUAMBIE HISTORIA YAKO FUPI YA KIELIMU;
".....Darasa la Kwanza Shule ya Msingi Mabatini-Mwanza, pia Mwimbi kule Sumbawanga vijijini nilikomalizia darasa la saba. Nilisoma O Level shule tatu tofauti, nilianza Kipoke Sec school kule Tukuyu nikasoma mpaka form two, nikahamishiwa Lutengano sec school nikasoma mpaka form three, sikumaliza form three yote kwasababu niliibiwa ada ya shule kwa kichupa cha dhahabu so nikaambiwa sitaki shule na hivyo nikaachia form three. 
Nikakaa mwaka mzima home, nilipoambiwa kurudi shule niligoma kurudia tena form three na kwahiyo sikumalizaga form three but nikaamua kusoma masomo ya jioni katika shule ya Iyunga Technical Sec ambako nilimalizia form four na kufeli kwa kupata division 111.24. 
Nikapangakiwa A Level Kigonsera High school, Songea kwa mchepuo wa HGL, nikasoma term moja, kasha nikahamia Sangu high school Mbeya nilikomalizia form six. Nilimaliza na kufeli kwa kupata div 1.8, nikaenda chuo kikuu Mzumbe nilipomaliza Bachalor ya Publick Admin-Human Resources Management."



HUYU KAKA KWA SASA NI MTAALAMU WA;Human Resources Management, NA ZAIDI NI Certified Facilitator
Anafanya Kazi KAMA:Partnership Facilitator,Human Resources Specialist na shirika la Compassion International Tanzania kwa mwaka wa tano tu mpaka sasa.

(Hapa nilimuuliza uzoefu au mambo mengineyo katika maisha yake,nae akafunguka kama hivi)


MAMBO MENGINEYO YA KIPEKEE KUMHUSU RAPHAEL;

".....Nilizaliwa baada ya miezi 11......mama alikufa nikiwa na miaka 10......niliishi mtaani kwasababu baba yangu alikuwa akinipiga sana toka nikiwa mdogo.
........nilianza kunywa gongo na kuvuta sigara na bangi, nilikuwa mwizi toka nikiwa mdogo.......nilishasafiri toka Mwanza mpaka Sumbawanga nikitafuta ndugu zangu bila kulipa nauli na kukaa njaa bila kula wala kunywa kwa siku kadhaa......nimeshauza mkaa na kuvua samaki ili nipate pesa za kujikimu......nilijifunza matusi toka nikiwa mdogo kutoka na jamii niliyokulia.......nimeshakuwa Mkatoliki, Mrastafari, Shahidi wa Yehova na pia Mbudha lakini mwisho nikakutana na Yesu nikiwa mwaka wa kwanza chuo kikuu pale Mzumbe........nimeshahudhuria makongamano mengi sana ya vijana ndani na nje ya Tanzania.........nilianza kuandika hadithi za kwenye magazeti nikiwa O level, nimeshaandika kitabu kimoja na vingi vinaandaliwa, ninaimba na nina nyimbo nyingi tu, ni mtunzi wa nyimbo, mwandishi wa vitabu, motivational speaker hasa kwa vijana"

MAONO NA NDOTO ZANGU;
 
".....Mwaka 2003 nilipata mawazo ya kuwasaidia vijana, nilianza kwa kuandika mawazo yangu kuhusu mahusiano kwenye karatasi na niliandika mawazo yangu ya kwanza yenye kichwa cha UTOPIAN PARADISE nikielezea maisha ya Furaha katika ulimwengu wa UTOPIA, mwaka 2007 nilianza huduma ya kutuma msg kwa vijana 24 kuwakumbusha umuhimu wa kuomba na kusogea karibu na Mungu wao,hi indo huduma ya Youth Kingdom Ministries iloiyopata shape mwaka 2012, YKM ni huduma inayowafikia vijana na njia ya kutuma msg kwa simu na mpaka sasa tunawafikia vijana zaidi ya 4000 kila zinapotumwa, YKM ina viongozi wa mkoa katika mikoa 15 mpaka sasa yaani DAR,MWANZA, MOROGORO, ARUSHA,LINDI,MTWARA,MARA, IRINGA, MBEYA,KILIMANJARO,KIGOMA,RUVUMA,DODOMA,SINGIDA,TABORA. Vijana ndio madhabahu yangu"
NILIMUULIZA SWALI,MPAKA SASA UMEATHIRIJE ULIMWENGU WAKO?
"....Mpaka sasa nimefikia vijana zaidi ya 4000 Tanzania nzima na Kenya pia, nina vijana zaidi ya mia moja waliojitoa kutumika katika huduma kwa simu zao toka maeneo mbali mbali, makazini, shuleni, vyuo, mtaani etc"


NI NINI UNACHOTAMANI KUKITIMILIZA MAISHANI MWAKO?

"....I want to die empty, kuachilia kila kilichowekwa na Mungu ndani yangu ili kutimiza kusudi la Mungu juu yangu, juu ya kizazi changu, juu ya taifa langu na juu ya familia yangu. Natamani kuona vijana wamesimama katika kanuni za Ufalme wa Mungu na kuleta mabadiliko yadumuyo katika kila eneo analopatikana Kijana. Natamani siku moja nipotelee kwenye biblia. Natamani nitumike kwa kiwango ambacho hata wakati wangu wa kulala utakapofika basi utukufu wa Mungu udhihirike kwa utukufu wa Omega. Sina chaguo linguine zaidi ya kumtumikia Mungu."

KIPEKEE NINAMPENDA SANA KAKA HUYU NA  TANGU NIMEMFAHAMU NINAJIVUNIA moyo wake,HAKIKA NI CHOMBO IMARA CHA BWANA!!
 
MAISHA YAKE YALICHANGAMSHA SANA NA KUNIKUMBUSHA MAISHA YANGU NILIYOPITIA NA MENGI YA MAMBO NI KAMA TUNASHARE....NA KWA SASA HUWA ANAANDIKA MASOMO MBALIMBALI KWA AJILI YA VIJANA KATIKA MADHABAHU HII KATIKA UKURASA UITWAO "Youth Platform"

Naamini umemfahamu mtumishi huyu vema,ama umemfahamu baba yako vema(kwa wewe ambaye ni mtoto) na zaidi naamini hautaacha kutembelea madhabahu ili ujifunze kila leo maana hapa kuna mengi sana ya kujifunza!!!

Na King Chavala-MC
Hotline; +255 713 883 797
*Jiunge uwe follower wa blog kisha utoe maoni yako au maswali yako!!!

Thursday, June 13, 2013

ITAMBUE NAFASI YAKO KAMA KIJANA ILI ULETE MABADILIKO KATIKA MAISHA YAKO NA JAMII KWA UJUMLA 02


SHALOM TENA WASOMAJI WANGU!!
BADO TUNAENDELEA KUJIFUNZA KAMA VIJANA....

Kama nilivyosema katika sehemu ya kwanza, ni muhimu sana kwako wewe kama kijana kujua nafasi yako katika maisha yako, ujue pia Nafasi yako katika familia yako, uelewe umuhimu ulionao kwa jamii inayokuzunguka na zaidi sana taifa lako.
Umuhimu wako haupatikani kwa kujitazama kwenye kioo na kudhani wewe ni muhimu, ni jambo linalohitaji kuwekeza katika ufahamu sahihi ama kujitambua sawa na vile Mungu alivyokusudia.

Ufike mahali uishi maisha yenye malengo na utambue thamani yako ili usinunuliwe na vitu vyenye thamani isiyolingana na wewe. Hapa inahitaji kujenga mtazamo utakaokusaidia kuwa thabiti katika maamuzi yako, ili ujenge msimamo wenye nidhamu katika maneno, mawazo na matendo yako.

 Jumla ya haya yote inahitaji kujitambua, na sasa tuendelee na maana ya kujitambua maana ni kujitambua tu ndiko kunaweza kukusaidia kujua Nafasi yako na kusimama katika zamu yako na kuleta mabadiliko uliyopangiwa na Mungu wako.

Maana ya Kujitambua
“Kujitambua ni hali ya kuwa na ufahamu au uelewa (kujua) wa kutosha juu ya maisha yako kwa ujumla pamoja na mazingira yanayokuzunguka na hivyo kukufanya uishi maisha yanayofanana au kulingana na kusudi la Mungu kwako, uishi katika ubora wa maisha yanayolingana na kiwango cha ufahamu ulionao au kiwango cha kujitambua kwako kutegemeana na nguvu ya taarifa unazopata” 
 Kijana aliyejitambua, ukimsikiliza maneno yako hutatia shaka kwamba yuko thabiti na hata ukiangalia matendo yake utaona ulinganifu wa ayasemayo na ayatenda. Kijana yoyote hawezi kujitambua mpaka amekutana na ufahamu sahihi ulio juu ya yote anayoyafahamu, aone kupungukiwa kwake kwasababu hajafahamu mambo ya msingi katika maisha yake. 

Juu ya yote ni lazima wewe kama Kijana ujue kuwa ipo sababu ya wewe kuwepo hapa duniani, lipo kusudi la wewe kuwepo hapa duniani, ipo sababu ya wewe kuwa Kijana, hii ni muhimu sana. 

Kujitambua ni kuwa na ufahamu au uelewa juu ya angalau mambo yafuatayo: 

 Historia ya asili yako au maisha yako, ni muhimu Kijana ukajua historia ya maisha yako bila kujali ilikuwa nzuri au sio nzuri, au ya kuvutia au siyo ya kuvutia ili ujue kuwa kuna mahali unatoka, kuna aina ya watu wameunganishwa na maisha yako, hii itakusaidia katika safari ya maisha yako 

 Maumbile yako, au mwili wako, ujue madhaifu ya mwili wako, uelewe na kuutambua mwili wako vizuri na kujua namna ya kuudhibiti katika mazingira tofauti tofauti 

 Kusudi la maisha yako, maono au malengo kwa pasipo kujua sababu ya wewe kuwepo duniani unapoteza maana ya kuwepo duniani 

 Makuzi na malezi yako, maana haya yanaathiri kwa kiwango kikubwa sana hali yako ya baadae, ujue melelewaje na umekua katika mazingira gani ili tabia zako na mwenendo wako zipate maana na uwe na uwezo wa kujifunza kwanini umekuwa na tabia Fulani Fulani, 

 Mazingira na jamii, taifa lako na zana nzima ya uzalendo, ujue kuwa uzalendo haufundishwi kwa kuwapa watu mali na pesa, Mungu amekupa wewe fursa ya kuzaliwa na kuishi Tanzania kwa makusudi na kama hujui basi utaishi kama mnyama na utapoteza ladha na kuwajibika 

 Hisia, utashi na ufahamu wako 

 Maneno na maamuzi yako, 

 Tabia na mwenendo UMUHIMU WA KUJITAMBUA Kujitambua ni muhimu sana kwani kunakusaidia kujua mambo juu ya maisha yako: 

 Ili kutembea au kuishi katika viwango asilia ambavyo umeumbwa navyo (The originality of you) 

 Ili kujua madhaifu uliyonayo kwa ajili ya kujua namna ya kuyashinda 

 Ili kujua thamani yako, uepuke kutumiwa vibaya, usijidharau wala kumtengenezea mtu mwingine mazingira ya kukudharau na hata usimdharau mtu mwingine 

 Ili ujua nafasi yako (majukumu) katika maisha yako na ya wale wanaokuzunguka 

 Ili kujua umuhimu ulionao kwa ajili ya kuleta matokeo yanayotarajiwa kwako 

 Itakusaidia kutumia vizuri rasilimali kama muda, watu nk 

NAAMINI LEO UMEPATA KITU CHA KUKUSAIDIA KATIKA SOMO HILI, NI MATUMAINI YANGU KUWA UTAANZA KUFANYA MABADILIKO KATIKO JAMII YAKO SASA!!
Usikose somo lojalo!
Na Mwl. Raphael Lyela kutoka Youth Kingdom Ministries,Jesus Up!
 
......LITAENDELEA!!!!!!!

TAMASHA KUBWA LA KUMSIFU MUNGU PAMOJA NA WATOTO WA MUNGU (HOCET)

 
SHALOM!!
IMETUPASA,NI VEMA NA HAKI KUMSIFU MUNGU WETU KILA SAA NA KILA WAKATI...MAANA AMETUUMBA ILI TUMWABUDU...LAKINI HIYO PEKE YAKE HAITOSHI,MTUME PAULO ANASEMA DINI ILIYO SAFI ISIYO NA TAKA MBELE ZA MUNGU BABA NI HII KUWATAZAMA YATIMA,WAJANE,WASIO NA MSAADA KATIKA DHIKI ZAO NA KUJILINDA NA DUNIA PASIPO MAWAA (YAK 1:26,27)
....BASI SASA SAFARI HII WATU WA MUNGU TUTAKUSANYIKA PAMOJA KWA AJILI YA KUMSIFU MUNGU,KUZINDUA DVD YA WATOTO WA MUNGU PAMOJA NA KUFANYA CHANGIZO LA KUWASIDIA MTAJI WA KUJIENDESHA WATOTO HAWA AMBAO WAFADHILI WAO WALIWAKIMBIA BAADA YA KUONA WANAMWAMINI MUNGU!....BASI UKIONA TANGAZO HILI NJOO UJUMUIKE NASI ILI TUTIMILIZE MAANDIKO YOTE!
WAIMBAJI WENGI SANA WATAKUWEPO KATIKA KUWASINDIKIZA WATOTO HAWA NA MALENGO MAKUBWA NI KUPATA FEDHA ZA KUTOSHA KUNUNUA CANTER,NG'OMBE WA MAZIWA PAMOJA NA MTAJI WA KUKU WA MAYAI NA NYAMA ILI SHULE HII IWEZE KUJIENDESHA PASIPO KUNGOJA MISAADA MAANA WATOTO HAWA WANAWEZA KUZALISHA NA KUJITEGEMEA HUKU WAKISOMA VIZURI NA KUSOMA NA KWA BIDII!!
IWENI MFANO WA KUIGWA!!!

UNAWEZA KUTUMA MCHANGO WAKO KWA M-PESA KWENDA 0754527955

GOSPEL STANDARD BASE BLOG TUWATAKIENI MAFANIKIO MEMA NA MNAKARIBISHWA KUTUSHIRIKISHA TENA WAKATI WOWOTE ULE MKIWA TAYARI!
President.

Tuesday, April 30, 2013

ITAMBUE NAFASI YAKO KAMA KIJANA ILI ULETE MABADILIKO KATIKA MAISHA YAKO NA JAMII KWA UJUMLA(01)

Jesus Up!
Karibu katika safu hii ya mafundisho ya vijana yanayoitwa Nafasi ya Kijana. Tutakuwa na mambo kadha wa kadha ya kujifunza kuhusu Nafasi ya Kijana kwa ujumla wake tukimwangalia Kijana na sehemu anazotakiwa kusimama au wajibu anaotegemewa kuwa nao na kuufanyia kazi au majukumu aliyonayo katika maeneo mbali mbali yanayomuhusu.
Ni mafundisho yanayolenga kuleta ufahamu sahihi juu ujana na Kijana kama Ufalme wa Mungu unavyomtambua na kumtegemea pia. Lengo letu kuu ni kuwafanya vijana wawe wanafunzi wa Yesu kwelikweli kwa kufundishwa KWELI ya Neno la Mungu kuhusu Nafasi yao katika upana wa maisha yao.

Ni muhimu kila Kijana akafahamu mambo yafuatayo kuhusu yeye:
1. Ni lazima ujitambue, upate ufahamu sahihi juu ya maisha yako pamoja na mambo yote na jamii inayokuzunguka
2. Ni muhimu ujue wajibu ulionao kwako wewe mwenyewe kama mtu binafsi juu ya maisha yako
3. Kuna haja ya kujua kuwa wewe ni sehemu ya familia yako na lazima ujue wajibu wako kwa wazazi na familia kwa ujumla
4. Ni lazima ujifunze kuwa mzalendo wa taifa lako sawa na jinsi ambavyo Mungu anataka, fahamu kuwa umeunganishwa na ardhi ya Tanzania kwa mafanikio yako, Mungu akikwambia nenda nje ya nchi nenda lakini

Thursday, April 25, 2013

TEACHING CONCERNING "NAFASI YA KIJANA" COMING SOOON!!!!

HELLO SHALOM!!
HERE IS THE SPECIAL PLATFORM FOR YOUTH ISSUES!
AND THE PAGE START THIS WAY!!!
Huwezi kuyajali maisha yako kama hujui thamani yake, huwezi kujua thamani ya maisha yako kama hujajitambua kwa Neno la Mungu, huwezi kuwa na maisha ya mafanikio kama maamuzi yako hayatengenezi mafanikio, hata usipoamua maisha yako yataendelea kama kawaida

NA MWALIMU RAPHAEL LYELA!!!
Jesus Up!