MFULULIZO
WA MATAMASHA YA KUCHEKA TENA(LAUGH AGAIN CONCERT SERIES) TANZANIA
Na. CLOWN
CHAVALA(MC na Muasisi wa Christian Stand Up Comedy Tz)
(Na. mwandishi maalum)
Ni muda mrefu wakristo wamekosa aina nyingine ya burudani
yenye maadili na iliyo katika misingi ya Kimungu, ambayo ni huru kwa familia
yote zaidi ya ibaada za kanisani, mikutano ya injili na matamasha ya uzinduzi
au ya kusifu na kuabudu. Na ni vijana wengi ambao wana vipaji makanisani ambao
wameshindwa kutumia au kuonyesha vipaji vyao kwasababu aitha mazingira ya
kanisa hayaruhusu vitu hivyo,wamekosa wangalizi,hawajiamini au kanisa lina mtizamo hasi juu ya mambo hayo.
Lakini ni dhahiri kuwa Mungu alituzawadia vipawa na karama
mbalimbali kwa makusudi na kila alichotupa kina nafasi ya kumrudishia sifa na ni
kiungo cha ibaada.
Sasa FREDY E. CHAVALA(CLOWN CHAVALA/PRESIDENT CHAVALA)
Amekuwa mbele katika kuasisi na kuhakikisha kuwa vile vipaji vilivyoko kanisani
vinapaki kanisani kwa Utukufu wa Bwana, amekuwa sana akikuza vipaji kama vile
Ngojera,Mashairi,Akapella,Simulizi,Dansi na Vichekesho lakini zaidi
Vichekesho,tena vichekesho vya mtu mmoja mmoja(Stand Up Comedy).
Muasisi huyu ana vipaji vingi(multi talented) na anapenda
sana sanaa, lakini kwa sasa amejikita sana kwenye uasisi wa vichekesho vya
kikristo.
Si jambo tulilolizoea machoni mwetu na halijawahi kutokea
nchini, kuona watu wakitumia sanaa ya vichekesho kufikisha habari njema za Yesu
kristo.
Tulizoea kuona vichekesho(comedy), zikifanywa sana na watu
tu wa huko duniani(secular), lakini sasa sanaa hii iko madhabahuni na
imethibitika kuwa na kibali na faida kubwa sana kwa wakristo, hii itabadilisha
kabisa mtazamo wa kuona kama kanisani ni mahali pa kuwa serious na kulia tu
wakati bila kucheka wala kufurahi.
Faida za kufurahi na kucheka,mbali ya zile za kiroho ni kama
vile
- Kuondoa sumu mwilini, maana unapocheka mishipa inafunguka na damu inatembea vizuri na homoni na viyeyushi tiba vinaachiliwa mwilini.
- Kuondoa au kupunguza msongo wa mawazo(stress), yaani nafsi na akili vinapata vitu laini vya kufanya ufanye kazi nyepesi na siyo hizo nzito zisizo na majibu kichwani.
- Kuongeza uzuri wa sura, uchangamfu wa mifupa na kudumisha urafiki, jambo ambalo linaongeza imani ya kawaida kuwa hauko mpweke, mbali na kuwa Mungu.
- Kucheka pia kunaongeza maisha na zaidi furaha ikitawala moyo wako unaweza waambukiza wengine waliokata tamaa kabisa na maisha yao.
- Zaidi ya hayo yote, vichekesho hivi vya kikristo humfanya mtu ajifunze kutafakari Biblia kwa undani zaidi, hivyo mtu hucheka na kupokea kwa wakati mmoja, yaani unacheka unapona mwili na roho na hii ndio tofauti kubwa kati ya Vichekesho vingine vya huko duniani na hivi vya Kikristo.
Chavala anasema alianza kufanya comedy muda mrefu lakini
katika kanisa ana kama miaka mitano hivi, na hapo kale alikuwa anafanya zaidi
Drama na Dramantic comedy,…zaidi Chavala alisema………….
“haikuwa rahisi watu
kuelewa haraka hii Stand up Comedy, ambayo ni Comedy halisi, nakumbuka mara ya
kwanza kusimama kwenye jukwaa kubwa ilikuwa mwaka 2009 katika Mkusanyiko wa
wanafunzi wa vyuo vikuu maarufu kama CAMPUS NIGHT,mikusanyiko ambayo hufanyika
kila mwaka na huandaliwa na Kanisa la VICTORY CHRISTIAN CENTRE(VCC), mkesha
ambao ilifanyika pale uwanja wa taifa na
ulikuwa na zaidi ya washiriki 12,000. Hapo watu walicheka sana na watu wengi
walijua kuwa kuwa jambo hili ni zuri na linafaa sana katika kanisa la leo,
Tangu hapo nikaendelea zaidi kushiriki mikutanoni,makanisani na mikusanyiko
mbalimbali ya wakristo na baada ya kuona ipo haja ya kufanya wazo hili
lijitegemee, ndipo nikaanzisha mfululizo(SERIES) wa matamasha ya kikristo ya
comedy. Mfululizo huu ulianza mwaka jana(Nov 20, 2011) pale Ubungo plaza na una
jina liitwalo “LAUGH AGAIN CONCERT SERIES” yaani MFULULIZO WA MATAMASHA YA
KUCHEKA TENA” Picha nyingi zinaonyesha namna siku hiyo ilivyokuwa imefana.”
LAUGH AGAIN CONCERTS zitaendelea kufanyika nchini mpaka hapo
ambapo mikoa yote itakuwa imefikiwa na kwa kuanzia Msimu huu wa kwanza (SEASON
ONE) itakuwa na matamasha nane(8) na kati ya hayo Dar es salaam(3), Arusha(1),
Mwanza(1),Dodoma(2) na Mbeya(1), ambayo yataanza March mpaka September 2012.
Matamasha haya yatakuwa yanahusisha vipaji vingi toka mkoa husika sambamba na
CLOWN CHAVALA, ambaye ndio mwasisi pamoja na watu watu wachache watakaobahatika
kusafiri nae, katika matamasha haya tutakuwa na waimbaji mbalimbali
watakaoalikwa mbali na sanaa zote za maonyesho nilizozitaja pale juu.
Hivyo kama una kipaji au unapenda kuwa mshiriki wa KUCHEKA
TENA, hakikisha unafungua masikio vizuri, maana unaweza ukapitwa!
MSIMU HUU UNAANZIA
DAR ES SALAAM 4th MARCH 2012,
LANDMARK HOTEL,RIVER SIDE,UBUNGO!
Unaweza kuwa umesikia matangazo ukawa unapuuzia tu,lakini
nikutie moyo tu,jitahidi usikose hii maana ni maalumu kwa ajili yako, tamasha
hili litaanza nane na nusu mchana mpaka moja na nusu usiku(2:30-8pm) na CLOWN
CHAVALA(The king of Stand Up Comedy) atawapandisha wachekeshaji wapya watano(5)
ambao ni Senior ABBY,Gerald Mrema,Lukweto J,Richard Chidundo na Emmanuel
Mathias(MC MANU au pilipili ya sherehe kutoka Dodoma), lakini pia vichekesho
vyote hivi vitasindikizwa na Glorious Celebration Band, Dar es salaam Gospel
Band, Vocapella Group, Dance group, Victor Aron pamoja na Madam Ruth na
Chriss(wa amenibamba Yesu) na wengine wengi.
Tiketi zinapatikana;
- Victory Christian Centre
- Praise Power Radio
- Tarakea Restaurant-mwenge
- Silver spoon na Tausi Fashion mlimani city kwa 5000/= tu
- au unaweza kununua kwa M-pesa(0753 883797) au Tigo Pesa(0713 883797) kwa 6000/= tu.
(hakikisha unatuma pesa ya tiketi kamili, tena kwa
kutumia namba yako iliyosajiliwa kwa jina lako, ili upate tiketi yako mlangoni
ukija)
LAUGH AGAIN CONCERT One One Ni kwa ajili ya WATU BORA wote
wenye UPENDO BORA WA KWELI KWA WOTE! (<<QualityLove for Quality
People>>)
MALENGO MAKUU YA
MATAMASHA HAYA;
Zaidi ya faida za kucheka nilizozisema hapo juu, matamasha
haya yameanzishwa kwa malengo makuu haya;
- Kuutangaza ufalme wa Mungu na ukuu wake, kuinjilisha na kuponya watu kupitia dawa asili ya kucheka.
- Kuanzisha aina nyingine ya burudani kwa familia za wapenda maadili, zaidi ya hizi chache tulizozizowea, yaani uzinduzi na mikutano ya injili.
- Kukuza na kuviendeleza vipaji halisi vya vijana kanisani, kwa faida ya kanisa, jamii na mafanikio ya maisha yao binafsi.
- Kukutanisha watu wa kada na nyanya/fani mbalimbali katika maisha,ili kuongeza upana wa wigo wa mtandao wa kubadilishana habari, ujuzi, uzoefu pamoja na biashara.
- Kukuza, kuendeleza na kuutangaza utamaduni wetu,hasa ule uliosahaulika kupitia sanaa, na hivyo kupigia kampeni Utalii wa ndani ya nchi yetu, ambayo Mungu ametubariki nayo.
KUHUSU MUASIS (FREDY CHAVALA);
Huyu ni
kijana wa kitanzania aliyeokoka, Mzungwa wa Iringa aliyehitimu elimu ya chuo
kikuu na ambaye amekuwa kwenye harakati za maendeleo ya Vijana kwa muda mrefu
sasa, kwa taaluma ni Mtaalamu wa Usimamizi na Utawala wa Biashara (Business
Administration and Management), ambaye
anafanya kazi kama Managing Director na Business & Management Consultant wa
Great Potentials Ltd.
Tofauti na
watu wengi wanavyochukulia sanaa ya uchekeshaji kama vile ni ya watu duni wasio
na mwelekeo, Chavala anaichukulia kama kitu cha thamani sana kwake na kwa jamii
na ndio maana pamoja ya Elimu yake ameamua kufanyia kazi vipaji vyake,zaidi
Stand Up Comedy.
Chavala
amekuwa akijishughulisha na mambo mengi sana kama vile uandaaji wa Semina,
Mikutano na matukio mbalimbali ya kidini na kiserikali, Ushauri,Uandishi wa
miradi,Uandishi wa Vitabu na makala, U-MC, Ufundishaji na uzungumzaji katika
maeneo mbalimbali ya nchi hususani katika eneo la Biashara, ujasiriamali,
ustawi wa Vijana na ukuzaji wa vipawa. Inawezekana umeshawi kumuona katika
mahojiano mbalimbali na vyombo vya habari, kumsikia au kukutana nae, nina
uhakika utakubaliana nami kuwa huyu ni kijana wa tofauti na wa kipekee.
Mpaka sasa
ameshatembea karibu Tanzania yote na kutembelea baadhi ya nchi za nje, kwa
ajili mambo hayo anayoyafanya.
Chavala
anaamini kila mtu ana uwezo ndani yake wa kufanya kile kitu ambacho Mungu
amemuandikia afanye maishani mwake na zaidi mafanikio ya mtu yako ndani mtu
mwenyewe.
UNAWEZA KUWA SEHEMU YA KAMPENI HII
Unaweza kuhusika kwa namna yeyote ile; maombi, ushauri,
ushiriki, kuchangia au kudhamini, pia Unaweza kupanda mbegu yako kwa kusaidia
kufanikwa kwa matamasha haya nchini, maana ni pesa nyingi inahitajika,ni zaidi
ya milioni 250 kwa msimu wa kwanza wenye matamasha nane nchini! Milango iko
wazi kwa yeyote mwenye nia njema, unaweza kuwasiliana nasi kuuliza au kuchangia
chochote kile unachoguswa kwa M-PESA(0753883797) au Tigo Pesa(0713 883797).
Tutabarikiwa sana kama tutasikia kutoka kwako, tunatamani
yale yote ambayo shetani ameyaiba kanisani na wale wote ambao amewaiba kanisani
warudi, maana hakuna jambo lolote zuri lenye asili yake kuzimu, vyote ni mali
ya Mungu. Saa inakuja ambapo mtu yeyote atakayekaa kinyume na Mungu basi huyo
ataonekana amechuja maradufu, tusaidiane kulea vijana wetu katika kumpenda
Mungu, bila kujutia karama, vipaji na vipawa walivyonavyo! Usiwe wa kwanza
kulaumu, kuhukumu na kudharau watu, hasa vijana, karibia ujifundishe au uje na
majibu/masuluhisho na sio maneno tu!
“Ninawashukuru watu wote, makanisa, huduma,vyombo vya habari,
makampuni, taasisi na asasi, ambao mmekuwa ni baraka kwa huduma hii kwa ujumla,
ni wengi mno mnaotuunga mkono siwezi kutaja majina, ninawashukuru wazazi na
walezi wa kimwili na kiroho na zaidi gazeti hili kwa kuhakisha ulimwengu wa
kikristo unahabarika kama hivi, Mungu awabariki sana na karibuni sana tuendelee
kuungana mkono”…Fredy Chavala(Mbeba maono)
“LAUGH AGAIN
CONCERT SERIES”
GREAT
POTENTIALS LTD,
C/o Box
34048,
DAR ES
SALAAM.
+255
713/753-883 797.
e-mail; lacs.project@gmail.com OR fchavala@mail.com
No comments:
Post a Comment