Tuesday, April 22, 2014

KEKE NA AYO WATIA FORA TAMASHA LA PASAKA 2014!!!


Sikukuu ya pasaka ya mwaka huu ilikuwa na mwimbaji mahiri toka Afrika kusini, ali maarufu kama Keke, huyu mbaba ni mwimbaji na mwabuduji mzuri tu na ni mchungaji pia
Katika tamasha hilo la pasaka ambalo huandaliwa na Msama Promotion pamoja na Changamoto ya mvua bado muitikio wa watu ulikuwa mzuri tu na waimbaji mbalimbali toka hapa nchini na nje  ya nchi walikuwepo kumtukuza huyo Kristo aliyefufuka


Miongoni mwa wanamuziki waliohudumu katika tamasha hilo ni pamoja na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Sara K kutoka Kenya, Glorious Worship Team, John Lisu, Jessica BM,Meccy Chengula,Edson Mwaisabwite,Masanja Mkandamizaji,Mwanamuziki kutoka UK na Keke Kutoka South Africa pamoja na Rose Muhando bila kumsahau Efraimu Sekeleti toka Zambia!

Mhe. Benard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo kwa niaba ya Mh.rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza risala kutoka kwa Mchungaji Mwasota ambaye ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Pentekoste Ukanda wa Dar-es-Salaam na baadaye kutoa hutuba fupi akiweka msisitizo wa Mchakato wa uundaji wa katiba mpya kuwa utakuwa wa amani tu na wananchi wasubiri kuipigia kura.

Keke mwanamuziki kutoka Africa Ya Kusini akihudumu katika Uwanja wa Taifa kwa makeke ya hali ya juu sana!


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Membe akiongea siku ya Jana kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya 

Laura Msama Mke wa Msama akiwa amekunja goti wakati akisalimiana na Mhe. Membe 

Mhe. Membe akiwa anasalimiana na Keke, mwimbaji toka Afrika kusini.
 Mwanamuziki kutoka Zambia Ephrahim Sekeleti akiwa anapasha pamoja na Backers Vocalists wake, aliowaomba hapo uwanjani maana hawa ni Living Water toka Makuti kawe kwa Apostle Onesmo Ndegi!. 

Upendo Kilahiro akiwa anaenda sawa katika Uwanja wa Taifa 

Mise Anaeli akuwa anapuliza tarumbeta Uwanjani sambamba na Upendo kilahiro

Sarah K Mwanamuziki Kutoka Kenya akiwa anaimba Wimbo Wake "Liseme" akisaidiwa back up na wanamuziki wa Glorious worship team


"Kwani Ni Jambo Lipi hilo, Yeye asiloliweza" 
 Baadhi ya Waimbaji Wa Glorious Worship Team wakiwa Jukwaani wakienda sawa 

Kijana ni Kijana tu, Hawa hawakuwa mbali kwenda sawa na mishindo ya jukwaani!

Mwanamuziki Nguli kutoka Africa Ya Kusini Keke akiwa Jukwaani 



Backers Vocalists wakiwa wanaenda sawa 

Mpiga drums nambari moja wa Keke akiwa anaenda sawa 

Na mpaka hapo kwa uchache ndivyo tamasha la pasaka lilivyokuwa, Mwanamuziki wa mwisho alikuwa Rose Mhando na alikuja na vibao vyake vipya vya album yake mpya ya Facebook na kwa hakika alifanya vizuri!
Tamasha lilimalizika majira ya saa 2 usiku na hapo ndiyo ikawa mwisho na tutaonana tena Christmass ijayo na pasaka Mungu akipenda!
Naamini mambo haya yakifanyika katika dhamira ya kweli tupu tutafika mbali sana, Mungu awabariki watumishi wote watumikao madhabahuni kwa uaminifu!!

No comments:

Post a Comment