Tuesday, October 29, 2013

MTU MWENYE HASIRA NA NG’OMBE WAKE!!!!




Mzee Majaliwa ni mfugaji mzuri wa ng’ombe. Anategemea ngo’mbe wake kwa kujipatia kipato, kusomesha wanawe, na kujikimu kimaisha. Bila hao ng’ombe, mzee Majaliwa hana tumaini kwa sababu amejitoa na kujikita katika ufugaji.

Mzee majaliwa ni mtu mpenda watu na anayejitoa kwa shughuli mbali mbali za kijamii. Udhaifu wake mkubwa ni HASIRA. Kila akasirishwapo na watu, yeye huenda moja kwa moja zizini na kuanza KUWAPIGA NG’OMBE WAKE KWA FIMBO HADI HASIRA IMSHUKE. Baada ya hasira kumalizika hurudi tena zizini kwa masikitiko makubwa na machozi akifikiri jinsi alivyo wapiga ngo’ombe wakati KASA SIO LAO. Akizingatia kwamba hao ng’ombe wamekua waaminifu siku zote kumpatia maziwa, mbolea, na vyanzo vingine vya mapato ikiwa ni pamoja na kua tayari KUCHINJWA BILA KULALAMIKA, ili mzee Majaliwa ajipatie fadha na faida.

Ni rahisi sana kumshangaa huyu mzee anavyopiga ng’ombe ambao hawajamkosea kitu, ila watu wengi sana wamemfanya MUNGU KAMA NG’OMBE wa Mzee majaliwa. Wanapokwazwa, kuumizwa na kuzongwa, wanampiga Mungu fimbo kwa kumtenda dhambi! Ukiwauliza eti wanasema “mume wangu ananizingua sana”, “isingekua mke wangu nisingekua hivi”, “kama maisha ni magumu na watu hawanisaidii nifanyeje?”, “nimewaomba wanisaidie wamekataa”, “kila mtu anafanya kwanini na mimi nisifanye?”, nk.

Yeremia 17:5 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. 6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. 7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni Tumaini Lake. 8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda. 9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?”

Kama unamtegemea Mungu, kwanini usimtegemee akuokoe na mashaka, mateso na maumivu yako pia? Kwanini kumtenda dhambi kwa kisingizio cha WATU kukuumiza na kutokukutenda kwa haki? Je! Utamchapa Mungu wako viboko kwa kukosewa na watu wengine hadi lini?

Frank Philip

No comments:

Post a Comment