Episode One......JUKWAA LA KIOO!!!
SHALOM!
KWA MARA YA KWANZA KATIKA CHUMBA HIKI KIPYA CHA "JUKWAA LA KIOO" CHINI YA UKURASA WA WA "Gospel Music" na "Talents"NA LEO KWA MARA YA KWANZA TUNAANZA NA 1ST Q DANCERS WENYE MAKAO YAO JIJINI DAR ES SALAAM,HILI NI KUNDI LENYE VIJANA MAHIRI NA NIMEBAHATIKA KUWAONA MARA KADHAA KATIKA MATUKIO KADHAA NA LEO NIMEPATA BAHATI YA KUFANYA MAHOJIANO NA MBEBA MAONO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA KUNDI HILI DADA GRACE LIFARD MLAWA,NA MAZUNGUMZO YETU YALIKUWA KAMA IFUATAVYO;
GoStaBa:Habari yako dada!
MGN:Ni nzuri sana sijui za kwako?
Mimi ni mzima sana na leo naona nikuhoji kidogo kuhusu kundi lako la 1st Q,naamini hutojali!
karinu sana wala usijali,na mimi ninafurahi kupata nafasi hii ya kuongea na Gospel Standard Base.
GoStaBa:
Okey,watu wangependa kujua Kundi lenu linaitwaje?
GoStaBa:
Nini maana ya jina hilo na kwa nini mnajiita hivyo?
MGN:1st Quadrant inatoka katika “XY plane”, ambapo
AXES zote katika 1st quadrant ni chanya (Positive), ndio maana
tukajiita hivyo, kama Biblia ilivyoandika katika Warumi 8:28…..Nasi twajua ya
kuwa katika mambo yote,Mungu hufanya kazi na wale wote wampendao katika
kuwapatia mema!.......kwa hiyo nasisi tunaamini kwetu yote ni mema kwasababu
tunafanya nae kazi.
GoStaBa:
Kundi lenu lilianza lini na lilianzishwa na nani?
MGN:Tulianza mwezi april
mwaka 2012 kwa halisia,lakini wazo lilikuwepo tangu mwaka 2010,Kundi hili ni
wazo langu(Grace) ila tulianza na watu watano nao ni Mimi,Belinda,Mgeni ,Tenes
na Lisa.Lakini mpaka sasa tunao dancers 12,wakiwemo wasichana 9 na wavulana 3.
GoStaBa:Hili ni wazo jipya kwa kanisa,hususani kundi linalowahusisha
wasichana wengi zaidi,Je nini Changamoto zipi mlizopambana nazo au mnazoendelea
kupambana nazo katika kukua kwenu?
MGN:Changamoto ni nyingi lakini hizi chache ndizo naweza
kuzisema kwa sasa; ya kwanza ni kuwa <Sio makanisa yote yanaelewa jambo hili
kwa hiyo watu hao hawawezi kuwaruhusu> ya pili<Kwa kuwa wengi wa dancers
ni wanafunzi wa secondary na vyuo hivyo
muda wa kukutana kufanya mazoezi ni adimu,yaani mpaka wakati wa likizo> ya
tatu <Kwasababu watu wengi bado hawajui na hawajakubali,basi kuungwa mkono
bado ni kugumu na kusemwa semwa
bila kusaidiwa> na nyingine ni
<hatuko Exposed,lakini bado tunalifanyia kazi ili kuhakikisha
tunafahamika> ,na nyinginezo lakini
zingine ni za kawaida na zinatatulika.
GoStaBa:
Mmefanikwa kwa kiasi gani mpaka sasa?
MGN:Bado hatujafanikiwa kufikia malengo yetu lakini mpaka sasa
tumeshahudhuria na kuhudumu katika matukio/matamasha zaidi 10 tangu mwaka jana
mpaka sasa,yakiwemo matamasha matatu ya mwisho ya King Chavala..LAUGH AGAIN
CONCERT SERIES na pia tumeshirikishwa kwenye Video ya wimbo wa “KATIKA NYUMBA
YA BWANA” wa Amani Kapama.
UNAWEZA KUANGALIA VIDEO CLIP HII KAMA SAMPLE
http://www.youtube.com/watch?v=SVVuCoKZTGg
UNAWEZA KUANGALIA VIDEO CLIP HII KAMA SAMPLE
http://www.youtube.com/watch?v=SVVuCoKZTGg
GoStaBa:
Mnalelewa na nani?
GoStaBa:
Nini mategemeo au mipango yenu mbeleni?
MGN:Mategemeo yetu makubwa sio kuendesha 1st Q kama
kundi bali kama ministry au organization ambayo itahusisha vipaji vingi sana
walivyo navyo vijana katika kuhubiri injili na sio Dar peke yake bali Tanzania
nzima.
GoStaBa:
Ni jambo gani ambalo mkisaidiwa mnafikiri mtalifurahia sana
kama kundi?
MGN:Tutafurahi sana kama tutapata nafasi ya kufanya
kazi/kupeform mahali wa makubaliano ya muda mrefu au uhakika wa kufanya
performance angalau mara moja kwa mwezi.
GoStaBa:
Ni nani mnatamani kufanya nae kazi?
MGN:Yeyote Yule aliye tayari kufanya kazi nasi kwa moyo mmoja.
GoStaBa:
Ni kundi gani(la ndani au nje ya nchi) ambalo mnavutiwa nalo
sana na mnatamani kuwa kama wao au kuwazidi? Kwanini?
MGN:Hakuna kundi tunalotamani kuwa kwa wao au kuwazidi ila kuna
makundi ambayo tunayakubali ni kama vile RIOT Dancers,DPC Dancers na mengine
mengi ya nje kama vile mastered seed
group.
GoStaBa:
Una neno au ushauri wowote kwa wasomaji wa Blog hii?
MGN:Naona niwape neno toka katika Biblia kitabu cha 1kor
10:31…..Basi,mlapo au mnywapo,au mtendapo neno lolote,fanyeni yote kwa utukufu wa Mun gu….. na pia 1kor
12:5-6……tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye Yule. 6-Kisha pana
tofauti ya kutenda kazi,bali Mungu ni
yeye Yule azitendaye kazi zote katika wote. Utofauti wetu (Wakristo) katika
kutenda kazi usituathiri, ikiwa wote tunafanya kazi ya Yesu Kristo
tukiongozwa na Roho mtakatifu. Amen.
GoStaBa: Ahsante sana mtumishi kwa muda wako na natumai tutaonana tena na tena!
MGN: Ahsante sana pia ninakushukuru sana na Mungu awabariki ili mzidi kungara ulimwenguni.
....................................................................................................................
MGN: Ahsante sana pia ninakushukuru sana na Mungu awabariki ili mzidi kungara ulimwenguni.
....................................................................................................................
BASI KWA UFUPI KAMA TULIVYOMSIKIA MBEBA MAONO NA
MKURUGENZI,GRACE LIFARD MLAWA, HILO NDIO KUNDI LA DANCE LA LA 1ST Q LENYE MAKAO YAKE JIJINI DAR ES SALAAM ,AMBALO
LINAENDELEA KUKUA NA WAKO TAYARI KUFANYA
KAZI NA KANISA,MWIMBAJI,DANCERS NA MTUMISHI YEYOTE YULE ALIYE TAYARI AITHA IWE
TAMASHA,IBAADA AU HATA KUFANYA VIDEO RECORDING KWA WAIMBAJI WA NDANI NA NJE YA
NCHI YA TANZANIA SAWASAWA NA MISINGI NA TARATIBU ZA KUNDI HILO KWA UTUKUFU WA
MUNGU.
NATAMANI TUWATIENI MOYO VIJANA HAWA WALIOAMUA KUMTUMIKIA
MUNGU KUPITIA VIPAJI VYAO,BASI KWA KUJUA ZAIDI AU KUWAALIKA AU KUTAKA
KUSHIRIKIANA NAO BASI WAWEZA KUWAPA KUPITIA ANAUANI ZIFUATAZO;
Simu; +255719868702, +255719406060, +255654767422
Barua pepe;lifarda1@gmail.com
Facebook; 1st Q
KARIBUNI SANA KWA MASWALI NA MAONI AMA USHAURI
+255 713 883 797
lacs.project@gmail.com
+255 713 883 797
lacs.project@gmail.com