UTANGULIZI
: MAANDIKO NA MISTARI YA
KUSIMAMIA
Kumb 28: 1-14; “Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako,
kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana
Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya dunia; na baraka hizi
zote zitakujilia na kukupata, usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.
Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako,
na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe
wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha
kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa utokapo. Bwana atawafanya adui
zako wainukao juu yako, kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini
watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Bwana ataiamuru baraka ije juu
yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye
atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. Bwana atakuweka uwe taifa
takatifu kwake … na mataifa yote ya dunia watakuona umeitwa kwa jina la
Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri,
katika uzao wa tumbo lako … Bwana atakufunulia hazina yake nzuri … nawe
utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe. Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si
mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakaposikiza maagizo ya Bwana,
Mungu wako
... kuyaangalia na kuyafanya; msipokengeuka … kwa lolote, kwenda mkono wa kuume
wala kushoto…”
Kumb 8:10-20; “Nawe utakula ushibe,
utamshukuru Bwana, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa. Jihadhari usije
ukamsahau Bwana, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na
sheria zake, ninazokuamuru leo. Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na
kujenga nyumba nzuri, na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng’ombe na kondoo
yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu
chako kitakapoongezeka; basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu
wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa … Hapo usiseme
moyoni mwako, nguvu zangu na uweza wa mkono wangu, ndio ulionipatia utajiri
huo. Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata
utajiri; ili alifanye imara agano lake …”
...........ITAENDELEA!!!
No comments:
Post a Comment