Saturday, August 31, 2013

RAIS WA JAMHURI WA TANZANIA, DK JAKAYA KIKWETE AMLILIA DK MOSES KULOLA!!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Kiongozi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Dkt Moses Kulola ambaye ameaga dunia asubuhi ya Alhamisi, Agosti 29, 2013 katika Hospitali ya AMI iliyoko Masaki mjini Dar Es Salaam akiwa na umri wa miaka 85, yaani alizaliwa 1928-2013!


 Kiongozi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT)  Marehemu Askofu Mkuu Moses Kulowa.
Rais kikwete ameelezea mshtuko na huzuni yake katika Salamu za Rambirambi alizomtumia Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Bwana Brown Mwakipesile kufuatia kifo cha Askofu Mkuu Kulowa. 
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za kifo cha Mtumishi wa Mungu wa muda mrefu na Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Marehemu Moses Kulola kutokana na maradhi yaliyomfanya wakati fulani apelekwe hadi India kupatiwa matibabu” amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete amesema alimfahamu Marehemu Askofu Moses Kulola kwa miaka mingi wakati wa enzi za uhai wake, kama Mtumishi Hodari wa Kiroho aliyejitoa vilivyo katika kuwahudumia Waumini wa Kanisa lake ambapo mahubiri yake yametoa mchango mkubwa katika kuimarisha imani za Waumini wake na kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu.
Aidha Rais Kikwete amesema kifo cha Askofu Mkuu, Moses Kulola kimeacha pengo kubwa siyo tu kwa Waumini wa Kanisa lake hapa nchini, bali pia miongoni mwa wapenda amani kote nchini na kwingineko duniani kwa vile enzi za uhai wake, Marehemu aliweza kufikisha ujumbe muhimu wa kiimani kupitia mahubiri yake kwa watu wa mataifa mbalimbali ndani na nje ya  Bara la Afrika.
“Kwa niaba yangu mwenyewe na Serikali ninayoingoza, ninakutumia wewe Katibu Mkuu wa Kanisa la Evangelical Assembies of God Tanzania, Bwana Brown Mwakipesile na Waumini wote wa Kanisa hilo Salamu za Rambirambi  kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza Kiongozi muhimu wa Kiroho.  Ninawajulisha kuwa niko nanyi katika wakati huu mgumu kwa sababu msiba wenu ni msiba wetu pia. Sala na mioyo yetu iko nanyi wakati wa maombolezo ya kifo cha Kiongozi huyo shupavu wa dini. Nawaomba wote muwe wavumilivu na wenye subira kwani yote ni Mapenzi yake Mola”, amesema Rais Kikwete.

“Vilevile kupitia kwako, naomba unifikishie Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu, Askofu Mkuu, Moses Kulola kwa kumpoteza Baba, Kiongozi Shupavu na Mhimili wa familia.  Natambua fika kwamba hiki ni kipindi kigumu sana kwao cha maombolezo.  Natambua machungu yenu wakati huu na naungana nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke peponi roho ya Marehemu Moses Kulowa. Amina.”

Mazishi ya Marehemu, Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) yatafanyika mjini Mwanza Jumatano ijayo tarehe 4 Septemba, 2013.  Heshima za mwisho kwa mwili wa Kiongozi huyo zimetolewa leo Jumamosi tarehe 31 Agosti, 2013 katika Kanisa la EAGT karibu na Hospitali ya Temeke kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni!
Kwa hisani kubwa ya Christian Bloggers network .

Thursday, August 15, 2013

....KWA MARA NYINGINE TENA WAIMBAJI WOTE WA INJILI MNAKARIBISHWA...."GOSPEL SINGERS' BREAKFAST".....Episode 5!!

Hello Shalom!
HABARI NJEMA KWA WAIMBAJI WOTE WA NYIMBO ZA INJILI!
Kwa mara ya TANO;<Chavala Ideas Platform> kupitia Blog ya Kikristo Gospel Standard Base(http://gospelstandardbase.blogspot.com/) inakukaribisha kwenye Chai Maalum ya Asubuhi ya Waimbaji wote wa Nyimbo za injili (TANZANIA GOSPEL SINGERS' BREAKFAST Episode 5), itakayonywewa JUMAMOSI HII (17th August, 2013);Kuanzia 2:30-6:30mchana pale Victory Christian Centre (VCC)-Victoria,barabara ya bagamoyo...Na mara hii tutakuwa na Walimu na Watumishi Kadhaa kama vile Samuel Sasali, Prosper Alfred Mwakitalima,King Chavala-MC na wengineo katika Panel kuzungumzia "NAMNA YA KUKUA KIROHO NA KUSTAWI KIHUDUMA"....Chai sio bure ingawa HAKUNA KIINGILIO.....Ikiwa wewe ni muimbaji wa kwaya,band,kikundi,mwimbaji binafsi,timu ya kusifu na kuabudu ya kanisani,ikiwa unaimba Hip hop,RnB,Rock ama Gospel Reggae basi hii ni nafasi yako,NJOO UJIFUNZE NA UJUMUIKE NA WENZAKO!
......HATA KAMA UNA KIPAJI,FEDHA NA JINA KIASI GANI,BADO IMEKUPASA KUTAFUTA SHULE ZAIDI ILI UWE STADI!!!!
Kwa maelezo zaidi +255 713 883 797 au Tembelea Http://gospelstandardbase.blogspot.com/ au Blog yeyote ile ya Kikristo!!!!
MUNGU AKUBARIKI WEWE UTAKAYEKUJA BILA KUKOSA NA KUWAHI NI MUHIMU SANA!!


KWA MAELEZO;
+255 713 883 797
E-mail; lacs.project@gmail.com
King Chavala-MC

Sunday, August 11, 2013

KUTOKA MADHABAHUNI......"BAADA YA KUSUBIRIA....HATIMAYE UTAMILIKI NA KUBARIKIWA!!"

SHALOM!
NAAMINI UNA JUMAPILI NJEMA HATA LEO!
SIKIA NENO LA BWANA TOKA MADHABAHUNI KWAKE KAMA VILE LINVYONENWA NA MCHUNGAJI WA VICTORY CHRISTIAN CENTRE (VCCT), MBEZI BEACH A, DAR ES SALAAM; DKT HURUMA NKONE!!


MAANDIKO; JOSHUA 1:29;11:23

Bwana Yesu asifiwe sana!
Leo ibaada yetu iko moja kwa moja kupitia Redio Wapo FM (98.1), na tutaendelea kuwa hewani moja kwa moja kupitia redio Wapo kila jumapili ya kwanza ya mwezi!

Habari hii inawahusu wana waisraeli wakiwa safarini kwenda nchi ya Ahadi chini ya Uongozi wa Joshua baada ya Muda wa Musa kuisha.
Na hapa Joshua alikuwa akipewa maagizo na mazingatio ya muhimu...Itakuwa mtakapotia miguu yenu kukanyaga nchi ile itakuwa mikononi mwenu, na muwe hodari na moyo wa ushujaa kwa maana ni haki yenu.

Wana waisraeli wakiwa na Joshua walishuhudia miujiza mingi pia ukiwapo ule wa Maji ya mto Yordni kugawanyika na wao kuvuka naam baada ya hapo Joshua na wanawaisraeli walianza kwa kuteka Yeriko na miji mingine mitatu mikubwa ya kati na kwa gia hii walikuwa wana nguvu ya kutosha kuendele kuichukua nchi nzima maana walikuwa wana mkakati bora.

NINI MUHIMU MAISHANI MWAKO SASA;
Ulipookoka umefanikiwa kuingia nchi ya ahadi; lakini bado ipo kazi ya kuendelea kuteka na kuchukua baraka zako...maana hapo kwanza kabl hujaokoka vilikuwa vinamilikiwa na shetani. Ni kweli umeweza kutikisa kuta za Yeriko na zimebomoka....naam usiishie hapo unapaswa kuendelea kuteka na kuteka mpaka hapo utakapomiliki nchi yako nzima...naamanisha ulimwengu wa wokovu wako.

 Lazima wakristo tubadilike...tuache kuamini maombi tu katika kila jambo bila kufanya jambo lingine lolote...kwa mfano hauwezi ukaomba upandishwe Cheo kazini na hali unaendelea kuchelewa kazini na kufanya uzembe mwingine haiwezekani....kama ukitimiza wajibu wako na kufanya yote yakupasayo kw haki na kwa bidiii, kwa hakika utapokea tu toka kwa Bwana...maana maandiko yanasema....KAMA MKITII MTAKULA MEMA YA NCHI!

Kumbuka hatuokoki ili tupate vitu fulani kwa Bwana kama vile fedha, majumba, waume na wake ama watoto, ila tunaokoka kwasababu tumechagu kumpenda Bwana na ukishaokoka na kuwa mwaminifu basi vyote hivyo unavyovistahili vinakujia kwa kujaa na kusukwa sukwa.

UJUMBE KWA VIJANA;
Lazima ujifunze kutulia na kusubiri,haiwezekani utoke chuo leo na utaka uendeshe Range Rover,acha kutamani kila kitu...ikiwa unavistahili basi ujue kwa hakika muda ukifika lazima utamiliki tu...vinginevyo utaumia sana ukitaka vitu visivyo saizi yako.

Natamani kama ungemtukuza Bwana katika maisha yako kwa namna ambayo watu watajiuliza wewe ni mtoto wa nani,maana ulimwengu umezoea watu wamnaopenya ni wale wenye watu wakubwa serikalini....Baraka yako ipo maana Mkono wa Mungu uko juu yako....na lazima ujue jambo moja kuwa penye Vita yako ndio penye baraka yako!

SEMA SALA HII KWA IMANI;
EEH BWAN YESU, NINAKUSHUKURU KWA NENO LAKO NA MTUMISHI WAKO, NIMESIKIA NA NIMEAMINI,NAAM NATAMANI NENO HILI LIWE HALISI MAISHANI MWANGU,NISAIDIE NIKUSIKIE KWA KINA ILI NIJUE NINI KINACHONIPASA KUFANYA KILA SIKU, MAOMBI YANGU LEO NI KUWA BWANA UNISAIDIE KILA WAKATI KUKUMBUKA KUWA VITA NI YAKO NA SIO YANGU,NIPE NEEMA YA KUWA NA SUBIRA NA KUSUBIRI BARAK YANGU, NISAIDIE KUITUMIA AKILI YANGU NA UTASHI ULIONIPA ILI NISIZEMBEE KIMKAKATI, AHSANTE YESU KWA MAANA KILA HATUA UTAKUWA NAMI,AHSANTE YESU KWA KUNISIKIA, KATIKA JINA LA YESU KRISTO,AMEN!!!

MUNGU ATUSAIDIE TUNAPOENDELEA KULITAFAKARI NENO HILI KUWA KILA MAHALI AMBAPO BWANA AMETUPA KUKANYAGA KATIKA ULIMWENGU W ROHO NA WA MWILI BASI HAPO AMETUPA KUMILIKI,NAAM UTAPATA VYOTE UNAVYOVISTAHILI KAMA UKIWA NA IMANI SAHIHI NA PIA UJUE VITA SIO YAKO BALI VITA NI YA BWANA, AMEN!

Mungu awabariki sana!!

Imeandikwa na
King Chavala MC
+255 713 883797

Thursday, August 8, 2013

JUMAPILI HII TUNAKUTANA KWA IBAADA MOJA TU...KUSIFU NA KUABUDU TU!!

VIJANA,WABABA NA WAMAMA KUTOKA PANDE ZOTE ZA JIJI LA DAR ES SALAAM NJOONI PAMOJA TUMSIFU NA KUMWABUDU BWANA JUMAPILI HII PAKE TAG MAGOMENI, HII NI BURE NA SI YA KUKOSA KWA MTU YEYOTE!!!
UKIPATA TAARIFA HIZI MTAARIFU NA MWENZAKO!!!

Wednesday, August 7, 2013

JITAMBUE..."CEREMONY AT THE BATTLE FIELD"!!!!





ENDELEA.......

BAHARI YA KIOO....MFAHAMU "EMMANUEL MGALLAH",MWIMBAJI WA INJILI ANAYEJITUMA KIPEKEE SANA!!

Bwana Yesu Asifiwe sana!
Natumai kila mmoja yuko vizuri!
Mimi binafsi ni mzima sana na namtukuza Jehova kwa upendeleo na zawadi ya uhai, sijui ni nini kesho imeshikilia kwa ajili yangu, lakini Ninamjua anayeimiliki Kesho, naam tunafahamiana vema na kwasababu yeye anaishi,Lazima nitaiona kesho.

Leo Baharini nimemwona kijana huyu mtumishi wa Bwana ambaye ana moyo wa kipekee wa kujituma katika Utumishi na katika kazi zake binafsi.

Leo ninamzungumzia Mtumishi EMMANUEL MGALLAH, Mwenyeji wa Igamba, Mbozi Mbeya, Mnyiha kwa kabila; mwimbaji wa nyimbo za injili aliweka makazi yake Jijini Dar es salaam.

Karibuni Bahari ya Kioo ya Gospel Standard Base Blog ilifanya mahojiano nae kwa kina ili kutaka kujua mengi yamhusuyo kijana huyo, na kwa hakika hii ndio habari kuhusu Emmanuel Mgallah;

HISTORIA KWA UFUPI;
Emmanuel ni mzaliwa wa Igamba, Mbozi,Mbeya...alianza Shule ya msingi pale TANDALE UZURI, shule ambayo alisoma mpaka darasa la sita na kwenda kumalizia darasa la saba IGAMBA SHULE YA MSINGI iliyo mbozi Mbeya, na hapo akajiunga ya shule ya Sekondari ya Mbozi Mission, shule inayomilikiwa na Kanisa la Moravian,

Emmanuel hakufanikiwa kumaliza kidato cha nne katika shule hiyo, hivyo alihamia Mbezi High School iliyoko jijini Dar es salaam na kumalizia kidato cha nne hapo, na baadae akajiunga na THE CONTEMPORARLY COLLEGE iliyo Kinondoni, mahali ambapo alifanya kozi ya lugha kwa mwaka mmoja na kisha kujiunga na EAST AFRIKA TRAINING COLLEGE mahali ambapo aliendelea kusoma Lugha pamoja na Kompyuta na kisha akafanya kozi ya Ujasiriamali kwa mwaka mmoja.

KAZI;
Mwaka 2009 alipata kazi kama Afisa Mikopo (Credit Officer) wa SIMKA, iliyo magomeni usalama.

Mwaka 2012 alibadili kazi na kuanza kufanya na General Credit Company mahali ambapo alifanya mpaka Jan 2013, wakati alipoamua kujiudhuru na kuanza kufanya kazi zake binafsi za kijasiriamali.

Emmanuel ana miliki na kuendesha Biashara yake ya Bodaboda, anafanya kazi kama Dereva wa gari ya shule Libermenn Pre & Primary, lakini pia anafanya kazi za ushereheshaji (MC),

hivyo maisha yao yanaenda hivyo....na mke wa Emmanuel au Mama Jonathan yeye ni nesi katika Dispensary moja pale manzese, hivyo nae anamsaidia mumewe kustawi huku wakimtumikia Mungu katika ndoa YAO AMBAYO ILIFUNGWA MWAKA 2011
 FAMILIA;
Emmanuel ameoa mke mmoja na ana mtoto aitwaye Jonathan na kwasasa wanaishi kwafuraha yeye na mke wake maeneo ya Kimara,kinondoni, Dar es salaam.


HISTORIA YA UIMBAJI YA EMMANUEL;

Habari ya Emmanuel kuimba  ilianzia Sunday school na kisha akajiunga na kwaya ya kanisa la moravian-Mbozi mission na hapo akajiunga na kwaya nyingine iitwayo Emmanuel ya hapo hapo mbozi mission moravian na baada ya kuja jijini Dar es salaam alijiunga na Faith kwaya ya magomeni moravian iliyo chini ya Mwenyekiti Paulo Mlawa kwa sasa na akiwa ndani ya kwaya hiyo ndio akaanza michakato ya kuimba mwenyewe.

Alifanikiwa kurekodi album yake ya kwanza  mwaka 2011 pale Magic Star Studio chini ya fundi Ayubu pale Sinza na Kisha kufanya Video ya album hiyo mwaka 2012, chini ya Muongozaji Gilbert Mgalama.

Albamu hiyo ina nyimbo nane na inaitwa "HABARI NJEMA"....Habari njema ni moja ya nyimbo zinazosikika kwenye vyombo vya habari pamoja na "Kwanini Uteseke" na "Tawala kwa maombi"

Emmanuel alifanikiwa kufanya Uzinduzi wa Album ya sauti Desemba 23, 2012 na mpaka sasa hajampata msambazaji, hivyo anasambaza mwenyewe.

NINI MALENGO YA EMMANUEL HAPO MBELENI??
Emmanuel ni mwimbaji wenye shauku kubwa sana ya kukua na kwa jinsi ninavyomuona, nauona uwezo mkubwa sana ndani yake na atang'aa sana kama akitulia na Mungu sawasawa.. lakini ni maneno ambayo yeye mwenyewe aliyasema;


"....Ninakusudia kuwa na Studio na zaidi nategemea kusaidia waimbaji wadogo wadogo wanaonyanyaswa kwa kukosa fedha na zaidi natamani kuwaandaa wahubiri wa injili"

......Nimetembea mikoa zaidi ya mitano kihuduma na nakusudia kutembea Tanzania nzima kadri Mungu atakavyoniwezesha.

Imekuwa ni kawaida kwa Waimbaji wengi wa injili kuruka ruka tu bila kuwa na walezi wao wa kiroho, na nilipomuuliza ndugu kuhusu kijana huyu, haya ndio alimalizia kwa kuyasema;



EMMANUEL UNALELEWA NA NANI?
".....Mimi nalelewa na Mchungaji NOEL MWAKALINGA pale Magomeni Moravian na hapo ndio ninaposali na kuendelea kuimba kwaya ya Faith ya kanisani hapo.....natamani sana kufika mbali, nayafurahia sana unayoyafanya wewe (akimaanisha Mimi King Chavala) na wewe kwa sasa ndio mtu ninayejifunza kwake na natamani kuwa kama wewe katika mengi ufanyayo....nakuombea Mungu akusaidie ili uimarike zaidi na zaidi katika kusaidia Tasnia ya Uimbaji wa injili Tanzania na hapo baadae uwe msambazaji maana wewe unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko hawa wa sasa maana hawahui hasa uzito injili,Ahsante sana na Mungu akubariki.!"

CHANGAMOTO;
Emmanuel alisema Changamoto zinazomkabili ni Gharama kubwa ya kufanya kazi na vyombo vya habari na pia gharama kubwa za Studio.


UJUMBE WA EMMANUEL KWA WAIMBAJI WOTE;
"..Watu waliotangulia wasidhani kama wengine hawawezi kufanya au kufika mahali walipo, hivyo natamani kuwepo na umoja kati yetu na hapo ndio tyunaweza kufika mbali zaidi...na sio umoja wa siasa tu bali Kama Kristo na Mungu walivyokuwa na Umoja."

BAHARI YA KIOO haina la ziada zaidi ya kumshukuru Emmanuel Kwa kufunguka na kuamua kufahamika kwa kina, naam naamini kila mtu sasa atakuwa anamfahamu kwa kina na mtumishi huyu anasema yuko tayari kufanya kazi na mtu,kanisa na huduma yoyote popote....yamkini unamwitaji kama Mshauri wa namna ya kutumia mikopo midogo midogo, au kuhusu Bodaboda, ama kumwalika Kuhudumu kwa Kuimba, kufundisha ama kusherehesha, basi haya ndio mawasiliano yake;

EMMANUEL MGALLAH
+255 713 635 898 AU +255 769 070 458
E-mail; emmanuelmgallah@yahoo.com
Facebook; Emmanuel Mgallah

BASI TUNAWATAKIA MAFANIKIO MEMA WOTE MTAKAOSHIRIKIANA NA EMMANUEL KATIKA KUINEZA INJILI YA BWANA WETU YESU KRISTO,AMEN!!

Na King Chavala-MC
Hotline; +255 713 883 797
(c)2013- Bahari ya Kioo ya GoStaBa