Wednesday, March 27, 2013

USIONEKANE TU MZURI KWA MBALI LAKINI UZURI UKO MBALI NA WEWE(01)

Shalom!

Nawasalimia wasomaji wote kwa Jina la Yesu Kristo, Bwana na mwokozi Yesu Kristo!

Natumai mko vema na mnaendelea vema, kuna mengi sana ya kuzungumza katika misingi hii ya Injili bora na leo nimesukumwa kuongea na wadada na wanawake jambo moja la muhimu kweli,lizingatieni hili litawasaidia mno.

Mungu alipokuumba mwanamke wala hakukosea,alikuumba kwa kusudi maalum na ana mpango kamili na maisha yako.
kila alichokiumba Mungu ni kizuri ingawa binadamu huona tofauti,maana wanadamu wametafsiri uzuri kama mapendezo ya macho sawasawa na tafsiri kichwa cha mwenye macho!
Mungu amewaumba wasichana na wanawake kwa namna ya kipekee na uzuri wa ajabu, ndio hata kama watu hawatasema lakini kuna uzuri upo unaowafanya muwe mapambo ya Dunia!

Mungu amemuumba mwanadamu kwa hatua,naama kila kiumbe pia hupitia hatua fulani katika kiushi kwake....mwanadamu huwa na maisha ndani ya wazazi na kisha kuzaliwa>huwa mtoto>hukua na kuanza kutembea na kufanya mengi>na muda ukifika hupevuka na hapa ndio mtu huwa mrembo na mzuri sana,kisha kuna kipindi chwa mwanzo cha ujana,ujana huja na hatimaye utu uzima na kisha uzee kabla ya kupumzika katika maisha haya ya ulimwengu!!

Kila hatua Mungu aliyoiumba ina raha na manufaa yake kwa kila kiumbe na kwa kuwa hapa nazungumza na wadada na wanawake, nataka nisistize kuwa kila hatua ya kukua kwenu ina maana sana katika maisha yenu na kwa Mungu pia! imekupasa kujifunza vema kutumia muda vizuri na kufurahia kwa kina kila hatua ya maisha yako.
ukiwa na ule usichana mdogo imekupasa kucheza michezo yote ya rika hilo na unapopevuka basi fanya yale maadili yote yakupasayo,maana nawaona watu wengi hufanya makosa sana na baadae kufanya mabo ya kitoto wakiwa watu wazima!


Mungu amekuumbia mpango maalum wa maisha ya baadae,kama hujaamua kuifuata njia ua utawa,maana yake unahitaji kuwa na familia bora,lakini hiyo familia bora haipatikani kwa nadharia bali kwa kujiandaa vema,katika ndoa mna ndio maana kila mahali biblia husema...mke mwema nani awezaye kumuona?

Nimeona wasichana wengi wa kipindi hiki wamekulia maisha ya kudeka na uvivu, kiasi cha mpaka nguo zao za ndani zinafuliwa na wasichana wa kazi au mashine,si ajabu kumuona binti mwenye miaka zaidi ya 20 hajui kupika wala kufanya kazi za nyumbani!

Si mbaya bado muda unao,kama kweli unataka kuolewa na kuwa na familia bora imekupasa kuanza kujiandaa sasa,kwa kujifunza yale yote yakupasayo kujua ili uwe mke mzuri na mama mwenye akili wa familia,zaidi unapaswa kujiandaa kisaikolojia,kiuchumi,kijamii na kiakili....kuna somo nimewahi kusikia mtumishi mmoja akifundisha na alisema;
.....UNTIL WHEN YOU ARE SINGLE,THEN YOU ARE REDY TO BE MARRIED!!!
na hapo kuwa single ina maanisha ukifika mahali unaweza kujitegemea na kujisimamia mwenyewe kimaamuzi,kimaisha,kiuchumi na kijamii,hapo ndipo unaweza ukamkaribisha mtu moyoni mwako ili awe mume wako!

kiini cha maada hii ni hiki,yamkini unajiona mzuri sana,na labda watu wengi wamekusifia hivyo na yamkini ndivyo ulivyo,na tangu umesifiwa na kusumbuliwa na vijana kadhaa kukutaka basi tena umekuwa na kiburi,madaha na nyodo za kutosha mrembo,na kwa kuwa una kazi nzuri labda na kagari basi tena umeona maisha yamefika mwisho,si mbaya siwezi kukulaumu labda ndivyo ulivyolelewa au ni ulimbukeni tu!

*******************************************************************************
lakini natamani utambue jambo moja uzuri wa msichana sio muonekano pekee bali na tabia, hivyo unaweza ukanga'ara sana kwa mbali lakini watu wakikukaribia hawatakaa watakimbia tu....jijengee heshima ya kipekee ambayo itawafanya watu wakuite dada hata kabla hujawakolomea
....."YOU LOOK GOOD FROM FAR BUT ON ACTUAL FACT YOU ARE VERY FAR FROM GOOD" (Unaonekana mzuri toka mbali lakini ukweli ni kuwa uko mbali na uzuri)
na yamkini sasa hivi hilo hulioni,jaribu tu basi kujitathmini na ujue watu wanakuonaje,itakuwa vizuri kama utaanza na marafiki wa karibu kabisa!
Uzuri na ubaya wa maisha ni huu,yaani hata kama wewe hujui kiasi gani bado ukweli utakuhukumu tu!
HONGERA SANA KWA KUWA MZURI,LAKINI JENGA TABIA YAKO.....A WOMAN IS NOTHING WITHOUT A CHARACTER!!!
......Your beauty might take you higher but what can make you remain there is character!!!!
Natamani kama ungenielewa,binafsi sipendi kabisa kuona wasichana warembo wanaangukia katika mikono ya waharibifu,wachafuaji,wafiraji na wasiojiheshimu eti kwa kutekwa na fedha na mali za wanaume hao ama kuwakomoa wale waliojisumbua kuwafuata!!!!
*******************************************************************************

Yamkini umekuwa ukiwajibu vibaya sana na kuwatesa wakaka au vijana wanaokutongoza kwa minajili ya kukuoa,sisemi uwakubali lakini unawajibuje? unajua hekina ni kitu kidogo sana lakini ndio msingi mkuu wa mafanikio!
YAWEZEKANA UNAJIDANGANYA SANA NA KIOO CHAKO CHA CHUMBANI NA UNADHANI UREMBO WAKO WA SASA UTADUMU, AU UNADHANI SASA UNA MUDA HIVYO UNAENDELEA KUWASUMBUA WAKAKA UKIAMINI KUWA WATAENDELEA KUJA TU....MMH NATAKA NIKWAMBIE MUDA WA UZURI NI MFUPI SANA,MUDA WA KUNG'ARA NA KUWAVUTIA WENGI NI WA KITAMBO TU,UKIONA MUDA HUO UMEPITA UTAPATA SHIDA SANA,MAANA UTATAMANI WAJE NA HATA WALE WALIOWAHI KUJA HUTAWAONA TENA NA HATA WALE WABAYA HAWATAKUJA,Hapo ndipo wengi hupata mishtuko na presha na kuamua tu kuolea na yeyote ilimradi na maisha hayo hayawezi kuwa mazuri hata kidogo,maana ni maamuzi ya ilimradi!!

NIMESHUHUDIA WASICANA NA WANAWAKE WENGI SANA AMBAO WARIRINGA WAKATI WA USICHANA WAO NA WAMEKUJA KUOLEWA NA 35,40 NA 45,TENA KWA KUJIOZESHA KWA VIJANA WADOGO AMA WAZEE WALIOFIWA NA WAKE ZAO NA WAKATI HUO HATA MAISHA HAWAYAFAIDI VIZURI.


Usijaribu kijiringanisha na wanaume maana wao hata umri ukienda bado wanaweza kuoa tu,tena wasichana wazuri wa kipindi hicho,hivyo acha maringo na madaha yasiyo na maana,acha kuwatesa vijana na achana na tabia ya kushindanisha wanaume kutokana na vitu walivyo navyo,ukimpata mtu anaekupenda kwa dhati tia baraka mfukoni kisha mshukuru Mungu, mali na vitu hupatikana tu na hasa kama wewe una akili njema vitakuja vingi sana tena sana!!

UKIWA KAMA MSICHANA UNAYO NAFASI NZURI YA KUFANYA VIZURI KATIKA MAISHA YAKO,USIKURUPUKE KUFANYA MAAMUZI,USIKIMBILIE VITU,USIPUPARIKIE MAISHA,JIFUNZE NA UJIPANGE KUAMUA NA HAKIKISHA UNAMUHUSISHA MUNGU 100%KATIKA MAAMUZI YAKO,NA MUHIMU UKUMBUKE KUWA UKIAMUA TU,HAYO NDIYO MAISHA YAKO!!!

#UNAWEZA UKARINGA NA KURUKARUKA UTAKAVYO LAKINI IKIFIKA SAA UTANASWA TU,SASA UKINASWA NA MTEGO NI MATESO YA MAISHA YAKO YOTE NA UKIANGUKIA KWA YULE AKUPENDAE BASI HIYO ITAKUWA PARADISO YAKO NDOGO HAPA DUNIANI!!!

natamani nimalizie andiko langu hili  kwa kusisitiza jambo hili
.....YOUTH IS GLORIOUS BUT IS NOT A CARRIER!!!

Na KING CHAVALA
+255 713 883 797

>>>>>>TO BE CONTINUED!!!!!!

No comments:

Post a Comment