Wednesday, April 3, 2013

SADAKA NA DHANA YA UTOAJI (The concept of Giving and Offerings)



UTANGULIZI  :  MAANDIKO NA MISTARI YA KUSIMAMIA

Kumb 28: 1-14; “Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya dunia; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata, usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa utokapo. Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako, kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.

Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake … na mataifa yote ya dunia watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako … Bwana atakufunulia hazina yake nzuri … nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe. Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakaposikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako ... kuyaangalia na kuyafanya; msipokengeuka … kwa lolote, kwenda mkono wa kuume wala kushoto…”

 Kumb 8:10-20; “Nawe utakula ushibe, utamshukuru Bwana, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa. Jihadhari usije ukamsahau Bwana, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo. Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri, na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu chako kitakapoongezeka; basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa … Hapo usiseme moyoni mwako, nguvu zangu na uweza wa mkono wangu, ndio ulionipatia utajiri huo. Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake …”


...........ITAENDELEA!!!

No comments:

Post a Comment