Thursday, February 7, 2013

#TANZIA#....BABA ASKOFU DK.THOMAS LAIZER WA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI AMEFARIKI DUNIA!!

Baba Askofu Dr.Thomas Laizer-KKKT Dayosisi ya Kaskazini kati
SHALOM!
NINA IMANI TUKO VIZURI NA TUNAENDELEA VEMA NA MAJUKUMU NA MAISHA YETU YA KILA SIKU, KWA HABARI ZILITHOBITIKA NI KUWA BABA ASKOFU DK.THOMAS LAIZER WA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI, AMEFARIKI DUNIA JANA JUMATANO JIONI(07/02/2013) KATIKA HOSPITALI YA LUTHERAN SELIAN, AMBAPO ALIKUWA AMELAZWA KWA MUDA KIDOGO, INASEMEKANA KUWA BABA ASKOFU ALIKUWA AKISUMBULIWA NA KIFUA AMBACHO KILIKUWA KIMEJAA MAJI!

ASKOFU HUYU KTOKA KABILA LA WAMASAI,AMEFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 68 NA NDIO ASKOFU WA KWANZA WA KKKT ARUSHA!


KWA HABARI ZAIDI JUU YA KIFO CHAKE TUTAPATA PUNDE TUTAKAPOWASILIANA NA WAHUSIKA NA ZIDI KWA MIPANGO YOTE YA IBAADA ZA KUAGA NA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO PAMOJA NA MAZIKO MTAJULISHWA KWA KADRI FAMILIA NA KANISA LITAKAVYOONA INAFAA!

PIA BLOG ITAKUANDALIA HISTORIA YA UHAI NA UTUMISHI WAKE HAPA DUNIANI,ILI UPATE KUTIWA MOYO KUWA SAFARI YA UTUMISHI INA THAWABU NJEMA!!
KWA NIABA YA WAANDISHI,WATUMISHI NA WAFANYAKAZI WOTE WA BLOG HII PAMOJA OFISI YA "CHAVALA IDEAS PLATFORM" TUNAWAPA POLE SANA FAMILIA YA MAREHEMU,NDUGU JAMAA NA WATOTO NA KANISA LA KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI KATI NATANZANIA KWA UJUMLA NA POLE IMFIKIE MKUU WA KKKT-TANZANIA,ASKOFU ALEX MALASUSA KWA KUMPOTEZA KIONGOZI WHAPANA SHAKA KWAMBA HAKUNA ATAKAYEWEZA KULIZIBA PENGO LAKE,ILA NI KAZI KWETU SOTE TULIOBAKI KUYAENDELEZA YALE MAZURI YOTE ALIYOYAASISI NA KUYAENZI NA ZAIDI KUWA TAYARI KWA SAFARI WAKATI WOWOTE MAANA MAANDIKO YANASEMA KESHENI MKIOMBA MAANA HAMJUI SIKU WALA SAA!

NINAYO AMANI KUSEMA KUWA MUNGU NA AMPUZISHE MAHALI ALIPOMKUSUDIA MTUMISHI WAKE,AMEN!!

FREDY CHAVALA
President-CHAVALA IDEAS PLATFORM
+255-(713/753)-883 797
lacs.project@gmail.com
DAR ES SALAAM!!

No comments:

Post a Comment