Sunday, February 17, 2013

Kutoka madhabahuni>>>HATMA (DESTINY)

SHALOM!
NAAMINI UKO SAWA NA BADO YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO!
HATA KAMA UNAPITIA MAMBO MAGUMU NATAKA NIKUTIE MOYO KUWA NEEMA YA MUNGU INAKUTOSHA NA USHINDI WAKO UKO DHAHIRI,JITAHIDI USIZIMIE MOYO,WEWE MWAMINI KRISTO TU!!
LEO TUNAPATA NENO TOKA MADHABAHU YA VICTORY CHRISTIAN CENTRE TABERNACLE(VCCT), MBEZI BEACH A KWA MCHUNGAJI DK HURUMA NKONE!
Na kabla YA Neno leo walikuwepo THE VOICE ambao wameimba wimbo wao "MAVUNO" na pia akaimba mwimbaji mwingine pamoja nao aitwae "ANGEL MAGOTI"


SOMO/MAHUBIRI YA LEO: "HATMA"
<<Mwazo 22:1-24>>
Hii ni habari ya Abrahamu na lile jaribu la Mungu kwake kuhusu kumtoa mwanae ISAKA kama sadaka ya kuteketeza, na jambo la kipekee ni kuwa Abrahamu hakumzuilia hata kidogo mwanae bali aliadhimia na kukubali kumtoa kwa Mungu,na Mungu hakusema neno mpaka alipoona uhakika wa Imani yake kwa Mungu na hapo Mungu akampatia mbadala wa sadaka na Kumwita Abrahamu "BABA WA IMANI" na yeye Abrahamu akayaita yale madhabahu "MUNGU MPAJI"(JEHOVA YIRE)

Mchungaji alianza kwa kusema:
UNAPOZUNGUMZIA HATMA,UNAZUNGUMZIA MWISHO HALISI ULIOKUSUDIWA, NA HAPA TUNAJIFUNZA MAMBO KADHAA KAMA
MUNGU ANAPOKUELEKEZA MAHALI PA KWENDA,HAKUPI HABARI KAMILI KWA WAKATI MMOJA,BALI HUWA ANAKUPA KIDOGO KIDOGO.......endelea!!!


sikia>>>MUNGU AKIKUPA HATMA(DESTINY) YA KWENDA HUWA HAKUPI MAAGIZO YOTE KWA WAKATI MMOJA LAKINI YEYE HUTOA MAAGIZO HAYO KWA HATUA,HIVYO UNATAKIWA KUTII NA KUCHUKUA HATUA YA IMANI NA KUFUATA YALE ULIYO NAYO MAANA MWISHO WA MAAGIZO YA KWANZA LAZIMA KUNA MAMBO YA PILI……Watu wengi hawako katika utumishi waliotiwa kwasababu wanataka kupata maagizo yote kabla ya kuanza safari ya utumishi wao.

ABRAHAMU ALIPOPATA MAAGIZO YA MUNGU,HAKUTAKA KUMSHIRIKISHA MTU HATA MKEWE,MAANA LAZIMA MKEWE ANGEMBISHIA TU….KIBINADAMU HATA KAMA UNGEKUWA WEWE LAZIMA UNGEGOMA TU,INAKUWAJE MUNGU ASEME ATAMFANYA ABRAHAMU BABA WA MATAIFA HALAFU AMTAKE MWANAE WA PEKEE ISAKA KAMA SADAKA?.....Hata wewe sasa Mungu akikupa maagizo unatakiwa kuyafuata na mara nyingine huhitaji kuwashirikisha watu maana mtu asiyeona hawezi kukushauri ushauri chanya!

JAMBO LINGINE LA KUSHANGAZA NI KUWA HATA ISAKA ALIKUWA MTII SANA KWA BABA YAKE IWAANDISHI WA HISTORIA WANASEMA ALIKUWA NA UWEZO WA KUMBISHIA BABA YAKE LAKINI ALITII HATA MWISHO MAANA ALIAMINI BABA YAKE ANAMPENDA NA NI MTUMISHI WA MUNGU,INGAWA ALIULIZA BABA SADAKA IKO WAPI? NA ABRAHAMU AKAMWAMBIA BWANA ATAJITWALIA MWANAKONDOO HUKO HUKO!....Sio kila mara unahitaji kubishana,wakati mwingine unahitaji kutii,maana sio kila maagizo ya Mungu hupitia njia nyepesi,na jambo la kuzingatia ni moja tu….SAUTI YA MUNGU ndio DIRA YETU,hivyo lazima uwe msikivu sana kusikia sauti ya Mungu kila hatua!!

ABRAHAMU ALIPOFIKA MLIMANI NA KUANDAA MADHABAHU,AKAMFUNGA MWANAE NA MARA ALIPOTAKA KUCHINJA SAUTI YA MUNGU IKAMWAMBIA,USIMCHINJE MWANAO ISAKA,TAZAMA PEMBENI KUNA MWANAKONDOO,HUYO MCHUKUE NA UMCHINJE,BASI ABRAHAMU AKAMFUNGUA MWANAE AMBAE NDIO MBEBA HATMA YAKE NA HATIMAYE AKAMTOA YULE MWANAKONDOO KAMA SADAKA,NA MAHALI PALE AKAMJENGEA BWANA MADHABAHU NA KUPAITA “YIRE” MUNGU MPAJI! NA ZAIDI ABRAHAMU AKAITWA BABA WA IMANI……Hata wewe unaweza ukafika mahali ambapo unaweza kuwa umeinua kisu juu kwasababu ya maagizo na mafunuo ya kale upate kuchinja na kumbe hicho unachotaka kuchinja ndio HATMA YAKO, sasa imekupasa kuwa makini na kuwa msikivu sana wa sauti ya Mungu,maana pale penye jaribu ndipo palipo na upenyo wa kutokea!

MSISITIZO MKUU NI KUWA MUNGU AMEMKUSUDIA KILA MTU HATMA YENYE MATUMAINI MEMA NA UTUKUFU MKUBWA IKIWA TU UTAAMINI NA KUTII NA KUFUATA KILA AGIZO LA MUNGU MAISHANI MWAKO BILA KUJIULIZA ULIZA!
MUNGU AKUBARIKI UNAPOENDELEA KUMTUMIKIA KWA UAMINIFU NA ROHO MTAKATIFU AKUFUNDISHE ZAIDI NA KAMA BADO HUJAMPOKEA YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO,BASI ZINGATIA KUMPOKEA SASA,KATIKA JINA LA YESU,AMEN!!

BY FREDY E. CHAVALA!!

No comments:

Post a Comment