Sunday, February 3, 2013

Kutoka Madhabahuni leo>>>NGUVU YA MUNGU KATIKATI MATATIZO ULIYO NAYO!!!

Shalom!
Natumai leo ni jumapili njema kwako na Mungu bado ana mambo anayafanya katika maisha yako!
Jumapili ya leo,Tunapata Mahubiri kutoka madhabahu ya Victory Christian Centre Tabernacle(VCCT) na Mchungaji Dk. Huruma Nkone(Mchungaji kiongozi)!
Akiwa ametoka ziara ya kitumishi nchini Sweeden leo ni jumapili yake ya kwanza na analo neno la kukujenga toka Katika maandiko matakatifu

Somo; Yohana 11:1-16,24-26
Hii ni ile habari ya Yesu na wale marafiki zake watatu waliofiwa na Ndugu yao Lazaro na ingawa Yesu alipata habari za kuumwa kwake,na hatimaye kufa kwake,bado hakuja haraka na Martha na wenzake iliwachanganya sana,kuona kwanini Yesu awaponye wengine huko na kwanini asije kumponya ndugu yao na hata saa alipokuja walimpokea kwa maneno ya kujifariji,Walimwambia umeshachelewa na hivyo amekwishakufa na tumemzika...Yesu alijibu Ugonjwa huo sio wa Kifo,na zaidi akasema Mungu atamfufua tu,bado wale ndugu hawakumuelewa Yesu na hiyo Martha alijifariji kwa kusema.....Najua atafufuka siku ile ya mwisho,lakini Yesu akasema Siyo siku ya mwisho ila leo!!

Mchungaji aliongea mambo matatu muhimu,katika somo lake la leo
1.ALISISITIZA; SIO KILA JAMBO GUMU MBELE YAKO NI LA KUKURUDISHA NYUMA AU KUUA MAFANIKIO YAKO...ila mengi huambatana na baraka ya kipekee,akasema usione mtu ana heshima au baraka fulani mara ukatamani kuwa kama yeye,bila kujua historia ya maumivu ya utukufu huo,hivyo tamani Bwana akupitishe katika mapito na mateso kwa ushindi wa utukufu huo ulio mbeleni....kama ambavyo kifo cha Lazaro kilikuwa ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu,basi na kwako yote yaliyokufa yawe ni kwa utukufu mwingi sana uliyo mbeleni!

2.PILI; USIACHE KUKIRI USHINDI HATA KATIKATI YA MATATIZO AU CHANGAMOTO ULIZONAZO AU UNAZOPITIA...kama ambavyo martha hakukata tamaa wala kulalamika na kwako iwe hivyo....wengi wakibanwa huanza kukiri kushindwa na kukiri matatizo mengine yaliyowahi kutokea huko nyuma,nataka nikutie moyo kuwa haijalishi ni magumu kiasi gani unapaswa kukiri ushindi na yale uyatazamiayo mbeleni....usiseme mimi ni bogus au wazazi wangu ni masikini au mimi sijawahi kupata hiki ama kile...bali unapaswa kukiri ushindi na kamwe usitarajie kuwashirikisha watu matatizo yako,lazima watakuvunja moyo tu maana na wao wana makubwa zaidi ya hayo yako,kwahiyo kikubwa mtazame Mungu na usiache kukiri ushindi katika JINA LA YESU,AMEN!!

3.TATU NA MWISHO; IPO NGUVU YA KUFUFUA  LOLOTE LILILOKUFA MAISHANI MWAKO!...na kimsingi ndio msingi wa somo au neno la leo, yawezekana kuna mengi yamekufa,ama ndoto zako nyingine hazina matumaini,Lakini nguvu ile ambayo ilimfufua lazaro ndiyo hiyo itakayofufua vyote vilivyokufa maishani mwako na kama unaamini sema Amen!!

NA HILO NDILO LILIKUWA NENO LA LEO,NINAOMBA MUNGU BABA NA MWANA NA ZAIDI ROHO MTAKATIFU,AMBAYE NI MWALIMU NA MSAIDIZI AKUFUNDISHE KWA KINA NA KWA UNDANI MAANA SOMO HILI LINAHITAJI UTAFAKARI WA KINA NA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU MWENYEWE,AMEN!!

Na FREDY E. CHAVALA
KUTOKA VCCT!!

No comments:

Post a Comment