Sunday, August 11, 2013

KUTOKA MADHABAHUNI......"BAADA YA KUSUBIRIA....HATIMAYE UTAMILIKI NA KUBARIKIWA!!"

SHALOM!
NAAMINI UNA JUMAPILI NJEMA HATA LEO!
SIKIA NENO LA BWANA TOKA MADHABAHUNI KWAKE KAMA VILE LINVYONENWA NA MCHUNGAJI WA VICTORY CHRISTIAN CENTRE (VCCT), MBEZI BEACH A, DAR ES SALAAM; DKT HURUMA NKONE!!


MAANDIKO; JOSHUA 1:29;11:23

Bwana Yesu asifiwe sana!
Leo ibaada yetu iko moja kwa moja kupitia Redio Wapo FM (98.1), na tutaendelea kuwa hewani moja kwa moja kupitia redio Wapo kila jumapili ya kwanza ya mwezi!

Habari hii inawahusu wana waisraeli wakiwa safarini kwenda nchi ya Ahadi chini ya Uongozi wa Joshua baada ya Muda wa Musa kuisha.
Na hapa Joshua alikuwa akipewa maagizo na mazingatio ya muhimu...Itakuwa mtakapotia miguu yenu kukanyaga nchi ile itakuwa mikononi mwenu, na muwe hodari na moyo wa ushujaa kwa maana ni haki yenu.

Wana waisraeli wakiwa na Joshua walishuhudia miujiza mingi pia ukiwapo ule wa Maji ya mto Yordni kugawanyika na wao kuvuka naam baada ya hapo Joshua na wanawaisraeli walianza kwa kuteka Yeriko na miji mingine mitatu mikubwa ya kati na kwa gia hii walikuwa wana nguvu ya kutosha kuendele kuichukua nchi nzima maana walikuwa wana mkakati bora.

NINI MUHIMU MAISHANI MWAKO SASA;
Ulipookoka umefanikiwa kuingia nchi ya ahadi; lakini bado ipo kazi ya kuendelea kuteka na kuchukua baraka zako...maana hapo kwanza kabl hujaokoka vilikuwa vinamilikiwa na shetani. Ni kweli umeweza kutikisa kuta za Yeriko na zimebomoka....naam usiishie hapo unapaswa kuendelea kuteka na kuteka mpaka hapo utakapomiliki nchi yako nzima...naamanisha ulimwengu wa wokovu wako.

 Lazima wakristo tubadilike...tuache kuamini maombi tu katika kila jambo bila kufanya jambo lingine lolote...kwa mfano hauwezi ukaomba upandishwe Cheo kazini na hali unaendelea kuchelewa kazini na kufanya uzembe mwingine haiwezekani....kama ukitimiza wajibu wako na kufanya yote yakupasayo kw haki na kwa bidiii, kwa hakika utapokea tu toka kwa Bwana...maana maandiko yanasema....KAMA MKITII MTAKULA MEMA YA NCHI!

Kumbuka hatuokoki ili tupate vitu fulani kwa Bwana kama vile fedha, majumba, waume na wake ama watoto, ila tunaokoka kwasababu tumechagu kumpenda Bwana na ukishaokoka na kuwa mwaminifu basi vyote hivyo unavyovistahili vinakujia kwa kujaa na kusukwa sukwa.

UJUMBE KWA VIJANA;
Lazima ujifunze kutulia na kusubiri,haiwezekani utoke chuo leo na utaka uendeshe Range Rover,acha kutamani kila kitu...ikiwa unavistahili basi ujue kwa hakika muda ukifika lazima utamiliki tu...vinginevyo utaumia sana ukitaka vitu visivyo saizi yako.

Natamani kama ungemtukuza Bwana katika maisha yako kwa namna ambayo watu watajiuliza wewe ni mtoto wa nani,maana ulimwengu umezoea watu wamnaopenya ni wale wenye watu wakubwa serikalini....Baraka yako ipo maana Mkono wa Mungu uko juu yako....na lazima ujue jambo moja kuwa penye Vita yako ndio penye baraka yako!

SEMA SALA HII KWA IMANI;
EEH BWAN YESU, NINAKUSHUKURU KWA NENO LAKO NA MTUMISHI WAKO, NIMESIKIA NA NIMEAMINI,NAAM NATAMANI NENO HILI LIWE HALISI MAISHANI MWANGU,NISAIDIE NIKUSIKIE KWA KINA ILI NIJUE NINI KINACHONIPASA KUFANYA KILA SIKU, MAOMBI YANGU LEO NI KUWA BWANA UNISAIDIE KILA WAKATI KUKUMBUKA KUWA VITA NI YAKO NA SIO YANGU,NIPE NEEMA YA KUWA NA SUBIRA NA KUSUBIRI BARAK YANGU, NISAIDIE KUITUMIA AKILI YANGU NA UTASHI ULIONIPA ILI NISIZEMBEE KIMKAKATI, AHSANTE YESU KWA MAANA KILA HATUA UTAKUWA NAMI,AHSANTE YESU KWA KUNISIKIA, KATIKA JINA LA YESU KRISTO,AMEN!!!

MUNGU ATUSAIDIE TUNAPOENDELEA KULITAFAKARI NENO HILI KUWA KILA MAHALI AMBAPO BWANA AMETUPA KUKANYAGA KATIKA ULIMWENGU W ROHO NA WA MWILI BASI HAPO AMETUPA KUMILIKI,NAAM UTAPATA VYOTE UNAVYOVISTAHILI KAMA UKIWA NA IMANI SAHIHI NA PIA UJUE VITA SIO YAKO BALI VITA NI YA BWANA, AMEN!

Mungu awabariki sana!!

Imeandikwa na
King Chavala MC
+255 713 883797

No comments:

Post a Comment