Wednesday, August 7, 2013

BAHARI YA KIOO....MFAHAMU "EMMANUEL MGALLAH",MWIMBAJI WA INJILI ANAYEJITUMA KIPEKEE SANA!!

Bwana Yesu Asifiwe sana!
Natumai kila mmoja yuko vizuri!
Mimi binafsi ni mzima sana na namtukuza Jehova kwa upendeleo na zawadi ya uhai, sijui ni nini kesho imeshikilia kwa ajili yangu, lakini Ninamjua anayeimiliki Kesho, naam tunafahamiana vema na kwasababu yeye anaishi,Lazima nitaiona kesho.

Leo Baharini nimemwona kijana huyu mtumishi wa Bwana ambaye ana moyo wa kipekee wa kujituma katika Utumishi na katika kazi zake binafsi.

Leo ninamzungumzia Mtumishi EMMANUEL MGALLAH, Mwenyeji wa Igamba, Mbozi Mbeya, Mnyiha kwa kabila; mwimbaji wa nyimbo za injili aliweka makazi yake Jijini Dar es salaam.

Karibuni Bahari ya Kioo ya Gospel Standard Base Blog ilifanya mahojiano nae kwa kina ili kutaka kujua mengi yamhusuyo kijana huyo, na kwa hakika hii ndio habari kuhusu Emmanuel Mgallah;

HISTORIA KWA UFUPI;
Emmanuel ni mzaliwa wa Igamba, Mbozi,Mbeya...alianza Shule ya msingi pale TANDALE UZURI, shule ambayo alisoma mpaka darasa la sita na kwenda kumalizia darasa la saba IGAMBA SHULE YA MSINGI iliyo mbozi Mbeya, na hapo akajiunga ya shule ya Sekondari ya Mbozi Mission, shule inayomilikiwa na Kanisa la Moravian,

Emmanuel hakufanikiwa kumaliza kidato cha nne katika shule hiyo, hivyo alihamia Mbezi High School iliyoko jijini Dar es salaam na kumalizia kidato cha nne hapo, na baadae akajiunga na THE CONTEMPORARLY COLLEGE iliyo Kinondoni, mahali ambapo alifanya kozi ya lugha kwa mwaka mmoja na kisha kujiunga na EAST AFRIKA TRAINING COLLEGE mahali ambapo aliendelea kusoma Lugha pamoja na Kompyuta na kisha akafanya kozi ya Ujasiriamali kwa mwaka mmoja.

KAZI;
Mwaka 2009 alipata kazi kama Afisa Mikopo (Credit Officer) wa SIMKA, iliyo magomeni usalama.

Mwaka 2012 alibadili kazi na kuanza kufanya na General Credit Company mahali ambapo alifanya mpaka Jan 2013, wakati alipoamua kujiudhuru na kuanza kufanya kazi zake binafsi za kijasiriamali.

Emmanuel ana miliki na kuendesha Biashara yake ya Bodaboda, anafanya kazi kama Dereva wa gari ya shule Libermenn Pre & Primary, lakini pia anafanya kazi za ushereheshaji (MC),

hivyo maisha yao yanaenda hivyo....na mke wa Emmanuel au Mama Jonathan yeye ni nesi katika Dispensary moja pale manzese, hivyo nae anamsaidia mumewe kustawi huku wakimtumikia Mungu katika ndoa YAO AMBAYO ILIFUNGWA MWAKA 2011
 FAMILIA;
Emmanuel ameoa mke mmoja na ana mtoto aitwaye Jonathan na kwasasa wanaishi kwafuraha yeye na mke wake maeneo ya Kimara,kinondoni, Dar es salaam.


HISTORIA YA UIMBAJI YA EMMANUEL;

Habari ya Emmanuel kuimba  ilianzia Sunday school na kisha akajiunga na kwaya ya kanisa la moravian-Mbozi mission na hapo akajiunga na kwaya nyingine iitwayo Emmanuel ya hapo hapo mbozi mission moravian na baada ya kuja jijini Dar es salaam alijiunga na Faith kwaya ya magomeni moravian iliyo chini ya Mwenyekiti Paulo Mlawa kwa sasa na akiwa ndani ya kwaya hiyo ndio akaanza michakato ya kuimba mwenyewe.

Alifanikiwa kurekodi album yake ya kwanza  mwaka 2011 pale Magic Star Studio chini ya fundi Ayubu pale Sinza na Kisha kufanya Video ya album hiyo mwaka 2012, chini ya Muongozaji Gilbert Mgalama.

Albamu hiyo ina nyimbo nane na inaitwa "HABARI NJEMA"....Habari njema ni moja ya nyimbo zinazosikika kwenye vyombo vya habari pamoja na "Kwanini Uteseke" na "Tawala kwa maombi"

Emmanuel alifanikiwa kufanya Uzinduzi wa Album ya sauti Desemba 23, 2012 na mpaka sasa hajampata msambazaji, hivyo anasambaza mwenyewe.

NINI MALENGO YA EMMANUEL HAPO MBELENI??
Emmanuel ni mwimbaji wenye shauku kubwa sana ya kukua na kwa jinsi ninavyomuona, nauona uwezo mkubwa sana ndani yake na atang'aa sana kama akitulia na Mungu sawasawa.. lakini ni maneno ambayo yeye mwenyewe aliyasema;


"....Ninakusudia kuwa na Studio na zaidi nategemea kusaidia waimbaji wadogo wadogo wanaonyanyaswa kwa kukosa fedha na zaidi natamani kuwaandaa wahubiri wa injili"

......Nimetembea mikoa zaidi ya mitano kihuduma na nakusudia kutembea Tanzania nzima kadri Mungu atakavyoniwezesha.

Imekuwa ni kawaida kwa Waimbaji wengi wa injili kuruka ruka tu bila kuwa na walezi wao wa kiroho, na nilipomuuliza ndugu kuhusu kijana huyu, haya ndio alimalizia kwa kuyasema;



EMMANUEL UNALELEWA NA NANI?
".....Mimi nalelewa na Mchungaji NOEL MWAKALINGA pale Magomeni Moravian na hapo ndio ninaposali na kuendelea kuimba kwaya ya Faith ya kanisani hapo.....natamani sana kufika mbali, nayafurahia sana unayoyafanya wewe (akimaanisha Mimi King Chavala) na wewe kwa sasa ndio mtu ninayejifunza kwake na natamani kuwa kama wewe katika mengi ufanyayo....nakuombea Mungu akusaidie ili uimarike zaidi na zaidi katika kusaidia Tasnia ya Uimbaji wa injili Tanzania na hapo baadae uwe msambazaji maana wewe unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko hawa wa sasa maana hawahui hasa uzito injili,Ahsante sana na Mungu akubariki.!"

CHANGAMOTO;
Emmanuel alisema Changamoto zinazomkabili ni Gharama kubwa ya kufanya kazi na vyombo vya habari na pia gharama kubwa za Studio.


UJUMBE WA EMMANUEL KWA WAIMBAJI WOTE;
"..Watu waliotangulia wasidhani kama wengine hawawezi kufanya au kufika mahali walipo, hivyo natamani kuwepo na umoja kati yetu na hapo ndio tyunaweza kufika mbali zaidi...na sio umoja wa siasa tu bali Kama Kristo na Mungu walivyokuwa na Umoja."

BAHARI YA KIOO haina la ziada zaidi ya kumshukuru Emmanuel Kwa kufunguka na kuamua kufahamika kwa kina, naam naamini kila mtu sasa atakuwa anamfahamu kwa kina na mtumishi huyu anasema yuko tayari kufanya kazi na mtu,kanisa na huduma yoyote popote....yamkini unamwitaji kama Mshauri wa namna ya kutumia mikopo midogo midogo, au kuhusu Bodaboda, ama kumwalika Kuhudumu kwa Kuimba, kufundisha ama kusherehesha, basi haya ndio mawasiliano yake;

EMMANUEL MGALLAH
+255 713 635 898 AU +255 769 070 458
E-mail; emmanuelmgallah@yahoo.com
Facebook; Emmanuel Mgallah

BASI TUNAWATAKIA MAFANIKIO MEMA WOTE MTAKAOSHIRIKIANA NA EMMANUEL KATIKA KUINEZA INJILI YA BWANA WETU YESU KRISTO,AMEN!!

Na King Chavala-MC
Hotline; +255 713 883 797
(c)2013- Bahari ya Kioo ya GoStaBa

No comments:

Post a Comment