Saturday, August 3, 2013

KUTOKA MADHABAHUNI LEO.......NGUVU YA MATOKEO YA UKIRI WAKO!

Shalom!
Naamini uko vizuri na jumapili hii ni nzuri kwako,amen!
Ubarikiwe na uzidi kubarikiwa sawasawa na neno la Mungu lisemavyo.
Leo neno kutoka madhabahuni,linatoka madhabahu ya TAG CAPITAL CHRISTIAN CENTRE (CCC) DODOMA kama linavyonenwa na Baba Askofu Mch SAMSON MKUYU
ASKOFU MCH.SAMSON MKUYU WA TCCC, DODOMA


Neno 
  Mithali 23:7 .....Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo
  Warumi 10:9......kwa kinywa mtu hukiri na kwa moyo mtu huamini......
Waefeso 3:20....
Wagalatia 5:9....

Somo; NGUVU YA MATOKEO YA UKIRI

Maisha yetu yenye matokeo ya kuwafanya wengine kupata tafsiri ya maisha mazuri yanategemea sana na ukiri wetu.
Maandiko yanasema aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, hii inamaanisha vile ulivyoujaza moyo wako navyo,kwa maana nyingine yale unayoyawaza na kuyafikiri kila wakati ndio hayo yanaongoza na ukiri wake wake kila siku.
Ukijaza moyo wako na uchafu,udhaifu na uzembe basi kila wakati utalaumu na kunung'unika na kukiri udhaifu maishani mwako na kama ukijaza moyo wako na Neno la Mungu na habari njema basi ukiri wako utakuwa ni kushinda na kushinda kila leo.

UKIRI HUZAA IMANI
Ukisema mimi ni masikini na akili yako inasikia na kudaka hiyo na wanahusika na hilo pia wanasikia na wanakuwa na nafasi ya kulifanyia kazi ili vile ulivyokiri iwe imani na iwe kweli.
Lakini ukisema mimi ni mshindi basi na akili yako husikia na kudaka hivyo na wote wanaohusika na hali hiyo lazima imani yako iwe hivyo.

Sikia hii ....KWA KINYWA MTU HUKIRI NA KWA MOYO MTU HUAMINI
Ukiri wa kinywa chako una nguvu sana na ndio hufanya moyo wako kupata imani ya yale uliokiri.

MIMI ZAMANI NILIMWAMINI BWANA KWA MAMBO MAKUBWA NA BADO NAENDELEA KUMWAMINI,KILA MWAKA AHADI YANGU YA KUMTOLEA BWANA INAENDA IKIPANDA,KUNA WAKATI TULIKUWA TUNAENDA KAMBI YA MAOMBI MAHALI FULANI NA ILITUPASA KUBEBA VYANDARUA,LAKINI MIMI NILIMWAMBIA BWANA (nilikiri na kuamini) MBU YEYOTE ATAKANIUMA AONYE UCHUNGU NA HATA KAMA NA WADUDU WA MALERIA WASINIPATE.....NA ILIKUWA HIVYO NA BADO NAMWAMINI BWANA HATA LEO.

MAMBO YA MUHIMU;
1. Chunga sana kinywa chako na linda moyo wako
2. Jifunze kutamka yale uyaamiyo na usindi uutakao,hata kama hali yako ya sasa haiendani na yale uyatazamiayo.
Usiache kusema....NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU!
3. Unaweza kuwatania watu na ndoto zao lakini usifany utani na Bwana maana Mungu hataniwi
4. Na kila unapokiri kumbuka unatangaza vita hivyo usiruhusu shetani akuletee mawazo mengine.

.....Atukuzwe yeye awezaye kufanya zaidi ya yale tuyawazayo na kuyafikiri kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.

SISI WACHUNGAJI TUMEZOEA KUWATUBISHA WATU DHAMBI WAKATI WAO WAKIMPOKEA KRISTO,LAKINI HUWA TUNASAHAU KUTUBU JUU YA VINYWA NA MIOYO YETU NA KUWATUBISHA HAO JUU YA MAMBO MAWILI PIA.

RUDI SASA KWENYE YALE MAKABRASHA NA MADAFTARI YA NDOTO ZAKO NA UANZE KUKIRI YALE UNAYOTAMANI KUWA NAYO HAPO BAADAE KUANZIA SASA.

BWANA NA AKUBARIKI SANA NA AKUSAIDIE KUCHUNGA KINYWA CHAKO NA MOYO WAKO,KATIKA JINA LA YESU AMEN!

Imeandikwa na
King Chavala
Moja kwa moja toka Dodoma!
KANISA LA TCCC,DODOMA

No comments:

Post a Comment