Wednesday, April 3, 2013

Kutoka Madhabahuni>>>...."MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI NA UPATE MAFANIKIO"(02)

SHALOM!
Ninatumai wote tu wazima na tumesherekea vyema sikukuu ya kumbukumbu ya kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo!
Jumapili hii hatukuwaletea somo toka madhabahuni,badala yake kuna somo kuhusu NGUVU YA KUFUFUKA KWAKE,ambalo utalisoma muda si murefu!

Leo nataka niendelee kidogo kuhusu KUMJUA MUNGU!!

Rejea somo la kwanza
http://gospelstandardbase.blogspot.com/2013/03/kutoka-madhabahunimjue-sana-mungu-ili.html


SASA ENDELEA!!

Nini maana ya KUMJUA MUNGU...TENA SANA?

Kumjua Mungu ni kufahamu zaidi kuhusu kwanini amekuumba,kusudi lako na anatarajia nini kwako...huwezi kujiuliza kwanini Mungu yupo ila unapaswa kujiuliza kwanini wewe upo,Mungu amekuandikia baraka nyingi sana ambazo utazipata tu ukifuata kila agizo akupalo....kumjua Mungu ni kujua neno lake,kushika amri zake,kuelewa hukumu zake,kufahamu kuhusu mamlaka yake na zaidi kujua nafasi yako katika yote hayo!!!
Ukisoma katika Kumb 28...Biblia inasema Itakuwa utapoyashika na kutunza na kufanya maagizo yangu yote baraka hizi zitaambatana nawe!!

Ukimjua Mungu utamfanya wa kwanza katika kila kitu ufanyacho na wala kamwe hutatamani ya duniani zaidi yake na ndio maana mahali pengine katika Mathayo akasema...Mtafuteni kwanza Mungu na haki yake yote na hayo mengine(ambayo mnayo) mtazidishiwa!!

SASA KWA KADRI UNAVYOMJUA MUNGU,NDIO UNAZIDI KUJUA SIRI NYINGI ZA MUNGU,NA HAPO BIBLIA INASEMA.....ILI UWE NA AMANI!

AMANI hii inayozungumziwa hapa sio utulivu kama ulimwengu huu,hapana! bali ni uhakika wa kipekee ukaao ndani ya moyo wa mwamini aupatao katika neno la Mungu pekee!!
Yesu alisema...Amani yangu nawapa, amani yangu nawaachieni,niwapavyo mimi si kama ulimwengu utoavyo! Maana yake ni kuwa amani hii nim zaidi ya amani ya ulimwengu...ni kama vile ulimwengu na sayansi ama ugunduzi unasema kutakuwa na janga ama tatizo fulani,lakini wewe ukisoma neno unagundua kuwa tatizo hilo halikutishi wala kukusumbua kwa kuwa wewe ni mtoto wa Mungu na unalindwa na Mungu na zaidi unayo mamlaka katika ulimwengu wa roho,na hivyo ukiwa na uhakika huo,utakua na amani tele hata kama ukiwa katkati ya watu wasio na amani hata kidogo!!

NA HAPO SASA MAANDIKO YANAMALIZIA KWA KUSEMA...NA NDIVYO MAFANIKIO YATAKAVYOKUJA!!

Mafanikio kibiblia sio mali wala pesa ama vitu vya kuonekana,bali ni baraka ya ukamilifu na utimilifu wa ndoto au mipango fulani aliyo nayo mtu. Afya njema,kukua kiroho,matumizi ya karama za rohoni,kujua kusudi,ulinzi na utulivu ni moja ya mafanikio makubwa sana,hayo magari na majumba huja tu maana ni matokeo ya mafanikio ya rohoni! Sasa shida moja ni kuwa watu wengi hukazia macho kwenye vitu na kusahau mmiliki wa vitu hivyo ambaye ni Mungu mwenyewe!!

KWA HIYO KUMJUA MUNGU NDIO UFUNGUO WA YOTE....KWANZA UNAPATA AMANI YA KUTOSHA NA UHAKIKA WA KILA KESHO NA JUU YA YOTE NDIO UNAYAONA MAFANIKIO MENGI MBELE YAKO!!

KUMBUKA;
Hutumtumikii Mungu au kuokoka ili tubarikiwe au tuwe matajiri,ila ukimtumikia Mungu kwa uaminifu Kufanikiwa na kubarikiwa hakuepukiki!!
BASI MUNGU ATUSAIDIE ILI TUONGEZE JUHUDI YA KUJUA ZAIDI KUHUSU MUNGU NA SIRI ZA NGUVU ZAKE,MAANA NDIPO ILIPO BARAKA YETU!
MUNGU AKUBARIKI,AMEN!


SOMO;
Na Mwl. Chavala,Fredy E.
+255 713 883 797

No comments:

Post a Comment