Wednesday, April 24, 2013

KIJANA "PAUL CLEMENT" KUIWEKA WAKFU ALBUM YAKE YA KWANZA "UMENIITA" NDANI YA VCCT,MBEZI BEACH A TAR 28/04/2013!!

SHALOM!
KWA WALE WASOMAJI WA BLOG HII NA WADAU WA MADHABAHU HII YA MTANDAONI,NATUMIA NAFASI KUMTAMBULISHA KWENU KIJANA MPOLE NA MTARATIBU SANA AITWAYE "PAUL CLEMENT", HUYU NI MMOJA WA WAIMBAJI WA KUNDI LA "GLORIOUS WORSHIP TEAM" AMBAYE ZAMANI PIA ALIKUWA "GLORIOUS CELEBRATION"
KIJANA HUYU AMEVUMA SANA NA WIMBO WA "UMENIFANYA IBADA" WA KUNDI HILO,SASA PAMOJA NA KUWA KATIKA KUNDI,SASA AMEKAMILISHA KUREKODI ALBUM YAKE BINAFSI INAYOKWENDA KWA JINA LA "UMENIITA"..KIJANA HUYU NI MMOJA KATI YA WAIMBAJI WACHACHE SANA WANAOWEZA SANA KUIMBA NYIMBO ZA KUABUDU,BASI JUMAPILI HII YA MWISHO WA MWEZI WA NNE,IMEMPENDEZA MUNGU NAE AWEKE WAKFU ALBUM YAKE HIYO NDANI YA HEMA LA VCCT CHINI YA MCHUNGAJI DK HURUMA NKONE KUANZIA SAA TISA MPAKA MUDA WA KUONDOKA!!
NJOO UMUUNGE MKONO KWA KULIPA KIINGILIO CHA 5000/+ AMA UKAE KITI MAALUM PAMOJA NA ZWADI YA CD KWA KULIPA 10,000/= NATUMAI WEWE NA YULE WOTE TUTAKUWEPO KUMUUNGA MKONO MTUMISHI HUYU WA MUNGU!!

"KAMA WEWE UNA MAONO NA UNATAMANI KUFIKA MBALI,BASI JIFUNZE KUWEKEZA KWENYE MAONO YA WENGINE"

MUNGU AKUBARIKI NA KARIBU SANA!!!!

No comments:

Post a Comment