Monday, April 16, 2012

****TANGAZO MAALUM****

TANGAZO MAALUMU KWA WAMILIKI WA BLOGS ZA KIKRISTO NA WANAPENDA KUANZISHA BLOGS ZA KIKRISTO NCHINI TANZANIA

Tarehe 21 April 2012 kuanzia saa 3:00 Asubuhi mpaka saa 5:00 Asubuhi katika mgahawa wa Maarufu wa Bulls(Esarp Village) Ulioko maeneo ya Survey pembeni ya Mlimani City.Kutafanyika mkutano maalumu utakaowakutanisha wamiliki wa blogs za kikristo nchini walio ndani na nje ya Dar es salaam. Sambamba na hilo pia itakuwa ni fursa kwa watumishi wote ambao kwa namna moja au nyingine wana nia kuanzisha blog kwa ajili ya huduma na taasisi zao,makanisa yao, pamoja na vikundi vya injili vilivyoko mashuleni,na vyuoni.
Lengo kubwa la mkutano huu ni
1.Kufahamiana
2.kusaidiana kiufundi namna ya kuboresha na ku-run Blog
3.Kuelimishana na kukumbushana misingi ya uandishi hususani huu wa kutumia blogs na mitandao ya jamii(Citizen Journalism).

Blog kama MADHABAHU, ikitumiwa Vizuri inaweza kumtukuza Mungu na ikitumiwa ndivyo sivyo inaweza kulitukanisha jina la Kristo.Ule mzigo wa Ki-Mungu, ambao Mungu ameuweka ndani ya wamiliki wa blogs na wote wenye nia ya kufungua blog ni HESHIMA kubwa.Hivyo namna ya kutembea na Heshima hiyo inamuhitaji Mungu na kukumbushana pamoja na kusaidiana kwa Upendo.Tafadhali fika Bila kukosa kwa kwa lengo la kuujenga ufalme wa Mungu.
Kwa Mawasiliano Zaidi

068-6255269
0713-763939

No comments:

Post a Comment