Thursday, March 1, 2012


PRESIDENT CHAVALA(THE STAND UP COMEDIAN) KUANZA  SEASON ONE YA MATAMASHA YA KUCHEKA TENA(LAUGH AGAIN CONCERT ) TAR 4 MARCH 2012,PALE LANDMARK HOTEL,UBUNGO,DSM.

Baada ya mafanikio makubwa ya uzinduzi wa matamasha hayo mwishoni mwa mwaka jana, Nov 20 2011 pale Crystall hall ya Blue pearl hotel, Ubungo plaza. Sasa mbeba IDEA huyo ameamua kuanza rasmi MSIMU WA KWANZA(SEASON ONE) wa matamasha hayo ya stand up comedy Tanzania, na Tamasha la kwanza ndio hili LAUGH AGAIN CONCERT One One litakalofanyika pale Ibungira hall ya LANDMARK HOTEL,Ubungo,river side, jumapili ya kwanza ya march(4th March 2012), kuanzia saa nane na nusu mpaka mbili usiku(2:30pm-8pm).

…….LAUGH AGAIN CONCERT ONE ONE, 4th March 2012 ,LANDMARK HOTEL,UBUNGO <<Quality-Love for Quality people>>
Mbali na CLOWN CHAVALA,Tamasha hili la Ubungo litawapandisha comedians chipkizi watano ambao ni Senior ABBY, Gerald Mrema, Richard Chidundo, Josephine Lukweto na MC MANU a.k.a Pilipili ya Sherehe toka Dodoma,Makundi mengine ya watu watakaonogesha tamasha hili ni pamoja na kundi maarufu la vijana waimbaji waitwao GLORIOUS CELEBRATION BAND, pia DAR ES SALAAM GOSPEL BAND, VOCAPELLA GROUP, VICTOR ARON,MADAM RUTH &CHRISS na wengine wengi bila kusahau kundi la DANCE.LAUGH AGAIN CONCERT One One litahusisha Stand Up Comedy(Zaidi), pamoja na Acapella, Dance,Sebene,Story telling, Zawadi & Suprises, Open Mic,Drama,na mengine mengi yatokanayo! Mbali na hayo kutakuwa na uzinduzi wa FORUM iitwayo QUALITY-LOVE.com, ambayo itakuwa maalumu kwa ajili ya kujadili maswala ya Upendo safi kwa kina,ubora,upana na ubora wake katika nyanja mbalimbali za maisha ya binadamu. Na kama mambo yataenda kama yalivyopangwa kutazinduliwa kitabu kiitwacho “NO MORE SCHOOL FOR YOU”(Your birth was your Graduation) By FREDY E. CHAVALA.

Kiingilio kwa tamasha hili itakuwa 5000/= kwa tiketi, ambazo zinapatikana

Victory Christian Centre(VCC);
Tarakea Restaurant(Mwenge),
Silver Spoon and Tausi Fashion pale Mlimani City,
Global Publisher na Praise Power Radio

Lakini pia mtu anaweza kununua tiketi kwa M-Pesa (0753 883 797) au Tigo Pesa (0713 883797) kwa kutuma 6000/= na atapata tiketi yake mlangoni,

(lakini hakikisha unatuma pesa kwa namba yako mwenyewe iliyosajiliwa kwa jina lako!)

LAUGH AGAIN CONCERT SERIES Season One…

LAUGH AGAIN CONCERT Season One itakuwa na matamasha nane katika mikoa mitano ya hapa nchini kwa kuanzia, Matamasha haya yatafanyika kuanzia March-August/September 2012 katika mikoa ya Dar es salaam(3),Arusha(1),Mwanza(1),Dodoma(2) na Mbeya(1).
Tar 1st April ni ARUSHA na 29th April ni ndani ya COLD CREST HOTEL,Mwanza then DSM tena !
Clown Chavala,The King of Stand up Comedy! Alimaarufu kama President Chavala!
Ambaye ni MC Maarufu ,Mchekeshaji(stand up comedian) na Muasisi wa christian stand up comedy Tanzania, ambaye ndiye Mchekeshaji mkuu na Project manager wa hii project,amesema matamasha haya yatakuwa endelevu na yatafika katika kila mkoa wa Tanzania na baadae mwaka huu tunategemea kuanzisha vipindi maalum katika televisheni  kadhaa nchini na mbeleni zaidi kutunza matamasha hayo katika DVDs. Zaidi mwaka huu tutakuwa na Movie project ambazo zitawahusisha vipaji vipya kabisa sana sana katika tasnia ya Stand Up Comedy.

2 comments: