Thursday, March 1, 2012

MFULULIZO WA MATAMASHA YA KUCHEKA TENA(LAUGH AGAIN CONCERT SERIES) TANZANIA
Na. CLOWN CHAVALA(MC na Muasisi wa Christian Stand Up Comedy Tz)
(Na. mwandishi maalum)
Ni muda mrefu wakristo wamekosa aina nyingine ya burudani yenye maadili na iliyo katika misingi ya Kimungu, ambayo ni huru kwa familia yote zaidi ya ibaada za kanisani, mikutano ya injili na matamasha ya uzinduzi au ya kusifu na kuabudu. Na ni vijana wengi ambao wana vipaji makanisani ambao wameshindwa kutumia au kuonyesha vipaji vyao kwasababu aitha mazingira ya kanisa hayaruhusu vitu hivyo,wamekosa wangalizi,hawajiamini au  kanisa lina mtizamo hasi juu ya mambo hayo.
Lakini ni dhahiri kuwa Mungu alituzawadia vipawa na karama mbalimbali kwa makusudi na kila alichotupa kina nafasi ya kumrudishia sifa na ni kiungo cha ibaada.

Sasa FREDY E. CHAVALA(CLOWN CHAVALA/PRESIDENT CHAVALA) Amekuwa mbele katika kuasisi na kuhakikisha kuwa vile vipaji vilivyoko kanisani vinapaki kanisani kwa Utukufu wa Bwana, amekuwa sana akikuza vipaji kama vile Ngojera,Mashairi,Akapella,Simulizi,Dansi na Vichekesho lakini zaidi Vichekesho,tena vichekesho vya mtu mmoja mmoja(Stand Up Comedy).

Muasisi huyu ana vipaji vingi(multi talented) na anapenda sana sanaa, lakini kwa sasa amejikita sana kwenye uasisi wa vichekesho vya kikristo.

Si jambo tulilolizoea machoni mwetu na halijawahi kutokea nchini, kuona watu wakitumia sanaa ya vichekesho kufikisha habari njema za Yesu kristo.

Tulizoea kuona vichekesho(comedy), zikifanywa sana na watu tu wa huko duniani(secular), lakini sasa sanaa hii iko madhabahuni na imethibitika kuwa na kibali na faida kubwa sana kwa wakristo, hii itabadilisha kabisa mtazamo wa kuona kama kanisani ni mahali pa kuwa serious na kulia tu wakati bila kucheka wala kufurahi.
Faida za kufurahi na kucheka,mbali ya zile za kiroho ni kama vile
 •    Kuondoa sumu mwilini, maana unapocheka mishipa inafunguka na damu inatembea vizuri na homoni na viyeyushi tiba vinaachiliwa mwilini.
 •    Kuondoa au kupunguza msongo wa mawazo(stress), yaani nafsi na akili vinapata vitu laini vya kufanya ufanye kazi nyepesi na siyo hizo nzito zisizo na majibu kichwani.
 •    Kuongeza uzuri wa sura, uchangamfu wa mifupa na kudumisha urafiki, jambo ambalo linaongeza imani ya kawaida kuwa hauko mpweke, mbali na kuwa Mungu.
 •    Kucheka pia kunaongeza maisha na zaidi furaha ikitawala moyo wako unaweza waambukiza wengine waliokata tamaa kabisa na maisha yao.
 •    Zaidi ya hayo yote, vichekesho hivi vya kikristo humfanya mtu ajifunze kutafakari Biblia kwa undani zaidi, hivyo mtu hucheka na kupokea kwa wakati mmoja, yaani unacheka unapona mwili na roho na hii ndio tofauti kubwa kati ya Vichekesho vingine vya huko duniani na hivi vya Kikristo.
Chavala anasema alianza kufanya comedy muda mrefu lakini katika kanisa ana kama miaka mitano hivi, na hapo kale alikuwa anafanya zaidi Drama na Dramantic comedy,…zaidi Chavala alisema………….

“haikuwa rahisi watu kuelewa haraka hii Stand up Comedy, ambayo ni Comedy halisi, nakumbuka mara ya kwanza kusimama kwenye jukwaa kubwa ilikuwa mwaka 2009 katika Mkusanyiko wa wanafunzi wa vyuo vikuu maarufu kama CAMPUS NIGHT,mikusanyiko ambayo hufanyika kila mwaka na huandaliwa na Kanisa la VICTORY CHRISTIAN CENTRE(VCC), mkesha ambao ilifanyika pale uwanja wa taifa  na ulikuwa na zaidi ya washiriki 12,000. Hapo watu walicheka sana na watu wengi walijua kuwa kuwa jambo hili ni zuri na linafaa sana katika kanisa la leo, Tangu hapo nikaendelea zaidi kushiriki mikutanoni,makanisani na mikusanyiko mbalimbali ya wakristo na baada ya kuona ipo haja ya kufanya wazo hili lijitegemee, ndipo nikaanzisha mfululizo(SERIES) wa matamasha ya kikristo ya comedy. Mfululizo huu ulianza mwaka jana(Nov 20, 2011) pale Ubungo plaza na una jina liitwalo “LAUGH AGAIN CONCERT SERIES” yaani MFULULIZO WA MATAMASHA YA KUCHEKA TENA” Picha nyingi zinaonyesha namna siku hiyo ilivyokuwa imefana.”

LAUGH AGAIN CONCERTS zitaendelea kufanyika nchini mpaka hapo ambapo mikoa yote itakuwa imefikiwa na kwa kuanzia Msimu huu wa kwanza (SEASON ONE) itakuwa na matamasha nane(8) na kati ya hayo Dar es salaam(3), Arusha(1), Mwanza(1),Dodoma(2) na Mbeya(1), ambayo yataanza March mpaka September 2012. Matamasha haya yatakuwa yanahusisha vipaji vingi toka mkoa husika sambamba na CLOWN CHAVALA, ambaye ndio mwasisi pamoja na watu watu wachache watakaobahatika kusafiri nae, katika matamasha haya tutakuwa na waimbaji mbalimbali watakaoalikwa mbali na sanaa zote za maonyesho nilizozitaja pale juu.

Hivyo kama una kipaji au unapenda kuwa mshiriki wa KUCHEKA TENA, hakikisha unafungua masikio vizuri, maana unaweza ukapitwa!

MSIMU HUU UNAANZIA DAR ES SALAAM  4th MARCH 2012, LANDMARK HOTEL,RIVER SIDE,UBUNGO!
Unaweza kuwa umesikia matangazo ukawa unapuuzia tu,lakini nikutie moyo tu,jitahidi usikose hii maana ni maalumu kwa ajili yako, tamasha hili litaanza nane na nusu mchana mpaka moja na nusu usiku(2:30-8pm) na CLOWN CHAVALA(The king of Stand Up Comedy) atawapandisha wachekeshaji wapya watano(5) ambao ni Senior ABBY,Gerald Mrema,Lukweto J,Richard Chidundo na Emmanuel Mathias(MC MANU au pilipili ya sherehe kutoka Dodoma), lakini pia vichekesho vyote hivi vitasindikizwa na Glorious Celebration Band, Dar es salaam Gospel Band, Vocapella Group, Dance group, Victor Aron pamoja na Madam Ruth na Chriss(wa amenibamba Yesu) na wengine wengi.

Tiketi zinapatikana;
 • Victory Christian Centre
 • Praise Power Radio 
 • Tarakea Restaurant-mwenge
 • Silver spoon na Tausi Fashion mlimani city kwa  5000/= tu
 • au unaweza kununua kwa M-pesa(0753 883797) au Tigo Pesa(0713 883797) kwa 6000/= tu.
(hakikisha unatuma pesa ya tiketi kamili, tena kwa kutumia namba yako iliyosajiliwa kwa jina lako, ili upate tiketi yako mlangoni ukija)

LAUGH AGAIN CONCERT One One Ni kwa ajili ya WATU BORA wote wenye UPENDO BORA WA KWELI KWA WOTE! (<<QualityLove for Quality People>>)
MALENGO MAKUU YA MATAMASHA HAYA;
Zaidi ya faida za kucheka nilizozisema hapo juu, matamasha haya yameanzishwa kwa malengo makuu haya;

 1.   Kuutangaza ufalme wa Mungu na ukuu wake, kuinjilisha na kuponya watu kupitia dawa asili ya kucheka.
 2.    Kuanzisha aina nyingine ya burudani kwa familia za wapenda maadili, zaidi ya hizi chache tulizozizowea, yaani uzinduzi na mikutano ya injili.
 3.   Kukuza na kuviendeleza vipaji halisi vya vijana kanisani, kwa faida ya kanisa, jamii na mafanikio ya maisha yao binafsi.
 4.    Kukutanisha watu wa kada na nyanya/fani mbalimbali katika maisha,ili kuongeza upana wa wigo wa mtandao wa kubadilishana habari, ujuzi, uzoefu pamoja na biashara.
 5.    Kukuza, kuendeleza na kuutangaza utamaduni wetu,hasa ule uliosahaulika kupitia sanaa, na hivyo kupigia kampeni Utalii wa ndani ya nchi yetu, ambayo Mungu ametubariki nayo.
KUHUSU MUASIS (FREDY CHAVALA);


Huyu ni kijana wa kitanzania aliyeokoka, Mzungwa wa Iringa aliyehitimu elimu ya chuo kikuu na ambaye amekuwa kwenye harakati za maendeleo ya Vijana kwa muda mrefu sasa, kwa taaluma ni Mtaalamu wa Usimamizi na Utawala wa Biashara (Business Administration and  Management), ambaye anafanya kazi kama Managing Director na Business & Management Consultant wa Great Potentials Ltd.

Tofauti na watu wengi wanavyochukulia sanaa ya uchekeshaji kama vile ni ya watu duni wasio na mwelekeo, Chavala anaichukulia kama kitu cha thamani sana kwake na kwa jamii na ndio maana pamoja ya Elimu yake ameamua kufanyia kazi vipaji vyake,zaidi Stand Up Comedy.

Chavala amekuwa akijishughulisha na mambo mengi sana kama vile uandaaji wa Semina, Mikutano na matukio mbalimbali ya kidini na kiserikali, Ushauri,Uandishi wa miradi,Uandishi wa Vitabu na makala, U-MC, Ufundishaji na uzungumzaji katika maeneo mbalimbali ya nchi hususani katika eneo la Biashara, ujasiriamali, ustawi wa Vijana na ukuzaji wa vipawa. Inawezekana umeshawi kumuona katika mahojiano mbalimbali na vyombo vya habari, kumsikia au kukutana nae, nina uhakika utakubaliana nami kuwa huyu ni kijana wa tofauti na wa kipekee.

Mpaka sasa ameshatembea karibu Tanzania yote na kutembelea baadhi ya nchi za nje, kwa ajili mambo hayo anayoyafanya.

Chavala anaamini kila mtu ana uwezo ndani yake wa kufanya kile kitu ambacho Mungu amemuandikia afanye maishani mwake na zaidi mafanikio ya mtu yako ndani mtu mwenyewe.
UNAWEZA KUWA SEHEMU YA KAMPENI HII

Unaweza kuhusika kwa namna yeyote ile; maombi, ushauri, ushiriki, kuchangia au kudhamini, pia Unaweza kupanda mbegu yako kwa kusaidia kufanikwa kwa matamasha haya nchini, maana ni pesa nyingi inahitajika,ni zaidi ya milioni 250 kwa msimu wa kwanza wenye matamasha nane nchini! Milango iko wazi kwa yeyote mwenye nia njema, unaweza kuwasiliana nasi kuuliza au kuchangia chochote kile unachoguswa kwa M-PESA(0753883797) au Tigo Pesa(0713 883797).

Tutabarikiwa sana kama tutasikia kutoka kwako, tunatamani yale yote ambayo shetani ameyaiba kanisani na wale wote ambao amewaiba kanisani warudi, maana hakuna jambo lolote zuri lenye asili yake kuzimu, vyote ni mali ya Mungu. Saa inakuja ambapo mtu yeyote atakayekaa kinyume na Mungu basi huyo ataonekana amechuja maradufu, tusaidiane kulea vijana wetu katika kumpenda Mungu, bila kujutia karama, vipaji na vipawa walivyonavyo! Usiwe wa kwanza kulaumu, kuhukumu na kudharau watu, hasa vijana, karibia ujifundishe au uje na majibu/masuluhisho na sio maneno tu!

“Ninawashukuru watu wote, makanisa, huduma,vyombo vya habari, makampuni, taasisi na asasi, ambao mmekuwa ni baraka kwa huduma hii kwa ujumla, ni wengi mno mnaotuunga mkono siwezi kutaja majina, ninawashukuru wazazi na walezi wa kimwili na kiroho na zaidi gazeti hili kwa kuhakisha ulimwengu wa kikristo unahabarika kama hivi, Mungu awabariki sana na karibuni sana tuendelee kuungana mkono”…Fredy Chavala(Mbeba maono)

“LAUGH AGAIN CONCERT SERIES”
GREAT POTENTIALS LTD,
C/o Box 34048,
DAR ES SALAAM.
+255 713/753-883 797.

No comments:

Post a Comment