Friday, December 14, 2012

MAISHA YA UREMBO NA WOKOVU (1)

Shalom ndugu msomaji!

Katika mada hii ningependa kuzungumzia maswala mazima ya mtazamo hasi wa watu waliookoka kuhusu urembo kwa ujumla. 

Urembo ninaozungumzia hapa ni pamoja na ubunifu wa mavazi, kushiriki mashindano ya urembo, kuwa mwanamitindo na kutangaza biashara za makampuni mbalimbali. 


 Watu wengi waliookoka wamekuwa wakipoteza fursa mbalimbali wanazopata katika fani hizi kutokana na mtazamo hasi walio nao kuhusiana na fani hizi. Wengine imewapelekea kuwakataza watoto wao, au ndugu zao kushiriki kwa kudai kwanba kazi hizo ni dhambi na ni mambo ya kidunia. Hii inatokana na baadhi ya walioko katika fani hizi kuwa na tabia ambazo hazimpendezi Mungu na wamekuwa sio mfano mzuri wa kuigwa kwa jamii. Sababu hizi zimewafanya wengi waliookoka kukumbatia fani zai na wengine kushindwa kushiriki katika fani hizi japokuwa sifa za kushiriki wanazo. 


Tukumbuke kuwa mtu mmoja aliyeokoka anawekaubadilisha mtazamo hasi uliopo na kufanyika kama kioo kwa jamii inayomzunguka kupitia fani hizi. Ubunifu wa mavazi: katika fani hii inasikitisha kuona mtu ameokoka na anauzoefu wa muda mrefu wa kushona na kubuni styles za mavazi lakini maisha yake ni duni na hana maendeleo wakati fursa za kushiriki katika maonyesho mbalimbali anazo lakini anaogopa na kudai hayo ni mambo ya kidunia. Akasahau kwamba kushiriki kwake kungempa kufahamika zaidi na kumpa wateja wengi na soko la kazi zake lingekua na kupato chake kingeongezeka. 

 Kushiriki mashindano ya urembo: Kama mtu uliyeokoka unaweza kushiriki mashindano haya na ikampa Mungu utukufu na pia ukafanyika kama chombo cha kuwafikishia wokovu watu wengi wakiwiwemo watu maarufu. Kwa njia hii pia utakuwa na nafasi nzuri ya kuisaidia jamii inayokuzunguka na ukawa mfano mzuri wa kuigwa. Na pia kupitia wewe wengi watajifunza mambo mengi mazuri yakiwemo kumcha Mungu na kufanya yanayompendeza Mungu.

ITAENDELEA......!!

No comments:

Post a Comment