Friday, September 13, 2013

NANI AJUAYE SIRI YA UPENDO?

  “Nakupenda kutoka moyoni mwangu”….ni sentensi maarufu katika ulimwengu wa mapenzi. Inaweza kuwa inasemwa kwa kumlizisha msikilizaji wa maneno hayo au ikiwa na maana kubwa kwa msemaji wa maneno hayo. Nani ajuaye ukweli wa maneno hayo ni siri ya moyo.
Mara nyingi huwa nasema hakuna asiyependa kupendwa. Ila sina hakika kama ni wote tunapenda kupenda. Katika utafiti wangu mdogo kuhusu maisha nimegundua mada kubwa miongoni mwa jamii ni mapenzi na muziki. 

Watu wanatumia nguvu nyingi kutafuta pesa ili tu wapate vitu wanavyovipenda. Wapate wasichana warembo kama wake zao, wavulana watanashati kama waume zao, nyumba wanayoipenda, magari wanayoyapenda, wakae sehemu au mahali wanapopapenda na kujiburudisha moyo kwa nyimbo au muziki wanaoupenda na miziki mingi imejaa maneno ya sifa na mapenzi.

Nami pia nikiumbe, napumua kama wewe,
Kukupa huu ujumbe, nimeamua mwenyewe,
Hivyo usifumbefumbe, nikosapo nikosowe,
Ila kukupenda wewe, si chanzo cha kunitesa.

Kwasababu hiyo watu wenye pesa hutafuta upendo wa kweli na watu masikini hutafuta pesa ili wakatafute upendo wa kweli. Burudani inaanzia hapo wanapokutana anayetafuta upendo wa kweli na anayetafuta pesa ili akatafute upendo wa kweli.
Unaweza kuwa umejiuliza kati ya watu wenye pesa na watu wenye uwezo wa kawaida na maskini ni watu gani hutumia nguvu nyingi kutafuta kupendwa. Nimekwisha kusema kila mtu anapenda kupendwa, lakini matajiri na watu wenye uwezo mkubwa hutumia nguvu nyingi sana kutafuta kupendwa, pia watu wahali ya kawaida wao hawatumii nguvu nyingi ukilinganisha na matajiri na wenye uwezo mkubwa. Tukirudi kwa masikini wao hutumia nguvu kidogo sana ili wapendwe.
Je unahitaji uwe na uwezo mkubwa au tajiri ili upendwe?
Je unahitaji kuwa mtu mwenye uwezo wa kawaida ili upendwe?
Je unahitaji kuwa masikini ili upendwe?
Endelea kufwatilia mada hii nzuri naya kusisimua wiki ijayo……
kwa maswali, maoni,mapendekezo na ushauri niandikie kupitia barua pepe makwayae07@gmail.com

No comments:

Post a Comment