Wednesday, July 3, 2013

JUKWAA LA KIOO......MTAMBUE "ORIDER NJOLE" MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI MCHAPAKAZI ASIYE NA MAKUU!!!

Shalom!
Leo ninayo furaha kumleta kwenu mwimbaji wa nyimbo za injili wa kipekee sana kati ya waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania!

#PART ONE#

Huyu dada ni mwenyeji wa Iringa(Mhehe aliyeokoka hivyo laana ya kujinyonga haiko juu yake tena) lakini anaishi na kufanya kazi zake Dar es salaam ingawa huzunguka sana Tanzania kwenye mikutano na semina mbalimbali kama mshiriki na mhudumu pia!

Mwimbaji huyu ana moyo wa tofauti sana, kwani mara nyingi kwenye mikutano ya injili kwa mfano wakati ule wa SHEREHE ZA ISHARA NA MIUJIZA...na mingine mingi nimemuona akiwa mhuhudumu tena anayejituma,tofauti na waimbaji wengi...wakishatoa album na kujulikana basi wanajiona mabosi hivyo hawawezi kufanya usafi,kushiriki kazi kanisani wala kuhudumu!!

Orider Njole ni mdada mtaratibu na mcheshi alijishusha,huduma yake iko mbele na sio fedha maana kuishi kwake kunatokana na Baraka ambazo Mungu ameziachilia kupitia kazi ya mikono yake!!

Kama wewe ni msikilizaji sana wa Wapo basi utakua umeshamsikia maana zaidi kupigwa sana nyimbo zake hapo pia amewahi kualikwa mara kadhaa kwenye kanisa la BCIC.

Nikiwa naandaa mikutano au makongamano hata vikao vya waimbaji wa injili amekuwa mbele kusaidia,kusambaza habari kwa wenzake na hata kutoa mchango wake wa fedha ili kufanikisha shughuli hizo!

Orider Njole Amesomea uhudumu wa afya lakini baada ya kuona kama hailipi alienda kusomea Uandishi wa habari....hivyo ni mhudumu wa afya  na kwasasa anaendesha duka lake la Dawa baridi lakini pia ni muandishi wa habari ambapo amefanya na anaendelea kufanya na vyombo kadhaa vya habari hapa nchini....wakati huo anaendelea kuimba nyimbo za injili na ni kiongozi kanisani kwake!

Orider anapenda pia kuwa na muda na watoto,hususani watoto yatima...na kwa hakika anapenda sana watoto na anampenda sana mwanae.

Akiwa nyumbani hujishughulisha na kilimo hata kama ni kidogo na upande mwingine ni mdada anayependa sana michezo!

Ametoa album yake ya kwanza ya nyimbo za injili iitwayo "DUNIANI TUWAPITAJI" yenye nyimbo 8 na tayari ameshafanya video ya album hiyo....na nyimbo zake hususani huo unaobeba album unaendelea kufanya vizuri kwenye redio nyingi na hata video yake pia inafanya vizuri na video hiyo ilifanyika maeneo ya Iringa!!
 MWIMBAJI HUYU NI MFANO WA KUIGWA NA WAIMBAJI WENGINE NA UNAWEZA KUWASILIANA NAE MOJA KWA MOJA KWA MIALIKO YA KIHUDUMA AMA UNAWEZA KUPITIA ANUANI YA BLOG HII!!

Mara nyingine tukipata nafasi ya kuhojiana nae basi tutakuletea habari kwa kina kuhusu mwanadada huyu,karibu sana!!!

.........ITAENDELEA!!!!(Part 2 itahusu mahojiano kati ya mwandishi na Orider Njole)....USIKOSE!!!

Na King Chavala-MC
Hotline; 0713 883 797

No comments:

Post a Comment