Tuesday, January 8, 2013

MAISHA YA UREMBO NA WOKOVU(2)

SHALOM WATUMISHI WA MUNGU!!!
MWAKA JANA MWISHONI TULIANZA KWA KUANGALIA MAISHA YA UREMBO NA WOKOVU NA SASA NI MUENDELEZO WA PALE SOMO LILIPOSHIA...

"UREMBO WAKO UNAVYOWEZA KUTUMIKA KATIKA MATANGAZO MBALIMBALI"

IKIWA wewe ni mrembo,Urembo wako unaweza Kutumika katika matangazo mbalimbali ya bidhaa: katika kipengele hiki, unaweza kutumika katika kutangaza biashara mbalimbali ilimradi tu sio kwa style iliyo nje ya maadili ya wokovu au sio katika bidhaa ambazo hazimpendezi Mungu kama kilevi nk.

Pia katika matangazo haya, hata kama ni tangazo la bidhaa kama mafuta, sabuni, au makampuni ya simu nk. Utaangalia ni sehemu gani tangazo hilo linafanyikia na ni aina gani ya mavazi unayotakiwa kuvaa, kama ni mavazi ya heshima sio mbaya kama ukifanya kwani itakuingizia kipato.

Katika suala hili la urembo, mtu wa Mungu kupendeza na kuonekana nadhifu sio dhambi jamani, kwasababu utamkuta mtu zile nguo mbaya mbaya ndo anaenda nazo kanisani, ila ukimkuta amealikwa sehemu unaweza kumsahau, anavaa vizuri sana na anapendeza. Hebu tubadilike, tuwe smart wakati wote, na hata kama una nguo zako mbili tu, jaribu kuziweka katika hali ya usafi. Na hakikisha umepaka deodorant yako vizuri (hii ni muhimu sana wapendwa, maana tunapokua makanisani tunacheza kwa furaha tukimtukuza Mungu wetu, huwa hatujali hata tukitoka jasho kiasi gani, ila unapokuwa umepaka deodorant utaepukana na kukwaza wengine, badala ya kuzama katika kumsifu Mungu, harufu ya jasho lako inawaharibia step) na pia unajipaka perfume kama unayo ila sio lazima, osha na utengeneza nywele zako vizuri, pasi nguo zako nk. Hakikisha kupitia wewe, kuanzia tabia yako, mpaka muonekano wako wa nje vinamtukuza Mungu, sio watu ambao hawajaokoka wakikuona waseme kama wokovu wenyewe mtu anakua rough hivi siokoki, hii ni mbaya kabisa wapendwa katika Kristo.

Mungu atusaidie ili tuweze kumtukuza kuanzia kwenye matendo, kuongea kwetu na muonekano wetu wa nje.
Yesu akubariki.

Na Upendo Benson

.......ITAENDELEA!!!!

No comments:

Post a Comment