Monday, May 14, 2012

......KARIBU UJADILI KWA KADIRI UWEZAVYO NA UJUAVYO!!!

TOPIC No.1# JE KUNA MTAKATIFU DUNIANI?


Imekuwa ni jambo la kubishaniwa sana hapa duniani miongoni wa wakristo na watu wengine wa kawaida!

Wapo wanaosema haiwezekani watu waitwe watakatifu kwa mfano. Papa au wale wote waliotunukiwa utakatifu huo?

Wengine bado wanajiuliza Je utakatifu ni shahada mpaka watu wajadiliane na kumtunuku mwingine?

Na Je hawa wanaojiita WAMEOKOKA je hawa ndio watakatifu?

Unawezaje kuwa mtakatifu na bado ukatenda dhambi?

Na Mbona Biblia imesema.....WATAKATIFU WALIO DUNIANI NDIO NINAOPENDEZWA NAO!

na mahali pengine imesema...IWENI WATAKATIFU KAMA MUNGU WENU ALIVYO MTAKATIFU!!!

Sijaweka vifungu vya Biblia maksudi nikikutaka wewe ujibu kwa kutumia Biblia takatifu!

Tunatamani tukusikie Je wewe unasemaje?

1.JE WEWE NI MTAKATIFU/MDHAMBI AU HUJIJUI?

2.UNASEMAJE KUHUSU UWEPO WA WATAKATIFU DUNIANI?

 3.UNAELEWA NINI KUHUSU UTAKATIFU?

No comments:

Post a Comment