Thursday, June 13, 2013

ITAMBUE NAFASI YAKO KAMA KIJANA ILI ULETE MABADILIKO KATIKA MAISHA YAKO NA JAMII KWA UJUMLA 02


SHALOM TENA WASOMAJI WANGU!!
BADO TUNAENDELEA KUJIFUNZA KAMA VIJANA....

Kama nilivyosema katika sehemu ya kwanza, ni muhimu sana kwako wewe kama kijana kujua nafasi yako katika maisha yako, ujue pia Nafasi yako katika familia yako, uelewe umuhimu ulionao kwa jamii inayokuzunguka na zaidi sana taifa lako.
Umuhimu wako haupatikani kwa kujitazama kwenye kioo na kudhani wewe ni muhimu, ni jambo linalohitaji kuwekeza katika ufahamu sahihi ama kujitambua sawa na vile Mungu alivyokusudia.

Ufike mahali uishi maisha yenye malengo na utambue thamani yako ili usinunuliwe na vitu vyenye thamani isiyolingana na wewe. Hapa inahitaji kujenga mtazamo utakaokusaidia kuwa thabiti katika maamuzi yako, ili ujenge msimamo wenye nidhamu katika maneno, mawazo na matendo yako.

 Jumla ya haya yote inahitaji kujitambua, na sasa tuendelee na maana ya kujitambua maana ni kujitambua tu ndiko kunaweza kukusaidia kujua Nafasi yako na kusimama katika zamu yako na kuleta mabadiliko uliyopangiwa na Mungu wako.

Maana ya Kujitambua
“Kujitambua ni hali ya kuwa na ufahamu au uelewa (kujua) wa kutosha juu ya maisha yako kwa ujumla pamoja na mazingira yanayokuzunguka na hivyo kukufanya uishi maisha yanayofanana au kulingana na kusudi la Mungu kwako, uishi katika ubora wa maisha yanayolingana na kiwango cha ufahamu ulionao au kiwango cha kujitambua kwako kutegemeana na nguvu ya taarifa unazopata” 
 Kijana aliyejitambua, ukimsikiliza maneno yako hutatia shaka kwamba yuko thabiti na hata ukiangalia matendo yake utaona ulinganifu wa ayasemayo na ayatenda. Kijana yoyote hawezi kujitambua mpaka amekutana na ufahamu sahihi ulio juu ya yote anayoyafahamu, aone kupungukiwa kwake kwasababu hajafahamu mambo ya msingi katika maisha yake. 

Juu ya yote ni lazima wewe kama Kijana ujue kuwa ipo sababu ya wewe kuwepo hapa duniani, lipo kusudi la wewe kuwepo hapa duniani, ipo sababu ya wewe kuwa Kijana, hii ni muhimu sana. 

Kujitambua ni kuwa na ufahamu au uelewa juu ya angalau mambo yafuatayo: 

 Historia ya asili yako au maisha yako, ni muhimu Kijana ukajua historia ya maisha yako bila kujali ilikuwa nzuri au sio nzuri, au ya kuvutia au siyo ya kuvutia ili ujue kuwa kuna mahali unatoka, kuna aina ya watu wameunganishwa na maisha yako, hii itakusaidia katika safari ya maisha yako 

 Maumbile yako, au mwili wako, ujue madhaifu ya mwili wako, uelewe na kuutambua mwili wako vizuri na kujua namna ya kuudhibiti katika mazingira tofauti tofauti 

 Kusudi la maisha yako, maono au malengo kwa pasipo kujua sababu ya wewe kuwepo duniani unapoteza maana ya kuwepo duniani 

 Makuzi na malezi yako, maana haya yanaathiri kwa kiwango kikubwa sana hali yako ya baadae, ujue melelewaje na umekua katika mazingira gani ili tabia zako na mwenendo wako zipate maana na uwe na uwezo wa kujifunza kwanini umekuwa na tabia Fulani Fulani, 

 Mazingira na jamii, taifa lako na zana nzima ya uzalendo, ujue kuwa uzalendo haufundishwi kwa kuwapa watu mali na pesa, Mungu amekupa wewe fursa ya kuzaliwa na kuishi Tanzania kwa makusudi na kama hujui basi utaishi kama mnyama na utapoteza ladha na kuwajibika 

 Hisia, utashi na ufahamu wako 

 Maneno na maamuzi yako, 

 Tabia na mwenendo UMUHIMU WA KUJITAMBUA Kujitambua ni muhimu sana kwani kunakusaidia kujua mambo juu ya maisha yako: 

 Ili kutembea au kuishi katika viwango asilia ambavyo umeumbwa navyo (The originality of you) 

 Ili kujua madhaifu uliyonayo kwa ajili ya kujua namna ya kuyashinda 

 Ili kujua thamani yako, uepuke kutumiwa vibaya, usijidharau wala kumtengenezea mtu mwingine mazingira ya kukudharau na hata usimdharau mtu mwingine 

 Ili ujua nafasi yako (majukumu) katika maisha yako na ya wale wanaokuzunguka 

 Ili kujua umuhimu ulionao kwa ajili ya kuleta matokeo yanayotarajiwa kwako 

 Itakusaidia kutumia vizuri rasilimali kama muda, watu nk 

NAAMINI LEO UMEPATA KITU CHA KUKUSAIDIA KATIKA SOMO HILI, NI MATUMAINI YANGU KUWA UTAANZA KUFANYA MABADILIKO KATIKO JAMII YAKO SASA!!
Usikose somo lojalo!
Na Mwl. Raphael Lyela kutoka Youth Kingdom Ministries,Jesus Up!
 
......LITAENDELEA!!!!!!!

No comments:

Post a Comment