Sunday, July 29, 2012

KUTOKA MADHABAHUNI...KKKT DAYOSISI YA KONDE,USHARIKA WA FOREST,MBEYA MJINI!

SERMON: MPENYO WAKO UNATEGEMEANA SANA NA MWITIKIO WAKO!
                 (YOUR BREAKTHROUGH DEPEND ON YOUR RESPONCE)

                      Na Mchungaji MATHEW J. SASALI

Leo siku nzuri aliyoifanya Bwana,nimefanikiwa kuhudhuria ibaada ya kilutheri katika usharika wa Forest,Mbeya ambako leo ilikuwa sikukuu ya Vijana katika kanisa hilo,na mimi kama mmoja wa Waalikwa niliyehudhuria ibaada pamoja na Tamasha la kumsifu na kumwabudu Mungu!
Mchungaji Mathew Sasali ambae ni Manager wa Ushindi FM radio ndio alikuwa mchungaji mwalikwa na mnenaji wa leo, ambaye leo ametulisha neno hilo la Mungu!!


....Kumb 28:1->>
Itakuwa utakapoyashika,kutunza na kuyafanya maagizo ya Mungu yote,baraka hizi zitaambatana nawe...utabarikiwa......


.....Kumb 28:15->>
Na utakaposhindwa kutenda sawasawa na hivi nikuagizavyo,laana hii itaambatana nawe....


Maisha yetu ya kila siku yanategemea sana na vile ambavyo tunaitikia mambo yale yanayokuja mbele yetu,kubarikiwa au kulaaniwa kunatokana na sisi wenyewe na sio shetani,ni dhahiri kuwa watu wengi wanapendwa sana kubarikiwa ila hawapendi kuwa na uhusiano na huyo mtoa baraka!!


Wengi hudhani baraka huja kwa kuwekewa mikono au kuombewa na ndio maana hawachi kutanga tanga huku na kule wakitafuta baraka na kuacha baraka ambazo zinawazunguka.


Sasas leo nataka tuone msingi wa baraka na mpenyo katika maisha yetu!


MPENYO KATIKA MAISHA YETU UNATEGEMEA SANA JINSI TUNAVYOITIKIA KWA


              A.NENO LA MUNGU
Ni namna gani unatii na kulifuata Neno la Mungu?
Ni mara ngapi neno limekwambia fanya hivi na wewe ukafanya vile?
Ni dhahiri kuwa imani yetu huja kwa njia ya neno na imani hiyo haiwi dhahiri mpaka matendo yaonekane wazi...Kwa mfano katika Biblia kuna mifano ya watu wengi sana ambao walitii neno la Mungu na wakapata mipenyo katika maisha yao,naomba nimseme mmoja tu na huyu ni Jemedali wa Vita NAAMANI aliyekuwa na ukoma; alipewa wito na mjakazi tu kuwa katika nchi yao(yule mjakazi) yupo mtu anayeweza kuleta majibu kwa shida yake....tunaona katika maandiko kuwa jemedali huyo aliitikia na akaenda mpaka nchi ile kumwona mtumishi wa Mungu huyo...UNAFIKIRI NI WATU WA NGAPI WENYE VYEO NA HADHI ZA JUU WANAWEZA KUTII NENO LA WATU WALIO CHINI YAO???
Na alipofika huko mtumishi yule wa Mungu hakufanya lolote lile ila alimwambia nenda kajichonvye mara 7 ndani ya mto Yordani basi....kikawaida yule jemedali alihisi kudharauliwa na akataka kugoma kufanya hivyo lakini wasaidizi wake wakamwambia..kwani ukifanya hivyo utapungua nini? na vipi kama angekwambia jambo kubwa usingelifanya?...basi Jemedali alitii neno lile na akafanya kama mtumishi alivyosema na akawa mzima hata leo...kama huamini tukifika mbinguni nikumbushe tumtafute nikuonyeshe!!!


UNAYO NAFASI KUBWA SANA YA KUPATA CHOCHOTE AMBACHO BWANA ANATAKA UPATE LAKINI,HAKIKISHA UNAITIKIA KILA NENO LA MUNGU LINAKUJA MOYONI WAKO!!!


     B. KWA WATU
Mpenyo wako pia unategemea sana jinsi unavyoitikia miito mbalimbali ya watu, Je ni mara ngapi umepata wageni na ukashindwa kuwakirimu ipasavyo? ni mara ngapi unapata wageni lakini umekuwa ukiwapuuzia?
Jinsi unavyokuza uhusiano na kutunza urafiki na kutokuchoka kutenda wema kwa watu mbalimbali wajao maishani mwako ndio unavyojitengenezea mpenyo wako wa kesho....kwa mfano tu huo wa hapo juu unaona jinsi ambavyo Naamani aliitikia wito wa wajakazi wake,lakini pia kuna wakati Ibrahimu alipokea wagen watatu na akawakirimiia sana na wale ndio wakamwambia majira kama haya mwaka ujao mkeo atakuwa na mtoto..
ANGALIA NI WATU WANGAPI UMEWAPOTEZA KWENYE MTANDAO WAKO WA WATU WA MUHIMU NA MARAFIKI!!!


      C.KWA FURSA MBALIMBALI ZINAZOTOKEA KATIKA MAISHA YAKO
Unajua kama daudi hakuitwa kumuua Goliathi lakini aliposikia matusi kwa Mungu wake,akaona hii si nafasi ya kuikosa,hivyo akajitokeza bila kujali vipingamizi vya ndugu na umri wake na akasema yeye anaweza kumuua Goliathi na akafanya hivyo na akawa mfalme!!


HIVYO NDIVYO ILIVYO HATA KWAKO,UPATAPO NAFASI HADIMU ITUMIE VEMA YAMKINI NDIO MPENYO WAKO...IWE KWENYE BIASHARA,KAZI,MAISHA,SHULE NA MENGINE KADHA WA KADHA!!!


Ahsanteni sana kwa kushiriki nasi katika neno hili na MUNGU AWABARIKINI NYOTE MNAPOOENDELEA KUYATAFAKARI MANENO HAYA NA KUYATENDEA KAZI,AMEN!!!



No comments:

Post a Comment