Thursday, June 21, 2012

.....SASA NI SAA YA BWANA KUJITUKUZA KUPITIA VIPAJI VYETU!!!!!

KING CHAVALA KUFANYA TAMASHA LA CHRISTIAN STAND COMEDY TENA DAR ES SALAAM J’PILI YA TAR.24TH JUNE 2012 NDANI YA CITY CHRISTIAN CENTRE-UPANGA.


http://www.facebook.com/events/298374726898828/

Baada ya kufanya Tamasha la KUCHEKA TENA la mwisho pale Landmark Hotel,Ubungo mwezi wa tatu na hatimaye Arusha mwanzoni mwa June hatimaye mkali na muasisi wa christian comedy nchini Tanzania anatua tena jijini Dar es salaam kwa Tamasha lake la nne toka ameanza mwishoni mwa mwaka jana pale Ubungo plaza.
Yaani ni kucheka na kucheka na kucheka tena huku ukimsifu Mungu na kujifunza yapasayo kutenda katika maisha yako ya utauwa.
Tamasha hili litawasimamisha Up Coming Comedians wa kutosha katika segment maalum ya OPEN MIC, na wale ambao wamezoeleka kama Richard Chidundo,Gerald Mrema,pilipili,Josephine na wengine watakuwa sambamba na waimbaji kama Sarah Shila, Deogratius, Meshack, Gee & Seth, WordAlive and Dar es salaam Gospel Bands,Golden Eagles and 1st Q dance groups katika kunogesha na kuhudumu pamoja na Mkali wa jukwaa, mtu aliye dawa.....The King Of Stand Up Comedy,CHAVALA.

Kwa wale wafuatiliaji wa mambo, naamini LAUGH AGAIN CONCERT SERIES sio jambo geni masikioni mwao!!
Huu ni ule mfululizo maalum wa matamasha ya vichekesho na vipaji halisi vya kikristo hapa nchini ambao unasimamiwa na MC/Comedian na Muasisi wake nchini CLOWN CHAVALA(The King of Stand Up Comedy) kupitia Chavala Ideas Platform chini ya udhamini mkubwa wa Great Potentials Ltd.
TAMASHA HILO LITAANZA SAA TISA JIONI MPAKA SAA MOJA NA NUSU USIKU(3-7:30PM) 
NA KIINGILIO KITAKUWA 5000/= 
NA 2000/= TU KWA WATOTO.
Katika SERIES hii bado tuko Msimu(SEASON) wa kwanza na hili Tamasha lijalo litakuwa Tamasha la tatu kwa Dar es salaam  na ni Episode II. Kama ilivyotaarifiwa mapema Tamasha hili la jpili ijayo(24th June 2012) pamoja na mawili yafuatayo kwa hapa Dar(Yaani Tar 23th Sept na 23/30th Novemba-mkesha wa mwisho) yatafanyika katika
 ukumbi wa CITY CHRISTIAN CENTRE-UPANGA(Mkabala na Mzumbe Dsm)
TAMASHA HILI LIMEDHAMINIWA NA GREAT POTENTIALS LTD,CITY CHRISTIAN CENTRE(CCC),TOUCHING VISION,AUTHOR2READERS,WORDALIVE CHURCH,OLYMPUS COMPUTERS AND CHAVALA IDEAS PLATFORM.
Akielezea mafanikio yaliyopatikana Chavala amesema;.....Kwa kweli mafanikio ni makubwa sana mpaka sasa ingawa mengine hayawezi kuonekana kwa macho ya nyama ila itoshe tu kusema mafanikio ni makubwa mno;yaani toka kule ambako nilikuwa sitambuliki na watu kwa makusudi walikuwa hawataki kuona umuhimu wa Comedy katika ulimwengu wa kikristo mpaka sasa ambako wengi wameanza kuelewa, wamepokea na wamekubali,kibali nilichokipata Arusha kwa mfano ni kikubwa mno kiasi cha kushangaza; kwa sasa nina vijana wengi sana ambao wamevutwa na kuona nao wanaweza kumtumikia Mungu kwa vipaji vyao kama vile Comedy,Dance na Mashairi na mengine mengi ya vipaji halisi, hivyo nina wanafunzi wakutosha na zaidi washika dau,wachangiaji na wanaounga mkono ni wengi sana na hata wewe unaesoma hapa unakaribishwa kuwa mmoja wao.
Nimeongeza marafiki na maadui(ingawa kwangu ni invalid) na nimekuza network base yangu hapa nchini, kwa msaada wa media ninaamini nitaweza kuyafikia majiji yote nchini na kutambulisha Christian Comedy na vipaji halisi isipokuwa Tanga peke yake,ambayo haiko katika ratiba ya msimu huu w kwanza.
Chavala ametoa ratiba yote ya mwaka iliyobaki kuwa anatarajia kufanya Matamasha makubwa hayo katika majiji yote ya Tanzania kabla ya Novemba,mpaka sasa matamasha hayo yameshafanyika Dar es salaam na Arusha na Mwishoni mwa July Chavala atakuwa Mbeya,mwishoni mwa August itakuwa Mwanza,September ni Dar tena,October itakuwa Dodoma na Mwisho wa Novemba nitamalizia kwa mkesha pale CCC-Upanga,huu utakuwa ni mkesha maalum wa kumaliza msimu wa kwanza na utahusisha wasanii wote na wengine wateule ambao wamepata nafasi ya kushiriki katika matamasha mbalimbali ya msimu huu wa kwanza!!
Kwa matamasha yote hayo yaliyo mbele bado kuna mengi na vingi vinahitajika,kama vile Pesa, Laptops,Kamera,Music system,Sudio na mengine mengi hivyo ikiwa unaguswa kuhusika/kuchangia/kudhamini/kushauri chochote katika Tamasha lolote wakati wowote tafadhali usisite kufanya hivyo, tutashukuru mno ingawa tunashikilia haki ya kutendea kazi au kutunza ushauri wowote ule ujao toka  nje.
Unaweza kutuandikia kupitia lacs.project@gmail.com 
au tupigie kupitia +255-(713/753)-883 797....pia unaweza kuchangia kwa benki za simu(M-pesa na Tigo Pesa) kupitia no.hizo hizo.
Lakini pia unaweza kutembelea blogs
1.       www.gospelstandardbase.blogspot.com......hii ina mafundisho zaidi kuhusu Neno la Mungu toka kwa watumishi wa Mungu mbalimbali
2.     www.chavalapf.blogspot.com.......hii inahusika na mawazo mbalimbali ya watu mbali ambayo ni muhimu na yanajenga!
3.     www.kingchavala.blogspot.com...... Hii ni maalum kwa ajili ya shughuli zote na matukio yote yamuhusuyo Clown Chavala,The King!
Na unaweza kutembelea page ya facebook; LAUGH AGAIN CONCERT SERIES
Au page mahususi ya Chavala...
www.facebook.com/KingChavala   au www.facebook.com/chavalapf na zaidi wale watumiaji wa Twitter mnaweza kumfuataPresident Chavala @ClownChavala
ANGALIZO;
Kama ungetamani kuwa mwanachama na unapenda kupata habari kila mara zikiwepo huhusu mizunguko ya Chavala katika kampeni hii na kufanyika kwa matukio haya kokote kule nchi usisite kutuandikia kwa e-mail hiyo hapo juu.
Na kwa wale wasanii wanaochipukia na wale wanaofahamika huko mikoani tafadhali wasiliana nasi mapema kama ungependa kushiriki katika mojawapo ya matamasha haya kwa namna yeyote ile.
SHUKRANI;(Na President Chavala)
Mwisho napenda kutoa shukrani kwa mashabiki na wafuasi wangu wote ambao ndio wanafanya jambo hili liiendelee kukuwa siku hadi siku,tunashukuru kwa wachangiaji wa fedha,mawazo,muda na ujuzi; ninawashukuru wote wanaotuombea na kututakia mema kila wakati majukumu haya;Ahsante kwa magazeti,ahsante watumiaji wa Social networks kama Twitter,facebook na blogs na wanahabari wote zaidi redio,magazeti na christian blogs,kuanzia wanahabari binafsi mpaka wale wanaofanya kwenye makampuni na Taasiss binafsi na za serikali ambao mmkekuwa mstari wa mbele katika kupigia debe jambo hili! Naamini Mungu lazima awalipe katika mambo yenu!
Natambua mchango wa wasanii wengine katika sanaa hii, maana peke yangu nisingefika popote pale,ahsanteni Emmanuel Mgaya(Masanja Mkandamizaji); Evance Bukuku(VuvuZela Comedy Show); pamoja na vijana wangu kama Richard Chidundo;Mrema Gerald, Senior ABBy na MC Manu/pilipili toka Dodoma na wengine wengi ambao kimsingi mchango wao unatambulika!
Naamini kila utakapoona tangazo popote hautasita kufika na kuwaalika wengine au wenzako...tafadhali anza kutekeleza hayo na Tamasha hili,ubarikiwe sana!! 


Unaweza tembelea facebook group yetu ;
 http://www.facebook.com/groups/lacs.project
Ahsanteni sana na karibuni sana sana kucheka tena na tena na tena maana kucheka ni dawa na kunaondoa sumu mwilini!!

No comments:

Post a Comment