Sunday, December 16, 2012

VIGEZO VYA UBORA/HESHIMA VYA MTUMISHI WA MUNGU HUSUSANI MWANA-SANAA (02)


VIGEZO VYA UBORA/HESHIMA VYA MTUMISHI WA MUNGU HUSUSANI MWANA-SANAA (02)

(Qualities of honor of a Christian Servant especially Christian Artist (Celebrity))
*****************************************************************************************

Shalom!!
Ninayo heshima kubwa sana kwenu na kwa Mungu na moyo wangu umejaa shukrani mno, ahsante kwa kupata muda wa kujifunza na kuyatafakari yale yafaayo kutafakariwa!

Mara ya Mwisho nilijenga tu msingi wa makala hii na nikasema 

HATUA ZA MSINGI kuwa;
Kipaji mtu hupewa na Bwana lakini maboresho ya kipaji huletwa na juhudi ya mwenye kipaji, yaani namaanisha huwezi kung’aa katika kipaji chako kama hujaweka juhudi za kutosha katika kipaji hicho, hivyo zifuatazo ni hatua za msingi kwa mtu yeyote;

a.     KUJITAMBUA
b.     KUJIVUMBUA
c.      KUJIFUNDISHA
d.     KUJIJARIBU
e. KUJIHUDHURISHA RASMI SASA

Sasa leo natamani nizungumze kidogo kuhusu;

                               a.     KUJITAMBUA
Kujitambua ni ile hali ya kujifahamu na kujijua vema zaidi ya maelezo ya kinywa chako. Kujitambua ni hatua ya kujua nini asili au chanzo chako, nini sababu ya kuwepo kwako, upi ulazima wa uwepo wako sasa na nini tofauti yako na watu wengine waishio sasa, nini kusudi la maisha yako na zaidi ni nini hatma yako katika maisha haya.
Watu wengi wanashindwa kujitambua kwasababu huwa wanashindwa kuelewa asili yao tangu hapo awali, sikiliza; Nadharia za sayansi na magunduzi yote ya Ulimwengu yatakupa majibu nadharia tu ambayo kamwe hayawezi kukupa majibu sahihi kuwa wewe nio nani?
Wewe ni zaidi Jina lako na mwili wako na akili yako....ndio maana mtu ukimuuliza jina lako nani atakwambia CHAVALA, na ukiuliza CHAVALA ni jina la nani atakwambia ni jina langu, ukiuliza huo mwili ni wa nani? atakwambia ni wangu,sasa unajiuliza wewe ni nani? Atakwambia mimi ni mimi mwenyewe, na ukitaka kuthibitisha hili, ni pale ambapo Mtu akifariki huwa yunasema  "Mwili wa Marehemu utasafirishwa au kuzikwa kesho" sasa hapo unagundua kuwa Kuna mtu anamiliki mwili na ndio marehemu, kwahiyo wewe ni zaidi ya hivi tukuonavyo kwa nje.
maandiko yanasema katika Mwanzo 1:26, Mungu akaupulizia Udongo pumzi ya UHAI nae akawa NAFSI HAI

Hivyo MTU=MWILI+NAFSI+ROHO

Mwili ni kasha linalobeba Roho(Pumzi ya Mungu) iliyombatana na Nafsi(Serikali ya Mtu) na hivyo kwa pamoja ndio unapatikana MTU.
Wewe haukuzaliwa kwasababu BABA na MAMA yako walikutana ama kuoana, ila kwasababu ULITAKIWA KUJA Ilibidi kwa namna yeyote ile wakutane tu ili wewe upitie mlango huo kama Mungu alivyopanga.
Kwahiyo kila siku tembea ukijua ulikuja kwa KUSUDI MAALUM na kusudi hilo likiisha utarudi pumzikoni,tayari kwa hukumu au malipo ya kazi uliyokuwa umetumwa kuifanya, na dio maana ninasisitiza kujitambua ili ufanye kazi sawasawa na kusudi la Mungu maishani mwako na usije ukaishia kuishi makusudi ya watu wengine.
Wewe ni Hekalu la Mungu, hivyo kama ukikubali kuishi kusudi la Mungu basi lazima utayafurahia sana maisha yako mpaka mwisho...watu wengi wanapata shida na kuhangaika sana kwasababu wako nje ya makusudi walioitiwa na Mungu.

THAMANI YAKO
"Thamani yako haina uhusiano na mahali unapokaa,watu wanaokuzunguka,marafiki ulionao,elimu uliyonayo ama chochote kile kinachohusiana na wewe, bali thamani yako ni juu wa wewe mwenyewe(jinsi wewe ulivyo)"
Watu wengi wanajisumbua sana na kutafuta thamani zao kupitia vitu mbalimbali na hii kwa kiingereza tunaita "IDENTITY CRISIS"
Mtu anafikiri akiwa Dar ana thamani kuliko wa Kigoma, au akiwa na Degree 3 basi yeye ni zaidi ya asiyejua kusoma na kuandika, au ukiwa unafahamiana na Rais basi wewe ni zaidi ya mwingine ama labda ukioa mtoto wa Tajiri basi na wewe thamani yhako inapanda,hapana!....THAMANI YAKO IKO KATIKA KUSUDI NA HATMA YA MAISHA YAKO!!
Ukijua thamani ya kipaji chako wala huwezi kuhangaika,mimi nakushauri uishi maisha yako na ujikubali kabisa kuwa Mungu kwa wakati wake atakufikisha mahali pa juu zaidi ya hapo hata kama hapatafanana na mahali pa yule mwingine!!

N.B; katika maisha haya haupaswi kushindana na yeyote yule, kwasababu hakuna hata mmoja aliye kipimio cha mafanikio yako, wewe ni mshindani wa wewe mwenyewe, unapaswa kuchamotishwa na ile taswira ya wewe uionayo hapo mbeleni, ukitaka uwe kama kila umuonaye utakufa siku sio zako...yaani ni kama vile mnaamka asubuhi kwenda STAND ili msafiri na kila mmoja kati yenu anaenda njia yake, sasa kuwahi au kuchelewa kwa yeyote kati yenu kunamuathirije yeyote kati yenu hali kila mmoja anapanda usafiri wake???

USIISHI MAISHA ILI WATU WAKUONE AU USHINDANE NA FULANI, ISHI KUSUDI LAKO!!

Ongeza juhudi kujifunza kuhusu wewe mwenyewe ili ujue lile kusudi la Mungu maishani mwako ni lipi na ujue majira ya kila hatua katika kusudi hilo la Mungu, zaidi utajua ni wapi unahitajika kwa sasa, nani uambatane nae na nini ukiseme kwa nani, maana ni muhimu sana!!
SOMO HILI NI PANA SANA LAKINI NAAMINI KWA KIASI UTAKUWA UMENIELEWA KUWA NI MPAKA UJITAMBUE VEMA NDIO UTAWEZA kuwa mtumishi mwenye VIGEZO VYA UBORA KWAKO BINAFSI,KWA MUNGU NA KWA KILA AKUTANAE NA WEWE!!

"Ni hatari sana watu wakikutambua kabla ya wewe kujitambua, maana hutaweza kusimama imara, kwani kila wakati utakuwa unaishi sawasawa na maoni yao na sio uhalisia wako"



TUTAENDELEA  ZAIDI KUCHAMBUA KIDOGO KIDOGO, MPAKA HAPO NITAKAPOMALIZA KIINI CHA UJUMBE HUU!!

KARIBU SANA!!!
King Chavala
+255 713 883 797

.........TUTAENDELEA!!!

No comments:

Post a Comment