VIGEZO VYA UBORA/HESHIMA VYA MTUMISHI WA MUNGU HUSUSANI MWANA-SANAA (01)
(Qualities of
honor of a Christian Servant especially Christian Artist (Celebrity))
*****************************************************************************************
Shalom!!
Ninayo
heshima kubwa sana kwenu na kwa Mungu na moyo wangu umejaa shukrani mno,
ahsante kwa kupata muda wa kujifunza na kuyatafakari yale yafaayo
kutafakariwa!!
Nimekuwa
na maswali mengi sana kichwani mwangu na mara kadhaa niwewahi kuwahoji watu
mbalimbali, kuwa….HIVI KWA MFANO UKIANDAA TUKIO FULANI MAHUSUSI NA UKATAMANI
MMOJA WA WASANII(WA SANAA YEYOTE ILE) AWE MGENI RASMI, UTAMCHUKUA NANI? KWA
NINI? NA KAMA UKIMPATA HUYO, NI KWA NINI HUYO NA SIO MWINGINE?
Bila shaka
umeshtuka na kichwani mwako bado una haha na yamkini hata nadharia zako
huziamini amini vile, lakini yote haya ni kwasababu gani?
Je hakuna
msanii mwenye hadhi ya kuwa mgeni rasmi? Je wasanii au watu maarufu wanajua
thamani yao? Je wanajua kujiweka sawasawa mbele ya jamii?
Nimeona
nianzie hap oleo na nitaendelea kuzungumza mambo muhimu ya kuzingatia kwa
mtumishi wa MUNGU anapokuwa maarufu au star kwa lugha ya leo!!
HATUA ZA MSINGI
Kipaji mtu hupewa na Bwana lakini
maboresho ya kipaji huletwa na juhudi ya mwenye kipaji, yaani namaanisha huwezi
kung’aa katika kipaji chako kama hujaweka juhudi za kutosha katika kipaji
hicho, hivyo zifuatazo ni hatua za msingi kwa mtu yeyote;
a.
KUJITAMBUA
Kila mtu anapaswa kujitambua vema, yeye ni nani? Anataka nini katika
maisha na anatamani kufika wapi? Zaidi nini makusudi ya Mungu kumleta hapa
duniani!!(HILO SI SOMO PANA SANA LAKINI HAPO MBELENI TUTAKUJA KUCHAMBUA KWA
KINA SANA)
b.
KUJIVUMBUA
Mtu akishajitambua sasa anakuwa na heshima ya kuwa mtu na sasa kuna uwezo
ambao Mungu ameuweka ndani ya kila mtu kipekee na uwezo huo ndio unaotoa
mwelekeo hata wa kusudi la maisha yako hapa duniani. Sasa unapaswa kupitia
hatua hii ya kujivumbua, hapa mtu anajua kwa hakika yeye ana kipaji Fulani na
hicho amepewa awe makini kwa manufaa yake na jamii nzima(PIA HAPA TUTAKUJA KUCHAMBUA
KWA KINA SANA HAPO MBELENI)
c.
KUJIFUNDISHA
Neno kujifundisha limesimama kwa niaba ya maneno MAFUNZO, yaani
ukishajivumbua sasa unajitaji elimu,utaalamu na ujuzi bora uliopangiliwa vema
sana juu ya hicho kipaji chako, watu wengi sana wakishajivumbua kuwa wao ni
wazuri katika jambo Fulani basi hawafanyi jambo lolote zaidi kuvimba kichwa na
kuanza kuishi maisha ya maigizo na unakuta hata hawavumi kivile kwasababu
hawajawekeza kwenye kujifunza(HAPO MBELENI TUTACHIMBA NDANI KABISA NA KTOA
MIFANO HAI)
d.
KUJIJARIBU
Hii ni hatua ambayo mtu anaanza kujihudhurisha mbele ya kadamnasi na
kujaribu kuonyesha kile anaweza kufanya na hapa ni kama elimu wa vitendo, kwa
maana hapa mtu anakuwa bado havijui vingi lakini anafanya vile ajuavyo na
kufungua masikio kwa ajili ya maoni na mafunzo zaidi, hapa wengi huruka na
kudhani wameshakuwa watu maarufu na ndio maana unaweza kuona mtu anakuja kwa
kasi sana kasha akapotelea matopeni!!!
N.B; HATUA
HII HUENDA IKIBOREKA NA KUBOREKA KADRI
MTU ANAVYOJITAHIDI KUONGEZA JUHUDI KATIKA KUJARIBU NA KUJARIBU
TENA(WAZUNGU WANASEMA…PRACTISE MAKES PERFECT)
e. KUJIHUDHURISHA RASMI SASA
Baada ya
muda wa kutosha sasa unafika wakati wa kuwekwa wakfu na kuanza kufanya na
kuishi kipaji chako, hapo unakuwa bidhaa na unakuwa mshauri na mwalimu wa wengine
wanakuja katika njia moja au katika tasnia uliyoipitia, na wakati huu na wewe
pia huendelea kukua na kama ukizingatia misingi ya kwanza basi wewe kwenye
sanaa uko salama….
HUU ULUKUWA NI MSINGI
TU WA UTANGULIZI NA….
TUTAENDELEA KUCHAMBUA KIDOGO KIDOGO, MPAKA HAPO
NITAKAPOMALIZA KIINI CHA UJUMBE HUU!!
KARIBU
SANA!!!
King Chavala
+255
713 883 797
.........TUTAENDELEA!!!
No comments:
Post a Comment