Katika
Weekend hii Big Events za wanafunzi zenye jina La Campus Night zimechukua
mkondo wake katika mikoa ya Dodoma na Mbeya.
Blogger
akiripoti kutoka Mbeya ameeleza kuwa Campus Night ya Mbeya imevunja Records ya
Makusanyiko ya vijana na wanafunzi katika jiji hilo, event hiyo iliyokusanya
wanafunzi zaidi ya 7000 ilikuwa na theme ya Raising The Standards.
Mwimbaji
wa Injili anayevuma na ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu mkoani humo
Ambwene Mwansongwe ndiye aliyeteka ukumbi kila aliposimama.
Wachekeshaji
wanaovuma katika tasnia ya Gospel, King Chavalla na Mc Pilipili walinogesha
Campus night yaJiji la Mbeya.
Wanenaji
Wakuu Katika Usiku huo Dr. Huruma Nkone, Dr. Kimambo, Ms Rose Mushi na Mr.
Msigwa wali Raise Standards za Wanafunzi.
Dr.
Huruma Nkone aliyekuwa akifundusha Spiritual Transformation usiku huo alilipuka
kinjilisti na kuwaambia wanafunzi 'Usharubalo na Utoz Toz,hautainua kiwango
chako cha Kiroho, isipikuwa kwa kumpokea Yesu' akinukuu andiko la kutoka kwenye
kitabu cha Yohana ikisema 'Mimi ndimi njia kweli na uzima, mtu haendi kwa Baba
Isipokuwa kwa njia ya Mimi"
Dr.
Kimambo alifundisha Academic and Career Challenges zinazowakabili wanafunzi.Dr.
Kimambo ambaye ni Mwajiriwa wa Serikali yaUingereza nchini Tanzania alieleza
'changamoto za mfumo wa elimu na mahitaji ya soko la ajira ni tatizo linalo
wakabili wanafunzi. Tatizo la Soft Skills mbali na ule ujuzi unaopatikana
vyuoni ni changamoto pia.Mbali na changamoto hizo maendeleo na matumizi ya
technolojia katika mfumo globalization ni changamoto inayowakabili wahitimu wa
Elimu Ya Juu.
Mwanadada
aliyekuwa
msemaji pekee katika Campus night na mdogo wa umri kuliko wasemaji
wote Dada Rose Mushi alifundisha RaisingThe Standard Of Ladies In the
Campus.
Rose Mushi ambaye ni Mchumi kwa taaluma na mwajiriwa wa Kanisa la KKKT
Dayosisi
ya Mashariki na Pwani. Aliamsha hamasa kubwa ya vijana alipoanza
kufundisha
kutoka kwenye Kitabu Cha Mwanzo kwenye story ya Yusufu na Mke wa Potifa.
Akifundisha Usiku huo Rose Mushi alisema ili kuinua Viwango vya Kiroho
Vya
Akina dada katika Campus inapaswa kwanza Ujue thamani yako kama Mdada,
pili inakupasa kuachana na mambo yote ambayo yanakusababishia
kukushikilia kwa mwanaume kama mi kufaulu, kama ni ada, kama ni laptop
kama ambavyo Yusufu alimwachia vazi Mke wa Potifa.
Somo
la Mahusiano lilifundishwa na Mr. Msigwa Meneja wa tawi la CRDB katika
wilaya ya Mbozi. Alieleza uhusiano wowote wa mwanaume na mwanamke
hauwezi kuwa mzuri kama wahusika wana uhusiano mbaya na Mungu wao.
Praise and Worship Leaders. Mr and Mrs Matthew Sasali
Event hiyo ilisimamiwa na Dr. Nyanda pamoja na Ze Blogger. Praise Team ilisimamiwa na Pastor Matthew Sasali na Rebecca Sasali
Dr. Nyanda, Rose Mushi na Papaa Ze Blogger hapo ilikuwa saa 1 Asubuhi baada ya event.
Matukio Katika Picha.
Sehemu Ya Umati Wa watu
Mrs. Rebecca Sasali akiongoza Praise Team
Wanafunzi Waliotoka Mbele Kumpa Yesu Maisha Yao Zaidi ya wanafuzi 90 walimpa Yesu Maisha yao.
Ndani Ya Uwepo
Watu Wakienda Sawa ndani ya Ukumbi
Full Shangwe Wanafunzi Wa Mbeya
Chezea Nyomi
Respected Event Manager Papaa Ze Blogger ndani ya Ukumbi
Ukumbi Mzima Kidole namba tatuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Watu Wakimpa Yesu Maisha Yao.
Rose Moshi Kikazi zaidi
Chezea Urefu
Wakienda sawa
Huu Mwili Khaaaa
Pilipili Kikazi Zaidi ndani ya Mbeya
Kikazi Zaidi hapa
Safari Hii akaja na Style ya Sketi aiseeee ilikuwa nouma inaitwa "Usiombe Kusutwa'
Dr. Maboko akizungumza kwenye Campus Night
King Chavallaaaaaaaa akienda sawa ndani ya Campus Night
Jamaa kumbe akivua Kofia ni handsome sanaaaaaaaa
HABARI INAKUJIA KWA HISANI KUBWA YA PAPAA ZE BLOGGER!!!!
No comments:
Post a Comment