NANI AJUAYE SIRI YA UPENDO?
“Nakupenda kutoka moyoni
mwangu”….ni sentensi maarufu katika ulimwengu wa mapenzi. Inaweza kuwa inasemwa
kwa kumlizisha msikilizaji wa maneno hayo au ikiwa na maana kubwa kwa msemaji
wa maneno hayo. Nani ajuaye ukweli wa maneno hayo ni siri ya moyo.
Mara nyingi huwa nasema hakuna
asiyependa kupendwa. Ila sina hakika kama ni wote tunapenda kupenda. Katika
utafiti wangu mdogo kuhusu maisha nimegundua mada kubwa miongoni mwa jamii ni
mapenzi na muziki.
Watu wanatumia nguvu nyingi kutafuta pesa ili tu wapate vitu
wanavyovipenda. Wapate wasichana warembo kama wake zao, wavulana watanashati
kama waume zao, nyumba wanayoipenda, magari wanayoyapenda, wakae sehemu au
mahali wanapopapenda na kujiburudisha moyo kwa nyimbo au muziki wanaoupenda na
miziki mingi imejaa maneno ya sifa na mapenzi.
Kukupa huu ujumbe, nimeamua mwenyewe,
Hivyo usifumbefumbe, nikosapo nikosowe,
Ila kukupenda wewe, si chanzo cha kunitesa.
Kwasababu hiyo watu wenye pesa
hutafuta upendo wa kweli na watu masikini hutafuta pesa ili wakatafute upendo
wa kweli. Burudani inaanzia hapo wanapokutana anayetafuta upendo wa kweli na
anayetafuta pesa ili akatafute upendo wa kweli.
Unaweza kuwa umejiuliza kati ya
watu wenye pesa na watu wenye uwezo wa kawaida na maskini ni watu gani hutumia
nguvu nyingi kutafuta kupendwa. Nimekwisha kusema kila mtu anapenda kupendwa,
lakini matajiri na watu wenye uwezo mkubwa hutumia nguvu nyingi sana kutafuta
kupendwa, pia watu wahali ya kawaida wao hawatumii nguvu nyingi ukilinganisha na
matajiri na wenye uwezo mkubwa. Tukirudi kwa masikini wao hutumia nguvu kidogo
sana ili wapendwe.
Je unahitaji uwe na uwezo mkubwa au tajiri ili upendwe?
Je unahitaji kuwa mtu mwenye uwezo wa kawaida ili upendwe?
Je unahitaji kuwa masikini ili upendwe?
Endelea kufwatilia mada hii nzuri naya kusisimua wiki ijayo……
kwa
maswali, maoni,mapendekezo na ushauri niandikie kupitia barua pepe makwayae07@gmail.com
No comments:
Post a Comment