Monday, September 30, 2013

JOHN LISSU KUANDIKA HISTORIA YA MUZIKI WA INJILI TANZANIA TAR 06/10/2013!!!



UKO HAPA DVD LIVE RECORDING
 NA JOHN LISSU,
06/10/2013,CCC-UPANGA, DAR ES SALAAM, TANZANIA.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE;
SALAM TANZANIA!

Shalom Dar es salaam, Shalom Tanzania!
Ndugu wanahabari na watanzania wote kwa ujumla!
Naamini tuko salama na tunaendelea na shughuli zetu za kila siku alizotupatia Mungu wa mbinguni, tumshukuru Mungu sana kwa Amani na utulivu aliotupa na tuendelee kumuomba ili atuepushe na kila aina ya dhahama na uharibifu wa Yule adui!
Kama tulivyosikia hivi karibuni, yale yaliyotokea nchi jirani ya Kenya, kwa hakika tunawapa pole sana kwa mkasa huo, pole kwa wale waliowapoteza wapendwa wao na wale waliojeruhika tunawaombea wapone haraka, tunaamini hekima ya Mungu itakuwa juu ya serikali yao kushughulikia jambo hilo kikamilifu.
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, hata sasa tunapoende kumalizia robo ya tatu ya mwaka 2013, tumeshuhudia mambo mengi sana mwaka huu ya kila aina, yapo yale yalionza kwa mara ya kwanza na mengine yamekuwa ni mwendelezo tu wa yale yadumuyo au yalioyaanza hapo kale, tumeshuhudia michezo mbalimbali na vipaji lukuki vikiinuka na kuimarika katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, na kwa yote mema na mazuri tunampa Mungu Utukufu kwa hakika!


UTANGULIZI JUU YA JOHN LISU;

John Lisu ni mmoja wa waimbaji/Waabudishaji wanaoheshimika katika Tasnia ya muziki wa Injili kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kukuza na kuendeleza muziki wa Injili nchini Tanzania na nje ya Nchi. Nyimbo nyingi alizozitunga na kuziimba zimekuwa zikitumika katika makanisa mbalimbali kama nyimbo za kusifu na kuabudu; pia waimbaji wengine waliokua wakiimba naye wameweza kukua na kufikia uwezo wa kuwa waimbaji wa kujitegemea. John Lisu pia ametia hamasa kubwa miongoni wa wanamuziki wa Injili kuanza kufanya muziki wa live. John Lisu ameweza kufanya tours za ndani ya Tanzania, Africa na Bara la Ulaya kwa ajili ya huduma.
CHRISTINA SHUSHO

John Lisu anategemea kufanya Project II ya Live recoding inayojulikana kama "UKO HAPA" baada ya project ya kwanza ya Jehova yu hai kufanya vizuri sana. Tamasha litafanyika ndani ya ukumbi wa City Christian Centre (CCC) Upanga tarehe 6 Octoba 2013, kuanzia saa 8. mpaka saa 2 usiku.
PAUL CLEMENT

 Tamasha litasindikizwa na waimbaji nguli kama Christina Shusho, Neema Gospel Choir, Paul Clement, Pastor Safari Paul, Bomby Johnson Waimbaji wote wamethibitisha kuwepo. 

BOMBY JOHNSON

VENUE:
City Christian Centre (CCC) mkabala na chuo kikuu cha mzumbe
Si mbali saana kutoka Diamond Jubilee
MIRIUM LUKINDO WA MAUKI


USAFIRI (basi zilizobandikwa matangazo ya tamasha) utakuwepo kutoka posta mpya kwenda ukumbini kuanzia saa saba na nusu mchana kwa bei ya kawaida.
PASTOR SAFARI PAUL

HABARI NJEMA-MUHTSARI!!!!!

Sasa kwa mara pili nchini Tanzania, mwimbaji WA NYIMBO ZA INJILI na mwabuduji JOHN LISSU wa jijini Dar Es Salaam, atakuwa anafanya Ibaada kubwa ama Tamasha la kusifu la Kuabudu(LIVE PERFORMANCE), litakalorekodiwa moja kwa moja (DVD LIVE RECORDING) lenye jina “UKO HAPA” (Yaani Mungu na Uwepo wake).
Tamasha hilo litafanyika jumapili ya Tarehe 6, Octoba 2013  katika Ukumbi mkubwa wa kisasa wa Kanisa la City Christian Centre (CCC)- Upanga, mkabala na Chuo Kikuu Mzumbe – tawi la Dar es salaam, kuanzia saa nane mchana.
Tunataraji watu 5000 kuwa sehemu ya tamasha hili la kipekee,Utakuwa sehemu ya tamasha hilo kwa tiketi ya 10,000/= (kawaida), 20,000/= (VIP) na 3000/= (Watoto);
na Kwale watakaohitaji tisheti maalum za tukio hilo, basi zinapatikana kwa kati ya 12,000-15,000/=, wewe wasiliana tu na (0713905118)
NELLY-MKE WA JOHN LISU


VITUO VYA KUUZIA TIKETI;
1.   MWENGE – Tarakea duka la Kanda
2.   KINONDONI – DPC
3.   MLIMANICITY – Silverspoon Restaurant
4.   KARIAKOO – Mbogo Shop
5.   UKONGA BANANA – KWA GIDO
6.   POSTA - DUKA LA MSAMA

T-SHIRTS

-T-shirts maalumu kwa wanaume na wanawake zinapatikana katika vituo vya kuuzia tiketi kwa bei ya elfu kumi, mpaka elfu 15(kutegmeana na aina).

N.B; Kwa tiketi ya VIP, mnunuzi atajipatia na Audio CD ya John Lissu ya “Uko Hapa”

USAFIRI UTAKUWEPO!!
Siku ya tamasha kutakuwepo usafiri kutoka Posta Mpya mpaka CCC-Upanga,eneo la tukio, hivyo kama wewe ni mgeni na hupafahamu mahali hapo, basi utakachotakiwa kufanya ni kupanda magari toka ulipo mpaka posta mpya kabla ya saa nane,na hapo utayakuta mabasi yenye mabango ya Tamasha, basi utajongea humo na hapo utawezeshwa kufika eneo la tukio, muhimu ni kuzingatia muda!

MUHIMU SANA!!

JOHN LISU NA TIMU NZIMA WAKIWA MAZOEZINI


Tamasha hili ni muhimu sana kwa Tanzania, hasa ukizingatia JOHN LISSU ni mmoja wa waimbaji wa kwanza kuimba live kila mahali anapoalikwa na ni mwimbaji wa kwanza binafsi kufanya LIVE DVD RECORDING pale Ubungo plaza, na ile ya kwanza iliitwa “JEHOVA YU HAI” na sasa anafanya LIVE RECORDING kwa viwango vingine bora zaidi, maana Mungu hutupa hatua moja zaidi kila siku.
Ni muhimu kwa kila mtanzania kujivunia kipaji na tukio hili muhimu katika historia, njoo umwabudu na kumsifu Mungu pamoja, Njoo ujifunze, Njoo umuunge mkono mtanzania mwenzako na njoo uje ufanyike sehemu ya Historia hii kwa Utukufu wa Jehova.
NEEMA GOSPEL CHOIR-KWAYA PEKEE ITAKAYOSHIRIKI "UKO HAPA"


MWALIKO MAALUM;
Kipekee Ninapenda kuwakaribisha wachungaji, mitume, manabii, wainjilisti, waalimu na viongozi wote wa makanisa na huduma mbalimbali, ninawakaribisha viongozi wote wa kisiasa na kijamii kutoka serikalini na vyama vya siasa vyote, ninapenda kuwakaribisha wanaharakati na wanataaluma wote, ninapenda kuwakaribisha waimbaji wote wa nyimbo za injili na wanasanaa wote, ninapenda kuwakaribisa wanafamilia wote, asiwepo wa kubaki nyuma, ninapenda sasa kukukaribisha wewe unaesoma hapa, naam nisaidie kumkaribisha na mwenzako na yeye aje na mwenzake, kimsingi tukio hili ni letu wote bila kujali kitu chochote, njooni tumsifu na kumwabudu Bwana na Mungu hataacha kuibariki Tanzania!
EMMANUEL NDIYE ATAKAYEMPIGIA JOHN LISU LEADING GUITOR


SHUKRANI;
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Hakneel Production (Wadhamini wakuu), na Jonn Lissu na timu nzima ya maandalizi; Kanisa la CCC-Upanga; vyombo vya habari hususani Praise Power na WAPO Radio; Clouds TV kupitia CHOMOZA na Clouds Radio kupitia GT; Sibuka Tv kupita Gospel Hits; Bloggers hususani Christian Bloggers, magazeti na vyombo vingine vyote vya habari! Shukrani hizi zimfikie kila mtu mmoja mmoja aliyetoa mchango wa mawazo, fedha, ushauri, maombi, ubunifu, yaani mchango wowote wa hali na mali na Mungu awabariki nyote!
MIRIUM LUKINDO WA MAUKI


MUHTASARI MKUU;
Tukio; TAMASHA LA KUSIFU NA KUABUDU, LITAKALOREKODIWA
(DVD LIVE RECORDING CONCERT)
Mhusika; JOHN LISSU
Jina: “UKO HAPA”
Mahali; UKUMBI WA KANISA LA CITY CHRISTIAN CENTRE (CCC)- UPANGA
Lini; 06TH OCTOBA, 2013
Muda; KUANZIA SAA NANE MCHANA
Kiingilio; Tsh 10,000/= (kawaida); 20,000/= (VIP) na 5000/= (Watoto)

Wasindikizaji; CHRISTINA SHUSHO, MIRIUM LUKINDO, PASTOR SAFARI, BOMBY JOHNSON, NEEMA GOSPEL CHOIR-AIC Chang’ombe na PAUL CLEMENT.

Mengineyo; USAFIRI UTAKUWEPO TOKA POSTA MPAKA CCC-UPANGA na Unaweza kujipatia Tisheti pia.
Wahusika; WATU WOTE MNAKARIBISHWA!


UKIPATA HABARI HII USIACHE KUMSHIRIKISHA NA MWENZAKO, NAAMINI HAUTAKOSA TUKIO HILI MUHIMU LA KIHISTORIA KATIKA NCHI YA TANZANIA KWA UTUKUFU WA MUNGU!!





KWA PICHA NA TAARIFA ZAIDI;





MAWASILIANO:
O713 240 397 – JOHN LISU
0713 905 118 –PROSPER MWAKITALIMA – EVENT MANAGER
0713 883 797 - FREDY CHAVALA - PUBLICITY


Imetolewa na;
Fredy E. Chavala <King Chavala (MC)>
Publicity Manager
+255 713 883 797
On Behalf of The Organizing Committee

Wednesday, September 18, 2013

RICHARD CHIDUNDO....MC/CHRISTIAN STAND UP COMEDIAN/INTERPRETER BUT ABOVE ALL EVANGELIST OF THE GOSPEL OF JESUS CHRIST!!!!!

 
RICHARD CHIDUNDO

THIS IS THE MAN WHO MEAN IN WHATEVER IS DOING!
I LOVE HIM FOR REAL!

HE KNOW HOW TO IT....HE LOVE DOING IT......HE FEELS PROUD TO IT AND HE KNOW THE VALUE OF DOING IT!!


YES HE IS A VERY GOOD SINGER AND ACTUALLY TEACHER/LEADER OF PRAISE AND WORSHIP...HE DO VERY WELL IN PIANO AND GUITOR!
HE IS A VERY GOOD MC AND LINGUISTIC EXPERT!

HE IS MY BEST STAND UP COMEDIAN AND ACTUALLY HE IS A MEMBER OF LAUGH AGAIN CONCERT SERIES!

 RICHARD CHIDUNDO MINISTERING TO STUDENTS BY SINGING AFTER PREACHING
 RICHARD CHIDUNDO MINISTRING TO SECONDARY STUDENTS!
STUDENTS SHOWING THEIR TALENTS AFTER WORD OF GOD

HERE ARE SOME POEMS AS COPIED FROM HIS FACEBOOK WALL!
AUGUST 23
"hayawi hayawi sasa yamekuwa..watu wameseeeeeeeeeema we, ooh rich kuna tatizo gani...mbona uko peke yako me nawaangaliaga tu..oh utaoa lini nawaangaliaga tu...waliooa nao wananikumbushia...ooh me nawaangaliaga tu..sasa hayawi hayawi yamekuwa ....MUngu kaona siyo vema niwe peke yangu ...akanipatia mtu wa muhimu sana yaani ..nikichoka napewa pole, nikihisi kuumia pole....nikisafiri nikirudi pole....sikohoi pole...hayawi hayawi sasa yamekuwa... japo hatufanani lakini wewe rafiki yangu unafaa...Mungu akubariki mno kwa kuwa rafiki mwema hapa face book...yani wewe unayesoma post hii.. Nakupenda"

RICHARD CHIDUNDO  LEADING A WORSHIP WITH MBEYA MASS CHOIR

 IT IS VERY GOOD WHEN PEOPLE COME TO DANCE BEFORE THE LORD!
EV. RICHARD CHIDUNDO

SEPTEMBER 9
"Rich kapatikana ,,, jamani nimepatwa mie, sasa mizunguko yangu itaisha, maana yuko wakunituliza,...siamini kwamba vimacho vyangu vimegoma kuangalia pengine...ha we mupenzi mbona nilichelewa kukuona, nimehangaika weeeeeeeee, na wengine, wamenipiga kibuti, wengine wamenikashifu, eee ninaorodha ndefu ya wapenzi hapa, kama kijiji, lakini wewe umezidi wote, eti huwezi kuniacha nitembee peke yangu, na jicho lako hunitazama kila mahali, naringaje..kumbe ulikuwa unasubiria siku ntakayojieleza mwenyewe,, ni mpole wewe, na maneno yangu mengi mpaka najistukia, saizi naanza kuongea kwa point..ama kweli heri kuwa wawili kuliko mmoja...sasa naomba nijieleze vile umenichanganya na luv yako, vile umenifanya niwe mdogo, ee bwana ee kiukweli me nakupenda saaaana..ndiyo maana ninaujasiri wa kukuelezea mbele za watu, naamini sana ahadi zako si kama za wengine waliopita, sure we ni mkweli, kila usemacho nikweli, nakukubali, nataka uwe wangu daima, nsije nikasahau kukupa siri ya Moyo wangu,,,Serious yani Jesus I LOVE YOU SO MUUUUUUUCH>>>>>"


 THE JOY OF THIS LIFE IS TO DO THE WILL OF THE HEAVENLY FATHER!

 BY ANY MEANS....THE GOSPEL OF JESUS CHRIST MUST BE PREACHED!!
INTELLECTUALS IN OVERNIGHT IN MBEYA

 WE ARE DOING A LOT IN THIS COUNTRY AND STILL WE HAVE A LOT TO DO!
WHEN YOU NEED AN MC IN A CONFERENCE, CAMP, CRUSADE OR SOCIAL FUNCTION LIKE WEEDING, SENDOFF AND OTHERS.....WHEN YOU NEED A TEACHER OF PRAISE AND WORSHIP, WHEN YOU NEED AN INTERPRETER IN ANY EVENT THAT HAS THAT NEED AND WHEN YOU HEAR ANYTHING ABOUT LAUGH AGAIN CONCERT SERIES EVENTS, THEN CHOOSE TO CONSIDER US AS YOUR PATNERS!

NOW RICHARD CHIDUNDO HAS ORGANIZED A MISSION IN KAHAMA, SHINYANGA FOR A WEEK WHERE I BELIEVE A VAST OF SOULS ARE GOING TO BE WINNED!

YOU CAN EVEN SUPPORT HIM AND THE TEAM BY PRAYING FOR THEM AND CONTRIBUTE A BIT TO SUPPORT THEM!!

RICHARD CHIDUNDO
+255 713 802107

Imeandikwa na
+255 713 883797
King Chavala(MC)





 

EV. RICHARD CHIDUNDO NA MASHAIRI KWA MPENZI WAKE!!!!

kanibembelezaaaaaaaa weeeeeeeeee!!!! me nimekubali bana....sasa angalau na mimi naweza tangazia uma kwamba I am in an OPEN and Clear, Unbrekable, unstopable RElationship.....asanteni kwa maombi yenu watumishi...nitakuwa nikiwajuza hatua kwa hatua juu ya yale ynayoendelea...sasa mtaniheshimu tu...na kama we ni singo aisee unakosa mambo...Jifunzeni kwa walio na watu wanaowapenda kwa Dhati....huyu wa sasa najutaa nimechelewa kumfahamu mapema...hivi mpenzi ungeniambiaga tangia mwanzo mbona ingekukubalia tu jamani!!! halafu na mimi nilikuwaga naogopa kukwambia kama Nakupenda...nilihisi ungenidharau sana Mpenzi..maana nilihisi unaviwango fulani unataka..lakini kumbe hata mie niliyejiona chini..khaaa umenikubali..ama kweli hapana chezea mapenzi..kumbe bora tu ningekwambia kipindi kile aisee...sasa ona watu wamenicheeeeeka, oooh mara richie ana roho ya kukataliwa, mara mizimu ya mababu, maagano ya kutopata kibali kwa wapenzi...mbona wewe sijakufuata umekuja mwenyewe..tena ukajieleza navyonipenda...ningejua nisingemwambia mtu eti nampenda...maana nimedharaulika ujue mpenzi...

sasa we umejileta Mwenyewe, halafu bonge la shopping umenifanyia, piga pamba moja hatari yaani...afu sio mlimani city maana haipatikani..cheki penzi lako umeliweka moyoni mwangu, saizi me naropoka bwana...Nakukubali mno...saizi jipangeni tu kupiga makofi na vigelegele...hapo wenye wivu wote waanze kuabudu...maana hana mpango wa kuniacha...sitaki mwingine saizi..ohoooo..maana hamchelewagi..nshapendwa ...na ndoa sitangazii hapa bongo maana hawachelewi kutoa sijui kikwazo ndoa isifungike....sema mtakuwa mnajisumbua maana mwenyewe ni bonge la mbabe, hela anayo, nguvu anazo akili ndo usiseme...hamtuwezi...sihitaji Gobole wala Binduki, hata Mzinga.....wa nini ulinzi wa nini..KAJA mwenyewe.. yuko fiti aisee usithubutu chezeya...usiku na lala tuli mchana namsifu..MPENZI UMEWAPITA WOTE>>>kwani ulikuwaga wapi? nimechelewa kukufahamu...

mapenzi matamu niwapo nawe Mpenzi.....wengine wote piga chini...achana nao..
ntawajuza kama nilivyosema hatua baada ya hatua lakini sasa niropoke tu I LUV YOU MY DARLING, YOU ARE SO SWEEEEEEEEEEEEEEET, thanks for luving me honey..i receive your Love JESUS!!!!!! MMWAaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
FROM; https://www.facebook.com/richard.chidundo?hc_location=stream

Friday, September 13, 2013

NANI AJUAYE SIRI YA UPENDO?

  “Nakupenda kutoka moyoni mwangu”….ni sentensi maarufu katika ulimwengu wa mapenzi. Inaweza kuwa inasemwa kwa kumlizisha msikilizaji wa maneno hayo au ikiwa na maana kubwa kwa msemaji wa maneno hayo. Nani ajuaye ukweli wa maneno hayo ni siri ya moyo.
Mara nyingi huwa nasema hakuna asiyependa kupendwa. Ila sina hakika kama ni wote tunapenda kupenda. Katika utafiti wangu mdogo kuhusu maisha nimegundua mada kubwa miongoni mwa jamii ni mapenzi na muziki. 

Watu wanatumia nguvu nyingi kutafuta pesa ili tu wapate vitu wanavyovipenda. Wapate wasichana warembo kama wake zao, wavulana watanashati kama waume zao, nyumba wanayoipenda, magari wanayoyapenda, wakae sehemu au mahali wanapopapenda na kujiburudisha moyo kwa nyimbo au muziki wanaoupenda na miziki mingi imejaa maneno ya sifa na mapenzi.

Nami pia nikiumbe, napumua kama wewe,
Kukupa huu ujumbe, nimeamua mwenyewe,
Hivyo usifumbefumbe, nikosapo nikosowe,
Ila kukupenda wewe, si chanzo cha kunitesa.

Kwasababu hiyo watu wenye pesa hutafuta upendo wa kweli na watu masikini hutafuta pesa ili wakatafute upendo wa kweli. Burudani inaanzia hapo wanapokutana anayetafuta upendo wa kweli na anayetafuta pesa ili akatafute upendo wa kweli.
Unaweza kuwa umejiuliza kati ya watu wenye pesa na watu wenye uwezo wa kawaida na maskini ni watu gani hutumia nguvu nyingi kutafuta kupendwa. Nimekwisha kusema kila mtu anapenda kupendwa, lakini matajiri na watu wenye uwezo mkubwa hutumia nguvu nyingi sana kutafuta kupendwa, pia watu wahali ya kawaida wao hawatumii nguvu nyingi ukilinganisha na matajiri na wenye uwezo mkubwa. Tukirudi kwa masikini wao hutumia nguvu kidogo sana ili wapendwe.
Je unahitaji uwe na uwezo mkubwa au tajiri ili upendwe?
Je unahitaji kuwa mtu mwenye uwezo wa kawaida ili upendwe?
Je unahitaji kuwa masikini ili upendwe?
Endelea kufwatilia mada hii nzuri naya kusisimua wiki ijayo……
kwa maswali, maoni,mapendekezo na ushauri niandikie kupitia barua pepe makwayae07@gmail.com