Saturday, August 31, 2013

RAIS WA JAMHURI WA TANZANIA, DK JAKAYA KIKWETE AMLILIA DK MOSES KULOLA!!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Kiongozi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Dkt Moses Kulola ambaye ameaga dunia asubuhi ya Alhamisi, Agosti 29, 2013 katika Hospitali ya AMI iliyoko Masaki mjini Dar Es Salaam akiwa na umri wa miaka 85, yaani alizaliwa 1928-2013!


 Kiongozi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT)  Marehemu Askofu Mkuu Moses Kulowa.
Rais kikwete ameelezea mshtuko na huzuni yake katika Salamu za Rambirambi alizomtumia Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Bwana Brown Mwakipesile kufuatia kifo cha Askofu Mkuu Kulowa. 
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za kifo cha Mtumishi wa Mungu wa muda mrefu na Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Marehemu Moses Kulola kutokana na maradhi yaliyomfanya wakati fulani apelekwe hadi India kupatiwa matibabu” amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete amesema alimfahamu Marehemu Askofu Moses Kulola kwa miaka mingi wakati wa enzi za uhai wake, kama Mtumishi Hodari wa Kiroho aliyejitoa vilivyo katika kuwahudumia Waumini wa Kanisa lake ambapo mahubiri yake yametoa mchango mkubwa katika kuimarisha imani za Waumini wake na kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu.
Aidha Rais Kikwete amesema kifo cha Askofu Mkuu, Moses Kulola kimeacha pengo kubwa siyo tu kwa Waumini wa Kanisa lake hapa nchini, bali pia miongoni mwa wapenda amani kote nchini na kwingineko duniani kwa vile enzi za uhai wake, Marehemu aliweza kufikisha ujumbe muhimu wa kiimani kupitia mahubiri yake kwa watu wa mataifa mbalimbali ndani na nje ya  Bara la Afrika.
“Kwa niaba yangu mwenyewe na Serikali ninayoingoza, ninakutumia wewe Katibu Mkuu wa Kanisa la Evangelical Assembies of God Tanzania, Bwana Brown Mwakipesile na Waumini wote wa Kanisa hilo Salamu za Rambirambi  kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza Kiongozi muhimu wa Kiroho.  Ninawajulisha kuwa niko nanyi katika wakati huu mgumu kwa sababu msiba wenu ni msiba wetu pia. Sala na mioyo yetu iko nanyi wakati wa maombolezo ya kifo cha Kiongozi huyo shupavu wa dini. Nawaomba wote muwe wavumilivu na wenye subira kwani yote ni Mapenzi yake Mola”, amesema Rais Kikwete.

“Vilevile kupitia kwako, naomba unifikishie Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu, Askofu Mkuu, Moses Kulola kwa kumpoteza Baba, Kiongozi Shupavu na Mhimili wa familia.  Natambua fika kwamba hiki ni kipindi kigumu sana kwao cha maombolezo.  Natambua machungu yenu wakati huu na naungana nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke peponi roho ya Marehemu Moses Kulowa. Amina.”

Mazishi ya Marehemu, Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) yatafanyika mjini Mwanza Jumatano ijayo tarehe 4 Septemba, 2013.  Heshima za mwisho kwa mwili wa Kiongozi huyo zimetolewa leo Jumamosi tarehe 31 Agosti, 2013 katika Kanisa la EAGT karibu na Hospitali ya Temeke kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni!
Kwa hisani kubwa ya Christian Bloggers network .

Thursday, August 15, 2013

....KWA MARA NYINGINE TENA WAIMBAJI WOTE WA INJILI MNAKARIBISHWA...."GOSPEL SINGERS' BREAKFAST".....Episode 5!!

Hello Shalom!
HABARI NJEMA KWA WAIMBAJI WOTE WA NYIMBO ZA INJILI!
Kwa mara ya TANO;<Chavala Ideas Platform> kupitia Blog ya Kikristo Gospel Standard Base(http://gospelstandardbase.blogspot.com/) inakukaribisha kwenye Chai Maalum ya Asubuhi ya Waimbaji wote wa Nyimbo za injili (TANZANIA GOSPEL SINGERS' BREAKFAST Episode 5), itakayonywewa JUMAMOSI HII (17th August, 2013);Kuanzia 2:30-6:30mchana pale Victory Christian Centre (VCC)-Victoria,barabara ya bagamoyo...Na mara hii tutakuwa na Walimu na Watumishi Kadhaa kama vile Samuel Sasali, Prosper Alfred Mwakitalima,King Chavala-MC na wengineo katika Panel kuzungumzia "NAMNA YA KUKUA KIROHO NA KUSTAWI KIHUDUMA"....Chai sio bure ingawa HAKUNA KIINGILIO.....Ikiwa wewe ni muimbaji wa kwaya,band,kikundi,mwimbaji binafsi,timu ya kusifu na kuabudu ya kanisani,ikiwa unaimba Hip hop,RnB,Rock ama Gospel Reggae basi hii ni nafasi yako,NJOO UJIFUNZE NA UJUMUIKE NA WENZAKO!
......HATA KAMA UNA KIPAJI,FEDHA NA JINA KIASI GANI,BADO IMEKUPASA KUTAFUTA SHULE ZAIDI ILI UWE STADI!!!!
Kwa maelezo zaidi +255 713 883 797 au Tembelea Http://gospelstandardbase.blogspot.com/ au Blog yeyote ile ya Kikristo!!!!
MUNGU AKUBARIKI WEWE UTAKAYEKUJA BILA KUKOSA NA KUWAHI NI MUHIMU SANA!!


KWA MAELEZO;
+255 713 883 797
E-mail; lacs.project@gmail.com
King Chavala-MC

Sunday, August 11, 2013

KUTOKA MADHABAHUNI......"BAADA YA KUSUBIRIA....HATIMAYE UTAMILIKI NA KUBARIKIWA!!"

SHALOM!
NAAMINI UNA JUMAPILI NJEMA HATA LEO!
SIKIA NENO LA BWANA TOKA MADHABAHUNI KWAKE KAMA VILE LINVYONENWA NA MCHUNGAJI WA VICTORY CHRISTIAN CENTRE (VCCT), MBEZI BEACH A, DAR ES SALAAM; DKT HURUMA NKONE!!


MAANDIKO; JOSHUA 1:29;11:23

Bwana Yesu asifiwe sana!
Leo ibaada yetu iko moja kwa moja kupitia Redio Wapo FM (98.1), na tutaendelea kuwa hewani moja kwa moja kupitia redio Wapo kila jumapili ya kwanza ya mwezi!

Habari hii inawahusu wana waisraeli wakiwa safarini kwenda nchi ya Ahadi chini ya Uongozi wa Joshua baada ya Muda wa Musa kuisha.
Na hapa Joshua alikuwa akipewa maagizo na mazingatio ya muhimu...Itakuwa mtakapotia miguu yenu kukanyaga nchi ile itakuwa mikononi mwenu, na muwe hodari na moyo wa ushujaa kwa maana ni haki yenu.

Wana waisraeli wakiwa na Joshua walishuhudia miujiza mingi pia ukiwapo ule wa Maji ya mto Yordni kugawanyika na wao kuvuka naam baada ya hapo Joshua na wanawaisraeli walianza kwa kuteka Yeriko na miji mingine mitatu mikubwa ya kati na kwa gia hii walikuwa wana nguvu ya kutosha kuendele kuichukua nchi nzima maana walikuwa wana mkakati bora.

NINI MUHIMU MAISHANI MWAKO SASA;
Ulipookoka umefanikiwa kuingia nchi ya ahadi; lakini bado ipo kazi ya kuendelea kuteka na kuchukua baraka zako...maana hapo kwanza kabl hujaokoka vilikuwa vinamilikiwa na shetani. Ni kweli umeweza kutikisa kuta za Yeriko na zimebomoka....naam usiishie hapo unapaswa kuendelea kuteka na kuteka mpaka hapo utakapomiliki nchi yako nzima...naamanisha ulimwengu wa wokovu wako.

 Lazima wakristo tubadilike...tuache kuamini maombi tu katika kila jambo bila kufanya jambo lingine lolote...kwa mfano hauwezi ukaomba upandishwe Cheo kazini na hali unaendelea kuchelewa kazini na kufanya uzembe mwingine haiwezekani....kama ukitimiza wajibu wako na kufanya yote yakupasayo kw haki na kwa bidiii, kwa hakika utapokea tu toka kwa Bwana...maana maandiko yanasema....KAMA MKITII MTAKULA MEMA YA NCHI!

Kumbuka hatuokoki ili tupate vitu fulani kwa Bwana kama vile fedha, majumba, waume na wake ama watoto, ila tunaokoka kwasababu tumechagu kumpenda Bwana na ukishaokoka na kuwa mwaminifu basi vyote hivyo unavyovistahili vinakujia kwa kujaa na kusukwa sukwa.

UJUMBE KWA VIJANA;
Lazima ujifunze kutulia na kusubiri,haiwezekani utoke chuo leo na utaka uendeshe Range Rover,acha kutamani kila kitu...ikiwa unavistahili basi ujue kwa hakika muda ukifika lazima utamiliki tu...vinginevyo utaumia sana ukitaka vitu visivyo saizi yako.

Natamani kama ungemtukuza Bwana katika maisha yako kwa namna ambayo watu watajiuliza wewe ni mtoto wa nani,maana ulimwengu umezoea watu wamnaopenya ni wale wenye watu wakubwa serikalini....Baraka yako ipo maana Mkono wa Mungu uko juu yako....na lazima ujue jambo moja kuwa penye Vita yako ndio penye baraka yako!

SEMA SALA HII KWA IMANI;
EEH BWAN YESU, NINAKUSHUKURU KWA NENO LAKO NA MTUMISHI WAKO, NIMESIKIA NA NIMEAMINI,NAAM NATAMANI NENO HILI LIWE HALISI MAISHANI MWANGU,NISAIDIE NIKUSIKIE KWA KINA ILI NIJUE NINI KINACHONIPASA KUFANYA KILA SIKU, MAOMBI YANGU LEO NI KUWA BWANA UNISAIDIE KILA WAKATI KUKUMBUKA KUWA VITA NI YAKO NA SIO YANGU,NIPE NEEMA YA KUWA NA SUBIRA NA KUSUBIRI BARAK YANGU, NISAIDIE KUITUMIA AKILI YANGU NA UTASHI ULIONIPA ILI NISIZEMBEE KIMKAKATI, AHSANTE YESU KWA MAANA KILA HATUA UTAKUWA NAMI,AHSANTE YESU KWA KUNISIKIA, KATIKA JINA LA YESU KRISTO,AMEN!!!

MUNGU ATUSAIDIE TUNAPOENDELEA KULITAFAKARI NENO HILI KUWA KILA MAHALI AMBAPO BWANA AMETUPA KUKANYAGA KATIKA ULIMWENGU W ROHO NA WA MWILI BASI HAPO AMETUPA KUMILIKI,NAAM UTAPATA VYOTE UNAVYOVISTAHILI KAMA UKIWA NA IMANI SAHIHI NA PIA UJUE VITA SIO YAKO BALI VITA NI YA BWANA, AMEN!

Mungu awabariki sana!!

Imeandikwa na
King Chavala MC
+255 713 883797

Thursday, August 8, 2013

JUMAPILI HII TUNAKUTANA KWA IBAADA MOJA TU...KUSIFU NA KUABUDU TU!!

VIJANA,WABABA NA WAMAMA KUTOKA PANDE ZOTE ZA JIJI LA DAR ES SALAAM NJOONI PAMOJA TUMSIFU NA KUMWABUDU BWANA JUMAPILI HII PAKE TAG MAGOMENI, HII NI BURE NA SI YA KUKOSA KWA MTU YEYOTE!!!
UKIPATA TAARIFA HIZI MTAARIFU NA MWENZAKO!!!

Wednesday, August 7, 2013

JITAMBUE..."CEREMONY AT THE BATTLE FIELD"!!!!





ENDELEA.......

BAHARI YA KIOO....MFAHAMU "EMMANUEL MGALLAH",MWIMBAJI WA INJILI ANAYEJITUMA KIPEKEE SANA!!

Bwana Yesu Asifiwe sana!
Natumai kila mmoja yuko vizuri!
Mimi binafsi ni mzima sana na namtukuza Jehova kwa upendeleo na zawadi ya uhai, sijui ni nini kesho imeshikilia kwa ajili yangu, lakini Ninamjua anayeimiliki Kesho, naam tunafahamiana vema na kwasababu yeye anaishi,Lazima nitaiona kesho.

Leo Baharini nimemwona kijana huyu mtumishi wa Bwana ambaye ana moyo wa kipekee wa kujituma katika Utumishi na katika kazi zake binafsi.

Leo ninamzungumzia Mtumishi EMMANUEL MGALLAH, Mwenyeji wa Igamba, Mbozi Mbeya, Mnyiha kwa kabila; mwimbaji wa nyimbo za injili aliweka makazi yake Jijini Dar es salaam.

Karibuni Bahari ya Kioo ya Gospel Standard Base Blog ilifanya mahojiano nae kwa kina ili kutaka kujua mengi yamhusuyo kijana huyo, na kwa hakika hii ndio habari kuhusu Emmanuel Mgallah;

HISTORIA KWA UFUPI;
Emmanuel ni mzaliwa wa Igamba, Mbozi,Mbeya...alianza Shule ya msingi pale TANDALE UZURI, shule ambayo alisoma mpaka darasa la sita na kwenda kumalizia darasa la saba IGAMBA SHULE YA MSINGI iliyo mbozi Mbeya, na hapo akajiunga ya shule ya Sekondari ya Mbozi Mission, shule inayomilikiwa na Kanisa la Moravian,

Emmanuel hakufanikiwa kumaliza kidato cha nne katika shule hiyo, hivyo alihamia Mbezi High School iliyoko jijini Dar es salaam na kumalizia kidato cha nne hapo, na baadae akajiunga na THE CONTEMPORARLY COLLEGE iliyo Kinondoni, mahali ambapo alifanya kozi ya lugha kwa mwaka mmoja na kisha kujiunga na EAST AFRIKA TRAINING COLLEGE mahali ambapo aliendelea kusoma Lugha pamoja na Kompyuta na kisha akafanya kozi ya Ujasiriamali kwa mwaka mmoja.

KAZI;
Mwaka 2009 alipata kazi kama Afisa Mikopo (Credit Officer) wa SIMKA, iliyo magomeni usalama.

Mwaka 2012 alibadili kazi na kuanza kufanya na General Credit Company mahali ambapo alifanya mpaka Jan 2013, wakati alipoamua kujiudhuru na kuanza kufanya kazi zake binafsi za kijasiriamali.

Emmanuel ana miliki na kuendesha Biashara yake ya Bodaboda, anafanya kazi kama Dereva wa gari ya shule Libermenn Pre & Primary, lakini pia anafanya kazi za ushereheshaji (MC),

hivyo maisha yao yanaenda hivyo....na mke wa Emmanuel au Mama Jonathan yeye ni nesi katika Dispensary moja pale manzese, hivyo nae anamsaidia mumewe kustawi huku wakimtumikia Mungu katika ndoa YAO AMBAYO ILIFUNGWA MWAKA 2011
 FAMILIA;
Emmanuel ameoa mke mmoja na ana mtoto aitwaye Jonathan na kwasasa wanaishi kwafuraha yeye na mke wake maeneo ya Kimara,kinondoni, Dar es salaam.


HISTORIA YA UIMBAJI YA EMMANUEL;

Habari ya Emmanuel kuimba  ilianzia Sunday school na kisha akajiunga na kwaya ya kanisa la moravian-Mbozi mission na hapo akajiunga na kwaya nyingine iitwayo Emmanuel ya hapo hapo mbozi mission moravian na baada ya kuja jijini Dar es salaam alijiunga na Faith kwaya ya magomeni moravian iliyo chini ya Mwenyekiti Paulo Mlawa kwa sasa na akiwa ndani ya kwaya hiyo ndio akaanza michakato ya kuimba mwenyewe.

Alifanikiwa kurekodi album yake ya kwanza  mwaka 2011 pale Magic Star Studio chini ya fundi Ayubu pale Sinza na Kisha kufanya Video ya album hiyo mwaka 2012, chini ya Muongozaji Gilbert Mgalama.

Albamu hiyo ina nyimbo nane na inaitwa "HABARI NJEMA"....Habari njema ni moja ya nyimbo zinazosikika kwenye vyombo vya habari pamoja na "Kwanini Uteseke" na "Tawala kwa maombi"

Emmanuel alifanikiwa kufanya Uzinduzi wa Album ya sauti Desemba 23, 2012 na mpaka sasa hajampata msambazaji, hivyo anasambaza mwenyewe.

NINI MALENGO YA EMMANUEL HAPO MBELENI??
Emmanuel ni mwimbaji wenye shauku kubwa sana ya kukua na kwa jinsi ninavyomuona, nauona uwezo mkubwa sana ndani yake na atang'aa sana kama akitulia na Mungu sawasawa.. lakini ni maneno ambayo yeye mwenyewe aliyasema;


"....Ninakusudia kuwa na Studio na zaidi nategemea kusaidia waimbaji wadogo wadogo wanaonyanyaswa kwa kukosa fedha na zaidi natamani kuwaandaa wahubiri wa injili"

......Nimetembea mikoa zaidi ya mitano kihuduma na nakusudia kutembea Tanzania nzima kadri Mungu atakavyoniwezesha.

Imekuwa ni kawaida kwa Waimbaji wengi wa injili kuruka ruka tu bila kuwa na walezi wao wa kiroho, na nilipomuuliza ndugu kuhusu kijana huyu, haya ndio alimalizia kwa kuyasema;



EMMANUEL UNALELEWA NA NANI?
".....Mimi nalelewa na Mchungaji NOEL MWAKALINGA pale Magomeni Moravian na hapo ndio ninaposali na kuendelea kuimba kwaya ya Faith ya kanisani hapo.....natamani sana kufika mbali, nayafurahia sana unayoyafanya wewe (akimaanisha Mimi King Chavala) na wewe kwa sasa ndio mtu ninayejifunza kwake na natamani kuwa kama wewe katika mengi ufanyayo....nakuombea Mungu akusaidie ili uimarike zaidi na zaidi katika kusaidia Tasnia ya Uimbaji wa injili Tanzania na hapo baadae uwe msambazaji maana wewe unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko hawa wa sasa maana hawahui hasa uzito injili,Ahsante sana na Mungu akubariki.!"

CHANGAMOTO;
Emmanuel alisema Changamoto zinazomkabili ni Gharama kubwa ya kufanya kazi na vyombo vya habari na pia gharama kubwa za Studio.


UJUMBE WA EMMANUEL KWA WAIMBAJI WOTE;
"..Watu waliotangulia wasidhani kama wengine hawawezi kufanya au kufika mahali walipo, hivyo natamani kuwepo na umoja kati yetu na hapo ndio tyunaweza kufika mbali zaidi...na sio umoja wa siasa tu bali Kama Kristo na Mungu walivyokuwa na Umoja."

BAHARI YA KIOO haina la ziada zaidi ya kumshukuru Emmanuel Kwa kufunguka na kuamua kufahamika kwa kina, naam naamini kila mtu sasa atakuwa anamfahamu kwa kina na mtumishi huyu anasema yuko tayari kufanya kazi na mtu,kanisa na huduma yoyote popote....yamkini unamwitaji kama Mshauri wa namna ya kutumia mikopo midogo midogo, au kuhusu Bodaboda, ama kumwalika Kuhudumu kwa Kuimba, kufundisha ama kusherehesha, basi haya ndio mawasiliano yake;

EMMANUEL MGALLAH
+255 713 635 898 AU +255 769 070 458
E-mail; emmanuelmgallah@yahoo.com
Facebook; Emmanuel Mgallah

BASI TUNAWATAKIA MAFANIKIO MEMA WOTE MTAKAOSHIRIKIANA NA EMMANUEL KATIKA KUINEZA INJILI YA BWANA WETU YESU KRISTO,AMEN!!

Na King Chavala-MC
Hotline; +255 713 883 797
(c)2013- Bahari ya Kioo ya GoStaBa

Tuesday, August 6, 2013

MSAADA WA DHARULA WA CHAKULA UNAHITAJIKA KWA WOTOTO YATIMA WA HOCET!!!!

 
SHALOM!
HABARI ZENU WAPENDWA!!
NINAAMINI MNA MOYO WA UPENDO, TENA WA KUWAJALI WENGINE KULIKO NINYI, NA HATA ZAIDI BIBLIA INASEMA UPENDO WA KWELI NI ULE WA KUWAPENDA WENGINE ZAIDI.
*****HANANASIFU ORPHANAGE CENTRE (HOCET)....HAWANA CHAKULA KABISAAAAA NA WEWE NA MIMI PEKEE NDIO TUNAWEZA KUWALISHA KWA SIKU 120, KABLA HAWAJAANZA KUJITEGEMEA****
LEO NINALO OMBI MAALUM KWENU, NI MUHIMU SANA SANA....KUNA KITUO KIMOJA CHA KULELEA WATOTO YATIMA (WATOTO WA MUNGU), KITUO KINACHOENDESHWA NA WATU TU WALIOJITOLEA, NA HAPO AWALI KILIKUWAQ KINAFADHILIWA NA WAZUNGU FULANI, LAKINI BAADA YA KUONA WATOTO HAO WAMEKAZANA NA MUNGU NA HAO WAZUNGU (WAFADHILI) WAKAWEKA MASHARTI, ETI KAMA WAKITAKA WAENDELEE KUPOKEA MISAADA YAO BASI WAACHANE NA HAYO MAMBO YA YESU YESU....NA KWA KUWA HAKUNA BABA MWINGINE ZAIDI YA MBINGUNI NA HAKUNA  NAMNA BINADAMU ANAWEZA KUISHI KWA MISAADA YA BINADAMU MWINGINE BAADA YA KUMKANA MUNGU WA KWELI.
 
SASA WATOTO HAO WAKO KWENYE ENEO LAO LA SHULE WANASOMA NA WANAYO MIRADI AMBAYO BADO HAIJAANZA KULETA FAIDA ILI WAWEZE KUJIENDESHA WENYEWE, NAHIYO ITAKUWA HIVYO TU BAADA YA MIEZI MITATU AU MINNE KUANZAIA SASA.
WATOTO HAWA KWA SASA HAWANA CHAKULA KABISA, NA HATA LEO WAMEKULA KWA MSAADA WA KIJANA MMOJA ALIJITOLEA YEYE BINAFSI NA FAMILIA YAKE....MBALI NA GHARAMA NYINGINE ZA UENDESHAJI KAMA MISHAHARA/POSHO ZA WALIMU;
************************************************************************************************
KITUO HIKI KINATUMIA UNGA KILO 30, MAHARAGE KILO 14 NA SUKARI KILO 5....NA IKIWA NI WALI,BASI HUHITAJIKA KILO 30 ZA MCHELE KWA MLO MMOJA....NA PIA UNAWEZA KUCHANGIA MAFUTA NA FEDHA KWA AJILI YA VITU VINGINE VINAVYOWEZA KUHITAJIKA.
************************************************************************************************

NINAAMINI KWA MSAADA WA WATANZANIA WOTE WENYE MAPENZI MEMA NA WATOTO WA KITANZANIA, WATOTO HAWA HAWATAKOSA CHAKULA KWA SIKU HIZI 120 ZA MPITO KABLA HAWAJAANZA KUJITEGEMEA WENYEWE, SIO LAZIMA ULETE MSAADA MKUBWA SANA, LAKINI NAAMINI UNAWEZA UKAJITOLEA CHAKULA KIASI JAPO KWA SIKU MOJA TU KAMA SIO TATU, YAWEZA KUWA WEWE BINAFSI AU KAMPUNI AU FAMILIA AU KANISA, LAKINI NINACHOKIAMINI NI KUWA KAMA KWELI TUNAAMINISHA KUMPENDA MUNGU NA KUWAPENDA WATOTO WATANZANIA TENA WANAOLELEWA KATIKA MALEZI YA KIMUNGU BASI LAZIMA WATOTO HAWA WATAISHI BILA HOFU YA CHAKULA KWA SIMU HIZI 120, NA KWA HAKIKA BWANA ATAKUBARIKI SAWASAWA NA IMANI YAKO KWAKE
YAK 1:27 "....DINI ILIYO SAFI ISIYO NA TAKA MBELE ZA MUNGUBABA NI HII, KUWATAZAMA WAJANE NA YATIMA KATIKA DHIKI YAO NA KUJILINDA NA DUNIA PASIPO NA MAWAA"
 
MSAADA HUO UNAHITAJIKA SANA SANA, NAAM KWA NAMNA YOYOTE ILE UNAYOWEZA KUCHANGIA BASI USISITE,FANYA HIVYO...SADAKA YAKO YA KUWALISHA WATOTO HAWA HAITASAHAULIKA HATA KIDOGO, UNAWEZA KULETA MCHANGO WAKO WA CHAKULA PALE OFISI ZA NIIM COMPUTERS, MOROCO HOTEL AU UKATUMA MCHANGO WAKO WA FEDHA KWA NJIA YA SIMU, NAAM KWA MAULIZO ZAIDI 
TAFADHALI WASILIANA NA WASIMAMIZI NA WARATIBU WA ZOEZI HILI KWA NO.
0713 26 1425 na 0754 527955, pia 0783 757051
KWA NIABA YA WASIMAMIZI WA KITUO HIKI NINAWASHUKURU HATA KABLA HAMJAFANYA JAMBO LOLOTE MAANA NAAMINI UMEGUSWA NA UKO TAYARI SASA KUWASAIDIA WATOTO HAWA...KAMA TUNAWEZA KUCHANGIA SHEREHE ZA HARUSI, NAFIKIRI HATMA YA WATOTO HAWA NI ZAIDI,MUNGU AKUBARIKI UNAPOMSHIRIKISHA NA MWENZAKO!!
 
Imeandikwa na
KING CHAVALA MC
KWA UDHAMINI MKUBWA WA CHAVALA IDEAS PLATFORM.

Saturday, August 3, 2013

KUTOKA MADHABAHUNI LEO.......NGUVU YA MATOKEO YA UKIRI WAKO!

Shalom!
Naamini uko vizuri na jumapili hii ni nzuri kwako,amen!
Ubarikiwe na uzidi kubarikiwa sawasawa na neno la Mungu lisemavyo.
Leo neno kutoka madhabahuni,linatoka madhabahu ya TAG CAPITAL CHRISTIAN CENTRE (CCC) DODOMA kama linavyonenwa na Baba Askofu Mch SAMSON MKUYU
ASKOFU MCH.SAMSON MKUYU WA TCCC, DODOMA


Neno 
  Mithali 23:7 .....Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo
  Warumi 10:9......kwa kinywa mtu hukiri na kwa moyo mtu huamini......
Waefeso 3:20....
Wagalatia 5:9....

Somo; NGUVU YA MATOKEO YA UKIRI

Maisha yetu yenye matokeo ya kuwafanya wengine kupata tafsiri ya maisha mazuri yanategemea sana na ukiri wetu.
Maandiko yanasema aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, hii inamaanisha vile ulivyoujaza moyo wako navyo,kwa maana nyingine yale unayoyawaza na kuyafikiri kila wakati ndio hayo yanaongoza na ukiri wake wake kila siku.
Ukijaza moyo wako na uchafu,udhaifu na uzembe basi kila wakati utalaumu na kunung'unika na kukiri udhaifu maishani mwako na kama ukijaza moyo wako na Neno la Mungu na habari njema basi ukiri wako utakuwa ni kushinda na kushinda kila leo.

UKIRI HUZAA IMANI
Ukisema mimi ni masikini na akili yako inasikia na kudaka hiyo na wanahusika na hilo pia wanasikia na wanakuwa na nafasi ya kulifanyia kazi ili vile ulivyokiri iwe imani na iwe kweli.
Lakini ukisema mimi ni mshindi basi na akili yako husikia na kudaka hivyo na wote wanaohusika na hali hiyo lazima imani yako iwe hivyo.

Sikia hii ....KWA KINYWA MTU HUKIRI NA KWA MOYO MTU HUAMINI
Ukiri wa kinywa chako una nguvu sana na ndio hufanya moyo wako kupata imani ya yale uliokiri.

MIMI ZAMANI NILIMWAMINI BWANA KWA MAMBO MAKUBWA NA BADO NAENDELEA KUMWAMINI,KILA MWAKA AHADI YANGU YA KUMTOLEA BWANA INAENDA IKIPANDA,KUNA WAKATI TULIKUWA TUNAENDA KAMBI YA MAOMBI MAHALI FULANI NA ILITUPASA KUBEBA VYANDARUA,LAKINI MIMI NILIMWAMBIA BWANA (nilikiri na kuamini) MBU YEYOTE ATAKANIUMA AONYE UCHUNGU NA HATA KAMA NA WADUDU WA MALERIA WASINIPATE.....NA ILIKUWA HIVYO NA BADO NAMWAMINI BWANA HATA LEO.

MAMBO YA MUHIMU;
1. Chunga sana kinywa chako na linda moyo wako
2. Jifunze kutamka yale uyaamiyo na usindi uutakao,hata kama hali yako ya sasa haiendani na yale uyatazamiayo.
Usiache kusema....NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU!
3. Unaweza kuwatania watu na ndoto zao lakini usifany utani na Bwana maana Mungu hataniwi
4. Na kila unapokiri kumbuka unatangaza vita hivyo usiruhusu shetani akuletee mawazo mengine.

.....Atukuzwe yeye awezaye kufanya zaidi ya yale tuyawazayo na kuyafikiri kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.

SISI WACHUNGAJI TUMEZOEA KUWATUBISHA WATU DHAMBI WAKATI WAO WAKIMPOKEA KRISTO,LAKINI HUWA TUNASAHAU KUTUBU JUU YA VINYWA NA MIOYO YETU NA KUWATUBISHA HAO JUU YA MAMBO MAWILI PIA.

RUDI SASA KWENYE YALE MAKABRASHA NA MADAFTARI YA NDOTO ZAKO NA UANZE KUKIRI YALE UNAYOTAMANI KUWA NAYO HAPO BAADAE KUANZIA SASA.

BWANA NA AKUBARIKI SANA NA AKUSAIDIE KUCHUNGA KINYWA CHAKO NA MOYO WAKO,KATIKA JINA LA YESU AMEN!

Imeandikwa na
King Chavala
Moja kwa moja toka Dodoma!
KANISA LA TCCC,DODOMA

A RADICAL TRANSFORMATION

SHALOM!
RECEIVE A VERY SPECIAL SERMON FROM TB JOSHUA
 

The evidence of Jesus Christ is lives changed. You need to get connected to God and when you have a relationship with God, you change and become a man or woman controlled by your Heavenly Father and not by mans direction or circumstances. Who knows what you will become tomorrow; therefore, don’t allow your circumstances or your weakness to weigh you down because your current negative circumstances are not a reflection of your tomorrow. Nothing in this life is permanent; everything is subject to change. How you handle your rough, difficult time matters. If you handle your pain carefully and with an eye to God, it will turn into joy – only believe. Faith is the transformative power of the universe - a change from sickness to health, yoke to deliverance, weakness to strength, a faithless generation to a faithful generation, poverty to blessing.

There is indeed a promise of radical transformation for you.
Are you poor? Remember Jabez! (1 Chronicles 4:9-10)
Are you barren? Remember Hannah! (1 Samuel 1:2-20)
Are you sick? Remember Job! (Job 42:10)
Are you rejected? Remember Jephthah! (Judges 11-12)

Right now, ask God to take you from where you are to where He wants you to be. Follow the direction of your calling and you will astonish yourself.
BLESS YOU ALL!!